Marko 12 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Marko 12:1-44

Mfano Wa Wapangaji Waovu

(Mathayo 21:33-46; Luka 20:9-19)

112:1 Isa 5:17Yesu akaanza kusema nao kwa mifano, akawaambia: “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu. Akajenga ukuta kulizunguka, akachimba shimo ndani yake kwa ajili ya shinikizo la kusindika divai, na akajenga mnara wa ulinzi. Kisha akalikodisha shamba hilo la mizabibu kwa wakulima fulani, kisha akasafiri kwenda nchi nyingine. 2Wakati wa mavuno ulipofika, mwenye shamba akamtuma mtumishi wake kwa hao wapangaji ili kuchukua sehemu yake ya mavuno ya shamba la mizabibu kutoka kwa hao wapangaji. 3Lakini wale wakulima walimkamata yule mtumishi, wakampiga, wakamfukuza mikono mitupu. 4Kisha yule mwenye shamba akamtuma mtumishi mwingine kwao; nao wale wakulima wakampiga kichwani na kumfanyia mambo ya aibu. 5Kisha akamtuma mtumishi mwingine, naye huyo wakamuua. Akawatuma wengine wengi; baadhi yao wakawapiga, na wengine wakawaua.

612:6 Ebr 1:1-3“Mwenye shamba alikuwa bado na mmoja wa kumtuma, mwanawe aliyempenda. Hatimaye akamtuma akisema, ‘Watamheshimu mwanangu.’

7“Lakini wale wapangaji wakasemezana pamoja, ‘Huyu ndiye mrithi. Njooni tumuue, nao urithi utakuwa wetu.’ 812:8 Ebr 13:12Hivyo wakamchukua na kumuua, wakamtupa nje ya lile shamba la mizabibu.

9“Sasa basi yule mwenye shamba atafanya nini? Atakuja na kuwaua hao wapangaji, kisha atawapa wapangaji wengine hilo shamba la mizabibu. 1012:10 Mdo 4:11Je, hamjasoma Andiko hili:

“ ‘Jiwe walilolikataa waashi

limekuwa jiwe kuu la pembeni;

1112:11 Za 119:22-23Bwana ndiye alitenda jambo hili,

nalo ni ajabu machoni petu’?”

1212:12 Mk 11:18; Mt 22:22Walipotambua kuwa amesema mfano huo kwa ajili yao, wakataka kumkamata, lakini wakaogopa ule umati wa watu. Wakamwacha, wakaondoka, wakaenda zao.

Swali Kuhusu Kulipa Kodi

(Mathayo 22:15-22; Luka 20:20-26)

1312:13 Mt 22:16; Mk 3:6; Mt 12:10Baadaye wakawatuma baadhi ya Mafarisayo na Maherode ili kwenda kumtega Yesu katika yale anayosema. 14Wakamjia, wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwadilifu. Wewe huyumbishwi na wanadamu, kwa kuwa huna upendeleo. Lakini wewe huifundisha njia ya Mungu katika kweli. Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la? 15Je, tulipe kodi au tusilipe?”

Lakini Yesu alijua unafiki wao. Akawauliza “Mbona mnajaribu kunitega? Nileteeni hiyo dinari12:15 Dinari moja ilikuwa sawa na mshahara wa kibarua wa siku moja. niione.” 16Wakamletea hiyo sarafu. Naye akawauliza, “Sura hii ni ya nani? Na maandishi haya ni ya nani?”

Wakamjibu, “Ni vya Kaisari.”

1712:17 Rum 13:7Ndipo Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, naye Mungu mpeni kilicho cha Mungu.”

Nao wakamstaajabia sana.

Ndoa Wakati Wa Ufufuo

(Mathayo 22:23-33; Luka 20:27-40)

1812:18 Mdo 4:1; 23:8; 1Kor 15:12Kisha Masadukayo, wale wasemao kuwa hakuna ufufuo wa wafu, wakamjia Yesu, 1912:19 Kum 25:5wakasema, “Mwalimu, Mose alituandikia kuwa kama ndugu wa mtu akifa na kumwacha mkewe bila mtoto, basi huyo mtu inampasa amwoe huyo mjane ili amzalie ndugu yake watoto. 20Basi palikuwepo ndugu saba. Yule wa kwanza akaoa mke, naye akafa pasipo kuwa na mtoto yeyote. 21Wa pili akamwoa yule mjane, lakini naye akafa bila kuacha mtoto yeyote. Ikawa vivyo hivyo kwa yule wa tatu. 22Hakuna hata mmojawapo wa hao ndugu wote saba aliyeacha mtoto. Hatimaye yule mwanamke naye akafa. 23Kwa hiyo wakati wa ufufuo, yeye atakuwa mke wa nani, maana aliolewa na ndugu wote saba?”

2412:24 2Tim 3:15-17Yesu akawajibu, “Je, hampotoki kwa sababu hamfahamu Maandiko wala uweza wa Mungu? 2512:25 1Kor 15:42, 49, 52Wafu watakapofufuka, hawataoa wala kuolewa, bali watakuwa kama malaika wa mbinguni. 2612:26 Kut 3:6Basi kuhusu wafu kufufuliwa, je hamjasoma katika Kitabu cha Mose jinsi Mungu alivyosema na Mose kutoka kile kichaka akisema, ‘Mimi ni Mungu wa Abrahamu, na Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo?’ 27Yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai. Kwa hiyo mmekosea kabisa.”

Amri Iliyo Kuu

(Mathayo 22:34-40; Luka 10:25-28)

2812:28 Lk 10:25-28; 20:39Mwalimu mmoja wa sheria akaja, akawasikia wakijadiliana. Akiona kwamba Yesu amewajibu vyema, naye akamuuliza, “Katika amri zote, ni ipi iliyo kuu?”

2912:29 Kum 6:4; Lk 10:27Yesu akajibu, “Amri iliyo kuu ndiyo hii: ‘Sikia ee Israeli. Bwana Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. 3012:30 Kum 6:4-5Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.’ 3112:31 Law 19:18; Mt 5:43Ya pili ndiyo hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.”

3212:32 Kum 4:35-39; Isa 46:9Yule mwalimu wa sheria akamwambia Yesu, “Mwalimu, umejibu vyema kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye. 3312:33 Hes 6:6; Ebr 10:8Kumpenda Mungu kwa moyo wote na kwa akili zote na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama mtu anavyojipenda mwenyewe ni bora zaidi kuliko kutoa sadaka za kuteketezwa na dhabihu zote.”

3412:34 Mt 3:2; 22:46; Lk 20:40Yesu alipoona kwamba amejibu kwa busara, akamwambia, “Wewe hauko mbali na Ufalme wa Mungu.” Tangu wakati huo, hakuna mtu yeyote aliyethubutu kumuuliza maswali tena.

Kristo Ni Mwana Wa Nani?

(Mathayo 22:41-46; Luka 20:41-44)

3512:35 Mt 26:55; 9:27Yesu alipokuwa akifundisha Hekaluni, akauliza, “Imekuwaje walimu wa sheria wanasema kwamba Kristo12:35 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. ni Mwana wa Daudi? 3612:36 2Sam 23:2; Za 110:1; Mt 22:24Kwa maana Daudi mwenyewe, akinena kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu, alisema:

“ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu:

“Keti mkono wangu wa kuume,

hadi nitakapowaweka adui zako

chini ya miguu yako.” ’

3712:37 Yn 12:9Kwa hiyo Daudi mwenyewe anamwita ‘Bwana.’ Awezaje basi yeye kuwa mwanawe?”

Ule umati wote wa watu wakamsikiliza kwa furaha.

Yesu Awatahadharisha Watu Kuhusu Walimu Wa Sheria

(Mathayo 23:1-36; Luka 20:45-47)

3812:38 Mk 4:2; Mt 23:1; Lk 20:46; 11:43Alipokuwa akifundisha, Yesu alisema, “Jihadharini na walimu wa sheria. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa kwa heshima masokoni. 3912:39 Lk 11:43Pia wao hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi, na kupewa nafasi za heshima katika karamu. 4012:40 Mt 23:14Wao hula nyumba za wajane, na ili waonekane kuwa wema wanasali sala ndefu. Watu kama hawa watapata hukumu iliyo kuu sana.”

Sadaka Ya Mjane

(Luka 21:1-4)

4112:41 2Fal 12:9; Yn 8:20Kisha Yesu akaketi mkabala na sehemu ambapo sadaka zilikuwa zinawekwa na kuangalia umati wa watu wakiweka fedha zao kwenye sanduku la hazina ya Hekalu. Matajiri wengi wakaweka kiasi kikubwa cha fedha. 42Lakini mjane mmoja maskini akaja na kuweka sarafu mbili ndogo za shaba zenye thamani ya senti mbili.

4312:43 2Kor 8:12 Yesu akawaita wanafunzi wake, akawaambia, “Amin, nawaambia, huyu mjane maskini ameweka katika sanduku la hazina zaidi ya watu wengine wote. 4412:44 2Kor 8:12Wengine wote wametoa kutokana na ziada ya mali zao. Lakini huyu mjane ametoa kutokana na umaskini wake, akaweka kila kitu alichokuwa nacho, hata kile alichohitaji ili kuishi.”

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

馬可福音 12:1-44

兇狠的佃戶

1耶穌用比喻對他們說:「有人開闢了一個葡萄園,在四周築起籬笆,又在園中挖了一個榨酒池,建了一座瞭望臺,然後把葡萄園租給佃戶,就出遠門了。

2「到葡萄成熟時,園主派一個奴僕去收取他該得的一份。 3那些佃戶卻捉住那個奴僕,打了他一頓,使他空手而歸。

4「園主又差另一個奴僕去。這一次,佃戶不但侮辱他,還把他打得頭破血流。 5園主再派一個奴僕前往,他們卻把他殺掉了。園主後來派去的人不是挨打,就是被殺。 6最後只剩下園主的愛子,園主就派他去,以為那些佃戶會尊重他的兒子。 7這班佃戶卻彼此商量說,『這個就是園主的繼承人。來吧!我們殺掉他,產業就歸我們了。』

8「於是他們抓住他,殺了他,把他拋到葡萄園外。 9那麼,園主會採取什麼行動呢?他必定會來殺掉這些佃戶,把葡萄園轉給別人。 10聖經上說,

『工匠丟棄的石頭已成了房角石。

11這是主的作為,

在我們看來奇妙莫測。』

你們沒有讀過這經文嗎?」

12他們聽出這比喻是針對他們說的,就想逮捕耶穌,但又害怕百姓,只好先離開了。

納稅給凱撒的問題

13後來,他們派了幾個法利賽人和希律黨人到耶穌那裡,企圖利用祂所說的話設計陷害祂。

14他們上前對耶穌說:「老師,我們知道你誠實無偽,不看人的情面,因為你不以貌取人,而是按真理傳上帝的道。那麼,向凱撒納稅對不對呢? 15我們該不該納呢?」耶穌看破他們的陰謀,就說:「你們為什麼試探我呢?拿一個銀幣來給我看。」

16他們就拿來一個銀幣,耶穌問他們:「上面刻的是誰的像和名號?」

他們說:「凱撒的。」

17耶穌說:「屬於凱撒的東西應該給凱撒,屬於上帝的東西應該給上帝。」

他們聽了這話,都很驚奇。

論復活

18撒都該人向來不相信有復活的事,他們來問耶穌: 19「老師,摩西為我們寫下律例,如果一個人死了,遺下妻子,又沒有兒女,他的兄弟就當娶嫂嫂,替哥哥傳宗接代。 20有弟兄七人,老大結了婚,沒有孩子就死了。 21二弟把大嫂娶過來,也沒有生孩子就死了,三弟也是一樣, 22七個人都沒有留下孩子。最後,那女人也死了。 23那麼,到復活的時候,她將是誰的妻子呢?因為七個人都娶過她。」

24耶穌說:「你們弄錯了,因為你們不明白聖經,也不知道上帝的能力。 25死人復活之後,將不娶也不嫁,就像天上的天使一樣。 26關於死人復活的事,你們沒有讀過摩西書有關火中荊棘的記載嗎?上帝對摩西說,『我是亞伯拉罕的上帝,以撒的上帝,雅各的上帝。』 27上帝不是死人的上帝,而是活人的上帝。你們大錯了!」

最大的誡命

28有一位律法教師聽到他們的辯論,覺得耶穌的回答很精彩,就走過去問道:「誡命中哪一條最重要呢?」

29耶穌回答道:「最重要的誡命是,『聽啊,以色列!主——我們的上帝是獨一的主。 30你要全心、全情、全意、全力愛主——你的上帝』; 31其次就是『要愛鄰如己』。再也沒有任何誡命比這兩條更重要了。」

32那位律法教師說:「老師,你說得對,上帝只有一位,除祂以外,別無他神。 33我們要全心、全意、全力愛祂,又要愛鄰如己。這樣做比獻什麼祭都好。」

34耶穌見他答得很有智慧,就告訴他:「你離上帝的國不遠了。」此後,沒人再敢問耶穌問題了。

基督的身分

35耶穌在聖殿裡教導的時候,問道:「律法教師為什麼說基督是大衛的後裔呢? 36大衛自己曾經受聖靈的感動,說,

『主對我主說,

你坐在我的右邊,

等我使你的仇敵伏在你腳下。』

37既然大衛自己稱基督為主,基督又怎能是大衛的後裔呢?」百姓聽得津津有味。 38耶穌又教導他們,說:「你們要提防律法教師,他們愛穿著長袍招搖過市,喜歡人們在大街上問候他們, 39又喜歡會堂裡的上座和宴席中的首位。 40他們侵吞寡婦的財產,還假意做冗長的禱告。這種人必受到更嚴厲的懲罰。」

窮寡婦的奉獻

41然後,耶穌走到聖殿的奉獻箱對面坐下,看大家怎樣奉獻。很多財主奉獻了大量的錢。 42後來一個窮寡婦來了,投進了相當於一文錢的兩個小銅錢。 43耶穌叫門徒來,說:「我實在告訴你們,這位窮寡婦比其他人奉獻的都多, 44因為他們不過奉獻了自己剩餘的,但這窮寡婦卻奉獻了她賴以為生的。」