Matendo 23 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Matendo 23:1-35

123:1 Mdo 22:30; 22:5; 1Tim 3:9; Ebr 10:22Paulo akawakazia macho wale wajumbe wa baraza, akasema, “Ndugu zangu, nimetimiza wajibu wangu kwa Mungu kwa dhamiri safi kabisa hadi leo.” 223:2 Mdo 24:1; Yn 14:22Kwa ajili ya jambo hili kuhani mkuu Anania akaamuru wale waliokuwa karibu na Paulo wampige kofi kinywani. 323:3 Mt 23:27; Law 19:15; Yn 7:31Ndipo Paulo akamwambia, “Mungu atakupiga wewe, ewe ukuta uliopakwa chokaa! Wewe umeketi hapo ili kunihukumu kwa mujibu wa sheria, lakini wewe mwenyewe unakiuka sheria kwa kuamuru kwamba nipigwe kinyume cha sheria!”

4Wale watu waliokuwa wamesimama karibu na Paulo wakamwambia, “Je, wewe wathubutu kumtukana kuhani mkuu wa Mungu?”

523:5 Kut 22:28Paulo akajibu, “Ndugu zangu, sikujua kwamba yeye alikuwa kuhani mkuu. Kwa maana imeandikwa, ‘Usimnenee mabaya kiongozi wa watu wako.’ ”

623:6 Mdo 22:5; 26:5; 21:15, 21; 26:8; Flp 3:5Paulo alipotambua ya kuwa baadhi yao walikuwa Masadukayo na wengine ni Mafarisayo, akapaza sauti kwenye baraza, “Ndugu zangu, mimi ni Farisayo, mwana Farisayo. Hapa nimeshtakiwa kuhusu tumaini langu katika ufufuo wa wafu.” 7Aliposema haya, farakano likaanza kati ya Mafarisayo na Masadukayo na baraza lote likagawanyika. 823:8 Mt 22:23; Mk 2:16; Lk 23:4; Mdo 22:7, 17, 18(Kwa maana Masadukayo wanasema kwamba hakuna ufufuo, wala hakuna malaika au roho, lakini Mafarisayo wanaamini haya yote.)

923:9 Mdo 25:25; 5:39; Mk 2:16; Mdo 23:29; Yer 26:16; Lk 23:4; Mdo 26:31; 28:18; 22:7; 18:18Kukawa na ghasia kubwa, nao baadhi ya walimu wa sheria ambao ni Mafarisayo, wakasimama wakapinga kwa nguvu wakisema, “Hatuoni kosa lolote la mtu huyu! Huenda ikawa roho au malaika amezungumza naye” 1023:10 Mdo 21:34Ugomvi ukawa mkubwa kiasi kwamba yule jemadari akahofu kuwa wangemrarua Paulo vipande vipande, akaamuru vikosi vya askari vishuke na kumwondoa Paulo katikati yao kwa nguvu na kumleta ndani ya ngome ya jeshi.

1123:11 Mdo 18:9; 19:21; 28:23Usiku uliofuata, Bwana akasimama karibu naye akamwambia, “Jipe moyo! Kama vile ulivyonishuhudia hapa Yerusalemu, hivyo imekupasa kunishuhudia huko Rumi pia.”

Hila Za Kumuua Paulo

1223:12 Mdo 20:3; 25:3; 25:3Kulipopambazuka Wayahudi wakafanya shauri pamoja na kujifunga kwa kiapo kwamba hawatakula wala kunywa mpaka wawe wamemuua Paulo. 13Waliofanya mpango huo walikuwa zaidi ya watu arobaini. 1423:14 Mdo 23:1; 14:15Wakawaendea viongozi wa makuhani na wazee na kusema, “Tumejifunga pamoja kwa kiapo kwamba hatutakula wala kunywa mpaka tuwe tumemuua Paulo. 1523:15 Mdo 22:30Hivyo basi, wewe pamoja na baraza, inawapasa mkamjulishe jemadari ili amteremshe Paulo kwenu, mjifanye kama mnataka kufanya uchunguzi wa kina zaidi wa shauri lake. Nasi tuko tayari kumuua kabla hajafika hapa.”

16Lakini mtoto wa dada yake Paulo aliposikia juu ya shauri hilo baya, alikwenda kule kwenye ngome ya askari na kumweleza Paulo.

17Ndipo Paulo akamwita mmoja wa viongozi wa askari, akamwambia, “Mpeleke huyu kijana kwa jemadari, analo jambo la kumweleza.” 1823:18 Efe 3:1Hivyo yule kiongozi wa askari akampeleka yule kijana kwa jemadari, akamwambia, “Paulo yule mfungwa aliniita na kuniomba nimlete huyu kijana kwako, kwa sababu ana neno la kukueleza.”

19Yule jemadari akamshika yule kijana mkono, akampeleka kando na kumuuliza, “Unataka kuniambia nini?”

2023:20 Mdo 23:13Yule kijana akasema, “Wayahudi wamekubaliana wakuombe umpeleke Paulo kwenye baraza lao kesho kwa kisingizio kwamba wanataka kufanya uchunguzi wa kina wa shauri lake. 21Lakini usishawishiwe nao kwa maana zaidi ya watu arobaini wanamvizia. Wamejifunga kwa kiapo kwamba hawatakula wala kunywa mpaka wawe wamemuua Paulo. Sasa wako tayari, wanangoja idhini yako kwa ajili ya ombi lao.”

22Yule jemadari akamruhusu yule kijana aende na akamwonya, akisema, “Usimwambie mtu yeyote kwamba umenieleza habari hizi.”

Paulo Ahamishiwa Kaisaria

2323:23 Mdo 8:40Kisha yule jemadari akawaita viongozi wake wawili wa askari akawaambia, “Jiandaeni kuondoka saa tatu usiku huu kuelekea Kaisaria pamoja na askari 200, wapanda farasi sabini na watu 200 wenye mikuki. 2423:24 Mdo 24:1-3, 10; 25; 14Pia tayarisheni na farasi watakaotumiwa na Paulo, mkampeleke salama kwa mtawala Feliksi.”

25Kisha akaandika barua kwa Feliksi kama ifuatavyo:

2623:26 Mdo 25:14; 15:23Klaudio Lisia,

Kwa Mtawala, Mtukufu Feliksi:

Salamu.

2723:27 Mdo 21:32; 21:33; 22:25-29Mtu huyu alikamatwa na Wayahudi wakakaribia kumuua, lakini nikaja na vikosi vyangu vya askari nikamwokoa, kwa kuwa nilipata habari kwamba yeye ni raiya wa Rumi. 2823:28 Mdo 22:30Nilitaka kujua kwa nini walikuwa wanamshutumu, hivyo nikamleta mbele ya baraza lao. 2923:29 Mdo 18:15; 25:19; 26:31Ndipo nikaona kuwa alikuwa anashutumiwa kwa mambo yanayohusu sheria yao, lakini hakuwa ameshtakiwa kwa jambo lolote linalostahili kifo au kifungo. 3023:30 Mdo 20:3; 24:19; 25:16Nilipoarifiwa kuwa kulikuwa na shauri baya dhidi ya mtu huyu, nilimtuma kwako mara moja. Niliwaagiza washtaki wake pia waeleze mashtaka yao dhidi yake mbele yako.

31Hivyo askari, kwa kufuata maelekezo waliyopewa, wakamchukua Paulo wakati wa usiku na kumleta mpaka Antipatri. 3223:32 Mdo 21:34Kesho yake wakawaacha wale wapanda farasi waendelee na safari wakiwa na Paulo, wao wakarudi kwenye ngome ya askari. 3323:33 Mdo 8:40Askari walipofika Kaisaria, walimpa mtawala ile barua, na kumkabidhi Paulo kwake. 3423:34 Mdo 6:9; 21:39Mtawala alipokwisha kuisoma ile barua alimuuliza Paulo alikuwa mtu wa jimbo gani. Alipojua kuwa anatoka Kilikia, 3523:35 Mdo 24:19; 25:16; 24:27alisema, “Nitasikiliza shauri lako washtaki wako watakapofika hapa.” Kisha akaamuru Paulo awekwe chini ya ulinzi kwenye jumba la kifalme la Herode.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

使徒行传 23:1-35

1保罗注视着公会的人,说:“弟兄们,我在上帝面前行事为人一向问心无愧。” 2大祭司亚拿尼亚一听,就命那些站在旁边的人打保罗的嘴。 3保罗亚拿尼亚说:“你这伪君子23:3 伪君子”希腊文是“粉饰的墙”。,上帝要击打你!你坐在那里不是应当依法审问我吗?你怎么违法叫人打我?”

4站在旁边的人说:“你竟敢辱骂上帝的大祭司?” 5保罗说:“弟兄们,我不知道他是大祭司。我知道圣经上说,‘不可咒诅百姓的官长。’”

6保罗发现他们一些是法利赛人,一些是撒都该人,就在公会中高声说:“弟兄们,我是法利赛人,也是法利赛人的子孙。我因为盼望死人复活,才在这里受审!” 7这句话立刻引起法利赛人和撒都该人之间的争论,公会分成了两派。 8因为撒都该人认为没有复活,也没有天使和灵,而法利赛人认为这些都有。

9众人大声喧嚷,有几个法利赛派的律法教师站起来争辩说:“我们找不出这人有什么错处,也许真的有灵或天使跟他说过话。” 10争论越来越激烈,千夫长怕保罗会被他们扯碎了,就派人把他从人群中救出来,带回军营。

11当天晚上,主站在保罗身旁对他说:“要勇敢!正如你在耶路撒冷为我做了见证,你也必须在罗马为我做见证。”

阴谋杀害保罗

12天亮后,犹太人设下阴谋,并起誓说:“不杀保罗,誓不吃喝!” 13有四十多人参与了这个阴谋。 14他们去见祭司长和长老,说:“我们已经发了誓,不杀保罗不吃饭。 15请你们和公会出面通知千夫长,请他把保罗押到你们这里来,就说要进一步审讯他。我们准备在他到达之前杀掉他!”

16保罗的外甥听到这一阴谋,就去军营通知保罗17保罗请来一位百夫长,说:“请赶快带这青年去见千夫长,他有要事禀告!” 18百夫长领那青年去见千夫长,说:“那囚犯保罗叫我带这青年来,说有要事禀告。”

19千夫长就拉着那青年的手走到一旁,私下问他:“你有什么事要告诉我?” 20他说:“那些犹太人约好了,要请求你明天带保罗到公会受审,假装要详细审问他的事。 21你不要答应他们,因为他们有四十多个人会埋伏在半路,并且还起誓说,‘不杀保罗就不吃不喝’。他们现在已经准备就绪,就等你答应了。”

22千夫长听后,就叫他回去,并叮嘱道:“你向我禀告的事,不要告诉别人。”

保罗被押往凯撒利亚

23于是,千夫长召来两名百夫长,吩咐道:“预备二百名步兵、七十名骑兵、二百名长枪手,今晚九时出发去凯撒利亚24要给保罗预备坐骑,护送他安全抵达腓利斯总督那里。”

25千夫长写了公文给腓利斯总督,内容如下: 26克劳狄·吕西亚敬问腓利斯总督大人安。 27这人被犹太人抓住,险些被他们杀害。我得知他是罗马公民,便带兵去救了他。 28为了弄清楚他们控告他的缘由,我押他到犹太人的公会受审, 29发现他被控告与他们的律法有关,他并没有犯该被监禁或处死的罪。 30我得知有人准备暗杀他,便立即护送他到你那里,并通知他的控告者去你那里告他。”

31军兵奉命行事,连夜护送保罗安提帕底32第二天,由骑兵继续护送,其余军兵返回军营。 33他们到了凯撒利亚,将公文呈交总督,把保罗交给他。 34总督看过公文,便问保罗是哪省的人,得知保罗基利迦人,就说: 35“等告你的人来了,我会审理你的案子。”于是下令把保罗关在希律的王府里。