Mathayo 18 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mathayo 18:1-35

Aliye Mkuu Katika Ufalme Wa Mbinguni

(Marko 9:33-37; Luka 9:46-48)

118:1 Mk 9:33; Lk 9:46; 22:24Wakati huo, wanafunzi wakamjia Yesu na kumuuliza, “Je, nani aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa Mbinguni?”

2Yesu akamwita mtoto mdogo na kumsimamisha katikati yao. 318:3 Mt 19:14; 2Pet 2:2; Mt 3:2Naye akasema: “Amin, nawaambia, msipookoka na kuwa kama watoto wadogo, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa Mbinguni. 418:4 Mk 9:35Kwa hiyo mtu yeyote anyenyekeaye kama huyu mtoto, ndiye aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa Mbinguni.

518:5 Mt 10:40; Yn 13:20“Yeyote amkaribishaye mtoto mdogo kama huyu kwa Jina langu, anikaribisha mimi. 618:6 Mt 5:29; Mk 9:42; Lk 17:2Lakini kama mtu yeyote akimsababisha mmojawapo wa hawa wadogo wanaoniamini kutenda dhambi, ingekuwa bora kwake afungiwe jiwe kubwa la kusagia shingoni mwake, na kutoswa katika kilindi cha bahari.

Kujaribiwa Ili Kutenda Dhambi

(Marko 9:42-48; Luka 17:1-2)

718:7 Lk 17:1“Ole kwa ulimwengu kwa sababu ya yale mambo yanayosababisha watu kutenda dhambi! Mambo hayo lazima yawepo, lakini ole wake mtu yule ambaye huyasababisha. 818:8 Mt 5:28; Mk 9:43-45Ikiwa mkono wako au mguu wako unakusababisha utende dhambi, ukate na uutupe mbali. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa huna mkono mmoja au mguu mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na kutupwa katika moto wa milele. 918:9 Mt 5:22, 29Nalo jicho lako likikusababisha kutenda dhambi, lingʼoe, ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili lakini ukatupwa katika moto wa jehanamu.

Mfano Wa Kondoo Aliyepotea

(Luka 15:3-7)

1018:10 Za 34:7; Ebr 1:14“Angalia ili usimdharau mmojawapo wa hawa wadogo, kwa maana nawaambia, malaika wao mbinguni daima wanauona uso wa Baba yangu aliye mbinguni. [ 1118:11 Lk 9:36; 19:10; Yn 1:17; 12:47Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kuokoa kile kilichopotea.]

1218:12 Lk 15:4“Mwaonaje? Ikiwa mtu ana kondoo mia moja, na mmoja wao akapotea, je, hatawaacha wale tisini na tisa vilimani na kwenda kumtafuta huyo mmoja aliyepotea? 1318:13 Lk 1:17Naye akishampata, amin, nawaambia, hufurahi zaidi kwa ajili ya huyo kondoo mmoja kuliko wale tisini na tisa ambao hawakupotea. 14Vivyo hivyo, Baba yenu wa mbinguni hapendi hata mmojawapo wa hawa wadogo apotee.

Ndugu Yako Akikukosea

1518:15 Law 19:17; Gal 6:1“Kama ndugu yako akikukosea, nenda ukamwonyeshe kosa lake, kati yenu ninyi wawili peke yenu. Kama akikusikiliza, utakuwa umempata tena ndugu yako. 1618:16 Kum 17:6; Ebr 10:28Lakini kama hatakusikiliza, nenda na mtu mwingine mmoja au wawili ili kila neno lithibitishwe kwa ushahidi wa mashahidi wawili au watatu. 1718:17 1Kor 6:1-6; Rum 16:17; 2The 3:6, 14Kama akikataa kuwasikiliza hao, liambie kanisa. Naye kama akikataa hata kulisikiliza kanisa, basi awe kwenu kama mtu asiyeamini au mtoza ushuru.

1818:18 Mt 16:18; Yn 20:23“Amin, nawaambia, lolote mtakalolifunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni, na lolote mtakalolifungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.

1918:19 Mt 7:7“Tena nawaambia, ikiwa wawili wenu watakubaliana duniani kuhusu jambo lolote watakaloomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. 2018:20 Mt 28:20; Yn 14:23Kwa kuwa wanapokusanyika pamoja watu wawili au watatu kwa Jina langu, mimi niko papo hapo pamoja nao.”

Kusamehe

2118:21 Mt 6:14; Lk 17:4Ndipo Petro akamjia Yesu na kumuuliza, “Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi nami nimsamehe? Je, hata mara saba?”

2218:22 Mwa 4:24Yesu akamjibu, “Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.

Mfano Wa Mtumishi Asiyesamehe

2318:23 Mt 13:24; 25:19“Kwa hiyo Ufalme wa Mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme aliyetaka kufanya hesabu zake za fedha na watumishi wake. 24Alipoanza kufanya hesabu zake, mtu mmoja aliyekuwa anadaiwa talanta18:24 Talanta moja ni sawa na mshahara wa kibarua wa miaka 15. 10,000, aliletwa kwake. 2518:25 Lk 7:42; 2Fal 4:1; Neh 5:5-8Kwa kuwa alikuwa hawezi kulipa deni hilo, bwana wake akaamuru kwamba auzwe, yeye, mkewe, watoto wake na vyote alivyokuwa navyo, ili lile deni lipate kulipwa.

2618:26 Mt 8:2“Yule mtumishi akampigia magoti, akamsihi yule bwana akisema, ‘Naomba univumilie, nami nitakulipa deni lako lote.’ 27Yule bwana wa huyo mtumishi akamwonea huruma, akafuta deni lake lote, akamwacha aende zake.

28“Lakini yule mtumishi alipokuwa anatoka nje, akakutana na mtumishi mwenzake aliyekuwa amemkopesha dinari18:28 Dinari moja ilikuwa kama mshahara wa kibarua wa siku moja. mia moja. Akamkamata, akamkaba koo akimwambia, ‘Nilipe kile ninachokudai!’

29“Yule mtumishi mwenzake akapiga magoti akamsihi akisema, ‘Naomba univumilie, nami nitakulipa deni lako lote.’

30“Lakini akakataa. Badala yake, alienda akamtupa gerezani hata atakapolipa hilo deni. 31Watumishi wenzake walipoona haya yaliyotukia wakaudhika sana, nao wakaenda na kumwambia bwana wao kila kitu kilichokuwa kimetukia.

32“Yule bwana akamwita yule mtumishi akamwambia, ‘Wewe mtumishi mwovu! Mimi nilikusamehe deni lako lote uliponisihi. 33Je, haikukupasa kumhurumia mtumishi mwenzako kama mimi nilivyokuhurumia wewe?’ 3418:34 Mt 5:26Kwa hasira, yule bwana wake akamtia yule mtumishi mikononi mwa askari wa gereza ili ateswe mpaka atakapolipa yote aliyokuwa anadaiwa.

3518:35 Mt 6:14; Yak 2:13“Hivi ndivyo Baba yangu wa mbinguni atakavyomfanyia kila mmoja wenu ikiwa hatamsamehe ndugu yake kutoka moyoni mwake.”

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

馬太福音 18:1-35

天國裡誰最偉大

1這時,門徒上前來,問耶穌:「在天國誰最偉大?」

2耶穌叫了一個小孩子來站在他們當中,然後說: 3「我實在告訴你們,你們若不變得像小孩子那樣,絕不能進天國。 4所以,凡像這小孩子一樣謙卑的人,在天國才是最偉大的。

5「任何人為了我的名而接待這樣一個小孩子,就是接待了我。 6但不論誰使這樣一個小信徒失足犯罪,他的下場比把大磨石拴在他脖子上沉到深海裡還要慘。 7這世界有禍了!因為裡面充滿了引人犯罪的事。這樣的事是免不了的,但那些引人犯罪的人有禍了!

8「如果你的手或腳使你犯罪,就砍掉它!因為肢體殘缺著進入永生,總比四肢健全卻被丟進永遠不滅的火中好。 9如果你的一隻眼睛使你犯罪,就剜出來丟掉它吧!獨眼進入永生,總比雙目健全卻被丟進地獄的火中好。 10你們切不可輕視任何一位卑微的人。我告訴你們,他們的天使在天上常見我天父的面。

迷失的羊

11「人子到世界來,為要拯救迷失的人。 12如果一個人有一百隻羊,其中有一隻走迷了路,他會怎麼辦呢?難道不會把那九十九隻撇在山上,去找那隻迷失的羊嗎? 13我實在告訴你們,如果找到了,他會非常歡喜,甚至比有那九十九隻沒有迷失的羊還歡喜。 14同樣,你們的天父也不願任何一個卑微的人失喪。

糾正信徒的過錯

15「如果你的弟兄得罪了你,你要找個機會跟他單獨在一起,指出他的錯處。如果他肯接受勸告,你就得了一位弟兄。 16如果他不聽勸告,你就帶一兩位弟兄去見他,讓兩三個人為談話作證。 17如果他仍然不聽,就應當告訴教會。如果他連教會也不聽,就把他看作異教徒或稅吏18·17 稅吏」即猶太人眼中的「漢奸」,幫助統治猶太人的羅馬政府收稅,常從中牟取暴利。18我實在告訴你們,你們在地上捆綁的,在天上也要捆綁;你們在地上釋放的,在天上也要釋放。

19「我又告訴你們,如果你們當中有兩個人在地上同心合意地祈求,不論求什麼,我天上的父必為你們成就。 20因為哪裡有兩三個人奉我的名聚會,我就在哪裡與他們同在。」

七十個七次

21彼得上前問耶穌:「主啊,如果我的弟兄得罪了我,我該饒恕他多少次呢?七次夠了吧?」

22耶穌回答說:「我告訴你,不是七次,是七十個七次。

23「因此,天國就像一個王,他要跟奴僕清算債務。 24正開始清算的時候,有人帶著一個欠了六千萬銀幣18·24 六千萬銀幣」希腊文是「一萬他連得」,一他連得相當於當時一個普通工人20年的工錢。的人進來。 25因為這個人無法清還債款,王就下令把他及其妻兒和所有財產全部賣掉還債。 26那奴僕跪在王面前乞求說,『請寬容我,我會把債務全部還清的。』 27王可憐他,不但釋放了他,而且免了他全部的債。

28「可是,那奴僕出去後,遇見一位欠他一百個銀幣18·28 一個銀幣相當於當時普通工人一天的工錢。的同伴,就揪住同伴,掐著他的喉嚨說,『還我錢!』 29同伴跪下哀求道,『請寬容我,我會還你的。』

30「那奴僕卻不肯,竟把同伴送進監獄,直到他還清債務為止。 31其他的奴僕目睹這一切,都憤憤不平,把這件事告訴了王。

32「於是,王把那奴僕召來,說,『你這可惡的奴才!你哀求我,我就免了你所有的債。 33難道你不應該憐憫你的同伴,就像我憐憫你一樣嗎?』 34王大怒,下令把他交給獄卒受刑,直到他還清全部的債務。 35如果你們不從心裡饒恕自己的弟兄,我的天父也要這樣對待你們。」