Mathayo 20 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mathayo 20:1-34

Mfano Wa Wafanyakazi Katika Shamba La Mizabibu

120:1 Mt 13:24; 21:28, 33“Kwa maana Ufalme wa Mbinguni unafanana na mtu mwenye shamba aliyetoka alfajiri ili kwenda kuajiri vibarua kufanya kazi katika shamba lake la mizabibu. 2Baada ya kukubaliana na hao vibarua kuwalipa ujira wa dinari20:2 Dinari moja ilikuwa kama mshahara wa kibarua wa siku moja. moja kwa siku, akawapeleka kwenye shamba lake la mizabibu.

3“Mnamo saa tatu akatoka tena, akawakuta wengine wamesimama sokoni bila kazi. 4Akawaambia, ‘Ninyi nanyi nendeni mkafanye kazi katika shamba langu la mizabibu, nami nitawalipa chochote kilicho haki yenu.’ 5Kwa hiyo wakaenda.

“Akatoka tena mnamo saa sita na pia saa tisa akafanya vivyo hivyo. 6Mnamo saa kumi na moja akatoka tena akawakuta wengine bado wamesimama bila kazi. Akawauliza, ‘Kwa nini mmesimama hapa kutwa nzima pasipo kufanya kazi?’

7“Wakamjibu, ‘Ni kwa sababu hakuna yeyote aliyetuajiri.’

“Akawaambia, ‘Ninyi nanyi nendeni mkafanye kazi katika shamba langu la mizabibu.’

820:8 Law 19:13; Kum 24:15“Ilipofika jioni, yule mwenye shamba la mizabibu akamwambia msimamizi, ‘Waite hao vibarua na uwalipe ujira wao, ukianzia na wale walioajiriwa mwisho na kuishia na wale walioajiriwa kwanza.’

9“Wale vibarua walioajiriwa mnamo saa kumi na moja, wakaja na kila mmoja wao akapokea dinari moja. 10Hivyo wale walioajiriwa kwanza walipofika, walidhani watalipwa zaidi. Lakini kila mmoja wao pia alipokea dinari moja. 1120:11 Yn 4:1Walipoipokea, wakaanza kulalamika dhidi ya yule mwenye shamba, 1220:12 Yn 4:8; Yak 1:11wakisema, ‘Hawa watu walioajiriwa mwisho wamefanya kazi kwa muda wa saa moja tu, nawe umewafanya sawa na sisi ambao tumestahimili taabu na joto lote la mchana kutwa?’

1320:13 Mt 22:12; 26:50“Yule mwenye shamba akamjibu mmoja wao, ‘Rafiki, sijakudhulumu. Je, hukukubaliana nami kwa ujira wa kawaida wa dinari moja? 14Chukua ujira wako na uende. Mimi nimeamua kumlipa huyu mtu aliyeajiriwa mwisho kama nilivyokupa wewe. 1520:15 Kum 15:9; Mk 7:22Je, sina haki yangu kufanya kile nitakacho na mali yangu mwenyewe? Au unaona wivu kwa kuwa nimekuwa mkarimu?’

1620:16 Mt 19:30“Vivyo hivyo, wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho.”

Yesu Atabiri Tena Kuhusu Kifo Chake

(Marko 10:32-34; Luka 18:31-34)

1720:17 Mk 10:32; Lk 18:31; Yn 12:12Basi Yesu alipokuwa anapanda kwenda Yerusalemu, aliwachukua kando wale wanafunzi wake kumi na wawili na kuwaambia, 1820:18 Lk 9:51; Mt 8:20; 16:21; 27:1-2“Tunapanda kwenda Yerusalemu, na Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa viongozi wa makuhani na walimu wa sheria. Nao watamhukumu kifo 1920:19 Mdo 2:23; Mt 16:21na kumtia mikononi mwa watu wa Mataifa ili wamdhihaki na kumpiga mijeledi na kumsulubisha msalabani. Naye atafufuliwa siku ya tatu!”

Ombi La Mama Yake Yakobo Na Yohana

(Marko 10:35-45)

2020:20 Mt 4:21; 8:2Kisha mama yao wana wa Zebedayo akamjia Yesu pamoja na wanawe, naye akapiga magoti mbele yake, akamwomba Yesu amfanyie jambo fulani.

2120:21 Mt 19:28Yesu akamuuliza, “Unataka nini?” Akajibu, “Tafadhali, wajalie wanangu hawa ili mmoja aketi upande wako wa kuume, na mwingine upande wako wa kushoto katika Ufalme wako.”

2220:22 Yer 49:12; Yn 18:11Yesu akawaambia, “Ninyi hamjui mnaloliomba. Je, mnaweza kukinywea kikombe nitakachonywea mimi?”

Wakajibu, “Tunaweza.”

2320:23 Mdo 12:2; Ufu 1:9Yesu akawaambia, “Kwa kweli kikombe changu mtakinywea, lakini kuketi upande wangu wa kuume au wa kushoto si langu mimi kuwapa. Nafasi hizo ni za wale ambao wameandaliwa na Baba yangu.”

2420:24 Lk 22:24-25Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia haya, waliwakasirikia hao ndugu wawili. 25Lakini Yesu akawaita wote pamoja na kuwaambia, “Mnafahamu kuwa watawala wa watu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, nao wenye vyeo huonyesha mamlaka yao. 2620:26 Mt 22:11; Mk 9:35Isiwe hivyo kwenu. Badala yake, yeyote anayetaka kuwa mkuu miongoni mwenu hana budi kuwa mtumishi wenu, 2720:27 Mt 18:4; Mk 9:35naye anayetaka kuwa wa kwanza miongoni mwenu hana budi kuwa mtumwa wenu: 2820:28 Mt 8:20; Isa 42:1; Flp 2:8; Kut 30:2; Ebr 9:28kama vile ambavyo Mwana wa Adamu hakuja ili kutumikiwa, bali kutumika na kuutoa uhai wake uwe fidia kwa ajili ya wengi.”

Yesu Awaponya Vipofu Wawili

(Marko 10:46-52; Luka 18:35-43)

2920:29 Mk 10:46; Lk 18:35Yesu na wanafunzi wake walipokuwa wakiondoka Yeriko, umati mkubwa wa watu ulimfuata. 3020:30 Mt 9:27; 15:22Vipofu wawili walikuwa wameketi kando ya barabara. Waliposikia kwamba Yesu alikuwa anapita, wakapiga kelele wakisema, “Bwana, Mwana wa Daudi, tuhurumie!”

31Ule umati wa watu ukawakemea na kuwaambia wanyamaze, lakini wao wakazidi kupaza sauti, wakisema, “Bwana, Mwana wa Daudi, tuhurumie.”

32Yesu akasimama na kuwaita, akawauliza, “Mnataka niwafanyie nini?”

33Wakamjibu, “Bwana, tunataka kuona.”

34Yesu akawahurumia na kuwagusa macho yao. Mara macho yao yakapata kuona, nao wakamfuata.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

马太福音 20:1-34

葡萄园工人的比喻

1耶稣接着说:“因为天国就像一个园主清早去外面请工人到他的葡萄园做工。 2他跟工人讲好一天的工钱是一个银币,然后派他们去葡萄园。

3“大约上午九点钟,园主出去看见一些人站在街市上无所事事, 4就对他们说,‘你们到我的葡萄园来工作吧,我会给你们合理的工钱。’

5“他们便去了。正午和下午三点钟,他又出去继续请人到葡萄园做工。 6到了下午五点钟的时候,他再次出去,看见还有人闲站在那里,就问他们,‘为什么你们整天站在这里无所事事呢?’ 7他们回答说,‘因为没有人雇用我们。’园主说,‘你们也到我的葡萄园来吧!’

8“到了傍晚,园主对工头说,‘叫工人来领工钱吧,最晚来的先领,最先来的后领。’

9“下午五点来的工人每人得了一个银币。 10最早来的工人来领的时候,以为必定可以多得一点工钱,谁知也各得一个银币。

11“他们拿着工钱满腹牢骚地对园主说, 12‘那些最晚来的人只工作了一小时,而我们在烈日之下辛苦了一整天,怎么会领同样的工钱呢?’

13“园主对他们当中的一个人说,‘朋友,我并没有欠你呀!我们不是讲好付你一个银币吗? 14拿着你的工钱走吧。我给那后来的和你一样的工钱,是我愿意。 15难道我不可随意使用自己的钱吗?因为我慷慨,你就眼红吗?’ 16因此,为首的将要殿后,殿后的将要为首。”

耶稣第三次预言自己受难

17在去耶路撒冷的途中,耶稣把十二个门徒带到一边,对他们说: 18“你们要留意,我们现在前往耶路撒冷,人子将被交给祭司长和律法教师。他们要判祂死刑, 19把祂交给外族人,受嘲弄、鞭打,被钉在十字架上。但第三天祂必复活。”

一个母亲的请求

20当时,西庇太的妻子带着两个儿子上前,跪在耶稣面前,有事要求祂。

21耶稣问她:“你要什么呢?”

她说:“在你的国度,请让我这两个儿子一个坐在你右边,一个坐在你左边。”

22耶稣回答说:“你们不知道自己在求什么。我要喝的那一杯,你们能喝吗?”

他们说:“我们能。”

23耶稣对他们说:“我要喝的那一杯,你们也要喝。不过谁坐在我的左右不是我来定,而是我父为谁预备的,就让谁坐。”

24其他十个门徒听见这事,都对他们兄弟二人十分恼火。 25于是,耶稣把他们叫来,说:“外族人有君王统治他们,有大臣管理他们。但你们不可这样。 26你们中间,谁要当首领,谁就要做大家的仆人; 27谁要居首位,谁就要做大家的奴仆。 28正如人子不是来受人服侍,而是来服侍人,并且牺牲性命,作许多人的赎价。”

治好两个瞎子

29耶稣和祂的门徒离开耶利哥时,有一大群人跟着祂。 30有两个瞎子正坐在路旁,听说耶稣经过,就高声喊叫:“主啊,大卫的后裔啊,可怜我们吧!” 31众人责备他们,叫他们不要出声,他们却喊得更大声了:“主啊,大卫的后裔啊,可怜我们吧!”

32耶稣停下脚步,叫了他们来,问他们:“你们要我为你们做什么?” 33他们说:“主啊,我们想能够看见。” 34耶稣就动了慈心,摸他们的眼睛,他们立刻得见光明,并跟从了耶稣。