Malaki 2 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Malaki 2:1-17

Onyo Kwa Makuhani

1“Sasa onyo hili ni kwa ajili yenu, enyi makuhani. 22:2 Kum 28:15Kama hamtasikiliza, na kama hamtaki kuielekeza mioyo yenu kuheshimu Jina langu, nitatuma laana juu yenu, nami nitalaani baraka zenu. Naam, nimekwisha kuzilaani, kwa sababu hamkuielekeza mioyo yenu kuniheshimu mimi,” Asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

3“Kwa sababu yenu nitawakatilia mbali wazao wenu. Nitazipaka nyuso zenu mavi, mavi ya dhabihu zenu. Nanyi mtafukuzwa pamoja nazo mtoke mbele zangu. 4Nanyi mtajua kuwa nimewapelekea onyo hili ili kwamba Agano langu na Lawi lipate kuendelea,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. 52:5 Hes 25:12; Kum 33:8“Agano langu lilikuwa pamoja naye, agano la uhai na amani, nami nilimpa yote, ili aniche na kuniheshimu, naye akaniheshimu na kusimama akilicha Jina langu. 62:6 Dan 12:3; Lk 1:16-17; Yak 5:20Fundisho la kweli lilikuwa kinywani mwake, wala hakuna uongo wowote uliopatikana katika midomo yake. Alitembea nami katika amani na unyofu, naye akawageuza wengi kutoka dhambini.

72:7 Kum 17:9; Isa 42:19; Hag 1:13; Gal 4:14“Kwa maana yapasa midomo ya kuhani kuhifadhi maarifa. Tena kutoka kinywani mwake watu wangepaswa kutafuta mafundisho, kwa sababu yeye ni mjumbe wa Bwana Mwenye Nguvu Zote. 82:8 1Sam 2:17Lakini mmegeuka mkaiacha njia, na kwa mafundisho yenu mmesababisha wengi kujikwaa. Mmevunja agano na Lawi,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. 9“Kwa hiyo nimewasababisha ninyi kudharauliwa na kufedheheshwa mbele ya watu wote, kwa sababu hamkufuata njia zangu, bali mmeonyesha upendeleo katika mambo ya sheria.”

Yuda Si Mwaminifu

102:10 Isa 51:2; Mt 3:9; 1Kor 8:6; Ebr 12:9; Za 100:3Je, sote hatuna Baba mmoja? Hatukuumbwa na Mungu mmoja? Kwa nini basi tunalinajisi Agano la baba zetu kwa kukosa uaminifu kila mmoja kwa mwenzake?

112:11 Neh 13:23Yuda amevunja uaminifu. Jambo la kuchukiza limetendeka katika Israeli na katika Yerusalemu: Yuda amepanajisi mahali patakatifu apendapo Bwana, kwa kuoa binti wa mungu mgeni. 12Kwa maana kwa mtu yeyote atendaye jambo hili, Bwana na amkatilie mbali kutoka hema za Yakobo, hata kama huwa anamletea Bwana Mwenye Nguvu Zote sadaka.

132:13 Yer 11:11; 14:12; Za 39:12; 66:18; Isa 58:2Kitu kingine mnachokifanya: Mnaifurikisha madhabahu ya Bwana kwa machozi. Mnalia na kuugua kwa sababu yeye haziangalii tena sadaka zenu wala hazikubali kwa furaha kutoka mikononi mwenu. 142:14 Mwa 21:30; 24:22; Mit 5:18; Ebr 13:4Mnauliza, “Kwa nini?” Ni kwa sababu Bwana ni shahidi kati yako na mke wa ujana wako, kwa sababu umevunja uaminifu naye, ingawa yeye ni mwenzako, mke wa agano lako la ndoa.

152:15 Mwa 2:24; Mt 19:4-6; Kum 14:2; 4:15; 1Kor 7:14; 7:10; Isa 54:6; Ebr 13:4Je, Bwana hakuwafanya wao kuwa mmoja? Katika mwili na katika roho wao ni wa Mungu. Kwa nini wawe mmoja? Kwa sababu Mungu alikuwa akitafuta mzao mwenye kumcha Mungu. Kwa hiyo jihadharini wenyewe katika roho zenu, mtu asivunje uaminifu kwa mke wa ujana wake.

162:16 Kum 24:1; Mt 5:31-32; 19:4-9; Isa 58:4; Mk 10:4-5; Mwa 6:11; 34:25; Mit 4:17; Za 51:10“Ninachukia kuachana,” asema Bwana, Mungu wa Israeli, “pia nachukia mtu anayejivika jeuri kama vazi,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

Kwa hiyo jihadharini wenyewe katika roho zenu, wala msije mkavunja uaminifu.

Siku Ya Hukumu

172:17 Isa 1:14; Eze 18:25; Za 5:4; Ay 8:3; Mwa 18:25Mmemchosha Bwana kwa maneno yenu.

Nanyi mnauliza, “Tumemchosha kwa namna gani?”

Mmemchosha kwa kusema, “Wote watendao mabaya ni wema machoni pa Bwana, naye anapendezwa nao” au “Mungu wa haki yuko wapi?”

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

瑪拉基書 2:1-17

1祭司們啊,這誡命是傳給你們的。 2萬軍之耶和華說:「如果你們不聽從我的話,也不從內心尊崇我的名,我必使咒詛臨到你們,把你們的福氣變成咒詛。事實上,因為你們不把我的誡命放在心上,我已經咒詛了你們。 3我必斥責你們的子孫,把你們祭牲的糞便抹在你們臉上,又把你們和糞便一同丟掉, 4你們便知道我這樣告誡你們,是為了維持我與你們祖先利未所立的約。這是萬軍之耶和華說的。 5我與他所立的是生命和平安之約,我將生命和平安賜給他,使他心存敬畏。他就尊崇我,敬畏我的名。 6他口中教導真理,嘴裡毫無詭詐。他與我同行,過著平安正直的生活,並引導許多人遠離罪惡。 7祭司的嘴唇應持守知識,人民應從他口中尋求訓誨,因為他是萬軍之耶和華的使者。 8然而,你們卻偏離正道,你們的教導使許多人跌倒,破壞了我和利未所立的約。」這是萬軍之耶和華說的。 9「因此,我必使你們在眾人面前遭藐視、輕賤。因為你們不遵守我的道,在教導上偏心待人。」

10難道我們不是出於同一位父親,由同一位上帝所造嗎?為何我們竟彼此欺騙,背棄上帝與我們祖先所立的約呢? 11猶大人不忠貞,在以色列耶路撒冷做了可憎的事,他們娶信奉外邦神明的女子為妻,褻瀆了耶和華所愛的聖所。 12願耶和華從雅各的帳篷中剷除所有做這事並獻供物給萬軍之耶和華的人!

13另外,你們哀哭悲歎,眼淚甚至淹沒了耶和華的祭壇,因為耶和華不再理會你們的供物,不再悅納你們所獻的。 14你們還問為什麼。因為耶和華在你和你的髮妻中間作證,她是你的配偶,是你盟約的妻子,你卻對她不忠。 15上帝不是把你們結合為一體,叫你們肉體和心靈都歸祂嗎2·15 此句希伯來文語意不清。?祂為何這樣做?是為了得敬虔的後裔。所以,你們要小心謹慎,不可對自己的髮妻不忠。 16以色列的上帝耶和華說:「我憎惡休妻和以暴虐待妻子的人。所以要守護你們的心,不可有不忠的行為。」這是萬軍之耶和華說的。 17你們說的話使耶和華厭煩,然而,你們還說:「我們在何事上令祂厭煩呢?」因為你們說:「耶和華將所有作惡者視為好人,並且喜悅他們」,還說:「公義的上帝在哪裡?」