Mathayo 9 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mathayo 9:1-38

Yesu Amponya Mtu Aliyepooza

(Marko 2:1-12; Luka 5:17-26)

19:1 Mt 4:13Yesu akaingia kwenye chombo, akavuka na kufika katika mji wa kwao. 29:2 Mt 4:24; 9:22; Yn 16:33; Lk 7:48Wakati huo huo wakamletea mtu aliyepooza, akiwa amelazwa kwenye mkeka. Yesu alipoiona imani yao, alimwambia yule mtu aliyepooza, “Mwanangu, jipe moyo mkuu. Dhambi zako zimesamehewa.”

39:3 Mt 26:65; Yn 10:33; Mk 2:7Kwa ajili ya jambo hili, baadhi ya walimu wa sheria wakasema mioyoni mwao, “Huyu mtu anakufuru!”

49:4 Za 94:11; Yn 2:22Lakini Yesu akiyafahamu mawazo yao, akawaambia, “Kwa nini mnawaza maovu mioyoni mwenu? 5Je, ni lipi lililo rahisi zaidi: kusema, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kusema, ‘Inuka, uende’? 69:6 Mt 9:22Lakini, ili mpate kujua kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani kusamehe dhambi…” Ndipo akamwambia yule aliyepooza, “Inuka, chukua mkeka wako, uende nyumbani kwako.” 7Yule mtu akasimama, akaenda nyumbani kwake. 89:8 Yn 15:8; Mdo 4:21Makutano walipoyaona haya, wakajawa na hofu ya Mungu, wakamtukuza Mungu ambaye alikuwa ametoa mamlaka kama haya kwa wanadamu.

Kuitwa Kwa Mathayo

(Marko 2:13-17; Luka 5:27-32)

99:9 Mt 4:19Yesu alipokuwa akienda kutoka huko, alimwona mtu mmoja jina lake Mathayo akiwa ameketi forodhani mahali pa kutoza ushuru. Yesu akamwambia, “Nifuate.” Mathayo akaondoka, akamfuata.

10Yesu alipokuwa akila chakula ndani ya nyumba ya Mathayo, watoza ushuru wengi na “wenye dhambi” wakaja kula pamoja naye na wanafunzi wake. 119:11 Lk 19:7; Gal 2:15Mafarisayo walipoona mambo haya, wakawauliza wanafunzi wake, “Kwa nini Mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na ‘wenye dhambi’?”

12Lakini Yesu aliposikia hayo, akawaambia, “Watu wenye afya hawahitaji tabibu, lakini wale walio wagonjwa ndio wanaohitaji tabibu. 139:13 Mik 6:6-8; Mt 12:7; Lk 19:10; 1Tim 1:15Nendeni mkajifunze maana ya maneno haya: ‘Nataka rehema, wala si dhabihu.’ Kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.”

Yesu Aulizwa Kuhusu Kufunga

(Marko 2:18-22; Luka 5:33-39)

149:14 Mt 11:18-19; Lk 18:12Wanafunzi wa Yohana Mbatizaji wakaja na kumuuliza Yesu, “Imekuwaje kwamba sisi na Mafarisayo tunafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?”

159:15 Yn 3:29; Mdo 13:2-3; 14:23Yesu akawajibu, “Wageni wa bwana arusi wawezaje kuomboleza wakati angali pamoja nao? Wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kwao. Hapo ndipo watakapofunga.

169:16 Yn 1:17“Hakuna mtu anayeshonea kiraka kipya kwenye nguo iliyochakaa, kwa maana kile kiraka kitachanika kutoka kwenye hiyo nguo, nayo hiyo nguo itachanika zaidi. 17Wala watu hawaweki divai mpya kwenye viriba vikuukuu. Kama wakifanya hivyo, viriba vitapasuka nayo divai itamwagika, navyo viriba vitaharibika. Lakini divai mpya huwekwa kwenye viriba vipya, na hivyo divai na viriba huwa salama.”

Mwanamke Aponywa

(Marko 5:21-43; Luka 8:40-56)

189:18 Mt 8:2; Mk 5:23Yesu alipokuwa akiwaambia mambo haya, mara akaingia kiongozi wa sinagogi akapiga magoti mbele yake, akamwambia, “Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini njoo uweke mkono wako juu yake, naye atakuwa hai.” 19Yesu akaondoka akafuatana naye, nao wanafunzi wake pia wakaandamana naye.

209:20 Mk 6:56; Lk 6:19Wakati huo huo, mwanamke mmoja, ambaye alikuwa na ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, akaja nyuma ya Yesu, akagusa upindo wa vazi lake, 219:21 Mt 14:36kwa maana alisema moyoni mwake, “Kama nikigusa tu vazi lake, nitaponywa.”

229:22 Lk 17:19; 18:42; Mt 15:28Yesu akageuka, naye alipomwona akamwambia, “Binti, jipe moyo mkuu, imani yako imekuponya.” Naye yule mwanamke akapona kuanzia saa ile ile.

Yesu Amfufua Binti Wa Kiongozi Wa Sinagogi

239:23 2Nya 35:25; Yer 9:17-18Yesu alipofika nyumbani kwa yule kiongozi wa sinagogi na kuwaona waombolezaji wakipiga filimbi za maombolezo na watu wengi wakipiga kelele, 249:24 Mdo 20:10; Dan 12:2; 1The 4:13-16; Yn 11:11akawaambia, “Ondokeni! Kwa maana binti huyu hakufa, bali amelala.” Wakamcheka kwa dhihaka. 259:25 Lk 7:14Lakini watu walipokwisha kutolewa nje, akaingia mle ndani na kumshika yule binti mkono, naye akaamka. 269:26 Mk 1:28, 45; Lk 5:15Habari hizi zikaenea katika maeneo yale yote.

Yesu Awaponya Vipofu

279:27 Mk 10:47; Lk 18:38-39Yesu alipokuwa akiondoka mahali pale, vipofu wawili wakamfuata wakipiga kelele kwa nguvu na kusema, “Mwana wa Daudi, tuhurumie!”

289:28 Mdo 14:19Alipoingia mle nyumbani wale vipofu wakamjia. Naye Yesu akawauliza, “Mnaamini kwamba ninaweza kufanya jambo hili?”

Wakamjibu, “Ndiyo, Bwana.”

299:29 Mt 8:11; 9:22Ndipo Yesu akagusa macho yao na kusema, “Iwe kwenu sawasawa na imani yenu.” 309:30 Mt 8:4Macho yao yakafunguka. Yesu akawaonya vikali, akisema, “Angalieni mtu yeyote asijue kuhusu jambo hili.” 319:31 Mt 9:26; Mk 7:36Lakini wao wakaenda na kueneza habari zake katika eneo lile lote.

Yesu Amponya Mtu Bubu

329:32 Mt 4:24; 12:22-24Walipokuwa wanatoka, mtu mmoja aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu na ambaye hakuweza kuongea aliletwa kwa Yesu. 339:33 Mk 2:12Yule pepo mchafu alipotolewa, yule mtu aliyekuwa bubu akaongea. Ule umati wa watu ukastaajabu na kusema, “Jambo kama hili kamwe halijapata kuonekana katika Israeli.”

349:34 Mt 12:24Lakini Mafarisayo wakasema, “Huyo anatoa pepo wachafu kwa uwezo wa mkuu wa pepo wachafu.”

Watendakazi Ni Wachache

359:35 Mt 4:23Yesu akazunguka katika miji yote na vijiji vyote, akifundisha katika masinagogi yao, akihubiri habari njema za Ufalme, na akiponya kila ugonjwa na kila aina ya maradhi. 369:36 Mt 15:32; Mk 8:2; 6:34; 1Fal 22:17Alipoona makutano, aliwahurumia kwa sababu walikuwa wanasumbuka bila msaada, kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. 379:37 Yn 4:35; Lk 10:2Ndipo akawaambia wanafunzi wake, “Mavuno ni mengi lakini watendakazi ni wachache. 389:38 2The 3:1Kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno, ili apeleke watendakazi katika shamba lake la mavuno.”

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

马太福音 9:1-38

医治瘫子

1耶稣坐船回到湖对岸自己住的城镇。

2有人用担架把一个瘫子抬到耶稣面前。耶稣看见他们的信心,就对瘫子说:“孩子,放心吧!你的罪得到赦免了。”

3几个律法教师听了,心里想:“这个人是在亵渎上帝。”

4耶稣知道他们的心思,就说:“你们为什么心怀恶念呢? 5说‘你的罪得到赦免了’容易呢?还是说‘你起来行走’容易呢? 6如今我要让你们知道人子在世上有赦罪的权柄。”于是祂对瘫子说:“起来!收拾你的担架回家去吧。”

7那人立刻站起来,回家去了。 8看见的人都充满了敬畏,就赞美把这样的权柄赐给人的上帝。

呼召马太

9耶稣离开那里往前走,看见一个名叫马太的人坐在收税站里,便对他说:“跟从我!”马太就站起来跟从了耶稣。

10耶稣在马太家里坐席的时候,很多税吏和罪人前来跟耶稣和祂的门徒一起坐席。 11法利赛人看见了,就质问耶稣的门徒:“你们的老师为何跟税吏和罪人一起吃饭?” 12耶稣听见后,答道:“健康的人不需要医生,有病的人才需要。 13圣经上说,‘我喜爱怜悯之心,而非祭物’,你们去揣摩这句话的意思吧。我来不是要召义人,乃是要召罪人。”

禁食的问题

14那时,约翰的门徒来问耶稣:“我们和法利赛人常常禁食,为什么你的门徒不禁食呢?”

15耶稣对他们说:“新郎和宾客还在一起的时候,宾客怎能悲伤呢?但有一天新郎将被带走,那时他们就要禁食了。

16“没有人用新布缝补旧衣,恐怕新布会把旧衣扯破,破洞会更大。 17也没有人用旧皮囊来盛新酒,否则皮囊会胀破,酒也漏了,皮囊也毁了。人们总是把新酒装在新皮囊里,以便两样都能保住。”

起死回生

18当耶稣在说话的时候,来了一个管理会堂的人跪在祂面前,说:“我的女儿刚刚死了,请你去把手按在她身上,她就会活过来。” 19耶稣和门徒就起身跟着他去了。 20途中,有一个患了十二年血漏病的女人挤到耶稣的背后,摸了一下祂衣服的穗边, 21因为她心想:“我只要摸到祂的衣服,病就会好。” 22耶稣转过头来,看见她,就说:“女儿,放心吧,你的信心救了你。”就在那一刻,她的顽疾痊愈了。

23耶稣来到管理会堂之人的家,看见殡葬的吹乐手和乱嚷嚷的人群, 24就吩咐他们:“你们出去吧,这女孩并没有死,只是睡着了。”他们都讥笑祂。

25耶稣让众人都出去,然后进去拉着女孩的手,女孩就起来了。 26这件事传遍了整个地区。

医治瞎子和哑巴

27耶稣从那里往前走,有两个瞎子跟着祂,高声呼叫:“大卫的后裔啊,可怜我们吧!”

28耶稣进了房子,那两个瞎子来到祂面前。耶稣问他们:“你们相信我能做这事吗?”他们说:“主啊,我们相信。”

29于是,耶稣摸他们的眼睛,并说:“照你们的信心成全你们吧。” 30他们立刻得见光明。耶稣郑重地叮嘱他们:“不要张扬这件事。” 31但他们出去后把祂所行的事传遍了那一带。

32他们正要离去,有人带着一个被鬼附身的哑巴来见耶稣。 33耶稣把鬼赶出去后,哑巴就能说话了。

众人都感到惊奇,说:“在以色列从未见过这样的事。”

34法利赛人却说:“祂只不过是靠鬼王赶鬼。”

耶稣怜悯众人

35耶稣走遍了各城各乡,在会堂里教导人,传讲天国的福音,医治各样的疾病。 36祂看见众人,心里怜悯他们,因为他们困苦无助,好像没有牧人的羊。 37耶稣对门徒说:“要收割的庄稼很多,工人却很少。 38因此,你们要祈求庄稼的主人派更多的工人去收割。”