Mhubiri 5 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mhubiri 5:1-20

Simama Katika Kicho Cha Mungu

15:1 Za 89:7; Kut 3:5; Hos 6:6Linda hatua zako uendapo katika nyumba ya Mungu. Karibia usikilize kuliko kutoa dhabihu ya wapumbavu, ambao hawajui kuwa wanafanya kosa.

25:2 Amu 11:35; Ay 6:24; Mit 10:19; 20:25Usiwe mwepesi kuzungumza,

usiwe na haraka katika moyo wako

kuzungumza lolote mbele za Mungu.

Mungu yuko mbinguni

nawe uko duniani,

kwa hiyo maneno yako

na yawe machache.

35:3 Ay 20:8; Mhu 10:14Kama vile ndoto huja

wakati kuna shughuli nyingi,

ndivyo yalivyo mazungumzo ya mpumbavu

wakati kuna maneno mengi.

45:4 Mwa 28:20; Kum 23:21; Hes 30:2; Za 76:11; 119:60; Amu 11:35Wakati unapomwekea Mungu nadhiri, usikawie kuitimiza. Yeye hafurahii wapumbavu; timiza nadhiri yako. 55:5 Yon 2:9; Mdo 5:4; Hes 30:2-4Ni afadhali usiweke nadhiri kuliko kuiweka na usiitimize. 6Usiruhusu kinywa chako kukuingiza dhambini. Tena usijitetee mbele ya huyo mjumbe wa hekaluni, ukisema, “Niliweka nadhiri kwa makosa.” Kwa nini Mungu akasirike kwa ajili ya yale unayosema na kuiharibu kazi ya mikono yako? 75:7 Kum 10:12; Mhu 3:14; 12:13Kuota ndoto kwingi na maneno mengi ni ubatili. Kwa hiyo simama katika kicho cha Mungu.

Utajiri Ni Ubatili

85:8 Mhu 3:16; 4:1; Za 12:5Kama ukiona maskini wanaonewa katika nchi, hukumu na haki vikipotoshwa, usishangazwe na mambo hayo, kwa maana afisa mmoja anaangaliwa na aliye juu yake zaidi na juu ya hao wawili kuna wengine walio juu zaidi yao. 9Mafanikio ya nchi ni kwa ajili ya wote, hata mfalme mwenyewe hufaidi kutoka mashambani.

10Yeyote apendaye fedha kamwe

hatosheki na fedha;

yeyote apendaye utajiri kamwe

hatosheki na kipato chake.

Hili nalo pia ni ubatili.

11Mali ikiongezeka, ndivyo walaji

wanavyoongezeka.

Hii nayo inamfaidia nini mwenye mali

isipokuwa ni kushibisha macho yake?

125:12 Ay 20:20Usingizi wa kibarua ni mtamu,

awe amekula kidogo au kingi,

lakini wingi wa mali

humnyima tajiri usingizi.

135:13 Mhu 6:1-2Nimeshaona uovu mzito chini ya jua:

Utajiri uliolimbikizwa kwa kujinyima

na kuleta madhara kwa mwenye mali,

14au utajiri uliopotea kwa bahati mbaya,

hivyo kwamba wakati akiwa na mwana

hakuna chochote kilichobaki kwa ajili yake.

155:15 Za 49:17; 1Tim 6:7; Ay 1:21; Mhu 1:3Mtu hutoka tumboni mwa mama yake uchi,

naye jinsi alivyokuja vivyo hivyo huondoka.

Hachukui chochote kutokana na kazi yake

ambacho anaweza kukibeba mkononi mwake.

165:16 Mit 11:29; Mhu 1:3Hili nalo ni baya la kusikitisha:

Kama vile mtu ajavyo, vivyo hivyo huondoka,

naye anapata faida gani,

maadamu hutaabika kwa ajili ya upepo?

17Siku zake zote hula gizani,

pamoja na fadhaa kubwa,

mateso na hasira.

185:18 Mhu 2:3, 10, 14, 24Ndipo nikatambua kwamba ni vyema na sahihi kwa mtu kula na kunywa na kutosheka katika kazi yake ngumu chini ya jua katika siku chache za maisha yake Mungu alizompa, kwa maana hili ndilo fungu lake. 195:19 1Nya 29:12; 2Nya 1:12; Ay 31:2; Mhu 2:24; 6:2Zaidi ya yote, Mungu anapompa mtu yeyote utajiri na milki, humwezesha kuvifurahia, kukubali fungu lake na kuwa na furaha katika kazi yake, hii ni karama ya Mungu. 205:20 Kum 12:7, 18; Kut 23:25Mara chache mtu huzifikiri siku za maisha yake, kwa sababu Mungu humfanya ashikwe na furaha ya moyoni.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

传道书 5:1-20

敬畏上帝

1你进入上帝的殿时要小心谨慎,近前倾听胜过愚人献祭,因为他们不知道自己是在作恶。 2在上帝面前不要冒失开口,不可急于发言,因为祂在天上,你在地上。所以,你要少言寡语。 3事务繁杂,夜里多梦;多言多语,显出愚昧。 4你向上帝许愿,不可迟迟不还,因为祂不喜欢这样的愚人。要还所许的愿。 5与其许了愿不还,倒不如不许。 6不要在言语上犯罪,也不要在祭司5:6 祭司”希伯来文是“使者”。面前说许错了愿。为什么用言语惹上帝发怒,以致祂摧毁你手中的工作呢? 7多梦多言都是虚空。你只要敬畏上帝!

财富虚空

8若你在某地看见穷人受欺压,公平正义被扭曲,不要震惊,因为官上有官,在众官之上还有更高的官。 9况且,地的出产滋养万物,就是君王也需要从田地得到供应。 10贪爱钱财的,金银不能使他满足;贪图富裕的,再多的利益也不能叫他称心。这也是虚空! 11财富增加,消费的人也增加,这对财富的主人有什么益处呢?只是过眼烟云罢了! 12劳力的人不管吃多吃少,总是睡得香甜;富人的万贯家财却害得他不能成眠。 13我看到日光之下有一件可悲的事:有人积攒财宝,反而害了自己。 14经营不善,便财富尽失,什么也不能留给儿子。 15人怎样从母腹空空而来,也必照样空空而去;劳碌一生,什么也不能带走。 16这是多么可悲啊!人怎样来,也要怎样去,为风劳碌有什么益处呢? 17他一生活在黑暗中,饱受烦恼、病痛和愤怒的困扰。 18我认为人生最美最善的是,在上帝所赐的短暂岁月中尽情吃喝,享受自己在日光之下劳苦得来的成果。因为这是人当得的。 19上帝不单给人财富,也叫他能吃能喝,享用自己所当得的,并在劳碌中得到快乐,这都是上帝的恩赐。 20他不用担忧自己寿命的长短,因为上帝使他心里充满喜乐。