Matendo 7 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Matendo 7:1-60

Hotuba Ya Stefano

1Ndipo kuhani mkuu akamuuliza Stefano, “Je, mashtaka haya ni ya kweli?”

27:2 Za 29:3; Mwa 11:31; 15:7; Mdo 22:1Stefano akajibu, “Ndugu zangu na baba zangu, nisikilizeni! Mungu wa utukufu alimtokea baba yetu Abrahamu, alipokuwa bado yuko Mesopotamia, kabla hajaishi Harani, 37:3 Mwa 12:1-5; 48:4akamwambia, ‘Ondoka kutoka nchi yako na kutoka kwa jamii yako, uende hadi nchi nitakayokuonyesha.’

47:4 Mwa 12:5; Ebr 11:13“Hivyo aliondoka katika nchi ya Wakaldayo akaenda kukaa Harani. Baada ya kifo cha baba yake, Mungu akamtoa huko akamleta katika nchi hii ambayo mnaishi sasa. 57:5 Mwa 17:8; 26:3; 12:7; Ebr 11:13Mungu hakumpa urithi wowote katika nchi hii, hakumpa hata mahali pa kuweka wayo mmoja. Bali Mungu alimwahidi kuwa yeye na uzao wake baada yake wangeirithi hii nchi, ingawa wakati huo Abrahamu hakuwa na mtoto. 67:6 Kut 1:8-11; 12:40Mungu akasema naye hivi: ‘Wazao wako watakuwa wageni kwenye nchi ambayo si yao, nao watafanywa watumwa na kuteswa kwa miaka mia nne.’ 77:7 Mwa 15:13-14; Kut 3:12Mungu akasema, ‘Lakini mimi nitaliadhibu taifa watakalolitumikia kama watumwa, na baadaye watatoka katika nchi hiyo na wataniabudu mahali hapa.’ 87:8 Mwa 17:9-14; 21:2-4; 29:31-35; 35:16-18, 22-26Ndipo akampa Abrahamu Agano la tohara. Naye Abrahamu akamzaa Isaki na kumtahiri siku ya nane. Baadaye Isaki akamzaa Yakobo, naye Yakobo akawazaa wale wazee wetu kumi na wawili.

97:9 Mwa 37:4-11; 37:28; 39:2, 21-23; Hag 2:4“Kwa sababu wazee wetu walimwonea wivu Yosefu ndugu yao, walimuuza kama mtumwa huko Misri. Lakini Mungu alikuwa pamoja naye. 107:10 Mwa 41:37-41; Za 105:20-22Akamwokoa kutoka mateso yote yaliyompata, tena akampa kibali na hekima aliposimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri, ambaye alimweka kuwa mtawala juu ya Misri na juu ya jumba lote la kifalme.

117:11 Mwa 41:54; 42:5“Basi kukawa na njaa katika nchi yote ya Misri na Kanaani, ikasababisha dhiki kubwa, nao baba zetu wakawa hawana chakula. 127:12 Mwa 42:12Lakini Yakobo aliposikia kwamba kuna nafaka huko Misri, aliwatuma baba zetu, wakaenda huko kwa mara yao ya kwanza. 137:13 Mwa 45:1-4Walipokwenda mara ya pili, Yosefu alijitambulisha kwa ndugu zake, nao ndugu zake Yosefu wakajulishwa kwa Farao. 147:14 Mwa 45:9-10; Kut 1:5; Kum 10:22Ndipo Yosefu akawatuma kumleta Yakobo baba yake pamoja na jamaa yake yote, jumla yao walikuwa watu sabini na watano. 157:15 Mwa 49:33Hivyo Yakobo akaenda Misri ambako yeye na baba zetu walifia. 167:16 Mwa 50:13; Yos 24:32Miili yao ilirudishwa Shekemu na kuzikwa katika kaburi ambalo Abrahamu alinunua kutoka kwa wana wa Hamori kwa kiasi fulani cha fedha.

177:17 Kut 1:6-7; Za 105:24“Lakini wakati ulipokuwa unakaribia wa kutimizwa kwa ile ahadi ambayo Mungu alikuwa amempa Abrahamu, watu wetu walizidi kuongezeka sana huko Misri. 187:18 Kut 1:8Ndipo mfalme mwingine ambaye hakujua lolote kuhusu Yosefu akatawala Misri. 197:19 Kut 1:8-22Huyu mfalme akawatendea watu wetu hila na kuwatesa baba zetu kwa kuwalazimisha wawatupe watoto wao wachanga ili wafe.

207:20 Kut 2:2; Ebr 11:23“Wakati huo Mose alizaliwa, naye hakuwa mtoto wa kawaida. Akalelewa nyumbani kwa baba yake kwa muda wa miezi mitatu. 217:21 Kut 2:3-10Waliposhindwa kumficha zaidi, wakamweka nje mtoni na binti Farao akamchukua akamtunza kama mtoto wake mwenyewe. 227:22 1Fal 4:30; Isa 19:11Mose akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa mtu hodari kwa maneno na matendo.

237:23 Kut 2:11; 2:12“Mose alipokuwa na umri wa miaka arobaini aliamua kuwatembelea ndugu zake Waisraeli. 24Aliona mmoja wao akidhulumiwa na Mmisri, akamtetea yule aliyeonewa, akampiga yule Mmisri akamuua kulipiza kisasi. 25Mose alidhani kuwa ndugu zake wangetambua kwamba Mungu anamtumia ili kuwaokoa, lakini wao hawakuelewa. 267:26 Kut 2:13Siku iliyofuata Mose aliwakuta Waisraeli wawili wakigombana, akajaribu kuwapatanisha kwa kuwaambia, ‘Enyi watu, ninyi ni ndugu, mbona mnataka kudhulumiana?’

277:27 Lk 12:14; Mdo 4:7; Mwa 19:9; Hes 16; 13; Kut 2:14“Lakini yule mtu aliyekuwa akimdhulumu mwenzake akamsukuma Mose kando, akamuuliza, ‘Ni nani aliyekufanya mtawala na mwamuzi juu yetu? 28Je, unataka kuniua kama ulivyomuua yule Mmisri jana?’ 297:29 Kut 2:11-15Mose aliposikia maneno haya, alikimbilia huko Midiani alikokaa kama mgeni, naye akapata watoto wawili wa kiume.

307:30 Kut 3:2; 2:15, 22; 18:3, 4“Basi baada ya miaka arobaini kupita, malaika wa Mungu akamtokea Mose jangwani karibu na Mlima Sinai katika kichaka kilichokuwa kinawaka moto. 317:31 Kut 3:1-5Alipoona mambo haya, alishangaa yale maono. Aliposogea ili aangalie kwa karibu, akaisikia sauti ya Bwana, ikisema: 327:32 Mt 22:32; Ebr 11:16; Mdo 3:13; Kut 3:6‘Mimi ndimi Mungu wa baba zako, Mungu wa Abrahamu, Isaki na Yakobo.’ Mose alitetemeka kwa hofu na hakuthubutu kutazama.

337:33 Kut 3:5-6; Yos 5:15“Ndipo Bwana akamwambia, ‘Vua viatu vyako kwa maana mahali unaposimama ni patakatifu. 347:34 Kut 3:7-10Hakika nimeona mateso ya watu wangu huko Misri. Nimesikia kilio chao cha uchungu, nami nimeshuka ili niwaokoe. Basi sasa njoo, nami nitakutuma Misri.’

357:35 Mdo 7:27; Kut 2:14“Huyu ndiye Mose yule waliyemkataa wakisema, ‘Ni nani aliyekufanya mtawala na mwamuzi juu yetu?’ Alikuwa ametumwa na Mungu mwenyewe kuwa mtawala na mkombozi wao, kwa njia ya yule malaika aliyemtokea katika kile kichaka. 367:36 Kut 12:41; 33; 1; 14:21Aliwaongoza wana wa Israeli kutoka Misri, baada ya kufanya ishara na maajabu mengi huko Misri, katika Bahari ya Shamu,7:36 Yaani Bahari ya Mafunjo. na katika jangwa kwa muda wa miaka arobaini.

377:37 Kum 18:15, 18; Mdo 3:22; Mt 15:5“Huyu ndiye yule Mose aliyewaambia Waisraeli, ‘Mungu atawainulia nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu wenyewe.’ 387:38 Kut 19:17; Law 27:34; Ebr 4:12; Rum 3:2Huyu ndiye yule Mose aliyekuwa katika kusanyiko huko jangwani, ambaye malaika alisema naye pamoja na baba zetu kwenye Mlima Sinai, naye akapokea maneno yaliyo hai ili atupatie.

397:39 Hes 14:3-4“Lakini baba zetu walikataa kumtii Mose, badala yake wakamkataa na kuielekeza mioyo yao Misri tena. 407:40 Kut 32:1-23Wakamwambia Aroni, ‘Tufanyie miungu watakaotuongoza, kwa maana mtu huyu Mose aliyetutoa nchi ya Misri, hatujui yaliyompata.’ 417:41 Za 106:19-20; Ufu 9:20Huu ni ule wakati walitengeneza sanamu katika umbo la ndama, wakailetea sadaka kufanya maadhimisho kwa ajili ya kile kitu walichokitengeneza kwa mikono yao wenyewe. 427:42 Yos 24:20; Isa 63:19; Yer 19:13Ndipo Mungu akageuka, akawaacha waabudu jeshi lote la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Manabii:

“ ‘Je, mliniletea dhabihu na sadaka

kwa miaka arobaini kule jangwani,

ee nyumba ya Israeli?

437:43 Amo 5:25-27La, ninyi mliinua madhabahu ya Moleki,

na nyota ya mungu wenu Refani,

vinyago mlivyotengeneza ili kuviabudu.

Kwa hiyo nitawapeleka mbali’ kuliko Babeli.

447:44 Kut 38:21; Hes 17:7; Kut 25:8“Baba zetu walikuwa na lile Hema la Ushuhuda huko jangwani. Lilikuwa limetengenezwa kama Mungu alivyokuwa amemwelekeza Mose, kulingana na kielelezo alichoona. 457:45 Yos 23:9; Za 132:1-5Baba zetu wakiisha kulipokea hema kwa kupokezana wakiongozwa na Yoshua katika milki ya nchi kutoka kwa yale mataifa ambayo Mungu aliyafukuza mbele yao, nalo likadumu katika nchi mpaka wakati wa Daudi, 467:46 1Fal 8:17; Za 44:2ambaye alipata kibali kwa Mungu, naye akaomba kwamba ampatie Mungu wa Yakobo maskani. 477:47 1Fal 6:1-38; 1Nya 17:12; 2Nya 3:1Lakini alikuwa Solomoni ndiye alimjengea Mungu nyumba.

487:48 1Fal 8:27; 2Nya 2:6“Hata hivyo, Yeye Aliye Juu Sana hakai kwenye nyumba zilizojengwa kwa mikono ya wanadamu. Kama nabii alivyosema:

497:49 Mt 5:32-35; Isa 66:1, 2; Mt 23:22“ ‘Mbingu ni kiti changu cha enzi,

nayo dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu.

Mtanijengea nyumba ya namna gani?

asema Bwana.

Au mahali pangu pa kupumzikia patakuwa wapi?

507:50 Isa 66:1-2; Lk 23:34Je, mkono wangu haukufanya vitu hivi vyote?’

517:51 Kut 32:9; 33:3-5; Law 26:41; Yer 9:26“Enyi watu wenye shingo ngumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio, daima hamwachi kumpinga Roho Mtakatifu, kama walivyofanya baba zenu. 527:52 2Nya 36:16; Mt 5:12; Mdo 3:14; 1The 2:15Je, kuna nabii gani ambaye baba zenu hawakumtesa? Waliwaua wale waliotabiri habari za kuja kwake yule Mwenye Haki. Nanyi sasa mmekuwa wasaliti wake na wauaji. 537:53 Gal 3:19; Ebr 2:2Ninyi ndio mlipokea sheria zilizoletwa kwenu na malaika, lakini hamkuzitii.”

Stefano Apigwa Mawe

547:54 Mt 5:33; Mdo 5:33Waliposikia haya wakaghadhibika, wakamsagia meno. 557:55 Mk 16:19; Mdo 6:5; Lk 22:69Lakini yeye Stefano, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, alikaza macho mbinguni, akaona utukufu wa Mungu, na Yesu akiwa amesimama mkono wa kuume wa Mungu. 567:56 Mt 3:16; 8:20; Eze 1:1; Mdo 10:11; Dan 7:13Akasema, “Tazameni! Naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama upande wa kuume wa Mungu.”

57Lakini wao wakapiga kelele kwa sauti kubwa, wakaziba masikio yao, wakamrukia kwa nia moja. 587:58 Lk 4:29; Law 24:14-16; Kum 13; 9; Mdo 22:20; 8:1Wakamtupa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao mashahidi wakaweka mavazi yao miguuni mwa kijana mmoja ambaye jina lake aliitwa Sauli.

597:59 Za 31:5; Lk 23:46Walipokuwa wakimpiga mawe, Stefano aliomba, “Bwana Yesu, pokea roho yangu.” 607:60 Lk 22:41; Mdo 9:40; Mt 5:44Kisha akapiga magoti, akalia kwa sauti kubwa akasema, “Bwana usiwahesabie dhambi hii.” Baada ya kusema hayo, akalala.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

使徒行傳 7:1-60

司提凡的申辯

1大祭司問:「這是真的嗎?」 2司提凡說:「各位父老兄弟,請聽我說!我們的祖先亞伯拉罕還未遷到哈蘭之前,住在美索不達米亞,榮耀的上帝向他顯現,說, 3『你要離開家鄉和親族,到我要指示你的地方去。』 4亞伯拉罕就離開迦勒底人的地方,在哈蘭住了下來。他父親過世以後,上帝又領他到你們現在居住的這個地方。 5當時在這片土地上,上帝沒有給他任何產業,他甚至連立足之地也沒有。但上帝應許要把這片土地賜給他和他的後裔作產業,儘管那時候亞伯拉罕還沒有兒子。 6上帝又說,『你的子孫必流落異鄉,受奴役、被虐待四百年。 7但我必懲罰奴役他們的國家,之後你的子孫要離開那裡,在這片土地上事奉我。』 8上帝又賜下割禮作為祂與亞伯拉罕立約的憑據。亞伯拉罕以撒出生後的第八天為他行割禮。照樣,以撒為他的兒子雅各行了割禮,雅各也為他的兒子——以色列十二位先祖行了割禮。7·8 第八節後半部分或譯「以撒生雅各,雅各生以色列十二位先祖。」

9「先祖們嫉妒自己的弟弟約瑟,把他賣到了埃及。但上帝一直與他同在, 10救他脫離一切危難,又賜他過人的智慧,使他在埃及法老面前得到恩寵,官拜宰相治理全國,並管理王室。 11後來,埃及迦南全境遭遇饑荒,災情嚴重,我們的先祖們斷了糧。 12雅各聽說埃及有糧,就派先祖們去那裡買糧,那是我們的先祖初次去埃及13他們第二次去的時候,約瑟才和弟兄們相認,並且領他們拜見埃及王。 14後來,約瑟派人去把父親雅各和全族七十五人都接到埃及15從此以後,雅各和其他先祖們便定居埃及,直到去世。 16後來他們的遺體被帶回示劍,安葬在亞伯拉罕買自哈抹子孫的墓地裡。

17「上帝對亞伯拉罕所應許的日子快到的時侯,以色列人在埃及的人口已大大增加。 18後來埃及有一位不認識約瑟的新王登基。 19他用毒計苦害我們的同胞,虐待我們的祖先,強令他們把嬰孩拋棄,不讓嬰孩存活。 20那時,摩西出生了,他長得俊美非凡。他的父母在家裡偷偷地撫養了他三個月, 21最後不得已才丟棄他。法老的女兒救了他,收為養子。

22摩西學會了埃及人一切的學問,成為一個說話辦事很有能力的人。 23他四十歲那年決定去探望自己的同胞以色列人。 24他到了他們那裡,看見一個埃及人正在欺負以色列人,就打抱不平,殺了那個埃及人。 25摩西以為同胞們會明白上帝要藉著他的手拯救他們,可是他們並不明白。 26第二天,他看見兩個以色列人在打架,就上前勸解說,『大家都是同胞,為什麼互相毆打呢?』 27不料那個欺負人的推開摩西說,『誰立你作我們的首領和審判官? 28難道你要殺我,像昨天殺那個埃及人一樣嗎?』 29摩西聽了這話,就逃到米甸寄居,在那裡成家,生了兩個兒子。

30「過了四十年,在西奈山的曠野,上帝的天使在荊棘火焰中向摩西顯現。 31摩西見狀很驚奇,正要上前看個究竟,就聽見主說, 32『我是你祖先的上帝,是亞伯拉罕以撒雅各的上帝。』摩西戰戰兢兢,不敢觀看。 33主又說,『脫下你腳上的鞋子,因為你所站的地方是聖地。 34我已清楚看見我子民在埃及所受的苦難,也聽見了他們的哀歎,我下來要救他們。你來,我要派你回埃及。』

35「百姓曾拒絕這位摩西,說,『誰立你作我們的首領和審判官?』上帝卻藉著在荊棘中顯現的天使親自差遣他,立他為首領和拯救者。 36摩西帶領以色列人出埃及,過紅海,越曠野,四十年間行了許多神蹟奇事。 37就是這位摩西曾對以色列人說,『上帝要在你們中間興起一位像我一樣的先知。』 38這位摩西曾在曠野與以色列的會眾——我們的祖先在一起,又在西奈山上與向他傳信息的天使在一起,並且領受了生命之道傳給我們。

39「可是我們的祖先不聽從他,甚至棄絕他,心裡對埃及戀戀不捨。 40他們請求亞倫說,『為我們造一些神像來帶領我們吧!領我們離開埃及的那個摩西不知怎樣了。』 41於是,他們造了一個牛犢像,向它獻祭,並為自己所做的事沾沾自喜。 42因此,上帝轉臉不顧他們,任由他們祭拜日月星辰,正如先知書的記載,

以色列家啊,

在曠野的四十年間,

你們向我獻過祭物和供品嗎?

43你們抬著為自己所造的神像,

就是摩洛的帳篷和理番神明的星,

祭拜它們,

所以我要把你們趕到比巴比倫還遠的地方去。』

44「我們的祖先在曠野的時候,一直帶著安放約櫃的聖幕,這聖幕是上帝吩咐摩西照他所看見的樣式造的。 45後來我們的祖先承受了聖幕。上帝從我們祖先面前趕走外族人,使他們得到了應許之地。他們同約書亞把聖幕帶到那裡,一直到大衛的時代。 46大衛蒙上帝悅納,祈求為雅各的上帝建造一座聖殿。 47結果是他的兒子所羅門為上帝建成了聖殿。

48「其實至高的上帝並不住人造的殿,祂曾藉著先知說, 49『天是我的寶座,地是我的腳凳,你們要為我造怎樣的殿宇?哪裡可作我的安歇之處? 50這一切不都是我親手創造的嗎?』

51「你們這些頑固不化、耳不聽心不悔的人7·51 耳不聽心不悔的人」希臘文是「心與耳未受割禮的人」。,經常抗拒聖靈,所作所為和你們的祖先如出一轍! 52哪一位先知沒有被你們祖先迫害?那些預言義者——彌賽亞要來的人也被你們的祖先殺害。如今你們竟出賣了那位公義者,殺害了祂! 53你們接受了上帝藉天使所傳的律法,竟不遵守!」

司提凡殉道

54眾人聽了這番話,怒火中燒,咬牙切齒。 55司提凡卻被聖靈充滿,定睛望天,看見上帝的榮耀和站在上帝右邊的耶穌。 56司提凡說:「看啊!我看見天開了,人子站在上帝的右邊。」

57眾人大喊大叫,捂著耳朵,蜂擁而上, 58司提凡拉到城外,用石頭打他。指控他的人把他們的衣服交給一個名叫掃羅的青年看管。 59在亂石擊打之下,司提凡呼求說:「主耶穌啊,接收我的靈魂吧!」然後跪下高聲說: 60「主啊,不要追究他們的罪!」說完後,就斷氣了。