Mahubiri Ya Yesu Kwenye Mlima
(Mathayo 5–7)
Sifa Za Aliyebarikiwa
(Luka 6:20-23)
15:1 Mk 3:13, 20; Lk 6:20-49Basi Yesu alipoona makutano, alipanda mlimani akaketi chini, nao wanafunzi wake wakamjia. 2Ndipo akaanza kuwafundisha, akisema:
35:3 Mt 5:10, 19; 25:34; Isa 57:15“Heri walio maskini wa roho,
maana Ufalme wa Mbinguni ni wao.
45:4 Isa 61:2-3; Ufu 7:17Heri wale wanaohuzunika,
maana hao watafarijiwa.
55:5 Za 37:11; Rum 4:13Heri walio wapole,
maana hao watairithi nchi.
65:6 Isa 55:1-2Heri wenye njaa na kiu ya haki,
maana hao watatoshelezwa.
75:7 Yak 2:13; Za 41:1; Mt 6:14; Mk 11:24Heri wenye huruma,
maana hao watapata rehema.
85:8 Za 24:3-4; 73:1; 17:15; Ebr 12:14Heri walio na moyo safi,
maana hao watamwona Mungu.
95:9 Mt 5:44, 45; Rum 8:14Heri walio wapatanishi,
maana hao wataitwa wana wa Mungu.
105:10 1Pet 3:14Heri wanaoteswa kwa sababu ya haki,
maana Ufalme wa Mbinguni ni wao.
115:11 Isa 51:7; 1Pet 4:14“Heri ninyi watu watakapowashutumu, na kuwatesa na kunena dhidi yenu mabaya ya aina zote kwa uongo kwa ajili yangu. 125:12 Za 9:2; 2Nya 36:16; 2Kor 6:10Furahini na kushangilia kwa maana thawabu yenu ni kubwa mbinguni, kwa kuwa hivyo ndivyo walivyowatesa manabii waliokuwa kabla yenu.
Chumvi Na Nuru
(Marko 9:50; Luka 14:34-35)
135:13 Mk 9:50; Lk 14:34-35“Ninyi ni chumvi ya ulimwengu. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake, yawezaje kurudishiwa ladha yake tena? Haifai tena kwa kitu chochote, ila kutupwa nje ikanyagwe na watu.
145:14 Yn 8:12“Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji uliojengwa kilimani hauwezi kufichika. 155:15 Mk 4:21; Lk 11:33Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa bakuli. Badala yake, huiweka kwenye kinara chake, nayo hutoa mwanga kwa kila mtu aliyemo ndani ya ile nyumba. 165:16 Efe 5:8-9; 1Pet 2:12Vivyo hivyo, nuru yenu iangaze mbele ya watu, ili wapate kuona matendo yenu mema wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
Kutimiza Sheria
175:17 Rum 3:31; 10:4; Gal 1:24“Msidhani kwamba nimekuja kufuta Sheria au Manabii; sikuja kuondoa bali kutimiza. 185:18 Za 119:89; Mk 13:31Kwa maana, amin nawaambia, mpaka mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata herufi moja ndogo wala nukta itakayopotea kwa namna yoyote kutoka kwenye Sheria, mpaka kila kitu kiwe kimetimia. 195:19 Yak 2:10; 1Kor 15:9Kwa hiyo, yeyote atakayevunja mojawapo ya amri ndogo kuliko zote ya amri hizi, naye akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa Mbinguni, lakini yeyote azitendaye na kuzifundisha hizi amri ataitwa mkuu katika Ufalme wa Mbinguni. 205:20 Rum 9:31; 10:3Kwa maana nawaambia, haki yenu isipozidi haki ya Mafarisayo na walimu wa sheria, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa Mbinguni.
Kuhusu Hasira
(Luka 12:57-59)
215:21 Kut 21:12; 5:17; Law 24:17“Mmesikia walivyoambiwa watu wa zamani kwamba, ‘Usiue. Yeyote atakayeua atapaswa hukumu.’ 225:22 1Yn 3:22; Yn 11:47; Mdo 6:12; Lk 16:24; Yak 3:6Lakini mimi nawaambia kwamba, yeyote atakayemkasirikia ndugu yake, atapaswa hukumu. Tena, yeyote atakayemwambia ndugu yake, ‘Raka,’5:22 Raka ni neno la Kiaramu ambalo maana yake ni dharau au dhihaka ya hali ya juu. atapaswa kujibu kwa Baraza la Wayahudi.5:22 Baraza la Wayahudi lilikuwa kundi kuu kabisa la utawala wa Wayahudi lililoundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu. Lakini yeyote atakayesema ‘Wewe mpumbavu!’ atapaswa hukumu ya moto wa jehanamu.
235:23 Mt 8:4; 23:19; Mk 11:25“Kwa hiyo, kama unatoa sadaka yako madhabahuni, ukakumbuka kuwa ndugu yako ana kitu dhidi yako, 245:24 Ay 42:8; 18:19; 1Tim 2:8; 1Pet 3:7iache sadaka yako hapo mbele ya madhabahu. Enda kwanza ukapatane na ndugu yako; kisha urudi na ukatoe sadaka yako.
255:25 Mt 18:35; Lk 12:58-59“Patana na mshtaki wako upesi wakati uwapo njiani pamoja naye kwenda mahakamani, ili mshtaki wako asije akakutia mikononi mwa hakimu, naye hakimu akakutia mikononi mwa askari, nawe ukatupwa gerezani. 26Amin, nakuambia, hautatoka humo hadi uwe umelipa senti ya mwisho.
Kuhusu Uzinzi
275:27 Kut 20:14; Kum 5:18“Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Usizini.’ 285:28 Mit 6:25; 2Pet 2:14Lakini mimi nawaambia kwamba, yeyote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. 295:29 Rum 14:21; 1Kor 8:13Jicho lako la kuume likikusababisha kutenda dhambi, lingʼoe ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako mzima ukatupwa jehanamu. 305:30 Mt 5:29Kama mkono wako wa kuume ukikusababisha kutenda dhambi, ukate, uutupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako mzima utupwe jehanamu.
Kuhusu Talaka
(Mathayo 19:9; Marko 10:11-12; Luka 16:18)
315:31 Kum 24:1-4“Pia ilinenwa kwamba, ‘Mtu yeyote amwachaye mkewe sharti ampe hati ya talaka.’ 325:32 Lk 16:18Lakini mimi nawaambia, yeyote amwachaye mkewe isipokuwa kwa kosa la uasherati, amfanya mkewe kuwa mzinzi. Na yeyote amwoaye yule mwanamke aliyeachwa, anazini.
Kuhusu Kuapa
335:33 Law 19:12; Hes 30:2; Mt 23:16-22“Tena mmesikia walivyoambiwa watu wa zamani kwamba, ‘Usiape kwa uongo, bali timiza kiapo kile ulichofanya kwa Bwana.’ 345:34 Yak 5:12; Isa 66:1; Mt 23:22Lakini mimi nawaambia, msiape kabisa: iwe kwa mbingu, kwa kuwa ni kiti cha enzi cha Mungu; 355:35 Za 48:2au kwa dunia, kwa kuwa ndipo mahali pake pa kuwekea miguu; au kwa Yerusalemu, kwa kuwa ndio mji wa Mfalme Mkuu. 36Nanyi msiape kwa vichwa vyenu, kwa kuwa hamwezi kuufanya hata unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. 375:37 Yak 5:12; Efe 6:16; 1Yn 3:12‘Ndiyo’ yenu iwe ‘Ndiyo,’ na ‘Hapana’ yenu iwe ‘Hapana.’ Lolote zaidi ya hili latoka kwa yule mwovu.
Kuhusu Kulipiza Kisasi
(Luka 6:29-30)
385:38 Law 24:20; Kum 19:21“Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Jicho kwa jicho na jino kwa jino.’ 395:39 1Kor 6:7; 1Pet 3:9Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu. Lakini kama mtu akikupiga kwenye shavu la kuume, mgeuzie na la pili pia. 405:40 1Kor 6:7Kama mtu akitaka kukushtaki na kuchukua joho lako, mwachie achukue na koti pia. 415:41 Mt 27:32; Mk 15:21Kama mtu akikulazimisha kwenda maili moja, nenda naye maili mbili. 425:42 Kum 15:8; Lk 16:30Mpe yeye akuombaye, wala usimgeuzie kisogo yeye atakaye kukukopa.
Upendo Kwa Adui
(Luka 6:27-28, 32-36)
435:43 Law 19:18; Gal 5:14; Kum 23:6; Za 139:21-22“Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Mpende jirani yako na umchukie adui yako.’ 445:44 Yn 15:20; Rum 8:35Lakini ninawaambia: Wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowatesa ninyi, 455:45 Lk 6:35; Rum 8:14; Ay 25:3ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu waovu na watu wema, naye huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. 465:46 Lk 6:32Kama mkiwapenda tu wale wanaowapenda, mtapata thawabu gani? Je, hata watoza ushuru hawafanyi hivyo? 47Nanyi kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mnafanya nini zaidi ya wengine? Je, hata watu wasiomjua Mungu, hawafanyi hivyo? 485:48 Law 19:2; 1Pet 1:16Kwa hiyo kuweni wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
1And seeing the multitudes, he went up into a mountain: and when he was set, his disciples came unto him: 2And he opened his mouth, and taught them, saying, 3Blessed are the poor in spirit: for theirs is the kingdom of heaven. 4Blessed are they that mourn: for they shall be comforted. 5Blessed are the meek: for they shall inherit the earth. 6Blessed are they which do hunger and thirst after righteousness: for they shall be filled. 7Blessed are the merciful: for they shall obtain mercy. 8Blessed are the pure in heart: for they shall see God. 9Blessed are the peacemakers: for they shall be called the children of God. 10Blessed are they which are persecuted for righteousness’ sake: for theirs is the kingdom of heaven. 11Blessed are ye, when men shall revile you, and persecute you, and shall say all manner of evil against you falsely, for my sake. 12Rejoice, and be exceeding glad: for great is your reward in heaven: for so persecuted they the prophets which were before you.
13¶ Ye are the salt of the earth: but if the salt have lost his savour, wherewith shall it be salted? it is thenceforth good for nothing, but to be cast out, and to be trodden under foot of men. 14Ye are the light of the world. A city that is set on an hill cannot be hid. 15Neither do men light a candle, and put it under a bushel, but on a candlestick; and it giveth light unto all that are in the house. 16Let your light so shine before men, that they may see your good works, and glorify your Father which is in heaven.
17¶ Think not that I am come to destroy the law, or the prophets: I am not come to destroy, but to fulfil. 18For verily I say unto you, Till heaven and earth pass, one jot or one tittle shall in no wise pass from the law, till all be fulfilled. 19Whosoever therefore shall break one of these least commandments, and shall teach men so, he shall be called the least in the kingdom of heaven: but whosoever shall do and teach them, the same shall be called great in the kingdom of heaven. 20For I say unto you, That except your righteousness shall exceed the righteousness of the scribes and Pharisees, ye shall in no case enter into the kingdom of heaven.
21¶ Ye have heard that it was said by them of old time, Thou shalt not kill; and whosoever shall kill shall be in danger of the judgment: 22But I say unto you, That whosoever is angry with his brother without a cause shall be in danger of the judgment: and whosoever shall say to his brother, Raca, shall be in danger of the council: but whosoever shall say, Thou fool, shall be in danger of hell fire. 23Therefore if thou bring thy gift to the altar, and there rememberest that thy brother hath ought against thee; 24Leave there thy gift before the altar, and go thy way; first be reconciled to thy brother, and then come and offer thy gift. 25Agree with thine adversary quickly, whiles thou art in the way with him; lest at any time the adversary deliver thee to the judge, and the judge deliver thee to the officer, and thou be cast into prison. 26Verily I say unto thee, Thou shalt by no means come out thence, till thou hast paid the uttermost farthing.
27¶ Ye have heard that it was said by them of old time, Thou shalt not commit adultery: 28But I say unto you, That whosoever looketh on a woman to lust after her hath committed adultery with her already in his heart. 29And if thy right eye offend thee, pluck it out, and cast it from thee: for it is profitable for thee that one of thy members should perish, and not that thy whole body should be cast into hell. 30And if thy right hand offend thee, cut it off, and cast it from thee: for it is profitable for thee that one of thy members should perish, and not that thy whole body should be cast into hell. 31It hath been said, Whosoever shall put away his wife, let him give her a writing of divorcement: 32But I say unto you, That whosoever shall put away his wife, saving for the cause of fornication, causeth her to commit adultery: and whosoever shall marry her that is divorced committeth adultery.
33¶ Again, ye have heard that it hath been said by them of old time, Thou shalt not forswear thyself, but shalt perform unto the Lord thine oaths: 34But I say unto you, Swear not at all; neither by heaven; for it is God’s throne: 35Nor by the earth; for it is his footstool: neither by Jerusalem; for it is the city of the great King. 36Neither shalt thou swear by thy head, because thou canst not make one hair white or black. 37But let your communication be, Yea, yea; Nay, nay: for whatsoever is more than these cometh of evil.
38¶ Ye have heard that it hath been said, An eye for an eye, and a tooth for a tooth: 39But I say unto you, That ye resist not evil: but whosoever shall smite thee on thy right cheek, turn to him the other also. 40And if any man will sue thee at the law, and take away thy coat, let him have thy cloke also. 41And whosoever shall compel thee to go a mile, go with him twain. 42Give to him that asketh thee, and from him that would borrow of thee turn not thou away.
43¶ Ye have heard that it hath been said, Thou shalt love thy neighbour, and hate thine enemy. 44But I say unto you, Love your enemies, bless them that curse you, do good to them that hate you, and pray for them which despitefully use you, and persecute you; 45That ye may be the children of your Father which is in heaven: for he maketh his sun to rise on the evil and on the good, and sendeth rain on the just and on the unjust. 46For if ye love them which love you, what reward have ye? do not even the publicans the same? 47And if ye salute your brethren only, what do ye more than others? do not even the publicans so? 48Be ye therefore perfect, even as your Father which is in heaven is perfect.