Mathayo 4 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mathayo 4:1-25

Kujaribiwa Kwa Yesu

(Marko 1:12-13; Luka 4:1-13)

14:1 Kut 34:28; 1Fal 19:8Kisha Yesu akaongozwa na Roho Mtakatifu kwenda nyikani ili akajaribiwe na ibilisi. 24:2 Kut 34:28; 1Fal 19:8Baada ya kufunga siku arobaini usiku na mchana, hatimaye akaona njaa. 34:3 1The 3:5; Mk 3:11; Ufu 2:18Mjaribu akamjia na kumwambia, “Ikiwa wewe ndiye Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”

44:4 Kum 8:3; Yn 4:34Lakini Yesu akajibu, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.’ ”

54:5 Neh 11:1; Mt 27:5Ndipo ibilisi akamchukua Yesu mpaka mji mtakatifu na kumweka juu ya mnara mrefu wa Hekalu, 64:6 Za 91:11-12; Mt 4:3akamwambia, “Kama wewe ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini. Kwa kuwa imeandikwa:

“ ‘Atakuagizia malaika zake,

nao watakuchukua mikononi mwao

ili usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.’ ”

74:7 Kum 6:16Yesu akamjibu, “Pia imeandikwa: ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’ ”

8Kwa mara nyingine, ibilisi akamchukua Yesu mpaka kwenye kilele cha mlima mrefu na kumwonyesha falme zote za dunia na fahari zake, 9kisha akamwambia, “Nitakupa hivi vyote kama ukinisujudia na kuniabudu.”

104:10 Ay 1:6-9; Rum 16:20; 6:13Yesu akamwambia, “Ondoka mbele yangu, Shetani! Kwa maana imeandikwa, ‘Mwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.’ ”

114:11 Lk 22:43; Ebr 1:14Ndipo ibilisi akamwacha, nao malaika wakaja na kumhudumia.

Yesu Aanza Kuhubiri

(Marko 1:14-15; Luka 4:14-15)

124:12 Mt 14:3; Mk 1:14Yesu aliposikia kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa ametiwa gerezani, alirudi Galilaya. 134:13 Mk 9:33; Yn 2:12Akaondoka Nazareti akaenda kuishi Kapernaumu, mji ulioko karibu na bahari, katika mipaka ya nchi ya Zabuloni na Naftali, 144:14 Isa 9:1, 2; 9:1; Mt 1:22ili kutimiza unabii wa nabii Isaya, kama alivyosema:

154:15 Isa 9:1, 2“Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali,

kwenye njia ya kuelekea baharini,

ngʼambo ya Yordani,

Galilaya ya watu wa Mataifa:

164:16 Isa 9:1-2; Yn 1:4-9watu wale waliokaa gizani

wameona nuru kuu;

nao wale walioishi katika nchi ya uvuli wa mauti,

nuru imewazukia.”

174:17 Mt 3:2; Mk 1:14, 15Tangu wakati huo, Yesu alianza kuhubiri akisema: “Tubuni, kwa maana Ufalme wa Mbinguni umekaribia.”

Yesu Awaita Wanafunzi Wake Wa Kwanza

(Marko 1:16-20; Luka 5:1-11)

184:18 Mk 7:31; Yn 6:1; Mt 16:17-18Yesu alipokuwa anatembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea ndugu yake. Walikuwa wakizitupa nyavu zao baharini kwa kuwa wao walikuwa wavuvi. 194:19 Lk 5:28; Yn 1:43Yesu akawaambia, “Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu.” 204:20 Mk 10:28; Lk 18:28; Mt 19:27Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.

214:21 Mk 3:17; Lk 8:51Alipoendelea mbele kutoka pale, akawaona ndugu wengine wawili, Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana nduguye, wakiwa wamekaa kwenye mashua pamoja na baba yao Zebedayo, wakizitengeneza nyavu zao. Yesu akawaita. 224:22 Mt 4:19Nao mara wakaiacha mashua yao, pamoja na baba yao, wakamfuata.

Yesu Ahubiri Na Kuponya Wagonjwa

(Luka 6:17-19)

234:23 Mk 1:39; Lk 4:15, 44; 7:22; Yn 18:20; 3:10; Mk 1:14; Mdo 20; 25; 28:23, 31Yesu akapita katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, akihubiri habari njema za Ufalme, na akiponya kila ugonjwa na kila aina ya maradhi miongoni mwa watu. 244:24 Lk 2:2; Mk 1:32; 5:15-18; Mt 17:15; Mk 2:3Kwa hiyo sifa zake zikaenea sehemu zote za Shamu, nao watu wakamletea wote waliokuwa na magonjwa mbalimbali na maumivu, waliopagawa na pepo wachafu, wenye kifafa na waliopooza, naye akawaponya. 254:25 Mk 3:7-8; Lk 6:17Makutano makubwa ya watu yakawa yanamjia kutoka Galilaya, Dekapoli,4:25 Yaani Miji Kumi. Yerusalemu, Uyahudi na kutoka ngʼambo ya Mto Yordani.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

馬太福音 4:1-25

耶穌受試探

1後來,耶穌被聖靈帶到曠野,去受魔鬼的試探。 2耶穌禁食了四十晝夜後,很饑餓。 3試探者前來對祂說:「如果你是上帝的兒子,可以叫這些石頭變成食物。」

4耶穌回答說:「聖經上說,『人活著不是單靠食物,乃是靠上帝口中的每一句話。』」

5魔鬼又帶祂進聖城,讓祂站在聖殿的最高處, 6說:「如果你是上帝的兒子,就跳下去吧!因為聖經上說,『上帝會差遣祂的天使用手托住你,不讓你的腳碰在石頭上。』」

7耶穌回答說:「聖經上也說,『不可試探主——你的上帝。』」

8魔鬼再帶耶穌到一座極高的山上,把世上萬國及其榮華富貴展示給祂看, 9說:「如果你俯伏敬拜我,我就把這一切都給你。」

10耶穌說:「撒旦,走開!聖經上說,『要敬拜主——你的上帝,單單事奉祂。』」

11於是魔鬼離開了耶穌,這時有天使前來伺候祂。

開始傳道

12耶穌聽見約翰被捕入獄,就回到加利利13後來,祂離開拿撒勒迦百農住。迦百農靠近湖邊,在西布倫拿弗他利地區。 14這就應驗了以賽亞先知的話:

15西布倫拿弗他利

沿海一帶及約旦河東、外族人居住的加利利啊!

16你們住在黑暗中的人看見了大光,

活在死亡陰影下的人被光照亮了!」

17從那時起,耶穌開始傳道:「悔改吧,因爲天國臨近了!」

呼召門徒

18耶穌沿著加利利湖邊行走的時候,看見被稱為彼得西門安得烈兩兄弟正在撒網打魚,他們是漁夫。 19耶穌對他們說:「來跟從我!我要使你們成為得人的漁夫。」 20他們立刻撇下漁網,跟從了耶穌。 21耶穌再往前走,又看見雅各約翰兩兄弟正和父親西庇太一起在船上補漁網。耶穌呼召他們, 22他們馬上離開漁船,辭別父親,跟從了耶穌。

教導和醫治

23耶穌走遍加利利,在各個會堂裡教導人,宣講天國的福音,醫治人們各樣的疾病。 24祂的名聲傳遍了整個敘利亞。人們把一切患病的,就是患各種疾病的、疼痛的、癲癇的、癱瘓的,以及被鬼附身的都帶到祂面前,祂都醫治了他們。 25因此,有大群的人跟從了祂,他們來自加利利低加坡里耶路撒冷猶太約旦河東。