Mathayo 3 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mathayo 3:1-17

Yohana Mbatizaji Atayarisha Njia

(Marko 1:1-8; Luka 3:1-18; Yohana 1:19-28)

13:1 Lk 3:2-19Siku hizo Yohana Mbatizaji alikuja akihubiri katika nyika ya Uyahudi, akisema, 23:2 Dan 7:14; Lk 17:20“Tubuni, kwa maana Ufalme wa Mbinguni umekaribia.” 33:3 Mal 3:1; Yn 1:23Huyu ndiye yule aliyenenwa habari zake na nabii Isaya aliposema:

“Sauti ya mtu aliaye huko nyikani,

‘Tayarisheni njia kwa ajili ya Bwana,

yanyoosheni mapito yake.’ ”

43:4 1Fal 1:8Basi Yohana alivaa mavazi yaliyotengenezwa kwa singa za ngamia, akiwa na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu. 53:5 Mk 1:5; Lk 3:7Watu walikuwa wakimwendea kutoka Yerusalemu, Uyahudi yote na nchi zote za kandokando ya Mto Yordani. 63:6 Mdo 19:4, 18; Mk 1:4Nao wakaziungama dhambi zao, akawabatiza katika Mto Yordani.

73:7 Mt 12:34; 23:33; Rum 1:18; 1The 1:10Lakini alipowaona Mafarisayo na Masadukayo wengi wakija ili kubatizwa, aliwaambia: “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu inayokuja? 83:8 Mdo 26:20Basi zaeni matunda yastahiliyo toba. 93:9 Rum 2:28-29Wala msidhani mnaweza kusema mioyoni mwenu kuwa, ‘Sisi tunaye Abrahamu, baba yetu.’ Nawaambia kuwa Mungu anaweza kumwinulia Abrahamu watoto kutoka kwa mawe haya. 103:10 Lk 3:9; Yn 15:2-6Hata sasa shoka limeshawekwa tayari kwenye shina la kila mti, basi kila mti usiozaa matunda mazuri, hukatwa na kutupwa motoni.

113:11 Mk 1:18; Isa 4:4; Mdo 2:3-4“Mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba. Lakini nyuma yangu anakuja yeye aliye na uwezo kuliko mimi, ambaye sistahili hata kuvichukua viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu3:11 …kwa Roho Mtakatifu hapa ina maana ya katika Roho Mtakatifu. na kwa moto. 123:12 Mt 13:30; 25:41Pepeto lake liko mkononi mwake, naye atasafisha sakafu yake ya kupuria, na kuikusanya ngano ghalani na kuyateketeza makapi kwa moto usiozimika.”

Yesu Abatizwa

(Marko 1:9-11; Luka 3:21-22)

133:13 Mt 3:1; Mk 1:4; Yn 1:31-34Kisha Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Mto Yordani ili Yohana ambatize. 14Lakini Yohana akajitahidi kumzuia, akimwambia, “Mimi ninahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu nikubatize?”

15Lakini Yesu akamjibu, “Kubali hivi sasa, kwa maana ndivyo itupasavyo kwa njia hii kuitimiza haki yote.” Hivyo Yohana akakubali.

163:16 Isa 11:2; 42:1; Mk 1:10; Lk 3:22; Yn 1:32-33Naye Yesu alipokwisha kubatizwa, mara alipotoka ndani ya maji, ghafula mbingu zikafunguka, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua na kutulia juu yake. 173:17 Kum 4:12; Yn 12:28; Za 2:7; 2:7; Mdo 13:33; Isa 42:1; 2Pet 1:17Nayo sauti kutoka mbinguni ikasema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa, ambaye ninapendezwa sana naye.”

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

馬太福音 3:1-17

開路先鋒

1那時,施洗者約翰來到猶太的曠野傳道,說: 2「悔改吧,因為天國臨近了!」 3約翰就是以賽亞先知所說的那位,他說:「有人在曠野大聲呼喊,『預備主的道,修直祂的路。』」

4約翰身穿駱駝毛的衣服,腰束皮帶,吃的是蝗蟲、野蜜。 5那時,耶路撒冷猶太各地和約旦河一帶的人都來到約翰那裡, 6承認他們的罪,在約旦河裡接受他的洗禮。

7約翰看見很多法利賽人和撒都該人也來受洗,就對他們說:「你們這些毒蛇的後代!誰指示你們逃避那將臨的烈怒呢? 8你們要結出與悔改相稱的果子。 9不要心裡說,『我們是亞伯拉罕的子孫。』我告訴你們,上帝可以從這些石頭中興起亞伯拉罕的子孫。 10現在斧頭已經放在樹根上了,不結好果子的樹都要被砍下,丟在火裡。 11我用水為你們施洗,叫你們悔改。但在我之後,有位比我更有能力的要來,我連替祂提鞋都不配。祂要用聖靈和火為你們施洗。 12祂手拿簸箕,要把穀場清理乾淨,將麥子存入倉裡,用不滅的火把糠秕燒盡。」

耶穌受洗

13後來,耶穌從加利利來到約旦河要約翰為祂施洗。 14約翰想要攔住祂,就說:「應該是你為我施洗才對,你反倒來找我?」

15耶穌回答說:「你就這樣做吧!我們理當這樣遵行上帝一切的要求。」於是約翰答應了。

16耶穌受了洗,剛從水裡上來,天就開了。祂看見上帝的聖靈像鴿子一樣降到祂身上, 17又有聲音從天上傳來:「這是我的愛子,我甚喜悅祂。」