Matendo 19 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Matendo 19:1-41

Paulo Huko Efeso

119:1 Mdo 18:1; 18:19Apolo alipokuwa huko Korintho, Paulo alisafiri sehemu za bara, akafika Efeso. Huko akawakuta wanafunzi kadhaa, 219:2 Yn 20:22; Mdo 2:38akawauliza, “Je, mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?”

Wakajibu, “Hapana, hata hatukusikia kuwa kuna Roho Mtakatifu.” 319:3 Mdo 18:25Ndipo Paulo akawauliza, “Je, mlibatizwa kwa ubatizo gani?” Wakajibu, “Kwa ubatizo wa Yohana.”

419:4 Yn 1:7; Mdo 13:24, 25Paulo akasema, “Ubatizo wa Yohana ulikuwa wa toba, aliwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja baada yake, yaani, Yesu.” 519:5 Mdo 8:16; 2:38Waliposikia haya, wakabatizwa katika jina la Bwana Yesu. 619:6 Mdo 6:6; 8:17; 2:4; 10:46; Mk 16:17Paulo alipoweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akawashukia, nao wakanena kwa lugha mpya na kutabiri. 7Walikuwa kama wanaume kumi na wawili.

819:8 Mdo 9:20; 1:3; 11:26Paulo akaingia katika sinagogi na kunena humo kwa ujasiri kwa muda wa miezi mitatu, akijadiliana na watu na kuwashawishi katika mambo ya Ufalme wa Mungu. 919:9 Mdo 14:4; 9:2Lakini baadhi yao walikaidi. Walikataa kuamini, na wakakashifu ujumbe wake mbele ya umati wa watu. Basi Paulo aliachana nao. Akawachukua wanafunzi naye, akahojiana nao kila siku katika darasa la Tirano. 1019:10 Mdo 20:31Jambo hili likaendelea kwa muda wa miaka miwili, kiasi kwamba Wayahudi na Wayunani wote walioishi huko Asia wakawa wamesikia neno la Bwana.

Wana Wa Skewa Wajaribu Kutoa Pepo Mchafu

1119:11 Mdo 8:13Mungu akafanya miujiza mingi isiyo ya kawaida kwa mkono wa Paulo, 1219:12 Mdo 5:15hivi kwamba leso au vitambaa vilivyokuwa vimegusa mwili wa Paulo viliwekwa juu ya wagonjwa, nao wakapona magonjwa yao, na pepo wachafu wakawatoka.

1319:13 Mt 12:27; Mk 9:38Basi baadhi ya Wayahudi wenye kutangatanga huku na huko wakitoa pepo wachafu wakajaribu kutumia jina la Bwana Yesu wale wenye pepo wakisema, “Kwa jina la Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo, nakuamuru utoke.” 1419:14 Mdo 23:29; 25:11, 19Wana saba wa Skewa, Myahudi aliyekuwa kiongozi wa makuhani, walikuwa wanafanya hivyo. 1519:15 Mk 1:34; Lk 4:41Lakini pepo mchafu akawajibu, “Yesu namjua na Paulo pia namjua, lakini ninyi ni nani?” 16Kisha yule mtu aliyekuwa na pepo mchafu akawarukia, akawashambulia vikali, akawashinda nguvu wote, wakatoka ndani ya ile nyumba wakikimbia wakiwa uchi na wenye majeraha.

1719:17 Mdo 18:19; 5:5, 11Habari hii ikajulikana kwa Wayahudi wote na Wayunani waliokaa Efeso, hofu ikawajaa wote, nalo jina la Bwana Yesu likaheshimiwa sana. 1819:18 Mt 3:6Wengi wa wale waliokuwa wameamini wakati huu wakaja na kutubu waziwazi kuhusu matendo yao maovu. 19Idadi kubwa ya wale waliofanya mambo ya uganga wakaleta vitabu vyao na kuviteketeza kwa moto hadharani. Walipofanya hesabu ya thamani ya vitabu vilivyoteketezwa ilikuwa drakma 50,00019:19 Drakma ilikuwa ni sarafu ya fedha, thamani yake ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku moja. za fedha. 2019:20 Mdo 6:7; 12:24Hivyo neno la Bwana likaenea sana na kuwa na nguvu.

2119:21 Mdo 21:4, 12, 15; Rum 15:25; Mdo 16:9Baada ya mambo haya kutukia, Paulo akakusudia rohoni kwenda Yerusalemu kupitia Makedonia na Akaya. Akasema, “Baada ya kufika huko, yanipasa pia kwenda Rumi.” 2219:22 Mdo 13:5; 16:1; Rum 16:23; 2Tim 4:20Hivyo akatuma wasaidizi wake wawili, Timotheo na Erasto, waende Makedonia, wakati yeye mwenyewe alibaki kwa muda kidogo huko Asia.

Ghasia Huko Efeso

2319:23 Mdo 9:2Wakati huo huo pakatokea dhiki kubwa kwa sababu ya Njia ile ya Bwana. 2419:24 Mdo 16:16, 19Mtu mmoja jina lake Demetrio mfua fedha aliyekuwa akitengeneza vinyago vya fedha vya Artemi na kuwapatia mafundi wake biashara kubwa, 2519:25 Mdo 16:16, 19, 20aliwaita pamoja watu wengine waliofanya kazi ya ufundi kama yake na kusema, “Enyi watu, mnajua ya kuwa utajiri wetu unatokana na biashara hii! 2619:26 Mdo 16:19; Za 115:4; 1Kor 8:4Pia ninyi mmeona na kusikia jinsi ambavyo si huku Efeso peke yake lakini ni karibu Asia yote, huyu Paulo amewashawishi na kuvuta idadi kubwa ya watu kwa kusema kuwa miungu iliyotengenezwa na watu si miungu. 27Kwa hiyo kuna hatari si kwa kazi yetu kudharauliwa tu, bali pia hata hekalu la mungu mke Artemi, aliye mkuu, anayeabudiwa Asia yote na ulimwengu wote, litakuwa limepokonywa fahari yake ya kiungu.”

2819:28 Mdo 18; 19Waliposikia maneno haya, wakaghadhibika, wakaanza kupiga kelele, “Artemi wa Waefeso ni mkuu!” 2919:29 Rum 16:23; 1Kor 1:14; Kol 4:10; Flp 1:24; Mdo 16:9Mara mji wote ukajaa ghasia. Wakawakamata Gayo na Aristarko, watu wa Makedonia waliokuwa wakisafiri pamoja na Paulo, na watu wakakimbilia katika ukumbi wa michezo kama mtu mmoja. 30Paulo akataka kuingia katikati ya umati huo, lakini wanafunzi hawakumruhusu. 31Hata baadhi ya viongozi wa sehemu ile, waliokuwa rafiki zake Paulo, wakatuma watu wakitamani asiingie katika ule ukumbi.

3219:32 Mdo 21:34Ule umati ulikuwa na taharuki. Wengine walikuwa wakipiga kelele, hawa wakisema hili na wengine lile. Idadi kubwa ya watu hawakujua hata ni kwa nini walikuwa wamekusanyika huko. 3319:33 Mdo 12:17Wayahudi wakamsukumia Aleksanda mbele na baadhi ya watu kwenye ule umati wakampa maelekezo. Akawaashiria kwa mkono ili watulie aweze kujitetea mbele ya watu. 34Lakini walipotambua kwamba alikuwa Myahudi, wote wakapiga kelele kwa sauti moja kwa karibu muda wa saa mbili, wakisema, “Artemi wa Efeso ni mkuu!”

3519:35 Mdo 18:19Baadaye karani wa mji akaunyamazisha ule umati wa watu na kusema, “Enyi watu wa Efeso, je, ulimwengu wote haujui ya kuwa mji wa Efeso ndio unaotunza hekalu la Artemi aliye mkuu na ile sanamu yake iliyoanguka kutoka mbinguni? 36Kwa hiyo, kwa kuwa mambo haya hayakanushiki, inawapasa mnyamaze na wala msifanye lolote kwa haraka. 3719:37 Rum 2:22Kwa kuwa mmewaleta hawa watu hapa, ingawa hawajaiba hekaluni wala kumkufuru huyu mungu wetu wa kike. 3819:38 Mdo 13:7, 8, 12Basi, ikiwa Demetrio na mafundi wenzake wana jambo zito dhidi ya mtu yeyote, mahakama ziko wazi na wasaidizi wa mwakilishi wa mtawala. Wanaweza kufungua mashtaka. 39Lakini kama kuna jambo jingine lolote zaidi mnalotaka kulileta, itabidi lisuluhishwe katika kusanyiko halali. 40Kama ilivyo sasa, tuko hatarini kushtakiwa kwa kufanya ghasia kwa sababu ya tukio la leo. Kwa kuwa hakuna sababu tutakayoweza kutoa kuhalalisha msukosuko huu.” 41Baada ya kusema haya akavunja mkutano.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

使徒行传 19:1-41

保罗在以弗所传道

1亚波罗哥林多时,保罗已取道内陆重回以弗所,在那里遇见几个门徒。 2保罗问他们:“你们信的时候有没有领受圣灵?”

他们说:“没有!我们从来没有听过圣灵的事。”

3保罗说:“那么,你们受的是什么洗礼呢?”

他们说:“是约翰的洗礼。”

4保罗说:“约翰的洗礼是悔改的洗礼,约翰告诉百姓要信在他以后来的那位——耶稣。”

5他们听后,立刻奉主耶稣的名受了洗。 6保罗把手按在他们身上时,圣灵便降在他们身上,他们就说方言,讲上帝的信息。 7这次共有十二个人。

8保罗一连三个月勇敢地在会堂里传道,与人辩论上帝国的事,劝导他们。 9可是有些人仍然顽固不信,还当众毁谤上帝的道。保罗便带着门徒离开他们,天天在推喇奴的学堂辩论。 10这样持续了两年,亚细亚全境的居民,无论是犹太人还是希腊人,都听见了主的道。 11上帝又借着保罗的手行了一些非凡的神迹, 12甚至只要将保罗身上的手帕或围裙放在病人身上,病人就痊愈了,邪灵也会离开所附的人。

13那时,有几个走江湖的犹太术士也想用耶稣的名赶鬼,他们向那些被邪灵附身的人说:“我奉保罗所传讲的耶稣之名,命令你们出来!” 14做这事的有犹太祭司长士基瓦的七个儿子。

15邪灵回答说:“耶稣,我认识;保罗,我也知道。但你们是谁?” 16被邪灵附身的人随即扑向他们,攻击他们,制服了他们,使他们赤着身子带着伤从屋里逃走了。

17以弗所犹太人和希腊人知道了这件事,都惊惧不已。主耶稣的名因此大受尊崇。 18许多已经信耶稣的人都前来认罪,公开承认自己的恶行。 19又有许多行邪术的人把他们的书堆在一起,当众焚烧。根据当时的估价,这些书约值五万银币。 20主的道就这样传开了,大大兴旺起来。

21这些事以后,保罗决定经过马其顿亚该亚回到耶路撒冷。他说:“到了那里之后,我必须去罗马看看。” 22于是,他派提摩太以拉都两位同工先去马其顿,自己暂时留在亚细亚

以弗所的骚乱

23就在这时,由于主的道,以弗所又起了很大的骚乱。 24一个名叫底米丢的银匠以制造亚底米女神银龛为业,使从事这门生意的工匠获利丰厚。 25他召集了工匠和同行的人,说:“各位都知道我们靠这一行发财, 26可是你们都看到了,也听见了,那个保罗以弗所亚细亚全境说服、误导了许多人,说什么人手所造的不是神。 27这样下去,不但我们的行业会遭人贬抑,连亚底米女神庙也会被人轻看,甚至全亚细亚及普世尊崇的女神也会威严扫地!”

28众人听后,怒气填胸,高声喊叫:“以弗所人的亚底米女神真伟大!” 29全城陷入一片混乱。众人抓住保罗的两个同伴——马其顿该犹亚里达古,拖着他们冲进戏院。 30保罗想进去,但门徒不许他去。 31他的好友——亚细亚的几位官员也派人劝他别冒险进入戏院。

32这时,戏院里面的人都在大喊大叫,混乱不堪。其实大部分人根本不知道自己为什么聚在那里。 33这时,人群中的犹太人把亚历山大推到前面,请他解释。亚历山大举手示意大家安静,听他发言。 34但众人认出他是个犹太人,便又开始一起高呼:“以弗所人的亚底米女神真伟大!”这样喊了两个小时。

35最后,城里的书记官出面调停,说:“各位以弗所市民,谁不知道以弗所城守护着亚底米女神庙和从宙斯那里掉下来的神像呢? 36既然这是无可否认的事实,你们就该安静,不可鲁莽行事。 37你们带来的这些人既没有偷庙里的东西,也没有亵渎我们的女神。 38如果底米丢和他的同行要控告谁,大可到法庭或总督那里提出诉讼。 39倘若你们还有其他的要求,也可以通过合法的会议解决。 40今天的骚乱实在没有道理,难免会被查问,到时候我们很难交代。” 41说完,便叫众人散去。