Marko 14 – NEN & CRO

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Marko 14:1-72

Shauri La Kumuua Yesu

(Mathayo 26:1-5; Luka 22:1-2; Yohana 11:45-53)

114:1 Yn 11:55; 13:1; Mt 12:14; 26:1-5; Lk 22:1-2Zilikuwa zimebaki siku mbili tu kabla ya Sikukuu ya Pasaka, na Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walikuwa wakitafuta njia ya kumkamata Yesu kwa hila na kumuua. 214:2 Mt 26:1-5; Lk 22:1-2Lakini walisema, “Tusilifanye jambo hili wakati wa Sikukuu, maana watu wanaweza wakafanya ghasia.”

Yesu Kupakwa Mafuta Huko Bethania

(Mathayo 26:6-13; Yohana 12:1-8)

314:3 Mt 21:17; Lk 7:37-39Yesu alikuwa Bethania nyumbani kwa Simoni aliyekuwa na ukoma. Wakati alipokuwa ameketi mezani akila chakula cha jioni, mwanamke mmoja aliingia akiwa na chupa ya marhamu yenye manukato ya nardo14:3 Nardo ni aina ya manukato yaliyotengenezwa kutokana na mimea yenye mizizi inayotoa harufu nzuri. safi ya thamani kubwa. Akaivunja hiyo chupa, akamiminia hayo manukato kichwani mwa Yesu.

4Baadhi ya watu waliokuwepo pale walikuwa wakisemezana wao kwa wao, “Upotevu huu wote ni wa nini? 5Mafuta haya yangeweza kuuzwa kwa zaidi ya dinari14:5 Dinari 300 ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku 300. 300, na fedha hizo wakapewa maskini.” Wakamkemea vikali huyo mwanamke.

6Lakini Yesu akawaambia, “Mbona mnamsumbua huyu mwanamke? Mwacheni! Yeye amenitendea jambo zuri sana. 714:7 Kum 15:11Maskini mtakuwa nao siku zote na mnaweza kuwasaidia wakati wowote mnaotaka. Lakini mimi hamtakuwa nami siku zote. 814:8 Yn 19:40Huyu mwanamke amenitendea lile aliloweza. Ameumiminia mwili wangu manukato ili kuniandaa kwa maziko yangu. 914:9 Mt 24:14; Mk 16:15Amin, nawaambia, mahali popote ulimwenguni ambapo Injili itahubiriwa, jambo hili alilolitenda huyu mwanamke litatajwa pia kwa ukumbusho wake.”

Yuda Akubali Kumsaliti Yesu

(Mathayo 26:14-16; Luka 22:3-6)

1014:10 Mk 3:16-19; Mt 10:4; 26:14-16; Lk 23:3-6Kisha Yuda Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi kumi na wawili, akaenda kwa viongozi wa makuhani ili kumsaliti Yesu kwao. 1114:11 Mt 26:14-16; Lk 22:3-6Walifurahi sana kusikia jambo hili na wakaahidi kumpa fedha. Hivyo yeye akawa anatafuta wakati uliofaa wa kumsaliti.

Yesu Ala Pasaka Na Wanafunzi Wake

(Mathayo 26:17-25; Luka 22:7-14, 21-23; Yohana 13:21-30)

1214:12 Kum 16:1-4; 1Kor 5:714:12 Mt 26:17-19; 22:7-13Siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, siku ambayo kwa desturi mwana-kondoo wa Pasaka huchinjwa, wanafunzi wa Yesu wakamuuliza, “Unataka twende wapi ili tukuandalie mahali pa kula Pasaka?”

1314:13 Mt 26:17-19; 22:7-13Basi akawatuma wawili miongoni mwa wanafunzi wake, akawaambia, “Nendeni mjini. Huko mtakutana na mwanaume amebeba mtungi wa maji. Mfuateni. 1414:14 Mt 26:17-19; 22:7-13Mwambieni mwenye nyumba ile atakayoingia, ‘Mwalimu anauliza: Kiko wapi chumba changu cha wageni, ambamo mimi na wanafunzi wangu tutakula Pasaka?’ 1514:15 Mdo 1:13; Mt 26:17-19; 22:7-19Atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani, kilichopambwa tena kilicho tayari. Tuandalieni humo.”

1614:16 Mt 26:17-19; 22:7-19Wale wanafunzi wakaondoka na kwenda mjini, nao wakakuta kila kitu kama Yesu alivyowaambia. Hivyo wakaiandaa Pasaka.

1714:17 Mt 26:20Ilipofika jioni, Yesu akaja pamoja na wale wanafunzi wake kumi na wawili. 1814:18 Za 41:10Walipoketi mezani wakila, Yesu akawaambia, “Amin, nawaambia, mmoja wenu atanisaliti, mmoja anayekula pamoja nami.”

19Wakaanza kuhuzunika na kumuuliza mmoja baada ya mwingine, “Je, ni mimi Bwana?”

2014:20 Yn 13:18-27Akawajibu, “Ni mmoja miongoni mwenu ninyi kumi na wawili, yule anayechovya mkate kwenye bakuli pamoja nami. 2114:21 Mt 8:20Mwana wa Adamu anaenda zake kama vile alivyoandikiwa. Lakini ole wake mtu yule amsalitiye Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu huyo kama hangezaliwa.”

Kuanzishwa Kwa Meza Ya Bwana

(Mathayo 26:26-30; Luka 22:14-20; 1 Wakorintho 11:23-25)

2214:22 Mt 14:22Walipokuwa wanakula, Yesu akachukua mkate, akashukuru, akaumega na kuwapa wanafunzi wake, akisema, “Twaeni mle; huu ndio mwili wangu.”

2314:23 1Kor 10:16Kisha akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, nao wote wakanywa kutoka humo.

2414:24 Mt 26:28Akawaambia, “Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi. 2514:25 Mt 3:2Amin, nawaambia, sitakunywa tena katika uzao wa mzabibu, hadi siku ile nitakapounywa mpya katika Ufalme wa Mungu.”

2614:26 Mt 21:1Walipokwisha kuimba wimbo, wakatoka wakaenda Mlima wa Mizeituni.

Yesu Atabiri Kuwa Petro Atamkana

(Mathayo 26:31-35; Luka 22:31-34; Yohana 13:36-38)

2714:27 Zek 13:7Yesu akawaambia, “Ninyi nyote mtaniacha, kwa maana imeandikwa:

“ ‘Nitampiga mchungaji,

nao kondoo watatawanyika.’

2814:28 Mk 16:7Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya.”

2914:29 Mt 26:33-34; Lk 22:33, 34; Yn 13:37, 38Petro akasema, “Hata kama wengine wote watakuacha, mimi sitakuacha.”

3014:30 Lk 22:34; Yn 13:38Yesu akamwambia, “Amin, nakuambia; leo, usiku huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, wewe mwenyewe utanikana mara tatu.”

3114:31 Lk 22:33; Yn 13:37Lakini Petro akasisitiza zaidi, “Hata kama itabidi kufa pamoja nawe, sitakukana kamwe.” Nao wale wengine wote wakasema vivyo hivyo.

Yesu Aomba Katika Bustani Ya Gethsemane

(Mathayo 26:36-46; Luka 22:39-46)

3214:32 Mt 26:36; Lk 22:29; Yn 13:37Wakaenda mahali paitwapo Gethsemane. Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kaeni hapa, nami niende nikaombe.” 33Kisha akawachukua pamoja naye Petro, Yakobo na Yohana. Akaanza kuhuzunika sana na kutaabika. 3414:34 Yn 12:27Akawaambia, “Moyo wangu umejawa na huzuni kiasi cha kufa. Kaeni hapa na mkeshe.”

3514:35 Mk 14:41; Mt 26:18Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akaomba kwamba kama ingewezekana saa hiyo ya mateso imwondokee. 3614:36 Rum 8:15; Gal 4:6; Mt 20:22; 26:39Akasema, “Abba,14:36 Abba ni neno la Kiaramu ambalo maana yake ni Baba; ni mtoto wa kuzaa tu angeweza kulitumia kwa baba yake. Baba, mambo yote yawezekana kwako. Niondolee kikombe hiki. Lakini si kama nipendavyo mimi, bali vile upendavyo wewe.”

37Akarudi kwa wanafunzi wake, akawakuta wamelala. Akamwambia Petro, “Simoni, umelala? Je, hukuweza kukesha hata kwa saa moja? 3814:38 Mt 6:13; Rum 7:22-23Kesheni na mwombe, msije mkaingia majaribuni. Roho iko radhi, lakini mwili ni mdhaifu.”

39Akaenda tena kuomba, akisema maneno yale yale. 40Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. Nao hawakujua la kumwambia.

4114:41 Mt 26:18Akaja mara ya tatu, akawaambia, “Bado mmelala na kupumzika? Imetosha! Saa imewadia. Tazameni, Mwana wa Adamu anasalitiwa na kutiwa mikononi mwa wenye dhambi. 4214:42 Mt 26:46; Yn 18:1, 2Inukeni, twende zetu! Tazameni, msaliti wangu yuaja!”

Yesu Akamatwa

(Mathayo 26:47-56; Luka 22:47-53; Yohana 18:3-12)

4314:43 Mt 10:4Yesu alipokuwa bado anazungumza, Yuda, mmoja wa wale wanafunzi Kumi na Wawili, akatokea. Alikuwa amefuatana na umati wa watu wenye panga na marungu, waliokuwa wametumwa na viongozi wa makuhani, walimu wa sheria, na wazee.

44Basi msaliti alikuwa amewapa hao watu ishara, kwamba: “Yule nitakayembusu ndiye. Mkamateni, mkamchukue chini ya ulinzi.” 4514:45 Mt 23:7Mara Yuda akamjia Yesu na kusema, “Rabi.”14:45 Rabi ni neno la Kiebrania ambalo maana yake ni daktari, mwalimu au bwana. Walikuwa na madaraja matatu: La chini kabisa Rab (bwana), la pili Rabi (bwana wangu), na la juu kabisa Raboni (mkuu wangu, bwana wangu mkuu). Akambusu. 46Wale watu wakamkamata Yesu, wakamweka chini ya ulinzi. 47Ndipo mmoja wa wale waliokuwa wamesimama karibu aliuchomoa upanga wake na kumpiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio.

4814:48 Mt 26:55; Lk 22:52Kisha Yesu akawaambia, “Mmekuja na panga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyangʼanyi? 4914:49 Mt 26:55; Isa 53:7-12Siku kwa siku nilikuwa pamoja nanyi nikifundisha Hekaluni, wala hamkunikamata. Lakini Maandiko sharti yatimie.” 5014:50 Za 88:8; Mk 14:27Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha, wakakimbia.

51Kijana mmoja, ambaye hakuwa amevaa kitu isipokuwa alijitanda nguo ya kitani, alikuwa akimfuata Yesu. Walipomkamata, 52alikimbia uchi, akaliacha vazi lake.

Yesu Mbele Ya Baraza La Wayahudi

(Mathayo 26:57-68; Luka 22:54-71; Yohana 18:13-24)

5314:53 Mt 26:57; Yn 18:13Wakampeleka Yesu kwa kuhani mkuu, nao viongozi wa makuhani wote, na wazee na walimu wa sheria wote wakakusanyika pamoja. 5414:54 Mt 26:3; Yn 18:18Petro akamfuata kwa mbali, hadi uani kwa kuhani mkuu. Huko akaketi pamoja na walinzi, akiota moto.

5514:55 Mt 5:22Viongozi wa makuhani na Baraza la Wayahudi14:55 Baraza la Wayahudi hapa ina maana ya Sanhedrin ambalo lilikuwa ndilo baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi, lililoundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu. lote wakatafuta ushahidi dhidi ya Yesu ili wapate kumuua. Lakini hawakupata jambo lolote. 56Wengi walitoa ushahidi wa uongo dhidi yake, lakini maelezo yao hayakukubaliana.

57Ndipo wengine wakasimama wakatoa ushahidi wa uongo dhidi yake, wakisema: 5814:58 Mk 15:29; Yn 2:19“Sisi tulimsikia akisema, ‘Mimi nitalibomoa Hekalu hili lililojengwa na wanadamu, na katika siku tatu nitajenga jingine ambalo halikujengwa na wanadamu.’ ” 59Lakini hata hivyo, ushahidi wao haukukubaliana.

6014:60 Mt 26:62Basi kuhani mkuu akasimama mbele yao, akamuuliza Yesu, “Je, wewe hutajibu? Ni ushahidi gani hawa watu wanauleta dhidi yako?” 6114:61 Isa 54:7; Lk 23:9; Mt 16:16; Yn 4:25-26Lakini Yesu akakaa kimya, hakusema neno lolote.

Kuhani mkuu akamuuliza tena, “Je, wewe ndiwe Kristo,14:61 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. Mwana wa Mungu Aliyebarikiwa?”

6214:62 Ufu 1:7; Dan 7:13Yesu akajibu, “Mimi ndimi. Nanyi mtamwona Mwana wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mwenye Nguvu, na akija juu ya mawingu ya mbinguni.”

6314:63 Hes 14:6; Mdo 14:14Kuhani mkuu akararua mavazi yake, akasema, “Tuna haja gani tena ya mashahidi zaidi? 6414:64 Law 24:16Ninyi mmesikia hayo makufuru. Uamuzi wenu ni gani?”

Wote wakamhukumu kwamba anastahili kifo. 6514:65 Mt 16:21Kisha baadhi ya watu wakaanza kumtemea mate; wakamfunga kitambaa machoni, wakampiga kwa ngumi na kumwambia, “Tabiri!” Walinzi wakamchukua na kumpiga makofi.

Petro Amkana Yesu

(Mathayo 26:69-75; Luka 22:56-62; Yohana 18:15-18, 25-27)

6614:66 Lk 22:55; Yn 18:16Petro alipokuwa bado yuko chini kwenye ua wa jumba la kifalme, tazama akaja mmoja wa watumishi wa kike wa kuhani mkuu. 6714:67 Mk 14:54; 1:24Alipomwona Petro akiota moto, akamtazama sana, akamwambia,

“Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu, Mnazareti.”

6814:68 Mk 14:30, 72Lakini Petro akakana, akasema, “Sijui wala sielewi unalosema.” Naye akaondoka kuelekea kwenye njia ya kuingilia.

6914:69 Mt 26:71; Lk 22:58; Yn 18:25Yule mtumishi wa kike alipomwona mahali pale, akawaambia tena wale waliokuwa wamesimama hapo, “Huyu mtu ni mmoja wao.” 7014:70 Mdo 2:7Lakini Petro akakana tena.

Baada ya muda kidogo wale waliokuwa wamesimama hapo karibu na Petro wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana wewe pia ni Mgalilaya!” 7114:71 Mk 14:30, 72Petro akaanza kujilaani na kuwaapia, “Mimi simjui huyu mtu mnayesema habari zake!”

7214:72 Mk 14:30, 68; Mt 26:75; Mk 14:50Papo hapo jogoo akawika mara ya pili. Ndipo Petro akakumbuka lile neno Yesu alikuwa amemwambia: “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Akavunjika moyo, akalia sana.

Knijga O Kristu

Marko 14:1-72

Zavjera protiv Isusa

(Mt 26:2-5; Lk 22:1-2; Iv 11:45-53)

1Bila su dva dana do Pashe i do Blagdana beskvasnih kruhova. Svećenički poglavari i pismoznanci još su čekali prigodu da Isusa na prijevaru uhvate i ubiju. 2“Nećemo na blagdanskoj svetkovini”, rekli su, “da se narod ne pobuni.”

Pomazanje u Betaniji

(Mt 26:6-13; Lk 7:37-38; Iv 12:1-8)

3Dok je Isus u međuvremenu bio u Betaniji u kući Šimuna gubavca, uđe neka žena s alabasternom posudom skupocjenoga nardova mirisnog ulja. Razbije grlo posude i izlije ulje Isusu na glavu.

4Neki se zbog toga naljute: “Čemu tako rasipati skupocjenu pomast! 5Mogla se skupo prodati,14:5 U grčkome: prodati za više od tristo denara. a novac dati siromasima.”

6Ali Isus im reče: “Pustite ju na miru! Zašto joj dodijavate? Učinila mi je dobro djelo. 7Siromaha će uvijek biti da im pomažete kad god budete htjeli, a ja neću uvijek biti s vama. 8Ona je učinila što je mogla. Unaprijed je pomazala moje tijelo za ukop. 9Zaista vam kažem, gdje god se diljem svijeta bude propovijedala Radosna vijest, spominjat će se i ovo njezino djelo, njoj na uspomenu.”

Juda pristaje izdati Isusa

(Mt 26:14-16; Lk 22:3-6)

10Tada Juda Iškariotski, jedan od Dvanaestorice, ode svećeničkim poglavarima da se dogovori kako će izdati Isusa. 11Oni se obraduju i obećaju mu dati novca. Tako Juda počne tražiti prigodu da izda Isusa.

Posljednja večera

(Mt 26:17-19; Lk 22:7-13)

12Na prvi dan Blagdana beskvasnih kruhova, kad je bio običaj žrtvovati pashalno janje, učenici upitaju Isusa: “Gdje želiš da ti pripravimo pashalnu večeru?”

13On pošalje dvojicu u Jeruzalem: “Idite u grad. Tamo ćete sresti čovjeka koji nosi vodu u vrču. Pođite za njim. 14U kući u koju uđe potražite domaćina pa mu recite: ‘Učitelj pita u kojoj sobi može blagovati pashalnu večeru sa svojim učenicima.’ 15On će vam pokazati veliku sobu na katu, posve pripremljenu. Ondje nam pripravite večeru.”

16Učenici odu u grad i nađu sve kako im je Isus rekao te ondje pripreme pashalnu večeru.

Juda pristaje izdati Isusa

(Mt 26:20-25; Lk 22:21-23)

17Uvečer Isus dođe s Dvanaestoricom. 18Dok su jeli za stolom, reče im: “Zaista vam kažem, jedan od vas koji sa mnom jedete izdat će me!”

19Oni se silno ražaloste pa ga jedan za drugim počnu pitati: “Nisam valjda ja taj?”

20On odgovori: “To je jedan od vas Dvanaestorice, koji sa mnom umače kruh u istu zdjelu. 21Jer ja, Sin Čovječji, moram umrijeti kao što piše u Svetome pismu. Ali teško onome koji izda Sina Čovječjega! Bilo bi mu bolje da se nije ni rodio!”

Posljednja večera

(1 Kor 11:23-25)

22Dok su blagovali, Isus uzme kruh, blagoslovi ga i razlomi ga i podijeli im govoreći: “Uzmite! Ovo je moje tijelo.”

23Zatim uzme čašu vina, zahvali Bogu i pruži njima. Svi su iz nje pili. 24A on im reče: “Ovo je moja krv, krv14:24 U nekim rukopisima: krv Novoga saveza. Saveza, koja se za mnoge prolijeva. 25Zaista vam kažem: Neću više piti vina14:25 U grčkome: neću piti od trsova roda. sve do onoga dana kada ću piti novo vino u Božjemu kraljevstvu.”

26Otpjevaju zatim psalme i zapute se prema Maslinskoj gori.

Isusovo proroštvo o Petru

(Mt 26:31-35; Lk 22:31-34; Iv 13:36-38)

27“Svi ćete me napustiti”, reče im Isus, “jer u Svetome pismu piše:

‘Udarit ću pastira

i ovce će se razbježati.’14:27 Zaharija 13:7.

28Ali kada uskrsnem, ići ću pred vama u Galileju.”

29Petar mu reče: “Napuste li te i svi ostali, ja te neću napustiti!”

30“Zaista ti kažem,” reče mu Isus, “još ove noći, prije nego što se pijetao drugi put oglasi, triput ćeš me se odreći.”

31“Neću!” stane ga uvjeravati Petar. “Makar morao s tobom i umrijeti, neću te se odreći!” Tako su se zaklinjali i svi ostali.

Isus se moli u Getsemaniju

(Mt 26:36-46; Lk 22:39-46)

32Dođu tako u maslinik nazvan Getsemani, a Isus reče učenicima: “Sjednite ovdje dok se ja pomolim!” 33Povede sa sobom Petra, Jakova i Ivana. Obuzmu ga tjeskoba i duboka žalost. 34Tada im reče: “Duša mi je nasmrt shrvana tugom. Ostanite ovdje i bdijte.”

35Ode malo dalje i padne ničice. Molio se da ga, ako je moguće, mimoiđe strašni trenutak koji ga čeka. 36“Abba!14:36 Na aramejskome: Oče! Oče!” molio je, “tebi je sve moguće. Otkloni ovu čašu od mene! Ipak, neka bude po tvojoj, a ne po mojoj volji.”

37Zatim se vrati trojici učenika i nađe ih spavati te reče Petru: “Šimune! Zar spavaš? Nisi mogao ni ure probdjeti? 38Ostanite budni i molite da vas ne bi svladala kušnja! Jer duh je spreman, ali je tijelo slabo.”

39Ode još jedanput i pomoli se istim riječima. 40I opet ih po povratku nađe spavati jer su im oči otežale. Nisu znali što bi mu rekli.

41Kad se treći put vratio, reče im: “Još spavate i odmarate se? Dosta je bilo! Kucnuo je čas! Ja, Sin Čovječji, predan sam grešnicima u ruke. 42Ustanite! Hajdemo! Evo, moj je izdajnik već tu!”

Isusovo uhićenje

(Mt 26:47-56; Lk 22:47-53; Iv 18:3-11)

43Upravo tada stigne Juda, jedan od Dvanaestorice, a s njime i svjetina naoružana mačevima i toljagama, koju su poslali svećenički poglavari, pismoznanci i drugi starješine. 44Izdajica im je dao znak: “To je onaj kojega poljubim. Uhvatite ga i odvedite pod stražom.”

45On odmah priđe Isusu i reče: “Učitelju!14:45 U grčkome: Rabbi!” i poljubi ga. 46Zatim podignu ruke na Isusa i uhvate ga. 47Jedan od nazočnih nato izvuče mač i njime odsiječe uho sluzi velikoga svećenika.

48Isus reče: “Pošli ste na mene mačevima i toljagama kao na prevratnika! 49A svaki dan sam u Hramu poučavao, pa me ipak niste uhvatili. Ali sve se ovo događa zato da bi se ispunilo ono što o meni piše u Pismu.”

50Nato ga svi učenici napuste i pobjegnu. 51Slijedio ga je samo neki mladić u noćnoj košulji od gruba platna na golom tijelu. Kad su ga pokušali uhvatiti, 52on ostavi košulju koju su mu strgnuli i gol pobjegne od njih.

Isus pred Velikim vijećem

(Mt 26:57-68; Lk 22:54-55, 63-71; Iv 18:12-13, 19-24)

53Isusa odvedu velikomu svećeniku i se ubrzo okupe ostali svećenički poglavari, pismoznanci i starješine. 54Petar ga je izdaleka slijedio i ušao u dvorište palače velikog svećenika. Sjeo je sa slugama uz vatru da se zagrije.

55Unutra su svećenički poglavari i cijelo Veliko vijeće tražili svjedočanstvo protiv Isusa na temelju kojega bi ga mogli smaknuti. Ali nisu ga mogli pronaći. 56Mnogi su lažno svjedočili, ali im se iskazi nisu podudarali. 57Zatim su neki o njemu lagali: 58“Čuli smo ga kad je rekao: ‘Srušit ću ovaj Hram izgrađen ljudskim rukama i za tri dana ću izgraditi drugi, bez ljudskih ruku!’” 59Ali ni tada im se svjedočanstvo nije podudaralo.

60Veliki svećenik zatim stane pred sud i upita Isusa: “Zar ništa ne odgovaraš na ove optužbe protiv tebe?” 61Isus ne odgovori. Tada ga veliki svećenik upita: “Jesi li ti Mesija, Sin Preslavnoga Boga?”

62Isus odgovori: “Jesam. I gledat ćete Sina Čovječjega kako sjedi zdesna Svemogućemu i kako dolazi na nebeskim oblacima.”

63Nato veliki svećenik razdere svoju odjeću i reče: “Što će nam još svjedoci? 64Čuli ste ga kako huli! Što kažete?” I svi ga osude na smrt.

65Neki počnu pljuvati po njemu. Pokrili su mu oči i onda ga udarali šakama rugajući se: “Pogodi tko te udario, proroče!” Čak su ga i sluge udarali.

Petar se odriče Isusa

(Mt 26:69-75; Lk 22:54-62; Iv 18:15-18, 25-27)

66Dok je Petar bio u dvorištu, dođe sluškinja velikog svećenika. 67Kad ugleda Petra da se grije pokraj vatre, pobliže ga promotri i reče: “I ti si bio s Isusom Nazarećaninom!”

68Petar zaniječe: “Niti znam niti razumijem o čemu govoriš!” I iziđe u predvorje. Upravo tada zakukuriče pijetao.

69Sluškinja ga opazi da ondje stoji pa opet počne govoriti ostalima: “Onaj je čovjek jedan od njih!” 70Petar ponovno zaniječe.

Poslije i ostali koji su se ondje našli počnu Petru govoriti: “Pa ti si doista jedan od njih, a i Galilejac si!”

71Petar se stane kleti i zaklinjati: “Ja i ne poznajem tog čovjeka o kojemu vi govorite!” 72I pijetao odmah drugi put zakukuriče. Petar se tada sjeti što mu je Isus rekao: “Prije nego što se pijetao drugi put oglasi, triput ćeš me se odreći.” I brizne u plač.