Maombolezo 4 – NEN & HTB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Maombolezo 4:1-22

4 Sura hii imetungwa kila beti likianzia, na pia kila mstari katika lile beti, na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22. 14:1 Eze 7:19Jinsi dhahabu ilivyopoteza mngʼao wake,

dhahabu iliyo safi haingʼai!

Vito vya thamani vimetawanywa

kwenye mwanzo wa kila barabara.

24:2 Isa 51:18; 2Kor 4:7Wana wa Sayuni wenye thamani,

ambao mwanzo uzito wa thamani yao

ulikuwa wa dhahabu,

sasa wanaangaliwa kama vyungu vya udongo,

kazi ya mikono ya mfinyanzi!

34:3 Ay 39:14-16Hata mbweha hutoa matiti yao

kunyonyesha watoto wao,

lakini watu wangu wamekuwa wasio na huruma

kama mbuni jangwani.

44:4 Mao 2:11-12; Za 22:15; 2Fal 18:31; Kum 28:48Kwa sababu ya kiu ulimi wa mtoto mchanga

umegandamana na kaakaa la kinywa chake,

watoto huomba mkate,

lakini hakuna yeyote awapaye.

54:5 Yer 6:2; Isa 3:26; Amo 6:3-7; Ay 24:8; Lk 15:16Wale waliokula vyakula vya kifahari

ni maskini barabarani.

Wale waliokuzwa wakivaa nguo za zambarau

sasa wanalalia majivu.

64:6 Mwa 19:25Adhabu ya watu wangu

ni kubwa kuliko ile ya Sodoma,

ambayo ilipinduliwa ghafula

bila kuwepo mkono wa msaada.

7Wakuu wao walikuwa wamengʼaa kuliko theluji

na weupe kuliko maziwa,

miili yao ilikuwa myekundu kuliko marijani,

kuonekana kwao kama yakuti samawi.

84:8 Ay 30:28; Za 102:3-5; Mao 3:4Lakini sasa ni weusi kuliko masizi;

hawatambulikani barabarani.

Ngozi yao imeshikamana juu ya mifupa yao,

imekuwa mikavu kama fimbo.

94:9 Yer 15:2; 16:4; 2Fal 25:3; Mao 5:10Wale waliouawa kwa upanga ni bora

kuliko wale wanaokufa njaa;

wanateseka kwa njaa, wanatokomea

kwa kukosa chakula kutoka shambani.

104:10 Mao 2:20; Law 26:29; Kum 28:53-57; Eze 5:10; Yer 19:9Kwa mikono yao wenyewe wanawake wenye huruma

wanapika watoto wao wenyewe,

waliokuwa chakula chao

watu wangu walipoangamizwa.

114:11 Yer 17:27; Kum 32:22; Yer 7:20; Ay 20:23; 2Nya 34:21; Eze 22:31Bwana ametoa nafasi kamilifu ya ghadhabu yake;

ameimwaga hasira yake kali.

Amewasha moto katika Sayuni

ambao umeteketeza misingi yake.

124:12 1Fal 9:9; Yer 21:13; Kum 29:24Wafalme wa dunia hawakuamini,

wala mtu yeyote wa duniani,

kwamba adui na watesi wangeweza kuingia

kwenye malango ya Yerusalemu.

134:13 Yer 5:31; Eze 22:28; Mik 3:11; 2Fal 21:16; Mt 23:31Lakini hili lilitokea kwa sababu ya dhambi za manabii wake,

na maovu ya makuhani wake,

waliomwaga ndani yake

damu ya wenye haki.

144:14 Isa 59:10; Yer 2:34; 19:4Sasa wanapapasa papasa barabarani

kama watu ambao ni vipofu.

Wamenajisiwa kabisa kwa damu,

hata hakuna anayethubutu kugusa mavazi yao.

154:15 Yer 44:14; Law 13:46; Mik 2:10Watu wanawapigia kelele, “Ondokeni! Ninyi ni najisi!

Ondokeni! Ondokeni! Msituguse!”

Wanapokimbia na kutangatanga huku na huko,

watu miongoni mwa mataifa wanasema,

“Hawawezi kukaa hapa zaidi.”

164:16 Isa 9:14-16; Mao 5:12Bwana mwenyewe amewatawanya;

hawaangalii tena.

Makuhani hawaonyeshwi heshima,

wazee hawakubaliki.

174:17 Mwa 15:18; Eze 29:16; Yer 37:7; Isa 20:5-6; 2Fal 24:7Zaidi ya hayo, macho yetu yalichoka,

kwa kutazamia bure msaada;

tuliangalia kutoka minara yetu

kwa taifa lisiloweza kutuokoa.

184:18 Eze 7:2-12; Amo 8:2; Yer 51:33; 2Fal 25:4; Yer 51:33Watu walituvizia katika kila hatua

hata hatukuweza kutembea katika barabara zetu.

Mwisho wetu ulikuwa karibu, siku zetu zilikuwa zimetimia,

kwa maana mwisho wetu ulikuwa umefika.

194:19 Kum 28:49; Law 26:36; Isa 5:26-28; Yer 52:7Waliotufuatia walikuwa wepesi

kuliko tai angani;

walitusaka juu milimani

na kutuvizia jangwani.

204:20 1Sam 26:9; 2Sam 19:21; Yer 39:5; Eze 19:4-8; 12:12-13; Mwa 2:7; Yer 52:9Mpakwa mafuta wa Bwana, pumzi ya uhai wetu hasa,

alinaswa katika mitego yao.

Tulifikiri kwamba chini ya kivuli chake

tungeliweza kuishi miongoni mwa mataifa.

214:21 Za 16:5; Yer 25:15; Eze 35:15; Hab 2:16; Mwa 10:23; Isa 34:6-10; Amu 1:11Shangilia na ufurahi, ee Binti Edomu,

wewe unayeishi nchi ya Usi.

Lakini kwako pia kikombe kitapitishwa,

Utalewa na kuvuliwa nguo ubaki uchi.

224:22 Isa 40:2; Yer 33:8; Eze 25:12-14; Mal 1:4; Za 137:7Ee Binti Sayuni, adhabu yako itaisha,

hatarefusha muda wako wa kukaa uhamishoni.

Lakini, ee Binti Edomu, ataadhibu dhambi yako,

na atafunua uovu wako.

Het Boek

Klaagliederen 4:1-22

De zonde van het volk en de toorn van God

1Ach, hoe heeft het goud zijn glans verloren, hoe dof is het geworden, de edelstenen van de tempel liggen verstrooid in de straten!

2De jongeren van Jeruzalem, ieder hun gewicht in goud waard, zijn behandeld als aardewerken potten, als het werk van mensenhanden!

3Zelfs de jakhalzen voeden hun jongen, maar mijn volk Israël doet dat niet. Zij lijken op wrede struisvogels uit de woestijn, die geen acht slaan op de kreten van hun jongen.

4De tongen van de babyʼs plakken aan hun gehemelte, want er is geen druppel water overgebleven. Kinderen schreeuwen om brood, maar niemand kan hun iets geven.

5Mensen die vroeger lekkernijen aten, zitten nu op straat te bedelen om maar iets te kunnen eten. Zij die in paleizen werden grootgebracht, grabbelen nu in de vuilnis op zoek naar voedsel.

6Want de zonde van mijn volk is groter dan die van Sodom, waar zich in één ogenblik een vreselijke ramp voltrok, waaraan geen mensenhand te pas kwam.

7Onze prinsen waren smetteloos en witter dan melk, de mooiste mannen die er waren.

8Maar nu zijn hun gezichten zo zwart als roet. Niemand herkent hen nog. Hun huid kleeft aan hun botten: hard, droog en verweerd.

9Die met het zwaard werden gedood, zijn beter af dan zij die een langzame hongerdood moeten sterven.

10Gevoelige vrouwen hebben zelfs hun eigen kinderen gekookt en opgegeten, op die manier overleefden zij het beleg.

11Met volle kracht heeft de Here zijn toorn laten woeden, al zijn toorn kwam tot ontlading. Hij stak een vuur aan in Jeruzalem dat de stad tot op haar fundamenten in de as legde.

12Geen koning ter wereld, geen enkel volk op aarde, zou hebben geloofd dat een vijand door de poorten van Jeruzalem naar binnen kon marcheren!

13Maar toch stond God dit toe vanwege de zonden van haar profeten en priesters die de stad ontheiligden door onschuldig bloed te vergieten.

14Nu wankelen deze zelfde mannen als blinden door de straten, besmeurd met bloed zodat niemand hen durft aan te raken.

15‘Maak dat je wegkomt,’ roepen de mensen hen toe. ‘Jullie zijn onrein! Ga weg. Raak ons niet aan!’ Zij vluchten naar andere landen en dwalen daar tussen de buitenlanders, maar niemand zal hun toestaan te blijven.

16De Here heeft hen zover verspreid, Hij helpt hen niet langer, want zij onderdrukten de priesters en leiders die trouw bleven aan God.

17Wij kijken uit of onze bondgenoten al in aantocht zijn om ons te helpen, maar tevergeefs. Het volk waarop wij het meest rekenden voor hulp, doet helemaal niets.

18Als wij op straat komen, begeven wij ons in levensgevaar. Ons einde is nabij, onze dagen zijn geteld.

19Onze achtervolgers zijn sneller dan arenden, ook al vluchten wij de bergen in, dan vinden zij ons nog. Als wij ons in de wildernis willen verbergen, staan zij ons daar op te wachten.

20Onze koning—de adem van ons volksleven, de gezalfde van de Here—werd in hun valstrikken gevangen. Ja, zelfs onze machtige koning, van wie wij dachten dat wij onder zijn leiding rustig te midden van de volken zouden kunnen leven!

21Volk van Edom, vier uw feest in het land van Uz. Ook ú zult kennismaken met de vreselijke toorn van de Here.

22Eens zal een einde komen aan de ballingschap, de straf die Israël om haar zonden kreeg opgelegd, maar de zonden van Edom zullen worden blootgelegd en de Here zal dit volk oordelen.