Mathayo 15 – NEN & NIV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mathayo 15:1-39

Mapokeo Ya Wazee

(Marko 7:1-13)

115:1 Mk 7:1-23Ndipo baadhi ya Mafarisayo na walimu wa sheria wakamjia Yesu kutoka Yerusalemu na kumuuliza, 215:2 Kum 4:2; Lk 11:38; Kum 4:2; Lk 11:38“Mbona wanafunzi wako wanakiuka mapokeo ya wazee? Kwa maana wao hawanawi mikono yao kabla ya kula!”

3Yesu akawajibu, “Mbona ninyi mnavunja amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu? 415:4 Kut 20:12; Efe 6:2; Kut 21:17; Law 9:20; Kut 20:12; Efe 6:2; Kut 21:17; Law 9:20Kwa maana Mungu alisema, ‘Waheshimu baba yako na mama yako,’ na, ‘Yeyote amtukanaye baba yake au mama yake, na auawe.’ 515:5 Mk 7:11, 12Lakini ninyi mwafundisha kwamba mtu akimwambia baba yake au mama yake, ‘Kile ambacho ningeweza kukusaidia kimewekwa wakfu kwa Mungu,’ 6basi hana tena sababu ya kumheshimu baba yake nacho. Basi kwa ajili ya mafundisho yenu mnavunja amri ya Mungu. 715:7 Isa 29:13Ninyi wanafiki! Isaya alikuwa sawa alipotabiri juu yenu kwamba:

815:8 Isa 29:11; Eze 33:31“ ‘Watu hawa huniheshimu kwa midomo yao,

lakini mioyo yao iko mbali nami.

915:9 Kol 2:20-22; Isa 29:13; Mal 2:2Huniabudu bure;

nayo mafundisho yao

ni maagizo ya wanadamu tu.’ ”

Vitu Vitiavyo Unajisi

(Marko 7:14-23)

1015:10 Mk 7:14Yesu akaita ule umati wa watu, akawaambia, “Sikilizeni na mwelewe: 1115:11 Mdo 10:14-15kinachomfanya mtu kuwa najisi mbele za Mungu si kile kiingiacho kinywani mwake, bali ni kile kitokacho kinywani mwake.”

12Kisha wanafunzi wake wakamjia na kumuuliza, “Je, unajua kwamba Mafarisayo walichukizwa sana waliposikia yale uliyosema?”

1315:13 Isa 60:21; Yn 15:2Akawajibu, “Kila pando ambalo Baba yangu wa mbinguni hakulipanda, litangʼolewa. 1415:14 Mt 23:16, 24; Rum 2:19; Lk 6:9Waacheni; wao ni viongozi vipofu, wanaoongoza vipofu. Kama kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, wote wawili watatumbukia shimoni.”

1515:15 Mt 13:36Petro akasema, “Tueleze maana ya huu mfano.”

1615:16 Mt 16:9Yesu akawauliza, “Je, bado ninyi hamfahamu? 1715:17 1Nya 6:13Je, hamwelewi kwamba chochote kiingiacho kinywani huenda tumboni, na hatimaye hutolewa nje kikiwa uchafu? 1815:18 Lk 6:45; Yak 3:6Lakini kitokacho kinywani hutoka moyoni, na hiki ndicho kimtiacho mtu unajisi. 1915:19 Gal 5:19-21Kwa maana ndani ya moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na masingizio. 2015:20 Rum 14:14Haya ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula bila kunawa mikono hakumtii mtu unajisi.”

Imani Ya Mwanamke Mkanaani

(Marko 7:24-30)

2115:21 Mt 11:21Yesu aliondoka mahali pale, akaenda sehemu za Tiro na Sidoni. 2215:22 Mt 9:27; 4:24Mwanamke mmoja Mkanaani aliyeishi sehemu jirani na hizo akaja kwake akilia, akasema, “Nihurumie, Ee Bwana, Mwana wa Daudi! Binti yangu amepagawa na pepo mchafu, na anateseka sana.”

23Lakini Yesu hakumjibu neno. Hivyo wanafunzi wake wakamwendea na kumsihi sana, wakisema, “Mwambie aende zake, kwa maana anaendelea kutupigia kelele.”

2415:24 Mt 10:6, 23; Rum 15:8Yesu akajibu, “Nimetumwa tu kwa ajili ya kondoo wa Israeli waliopotea.”

2515:25 Mt 8:2; Yn 12:25; Lk 17:33Lakini yule mwanamke akaja, akapiga magoti mbele ya Yesu, akasema, “Bwana, nisaidie!”

26Yesu akajibu, “Si haki kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.”

27Yule mwanamke akajibu, “Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yanayoanguka kutoka kwenye meza za bwana zao.”

2815:28 Mt 9:22Ndipo Yesu akamwambia, “Mwanamke, imani yako ni kubwa! Iwe kwako kama unavyotaka.” Naye binti yake akapona tangu saa ile.

Yesu Aponya Watu Wengi

29Yesu akaondoka na kwenda kando ya Bahari ya Galilaya. Kisha akapanda mlimani, akaketi huko. 3015:30 Mt 4:23Umati mkubwa wa watu ukamjia, wakiwaleta vilema, vipofu, viwete, bubu na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; naye akawaponya. 3115:31 Mt 9:8Hao watu wakashangaa walipoona bubu wakisema, vilema wakipona, viwete wakitembea na vipofu wakiona, wakamtukuza Mungu wa Israeli.

Yesu Alisha Watu Elfu Nne

(Marko 8:1-10)

3215:32 Mt 14:19Kisha Yesu akawaita wanafunzi wake, akawaambia, “Ninauhurumia huu umati wa watu, kwa sababu sasa wamekuwa pamoja nami kwa muda wa siku tatu, na hawana chakula chochote. Nami sipendi kuwaaga wakiwa na njaa, wasije wakazimia njiani.”

33Wanafunzi wake wakasema, “Tutapata wapi mikate ya kutosha kuwalisha umati huu wa watu mkubwa namna hii, nasi tuko nyikani?”

34Yesu akawauliza, “Mnayo mikate mingapi?”

Wakamjibu, “Tunayo mikate saba na visamaki vichache.”

35Yesu akawaambia ule umati wa watu waketi chini. 3615:36 Mt 14:19Kisha akachukua ile mikate saba na wale samaki, naye akiisha kumshukuru Mungu, akavimega na kuwapa wanafunzi wake, nao wakawapa ule umati wa watu. 3715:37 Mt 16:10Wote wakala na kushiba. Baadaye wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu saba. 38Idadi ya watu walikuwa wanaume 4,000, bila kuhesabu wanawake na watoto. 39Baada ya kuaga ule umati wa watu, Yesu aliingia katika mashua, akaenda sehemu za Magadani.15:39 Magadani ni Magdala, mji wa Galilaya, kama kilomita 16 kusini mwa Kapernaumu.

New International Version

Matthew 15:1-39

That Which Defiles

1Then some Pharisees and teachers of the law came to Jesus from Jerusalem and asked, 2“Why do your disciples break the tradition of the elders? They don’t wash their hands before they eat!”

3Jesus replied, “And why do you break the command of God for the sake of your tradition? 4For God said, ‘Honor your father and mother’15:4 Exodus 20:12; Deut. 5:16 and ‘Anyone who curses their father or mother is to be put to death.’15:4 Exodus 21:17; Lev. 20:9 5But you say that if anyone declares that what might have been used to help their father or mother is ‘devoted to God,’ 6they are not to ‘honor their father or mother’ with it. Thus you nullify the word of God for the sake of your tradition. 7You hypocrites! Isaiah was right when he prophesied about you:

8“ ‘These people honor me with their lips,

but their hearts are far from me.

9They worship me in vain;

their teachings are merely human rules.’15:9 Isaiah 29:13

10Jesus called the crowd to him and said, “Listen and understand. 11What goes into someone’s mouth does not defile them, but what comes out of their mouth, that is what defiles them.”

12Then the disciples came to him and asked, “Do you know that the Pharisees were offended when they heard this?”

13He replied, “Every plant that my heavenly Father has not planted will be pulled up by the roots. 14Leave them; they are blind guides.15:14 Some manuscripts blind guides of the blind If the blind lead the blind, both will fall into a pit.”

15Peter said, “Explain the parable to us.”

16“Are you still so dull?” Jesus asked them. 17“Don’t you see that whatever enters the mouth goes into the stomach and then out of the body? 18But the things that come out of a person’s mouth come from the heart, and these defile them. 19For out of the heart come evil thoughts—murder, adultery, sexual immorality, theft, false testimony, slander. 20These are what defile a person; but eating with unwashed hands does not defile them.”

The Faith of a Canaanite Woman

21Leaving that place, Jesus withdrew to the region of Tyre and Sidon. 22A Canaanite woman from that vicinity came to him, crying out, “Lord, Son of David, have mercy on me! My daughter is demon-possessed and suffering terribly.”

23Jesus did not answer a word. So his disciples came to him and urged him, “Send her away, for she keeps crying out after us.”

24He answered, “I was sent only to the lost sheep of Israel.”

25The woman came and knelt before him. “Lord, help me!” she said.

26He replied, “It is not right to take the children’s bread and toss it to the dogs.”

27“Yes it is, Lord,” she said. “Even the dogs eat the crumbs that fall from their master’s table.”

28Then Jesus said to her, “Woman, you have great faith! Your request is granted.” And her daughter was healed at that moment.

Jesus Feeds the Four Thousand

29Jesus left there and went along the Sea of Galilee. Then he went up on a mountainside and sat down. 30Great crowds came to him, bringing the lame, the blind, the crippled, the mute and many others, and laid them at his feet; and he healed them. 31The people were amazed when they saw the mute speaking, the crippled made well, the lame walking and the blind seeing. And they praised the God of Israel.

32Jesus called his disciples to him and said, “I have compassion for these people; they have already been with me three days and have nothing to eat. I do not want to send them away hungry, or they may collapse on the way.”

33His disciples answered, “Where could we get enough bread in this remote place to feed such a crowd?”

34“How many loaves do you have?” Jesus asked.

“Seven,” they replied, “and a few small fish.”

35He told the crowd to sit down on the ground. 36Then he took the seven loaves and the fish, and when he had given thanks, he broke them and gave them to the disciples, and they in turn to the people. 37They all ate and were satisfied. Afterward the disciples picked up seven basketfuls of broken pieces that were left over. 38The number of those who ate was four thousand men, besides women and children. 39After Jesus had sent the crowd away, he got into the boat and went to the vicinity of Magadan.