Matendo 13 – NEN & CCL

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Matendo 13:1-52

Safari Ya Kwanza Ya Paulo Kueneza Injili

(13:1–14:28)

Barnaba Na Sauli Wanatumwa

113:1 Mdo 11:19, 27; Efe 4:11; Mdo 4:36; Mt 27:32; 14:1Katika kanisa huko Antiokia ya Shamu walikuwako manabii na walimu, yaani: Barnaba, Simeoni aitwaye Nigeri, Lukio Mkirene, Manaeni aliyekuwa amelelewa pamoja na Mfalme Herode Agripa, na Sauli. 213:2 Mdo 8:29; 14:26; 9:15; 22:21Walipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, “Nitengeeni Sauli na Barnaba kwa kazi ile maalum niliyowaitia.” 313:3 Mdo 6:6; 14:26; 1Tim 4:14; 5:22Ndipo baada ya kufunga na kuomba, wakawawekea mikono yao na wakawatuma waende zao.

Barnaba Na Sauli Waenda Kipro

413:4 Mdo 13:2, 3; 4:36; 15:39Hivyo, wakiwa wametumwa na Roho Mtakatifu, wakashuka kwenda Seleukia na kutoka huko wakasafiri baharini mpaka kisiwa cha Kipro. 513:5 Ebr 4:12; 9:20; 12:12Walipowasili katika mji wa Salami, wakahubiri neno la Mungu katika sinagogi la Wayahudi. Pia walikuwa na Yohana Marko kuwa msaidizi wao.

613:6 Mdo 8:9; Mt 7:15Walipokwisha kupita katika nchi zote hizo wakafika Pafo, ambapo walikutana na Myahudi mmoja mchawi aliyekuwa nabii wa uongo, jina lake Bar-Yesu. 713:7 Mdo 13:8, 12; 18:12; 19:38Mtu huyu alikuwa pamoja na Sergio Paulo, mtu mwenye hekima aliyekuwa msaidizi wa mwakilishi wa mtawala wa kile kisiwa. Sergio Paulo akawaita Sauli na Barnaba akitaka kusikia neno la Mungu. 813:8 Mdo 8:9; Isa 30:11; Mdo 6:7; 2Tim 3:8Lakini Elima yule mchawi (hii ndiyo maana ya jina lake), aliwapinga Barnaba na Sauli na kujaribu kumpotosha yule mkuu wa kile kisiwa aiache imani. 913:9 Lk 1; 15Ndipo Sauli, ambaye pia aliitwa Paulo, akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, akamkazia macho Elima huyo mchawi, 1013:10 Mt 13:38; Yn 8:44; Hos 14:9akamwambia, “Ewe mwana wa ibilisi, wewe ni adui wa kila kilicho haki! Umejaa kila aina ya udanganyifu na ulaghai. Je, hutaacha kuzipotosha njia za Bwana zilizonyooka? 1113:11 Kut 9:3; 1Sam 5:6, 7; Za 32:4; Mwa 19:10, 11Nawe sasa sikiliza, mkono wa Bwana u dhidi yako. Utakuwa kipofu, wala hutaona jua kwa muda.”

Mara ukungu na giza vikamfunika, naye akaenda huku na huko akitafuta mtu wa kumshika mkono ili amwonyeshe njia. 1213:12 Mdo 13:7Yule mkuu wa kile kisiwa alipoona yaliyotukia, akaamini kwa sababu alistaajabishwa na mafundisho kuhusu Bwana.

Paulo Na Barnaba Huko Antiokia Ya Pisidia

1313:13 Mdo 13:6; 2:10; 12:12Kisha Paulo na wenzake wakasafiri toka Pafo wakafika Perga huko Pamfilia. Lakini, Yohana Marko akawaacha huko, akarejea Yerusalemu. 1413:14 Mdo 14:19, 21; 13:27, 42, 44; 16:13; 18:4; 9:20Kutoka Perga wakaendelea hadi Antiokia ya Pisidia. Siku ya Sabato wakaingia ndani ya sinagogi, wakaketi. 1513:15 Mdo 15:21; Lk 4:16; Ebr 13:22Baada ya Sheria ya Mose na Kitabu cha Manabii kusomwa, viongozi wa sinagogi wakawatumia ujumbe wakisema, “Ndugu, kama mna neno la kuwafariji watu hawa, tafadhali lisemeni.”

1613:16 Mdo 12:17; 10:35Paulo akasimama, akawapungia mkono na kusema: “Enyi wanaume wa Israeli na ninyi nyote mnaomcha Mungu. 1713:17 Kut 6:6, 7; Kum 7:6-8Mungu wa watu hawa wa Israeli aliwachagua baba zetu, akawafanya kustawi walipokuwa huko Misri, kwa uwezo mwingi akawaongoza na kuwatoa katika nchi ile. 1813:18 Kum 1:31; Hes 14:33; Za 95:10; Mdo 7:36Kwa muda wa miaka arobaini alivumilia matendo yao walipokuwa jangwani. 1913:19 Kum 7:1; Yos 14:2; Za 78:55Naye baada ya kuyaangamiza mataifa saba waliokuwa wakiishi katika nchi ya Kanaani, akawapa Waisraeli nchi yao iwe urithi wao. 2013:20 Amu 2:17; 1Sam 3:19, 20; Mdo 3:24Haya yote yalichukua kama muda wa miaka 450.

“Baada ya haya, Mungu akawapa waamuzi mpaka wakati wa nabii Samweli. 2113:21 1Sam 8:5, 19; 10:1; 9:1, 2Ndipo watu wakaomba wapewe mfalme, naye Mungu akawapa Sauli mwana wa Kishi wa kabila la Benyamini, aliyetawala kwa miaka arobaini. 2213:22 1Sam 15:23, 26; 16:13; Za 89:20; Yer 3:15; Isa 44:28; 1Sam 13:14Baada ya kumwondoa Sauli katika ufalme, akawainulia Daudi kuwa mfalme wao. Mungu pia alimshuhudia, akisema, ‘Nimemwona Daudi mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayetimiza mapenzi yangu yote.’

2313:23 Mt 1:1; Lk 2:11; Mt 1:21; 2Sam 7:11; 22:51; Yer 30:9“Kutoka uzao wa mtu huyu, Mungu amewaletea Israeli Mwokozi Yesu, kama alivyoahidi. 2413:24 Mk 1:4; Lk 3:3Kabla ya kuja kwa Yesu, Yohana alihubiri toba na ubatizo kwa watu wote wa Israeli. 2513:25 Mdo 20:24; Yn 1:20; Mt 3:11; Yn 1:27Yohana alipokuwa anakamilisha kazi yake, alisema: ‘Ninyi mnadhani mimi ni nani? Mimi si yeye. La hasha, lakini yeye yuaja baada yangu, ambaye mimi sistahili kufungua kamba za viatu vya miguu yake.’

2613:26 Mdo 22:5; Lk 3:8; Mt 4:12; Mdo 28:28; Mt 10:6“Ndugu zangu, wana wa Abrahamu, nanyi watu wa Mataifa mnaomcha Mungu, ujumbe huu wa wokovu umeletwa kwetu. 2713:27 Mdo 3:17; Lk 24:27; Mt 1:22Kwa sababu wakaao Yerusalemu na viongozi wao hawakumtambua wala kuelewa maneno ya manabii yasomwayo kila Sabato, bali waliyatimiza maneno hayo kwa kumhukumu yeye. 2813:28 Mt 27:20-25; Mdo 3:13Ijapokuwa hawakupata sababu yoyote ya kumhukumu kifo, walimwomba Pilato aamuru auawe. 2913:29 Mt 1:22; Lk 8:31; Mdo 5:30; Lk 23:53Walipokwisha kufanya yale yote yaliyoandikwa kumhusu, walimshusha kutoka msalabani na kumzika kaburini. 3013:30 Mt 16:21; 28:6; Mdo 2:24Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. 3113:31 Mt 28; 16; Lk 24:48Naye kwa siku nyingi akawatokea wale waliokuwa pamoja naye kuanzia Galilaya hadi Yerusalemu. Nao sasa wamekuwa mashahidi wake kwa watu wetu.

3213:32 Isa 40:9; 52:7; Mdo 5:42; 8:35; 10:36; Rum 12; 4:13; 9:4“Nasi tunawaletea habari njema, kwamba yale Mungu aliyowaahidi baba zetu 3313:33 Mdo 2:24; Za 2:7; Mt 3:17sasa ameyatimiza kwetu sisi watoto wao, kwa kumfufua Yesu, kama ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili:

“ ‘Wewe ni Mwanangu;

leo mimi nimekuzaa.’

3413:34 Isa 55:6; 55:3Kwa kuwa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu asioze kamwe, alitamka maneno haya:

“ ‘Nitakupa wewe baraka takatifu zilizo za hakika

nilizomwahidi Daudi.’

3513:35 Za 16; 10; Mdo 2:27Kama ilivyosemwa mahali pengine katika Zaburi,

“ ‘Hutamwacha Aliye Mtakatifu wako kuona uharibifu.’

3613:36 Mt 9:24; 2Sam 7:12; 1Fal 2:10; 2Nya 29:28; Mdo 2:29“Kwa maana Daudi akiisha kulitumikia kusudi la Mungu katika kizazi chake, alilala; akazikwa pamoja na baba zake na mwili wake ukaoza. 3713:37 Mdo 2:24Lakini yule ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu hakuona uharibifu.

3813:38 Lk 24:47; Mdo 2:38“Kwa hiyo ndugu zangu, nataka ninyi mjue kwamba kwa kupitia huyu Yesu msamaha wa dhambi unatangazwa kwenu. 3913:39 Yn 3:15; Rum 3:28; 10:4Kwa kupitia yeye, kila mtu amwaminiye anahesabiwa haki kwa kila kitu ambacho asingeweza kuhesabiwa haki kwa sheria ya Mose. 4013:40 Hab 1:4Kwa hiyo jihadharini ili yale waliyosema manabii yasiwapate:

4113:41 Hab 1:5“ ‘Angalieni, enyi wenye dhihaka,

mkastaajabu, mkaangamie,

kwa maana nitatenda jambo wakati wenu

ambalo hamtasadiki,

hata kama mtu akiwaambia.’ ”

4213:42 Mdo 13:14Paulo na Barnaba walipokuwa wakitoka nje ya sinagogi, watu wakawaomba wazungumze tena mambo hayo Sabato iliyofuata. 4313:43 Mdo 11:23; 14:22; Rum 3:24Baada ya kusanyiko la Sinagogi kutawanyika, wengi wa Wayahudi na waongofu wa dini ya Kiyahudi wakawafuata Paulo na Barnaba, wakazungumza nao na kuwahimiza wadumu katika neema ya Mungu.

44Sabato iliyofuata, karibu watu wote wa mji walikuja kusikiliza neno la Bwana. 4513:45 Mdo 18:6; 1Pet 4:4; 1The 2:16Lakini Wayahudi walipoona ule umati mkubwa wa watu walijawa na wivu, wakayakanusha maneno Paulo aliyokuwa akisema.

4613:46 Mdo 13:26; 3:26; 18:6; 22:21; 26:20; 28:28; Rum 11:11; Mt 21:41Ndipo Paulo na Barnaba wakawajibu kwa ujasiri, wakisema, “Ilitupasa kunena nanyi neno la Mungu kwanza. Lakini kwa kuwa mmelikataa, mkajihukumu wenyewe kuwa hamstahili uzima wa milele, sasa tunawageukia watu wa Mataifa. 4713:47 Lk 2:32; Isa 49:6Kwa maana hili ndilo Bwana alilotuamuru:

“ ‘Nimewafanya ninyi kuwa nuru kwa watu wa Mataifa,

ili mpate kuuleta wokovu hadi miisho ya dunia.’ ”

4813:48 Mdo 13:49; 8:25; Rum 8:29Watu wa Mataifa waliposikia haya wakafurahi na kulitukuza neno la Bwana; nao wote waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.

4913:49 Mdo 13:48Neno la Bwana likaenea katika eneo lile lote. 5013:50 1The 2:16Lakini Wayahudi wakawachochea wanawake wenye kumcha Mungu, wenye vyeo pamoja na watu maarufu katika mji, wakachochea mateso dhidi ya Paulo na Barnaba na kuwafukuza kutoka eneo hilo. 5113:51 Mt 10:14; Mdo 14:1; 19:21; 2Tim 3:11Hivyo Paulo na Barnaba wakakungʼuta mavumbi ya miguu yao ili kuwapinga, nao wakaenda Ikonio. 5213:52 Mdo 11:26; Lk 1:5Wanafunzi wakajawa na furaha na Roho Mtakatifu.

Mawu a Mulungu mu Chichewa Chalero

Machitidwe a Atumwi 13:1-52

Barnaba ndi Saulo Atumidwa ndi Mpingo

1Mu mpingo wa ku Antiokeya munali aneneri ndi aphunzitsi awa: Barnaba, Simeoni, Lukia wa ku Kurene, Manayeni (amene analeredwa pamodzi ndi mfumu Herode), ndiponso Saulo. 2Iwo pamene ankapembedza Ambuye ndi kusala kudya, Mzimu Woyera anati, “Mundipatulire Barnaba ndi Saulo kuti akagwire ntchito imene ndinawayitanira.” 3Ndipo atasala kudya ndi kupemphera anasanjika manja awo pa iwo nawatumiza.

Ku Kupro

4Barnaba ndi Saulo motumidwa ndi Mzimu Woyera, anapita ku Selukeya ndipo kuchokera kumeneko anakwera sitima ya pamadzi kupita ku Kupro. 5Pamene anafika ku Salamisi, analalikira Mawu a Mulungu mʼMasunagoge a Ayuda. Iwo anali ndi Yohane monga wowatumikira.

6Iwo anayenda pa chilumba chonse mpaka anafika ku Pafo, kumeneko anapezanako ndi Myuda, wamatsenga amene analinso mneneri wonama dzina lake Barayesu. 7Iyeyu, amathandiza mkulu wa boma, Sergio Paulo. Mkulu wa bomayu, munthu wanzeru, anayitana Barnaba ndi Saulo chifukwa anafuna kumva Mawu a Mulungu. 8Koma Elima wamatsengayo, (Elima tanthauzo lake ndi wamatsenga), anatsutsana nawo ndipo anafuna kumuletsa mkulu wa bomayo kuti asakhulupirire. 9Koma Saulo, amenenso amatchedwa Paulo, wodzazidwa ndi Mzimu Woyera anamuyangʼanitsitsa Elima ndipo anati, 10“Iwe ndiwe mwana wa mdierekezi ndiponso mdani wa chilungamo! Ndiwe wodzaza ndi chinyengo cha mtundu uliwonse ndi kuchenjera konse. Kodi sudzaleka kupotoza njira zolungama za Ambuye? 11Tsopano dzanja la Ambuye likukutsutsa iwe. Udzakhala wosaona ndipo kwa kanthawi sudzatha kuona kuwala kwa dzuwa.”

Nthawi yomweyo khungu ndi mdima zinamugwera ndipo anafunafuna munthu woti amugwire dzanja kuti amutsogolere. 12Pamene mkulu wa bomayo anaona zimene zinachitika anakhulupirira pakuti anadabwa ndi chiphunzitso cha Ambuye.

Antiokeya wa ku Pisidiya

13Kuchokera ku Pafo, Paulo ndi anzake anayenda pa sitima ya pamadzi kupita ku Perga wa ku Pamfiliya, kumeneko Yohane anawasiya nabwerera ku Yerusalemu. 14Kuchokera ku Perga anapita ku Pisidiya wa ku Antiokeya. Pa tsiku la Sabata analowa mʼsunagoge, nakhala pansi. 15Atawerenga mawu a mʼMalamulo ndi Aneneri, akulu a sunagoge anawatumizira mawu ndi kuti, “Abale ngati muli ndi mawu olimbikitsa nawo anthuwa, nenani.”

16Atayimirira, Paulo anakweza dzanja lake ndi kuti, “Inu Aisraeli ndiponso inu a mitundu ina amene mumapembedza Mulungu, tandimverani! 17Mulungu wa Aisraeli anasankha makolo athu ndipo anawapatsa chuma chambiri pamene amakhala ku Igupto. Anawatulutsa mʼdzikomo ndi dzanja lake lamphamvu. 18Ndipo Iye anapirira khalidwe lawo mʼchipululu kwa zaka makumi anayi. 19Mulungu anawagonjetsera mitundu isanu ndi iwiri ya ku Kanaani ndipo anapereka dzikolo kwa Israeli kuti likhale lawo. 20Izi zonse zinatenga zaka 450.

“Zitatha izi, Mulungu anawapatsa oweruza mpaka nthawi ya mneneri Samueli. 21Kenaka anthu anapempha kuti awapatse mfumu, ndipo anawapatsa Sauli mwana wa Kisi, wa fuko la Benjamini amene analamulira zaka makumi anayi. 22Mulungu atamuchotsa Sauli, anayika Davide kukhala mfumu yawo. Mulungu anamuchitira umboni kuti, ‘Ndapeza Davide mwana wa Yese munthu wa pamtima panga; iye adzachita zonse zimene ine ndikufuna kuti iye achite.’

23“Kuchokera mwa zidzukulu za munthu ameneyu, Mulungu anawutsa Yesu kukhala Mpulumutsi wa Aisraeli, monga analonjezera. 24Yesu asanabwere, Yohane analalikira kwa anthu onse Aisraeli za kutembenuka mtima ndi ubatizo. 25Pamene Yohane amatsiriza ntchito yake anati: ‘Mukuganiza kuti ine ndine yani? Ine sindine ameneyo ayi, koma Iye akubwera pambuyo panga, amene ine sindine woyenera kumasula zingwe za nsapato zake.’

26“Abale, ana a Abrahamu, ndiponso inu a mitundu ina amene mumaopa Mulungu, Iye watumiza uthenga wachipulumutsowo kwa ife. 27Anthu a ku Yerusalemu ndi atsogoleri awo sanazindikire Yesu, komabe pomuweruza Yesu anakwaniritsa mawu a Aneneri amene amawerengedwa Sabata lililonse. 28Ngakhale sanapeze chifukwa choti afe, anapempha Pilato kuti amuphe. 29Atachita zonse zimene zinalembedwa za Iye, iwo anamuchotsa pa mtengo ndipo anamuyika mʼmanda. 30Koma Mulungu anamuukitsa, 31ndipo kwa masiku ambiri anaonekera kwa amene anayenda naye kuchokera ku Galileya mpaka ku Yerusalemu. Iwowa tsopano ndi mboni zake kwa anthu a Israeli.

32“Ife tikukuwuzani Uthenga Wabwino; umene Mulungu analonjeza makolo athu. 33Iye wakwaniritsa zimenezi kwa ife ana awo, poukitsa Yesu kuchokera kwa akufa. Monga zinalembedwa mu Salimo lachiwiri kuti,

“Iwe ndiwe mwana wanga;

lero ine ndakhala Atate ako.”

34Zakuti Mulungu anamuukitsa kuti asawole konse, zinanenedwa mʼmawu awa:

“ ‘Ine, ndidzakupatsa madalitso opatulika ndi odalirika amene ndinalonjeza Davide.’

35Nʼchifukwa chakenso zinalembedwa mu Salimo lina kuti,

“ ‘Simudzalekerera woyera wanu kuti awole.’

36“Pakuti pamene Davide anatsiriza kutumikira Mulungu mu mʼbado wake, anamwalira, iye anayikidwa mʼmanda pamodzi ndi makolo ake ndipo thupi lake linawola. 37Koma amene Mulungu anamuukitsa kwa akufa sanawole ayi.

38“Nʼchifukwa chake, abale anga, dziwani kuti mwa Yesu chikhululukiro cha machimo chikulalikidwa. 39Kudzera mwa Iye aliyense amene akhulupirira, alungamitsidwa kuchoka ku tchimo lililonse limene silingachoke ndi Malamulo a Mose. 40Samalani kuti zimene aneneri akunena zisakuchitikireni inu:

41“ ‘Onani, inu anthu onyoza,

dabwani ndipo wonongekani,

chifukwa ine ndidzachita china chake mʼmasiku anu,

inu simudzazikhulupirira

ngakhale wina atakufotokozerani!’ ”

42Pamene Paulo ndi Barnaba amatuluka mʼSunagoge, anthu anawapempha kuti adzapitirize kuyankhula zinthu zimenezi Sabata linalo. 43Atatha mapemphero, Ayuda ambiri ndi anthu odzipereka otembenukira ku Chiyuda anatsatira Paulo ndi Barnaba, iwo anayankhula ndi anthuwo ndipo anawapempha kuti apitirire mʼchisomo cha Mulungu.

44Pa Sabata linalo pafupifupi anthu onse a mu mzindawo anasonkhana kudzamva Mawu a Ambuye. 45Pamene Ayuda anaona gulu la anthu, anachita nsanje ndipo anayankhula zamwano kutsutsana ndi zimene Paulo amanena.

46Ndipo Paulo ndi Barnaba anawayankha molimba mtima kuti, “Ife tinayenera kuyankhula Mawu a Mulungu kwa inu poyamba. Popeza inu mwawakana ndi kudziyesa nokha osayenera moyo wosatha, ife tsopano tikupita kwa anthu a mitundu ina. 47Pakuti izi ndi zimene Ambuye anatilamula ife:

“ ‘Ine ndakuyika iwe ukhale kuwunika kwa anthu a mitundu ina,

kuti ukafikitse chipulumutso ku malekezero a dziko lapansi!’ ”

48Anthu a mitundu ina atamva izi, anakondwa ndipo analemekeza Mawu Ambuye; ndipo onse amene anawasankha kuti alandire moyo osatha anakhulupirira.

49Mawu a Ambuye anafalikira mʼchigawo chonse. 50Koma Ayuda anawutsa mitima ya akazi otchuka opembedza Mulungu ndi akulu a mu mzindamo. Iwo anabweretsa mazunzo kwa Paulo ndi Barnaba ndipo anawathamangitsa mʼchigawo chawo. 51Tsono iwo anasasa fumbi la ku mapazi awo powatsutsa, ndipo anapita ku Ikoniya. 52Ndipo ophunzira anadzazidwa ndi chimwemwe ndiponso ndi Mzimu Woyera.