Matendo 11 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Matendo 11:1-30

Petro Aeleza Alivyotumwa Kwa Watu Wa Mataifa

111:1 Mdo 1:16; Ebr 4:12Mitume na ndugu walioamini waliokuwa huko Uyahudi wakasikia kuwa watu wa Mataifa nao wamepokea neno la Mungu. 211:2 Mdo 10:45; Gal 2:12Hivyo Petro alipopanda Yerusalemu, wale wa tohara waliokuwa wameamini wakamshutumu, 311:3 Mdo 10:25-28; Gal 2:12wakisema, “Ulikwenda kwa watu wasiotahiriwa na kula pamoja nao.”

411:4 Lk 1:3Ndipo Petro akaanza kuwaeleza kuhusu mambo yote yalivyotokea hatua kwa hatua akisema, 511:5 Mdo 10:9-32; 9:10“Nilikuwa katika mji wa Yafa nikiomba, nami nikapitiwa na usingizi wa ghafula, nikaona maono. Kulikuwa na kitu kama nguo kubwa ikishuka kutoka mbinguni, ikishushwa kwa ncha zake nne, nayo ikanikaribia. 6Nilipoangalia ndani yake kwa karibu niliona wanyama wenye miguu minne wa nchini, wanyama wa mwitu, watambaao na ndege wa angani. 7Ndipo nikasikia sauti ikiniambia, ‘Petro, ondoka uchinje na ule.’

8“Nikajibu, ‘La hasha Bwana! Kitu chochote kilicho najisi hakijaingia kinywani mwangu.’

911:9 Mdo 10:15“Sauti ikasema kutoka mbinguni mara ya pili, ‘Usikiite najisi kitu chochote Mungu alichokitakasa.’ 10Jambo hili lilitokea mara tatu, ndipo kile kitu kikavutwa tena mbinguni.

11“Wakati ule ule watu watatu, waliokuwa wametumwa kutoka Kaisaria waliwasili katika nyumba niliyokuwa nikikaa. 1211:12 Mdo 8:29; 15:9; Rum 3:22; Mdo 1:16; Yn 16:13Roho Mtakatifu akaniambia niende nao bila kuwa na ubaguzi kati yao na sisi. Hawa ndugu sita pia walifuatana nami, nasi tukaingia nyumbani mwa huyo Kornelio. 1311:13 Mdo 5:19; 10:30Akatuambia jinsi alivyoona malaika aliyekuwa amesimama katika nyumba yake na kusema, ‘Tuma watu waende Yafa wakamlete Simoni aitwaye Petro. 1411:14 Yn 4:53; 1Kor 1:11-16Yeye atakupa ujumbe ambao kwa huo wewe na wa nyumbani mwako wote mtaokoka.’

1511:15 Mdo 10:44; 2:4“Nami nilipoanza kusema, Roho Mtakatifu akashuka juu yao kama vile alivyotushukia sisi hapo mwanzo. 1611:16 Mk 1:8; Mdo 1:5Nami nikakumbuka neno la Bwana alivyosema, ‘Yohana alibatiza kwa maji, lakini ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu.’ 1711:17 Mdo 10:45-47Basi ikiwa Mungu aliwapa hawa watu kipawa kile kile alichotupa sisi tuliomwamini Bwana Yesu Kristo, mimi ni nani hata nifikirie kuwa ningeweza kumpinga Mungu?”

1811:18 Rum 10:12-13; 2Kor 7:10Waliposikia haya hawakuwa na la kupinga zaidi. Nao wakamwadhimisha Mungu wakisema, “Basi, Mungu amewapa hata watu wa Mataifa toba iletayo uzima wa milele.”

Kanisa La Antiokia

1911:19 Mdo 8:1-4; 14:26; Gal 2:11Basi wale waliotawanyika kwa ajili ya mateso yaliyotokana na kifo cha Stefano, wakasafiri hadi Foinike na Kipro na Antiokia. Nao hawakuhubiri lile Neno kwa mtu yeyote isipokuwa Wayahudi. 2011:20 Mdo 4:36; Mt 27:32; Mdo 4:36; Mt 27:32Lakini baadhi yao walikuwepo watu wa Kipro na Kirene, ambao walipokuja Antiokia walinena na Wayunani pia wakiwahubiria habari njema za Bwana Yesu. 2111:21 Lk 1:66; Mdo 2:41-47Mkono wa Bwana ulikuwa pamoja nao, nayo idadi kubwa ya watu wakaamini na kumgeukia Bwana.

2211:22 Mdo 4:36Habari hizi zilipofika masikioni mwa kanisa huko Yerusalemu, wakamtuma Barnaba aende Antiokia. 2311:23 Mdo 15:40; 20:24; 14:22Alipofika na kuona madhihirisho ya neema ya Mungu, akafurahi na kuwatia moyo waendelee kuwa waaminifu kwa Bwana kwa mioyo yao yote. 2411:24 Mdo 2:41; 5:14Barnaba alikuwa mtu mwema, aliyejaa Roho Mtakatifu, mwenye imani, nayo idadi kubwa ya watu wakaongezeka kwa Bwana.

2511:25 Mdo 9:11Kisha Barnaba akaenda Tarso kumtafuta Sauli, 2611:26 Mdo 6:1-2; 9:19-26; 26:28; 1Pet 4:16naye alipompata akamleta Antiokia. Hivyo kwa mwaka mzima Barnaba na Sauli wakakutana na kanisa na kufundisha idadi kubwa ya watu. Ilikuwa ni katika kanisa la Antiokia kwa mara ya kwanza wanafunzi waliitwa Wakristo.

2711:27 1Kor 11:4; Efe 4:11Wakati huo manabii walishuka toka Yerusalemu hadi Antiokia. 2811:28 Mdo 21:10; Mt 24:14; Mdo 18:2Mmoja wao, jina lake Agabo, akasimama akatabiri kwa uweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itaenea ulimwengu mzima. Njaa hiyo ilitokea wakati wa utawala wa Klaudio. 2911:29 Rum 15:26; 2Kor 8:1-4; Mdo 1:16Mitume wakaamua kwamba kila mtu, kulingana na uwezo alio nao, atoe msaada kwa ajili ya ndugu wanaoishi Uyahudi. 3011:30 Mdo 14:23; 15:2; 22; 20:17; 1Tim 5:17; Tit 1:5; Yak 5:14; 1Pet 5:1; Mdo 4:36; 12:25Wakafanya hivyo, misaada yao ikapelekwa kwa wazee kwa mikono ya Barnaba na Sauli.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

使徒行传 11:1-30

彼得的解释

1使徒和犹太全境的弟兄姊妹都听说外族人接受了上帝的道。 2彼得一回到耶路撒冷,严守割礼的门徒就指责他: 3“你竟然去未受割礼之人的家,还和他们一同吃饭!”

4彼得就把事情的经过一一向他们解释,说: 5“我在约帕城祷告的时候,看见一个异象,有一大块像布的东西四个角吊着从天上降到我面前。 6我定睛一看,里面有牲畜、野兽、爬虫和飞禽。 7接着,我听见有声音对我说,‘彼得,起来,宰了吃!’ 8我说,‘主啊,这可不行!我从未吃过任何污秽不洁之物!’ 9那从天上来的声音又说,‘上帝已经洁净的,你不可再称之为不洁净。’ 10这样一连三次,然后一切都被收回天上去了。 11就在那时候,有三个从凯撒利亚来的人到我住处的门口来找我。 12圣灵吩咐我跟他们同去,不要犹豫。就这样,我和这六位弟兄一同到了哥尼流家。 13他告诉我们天使如何在他家中向他显现,并对他说,‘你派人去约帕,请一位名叫西门·彼得的人来。 14他有话告诉你,能使你和你的全家得救。’

15“我开口讲话时,圣灵降在他们身上,跟当初降在我们身上的情形一模一样。 16我就想起主的话,‘约翰用水施洗,但你们要受圣灵的洗礼。’ 17既然上帝给他们恩赐,就如我们信主耶稣基督时给我们一样,我是谁,怎能拦阻上帝?” 18大家听了便安静下来,转而归荣耀给上帝,说:“如此看来,上帝把悔改得永生的机会也赐给了外族人。”

安提阿的教会

19司提凡殉道后,信徒们因受迫害而四散到各处,远至腓尼基塞浦路斯安提阿,他们只向那里的犹太人传福音。 20不过,有些塞浦路斯古利奈的信徒到了安提阿之后,也向希腊人传讲主耶稣的福音。 21上帝的能力伴随着他们,有许多人信了主。

22耶路撒冷教会的人听到这消息后,就派巴拿巴安提阿23他到达后,看见上帝所赐的恩典,就万分高兴,劝勉他们要全心地忠于主。

24巴拿巴是个被圣灵充满、信心坚定的好人。那时信主的人大大增加。 25他又到大数去找扫罗26找到后,便带他回安提阿。他们在教会待了一年之久,教导了许多人。门徒被称为“基督徒”就是从安提阿开始的。

27当时,有几位先知从耶路撒冷下到安提阿28其中一位名叫亚迦布,他得到圣灵的启示,站起来预言天下将有严重的饥荒。后来,这事果然在克劳狄执政期间发生了。 29门徒决定各尽所能,捐款救济住在犹太境内的弟兄姊妹。 30他们捐完后,委托巴拿巴扫罗将款项送交耶路撒冷教会的长老。