Mhubiri 2 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mhubiri 2:1-26

Anasa Ni Ubatili

12:1 Za 10:6; Lk 12:19; Mhu 7:4; 8:15Nikafikiri moyoni mwangu, “Haya basi, nitakujaribu kwa anasa nione ni lipi lililo jema.” Lakini hilo nalo likaonekana ni ubatili. 22:2 Mit 14:13; Isa 22:12-13; Mhu 7:6Nikasema, “Kicheko nacho ni upumbavu. Nayo matokeo ya anasa ni nini?” 32:3 Amu 9:13; Rut 3:3; Amo 6:3-6; Mhu 3:12-13; 5:18; 8:15Nikajaribu kujifurahisha kwa mvinyo na kukumbatia upumbavu, huku bado akili yangu inaniongoza kwa hekima. Nilitaka kuona ni lipi bora watu wafanye kwa siku chache wanazoishi chini ya mbingu.

42:4 1Fal 7:1-12; Wim 8:11; 2Nya 2:1Nikafanya miradi mikubwa: Nikajijengea majumba na kulima mashamba ya mizabibu. 5Nikatengeneza bustani na viwanja vya starehe nikaotesha huko kila aina ya miti ya matunda. 6Nikajenga mabwawa ya kukusanya maji ya kunyweshea hii miti iliyokuwa inastawi vizuri. 7Nikanunua watumwa wa kiume na wa kike na watumwa wengine walizaliwa nyumbani mwangu. Pia nilikuwa na makundi ya ngʼombe, kondoo na mbuzi kuliko mtu yeyote aliyewahi kuishi Yerusalemu kabla yangu. 82:8 1Fal 9:28; 10:10-21; 2Sam 19:35; Amu 3:15Nikajikusanyia fedha na dhahabu, hazina za wafalme na za majimbo. Nikajipatia waimbaji wanaume na wanawake, nazo nyumba za masuria: vitu ambavyo moyo wa mwanadamu hufurahia. 92:9 1Nya 29:25; Mhu 1:12-16Nikawa maarufu sana kuliko mtu mwingine yeyote aliyepata kuishi Yerusalemu kabla yangu. Katika haya yote bado nikawa nina hekima.

10Sikujinyima kitu chochote ambacho macho yangu yalikitamani,

hakuna anasa ambayo niliunyima moyo wangu.

Moyo wangu ulifurahia kazi zangu zote,

hii ilikuwa thawabu ya kazi zangu zote.

11Hata hivyo nilipokuja kuangalia yote ambayo

mikono yangu ilikuwa imefanya

na yale niliyotaabika kukamilisha,

kila kitu kilikuwa ni ubatili, ni kukimbiza upepo;

hapakuwa na faida yoyote chini ya jua.

Hekima Na Upumbavu Ni Ubatili

12Kisha nikageuza mawazo yangu kufikiria hekima,

wazimu na upumbavu.

Ni nini zaidi mtu anayetawala baada ya mfalme

anachoweza kufanya ambacho hakijafanywa?

132:13 Mhu 7:11-12, 19; 9:18Nikaona kuwa hekima ni bora kuliko upumbavu,

kama vile nuru ilivyo bora kuliko giza.

142:14 Za 49:10; Mit 17:24; Mhu 8:1; 3:19; 7:2; 9:3, 11-12Mtu mwenye hekima ana macho katika kichwa chake,

lakini mpumbavu anatembea gizani;

lakini nikaja kuona kwamba

wote wawili hatima yao inafanana.

152:15 Mhu 6:8Kisha nikafikiri moyoni mwangu,

“Hatima ya mpumbavu itanipata mimi pia.

Nitafaidi nini basi kwa kuwa na hekima?”

Nikasema moyoni mwangu,

“Hili nalo ni ubatili.”

162:16 Za 49:10; 112:6; Mhu 1:11Kwa maana kwa mtu mwenye hekima,

kama ilivyo kwa mpumbavu,

hatakumbukwa kwa muda mrefu,

katika siku zijazo wote watasahaulika.

Kama vile ilivyo kwa mpumbavu,

mtu mwenye hekima pia lazima atakufa!

Kutaabika Ni Ubatili

17Kwa hiyo nikachukia maisha, kwa sababu kazi inayofanyika chini ya jua ilikuwa masikitiko kwangu. Yote hayo ni ubatili, ni kukimbiza upepo. 182:18 Za 39:6; 49:10; 1Fal 12:13Nikachukia kila kitu nilichokuwa nimetaabikia chini ya jua, kwa sababu ni lazima nimwachie yule ajaye baada yangu. 19Nani ajuaye kama atakuwa ni mtu mwenye hekima au mpumbavu? Lakini hata hivyo yeye ndiye atakayetawala kazi zote ambazo nimemiminia juhudi na ustadi chini ya jua. Hili nalo ni ubatili. 20Kwa hiyo moyo wangu ukaanza kukata tamaa juu ya kazi yangu yote niliyoifanya kwa taabu chini ya jua. 21Kwa kuwa mtu anaweza kufanya kazi yake kwa hekima, maarifa na ustadi, kisha analazimika kuacha vyote alivyo navyo kwa mtu mwingine ambaye hajavifanyia kazi. Hili nalo pia ni ubatili tena ni balaa kubwa. 222:22 Mhu 3:9; 1:3Mtu atapata nini kwa taabu yote na kuhangaika kwa bidii katika kazi anayotaabikia chini ya jua? 232:23 Ay 5:7; 7:2; 14:1; Mhu 1:18; Mwa 3:17Siku zake zote kazi yake ni maumivu na masikitiko, hata usiku akili yake haipati mapumziko. Hili nalo pia ni ubatili.

242:24 1Kor 15:32; Mhu 3:12-13, 22; 7:7-10; 8:15; 5:17-19; 9:7-10; 11:7-10; Ay 2:10Hakuna kitu bora anachoweza kufanya mtu zaidi ya kula na kunywa na kuridhika katika kazi yake. Hili nalo pia, ninaona, latokana na mkono wa Mungu, 25kwa sababu pasipo yeye, ni nani awezaye kula na kufurahi? 262:26 Ay 27:17; 9:4; Mit 13:22Kwa yule mtu anayempendeza Mungu, Mungu humpa hekima, maarifa na furaha, bali kwa mwenye dhambi Mungu humpa kazi ya kukusanya na kuhifadhi utajiri ili Mungu ampe yule anayempenda. Hili nalo pia ni ubatili, ni kukimbiza upepo.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

传道书 2:1-26

1我心里想:“来吧,不如尽情享乐,好好享受!”唉!结果这也是虚空。 2我说:“欢笑只不过是一阵狂妄,享乐又有什么用!” 3于是,我决意用酒使自己快乐,在体验愚昧的同时仍然保持理智,直到我明白在短暂的人生岁月中做何事才有益。 4我大动工程,为自己建造房屋,栽种葡萄园, 5开垦花圃园囿,种植各种果树, 6开凿池塘,浇灌茂林。 7我买了仆婢,又有生在家中的仆婢,拥有的牛羊远超过有史以来耶路撒冷的任何人。 8我为自己积聚金银,搜罗列王和各省的奇珍异宝,得到男女歌优及许多妃嫔——都是世人所想望的。 9这样,我便财势日增,享誉盛名,超过耶路撒冷历来所有的人。然而,我仍然保持智慧。 10凡我眼睛爱看的、心里渴慕的,我都随心所欲,尽情享受。我的心从劳碌中得到欢乐,这是我劳碌所得的回报。 11然而,当我回顾双手辛勤经营的一切成就时,唉,却发现都是虚空,都是捕风;日光之下的一切都毫无益处。 12于是,我转念思考什么是智慧、狂妄和愚昧。其实以后接替君王的人除了重演历史之外,还能做什么呢? 13我领悟到智慧胜过愚昧,如同光明胜过黑暗。 14智者高瞻远瞩,愚人却在黑暗中摸索。但我知道两者终必有同样的命运。 15于是,我想:“既然愚人的命运也将是我的命运,我有智慧又怎么样呢?我只能说,‘这也是虚空。’” 16因为智者和愚人一样,不过被人记得一时,日后都会被遗忘。两者都难逃死亡。 17所以,我憎恶生命,因为在日光之下所做的一切都令我愁烦。唉!这一切都是虚空,都是捕风。 18我憎恶自己在日光之下劳碌得来的一切,因为这些必留给后人。 19谁知道那人是智者还是愚人呢?然而,他却要接管我在日光之下用智慧辛勤经营的产业。这也是虚空。 20因此,我对自己在日光之下一切的劳碌感到绝望。 21一个人用智慧、知识和技能所得来的一切,却要留给不劳而获的人享用,这也是虚空,是极大的不幸! 22世人在日光之下劳心劳力,究竟得到什么呢? 23他们一生充满痛苦,劳碌中尽是愁烦,即使夜间心里也不安宁。这也是虚空。 24对人而言,没有什么比吃喝并享受劳碌之乐更好,我看这也是出自上帝的手。 25离了上帝,谁还能吃喝享受呢? 26上帝把智慧、知识和喜乐赐给祂喜悦的人,却让罪人忙于积攒财富,然后把他们的财富赐给祂喜悦的人。这也是虚空,也是捕风。