Luka 9 – NEN & HHH

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Luka 9:1-62

Yesu Awatuma Wale Kumi Na Wawili

(Mathayo 10:5-15; Marko 6:7-13)

19:1 Mt 10:1; 4:23; Lk 5:17Yesu kisha akawaita wale kumi na wawili pamoja, akawapa mamlaka na uwezo wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya magonjwa yote, 29:2 Mt 3:2kisha akawatuma waende wakahubiri Ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa. 39:3 Lk 10:4; 22:35Akawaagiza akisema, “Msichukue chochote safarini: sio fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, hata msichukue kanzu ya ziada. 49:4 Mt 10:11; Mk 6:10Katika nyumba yoyote mwingiayo, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo. 59:5 Lk 10:14Kama watu wasipowakaribisha, mnapoondoka katika mji wao, kungʼuteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu ili kuwa ushuhuda dhidi yao.” 69:6 Mk 6:12Hivyo wale wanafunzi wakaondoka wakaenda kutoka kijiji hadi kijiji, wakihubiri habari njema na kuponya wagonjwa kila mahali.

Herode Afadhaika

(Mathayo 14:1-12; Marko 6:14-29)

79:7 Mt 3:1; 14:1Basi Mfalme Herode, mtawala wa Galilaya, alisikia habari za yote yaliyotendeka. Naye akafadhaika, kwa kuwa baadhi ya watu walikuwa wakisema Yohana Mbatizaji amefufuliwa kutoka kwa wafu. 89:8 Mt 11:14; Yn 1:21Wengine wakasema Eliya amewatokea, na wengine wakasema kwamba mmoja wa manabii wa kale amefufuka. 99:9 Lk 23:8Herode akasema, “Yohana nilimkata kichwa. Lakini ni nani huyu ambaye ninasikia mambo kama haya kumhusu?” Akatamani sana kumwona.

Yesu Awalisha Wanaume 5,000

(Mathayo 14:13-21; Marko 6:30-44; Yohana 6:1-14)

109:10 Mk 6:30; Mt 11:21Mitume wake waliporudi, wakamweleza Yesu yote waliyofanya. Akawachukua, akaenda nao faraghani mpaka mji uitwao Bethsaida. 119:11 Lk 9:2Lakini umati wa watu ukafahamu alikokwenda, ukamfuata. Akawakaribisha na kunena nao kuhusu Ufalme wa Mungu na kuwaponya wale wote waliokuwa wanahitaji uponyaji.

129:12 Mt 14:15; Mk 6:35; Yn 6:1, 5Ilipokaribia jioni, wale mitume kumi na wawili wakaenda kwa Yesu na kumwambia, “Waage makutano ili waende vijijini jirani na mashambani, ili wapate chakula na mahali pa kulala, kwa maana hapa tuko nyikani.”

13Yesu akawajibu, “Ninyi wapeni chakula.”

Nao wakajibu, “Hatuna zaidi ya mikate mitano na samaki wawili. Labda twende tukanunue chakula cha kuwatosha watu hawa wote.” 14Walikuwako wanaume wapatao 5,000.

Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Waketisheni katika makundi ya watu hamsini hamsini.” 15Wanafunzi wakafanya hivyo, wakawaketisha wote. 169:16 Mt 14:19Yesu akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akavibariki na kuvimega. Kisha akawapa wanafunzi ili wawagawie watu. 17Wote wakala, wakashiba. Nao wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu kumi na viwili.

Petro Amkiri Yesu Kuwa Ndiye Kristo

(Mathayo 16:13-19; Marko 8:27-29)

189:18 Lk 3:21Wakati mmoja, Yesu alipokuwa akiomba faraghani, nao wanafunzi wake wakiwa pamoja naye, akawauliza, “Watu husema mimi ni nani?”

199:19 Mt 14:2; Lk 9:7; 8Wakamjibu, “Baadhi husema wewe ni Yohana Mbatizaji, wengine husema ni Eliya, na bado wengine husema kwamba ni mmoja wa manabii wa kale amefufuka kutoka kwa wafu.”

209:20 Yn 1:49; 11:27Kisha akawauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?”

Petro akajibu, “Wewe ndiwe Kristo9:20 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. wa Mungu.”

219:21 Mt 16:20; Mk 8:30Yesu akawakataza wasimwambie mtu yeyote jambo hilo. 229:22 Mt 8:20; 16:21; 27:1-2; Mdo 2:23; 3:13Yesu akasema, “Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi na kukataliwa na wazee, viongozi wa makuhani, na walimu wa sheria, na itampasa auawe, lakini siku ya tatu kufufuliwa kutoka mauti.”

239:23 Mt 10:38; Lk 14:27Kisha akawaambia wote, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake kila siku, anifuate. 249:24 Yn 12:25Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayaokoa. 259:25 Mt 16:26; Mk 8:36Je, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akapoteza au kuangamiza nafsi yake? 269:26 2Tim 2:12; Mt 16; 27; 10:33Mtu yeyote akinionea aibu mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu naye atamwonea aibu atakapokuja katika utukufu wake na katika utukufu wa Baba, pamoja na malaika watakatifu. 279:27 Mt 16:28; Mk 9:1Amin, nawaambia, wako baadhi ya watu waliosimama hapa ambao hawataonja mauti kabla ya kuuona Ufalme wa Mungu.”

Bwana Yesu Abadilika Sura

(Mathayo 17:1-8; Marko 9:2-8)

289:28 Mt 4:21; Lk 3:21Yapata siku nane baada ya Yesu kusema hayo, aliwachukua Petro, Yakobo na Yohana, akaenda nao mlimani kuomba. 29Alipokuwa akiomba, sura ya uso wake ikabadilika, nayo mavazi yake yakametameta kama mwanga wa umeme wa radi. 30Ghafula wakawaona watu wawili, ndio Mose na Eliya, wakizungumza naye. 319:31 2Pet 1:15Walionekana katika utukufu wakizungumza na Yesu kuhusu kifo chake ambacho kingetokea huko Yerusalemu. 329:32 Mt 26:43Petro na wenzake walikuwa wamelala usingizi mzito. Walipoamka, wakaona utukufu wa Yesu na wale watu wawili waliokuwa wamesimama pamoja naye. 339:33 Lk 5:5Mose na Eliya walipokuwa wanaondoka, Petro akamwambia Yesu, “Bwana, ni vizuri tukae hapa! Tutajenga vibanda vitatu: kimoja chako, kingine cha Mose na kingine cha Eliya.” Lakini Petro alikuwa hajui asemacho.

34Alipokuwa bado anazungumza, pakatokea wingu, likawafunika, nao wakaogopa walipoingia mle kwenye wingu. 359:35 Isa 42:12; Mt 3:17Sauti ikatoka kwenye lile wingu ikisema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa, niliyemchagua. Msikieni yeye.” 369:36 Mt 17:9Baada ya sauti hiyo kusema, walimkuta Yesu akiwa peke yake. Wale wanafunzi wakalihifadhi jambo hili, wala kwa wakati huo hawakumwambia mtu yeyote yale waliyokuwa wameyaona.

Kuponywa Kwa Kijana Mwenye Pepo Mchafu

(Mathayo 17:1-8; Marko 9:2-8)

379:37 Mt 17:14; Mk 9:14, 179:37 Mt 17:14-23; Mk 9:14-32Kesho yake waliposhuka kutoka mlimani, alikutana na umati mkubwa wa watu. 38Mtu mmoja katika ule umati wa watu akapaza sauti, akasema, “Mwalimu, naomba umwangalie mwanangu, kwani ndiye mtoto wangu wa pekee. 39Mara kwa mara pepo mchafu humpagaa na kumfanya apige kelele, kisha humwangusha na kumtia kifafa hata akatokwa na povu kinywani. Huyo pepo mchafu anamtesa sana, na hamwachi ila mara chache. 40Niliwaomba wanafunzi wako wamtoe huyo pepo mchafu, lakini hawakuweza.”

419:41 Kum 32:5Yesu akawajibu, “Enyi kizazi kisichoamini na kilichopotoka! Nitakaa nanyi na kuwavumilia mpaka lini? Mlete mwanao hapa.”

429:42 Lk 7:15Hata yule mtoto alipokuwa akija, yule pepo mchafu akamwangusha, akamtia kifafa. Lakini Yesu akamkemea yule pepo mchafu amtoke, akamponya yule mtoto, na akamrudisha kwa baba yake. 43Watu wote wakastaajabia uweza mkuu wa Mungu.

Wakati bado watu walikuwa wanastaajabia hayo yote aliyokuwa akiyafanya Yesu, yeye akawaambia wanafunzi wake: 449:44 Lk 9:22; Mt 17:22“Sikilizeni kwa makini haya nitakayowaambia sasa: Mwana wa Adamu atasalitiwa na kutiwa mikononi mwa watu.” 459:45 Mk 9:32Lakini wao hawakuelewa alimaanisha nini. Maana ya maneno hayo ilifichika kwao, hivyo hawakuyaelewa, nao wakaogopa kumuuliza maana yake.

Ni Nani Atakayekuwa Mkubwa Kuliko Wote

(Mathayo 18:1-5; Marko 9:33-37)

469:46 Lk 22:24Kukazuka mabishano miongoni mwa wanafunzi kuhusu ni nani miongoni mwao atakayekuwa mkuu kuliko wote. 479:47 Mt 9:4Lakini Yesu akayatambua mawazo yao, naye akamchukua mtoto mdogo, akamsimamisha kando yake. 489:48 Mt 10:40; Mk 9:35Kisha akawaambia, “Yeyote amkaribishaye mtoto huyu mdogo kwa Jina langu, anikaribisha mimi, na yeyote atakayenikaribisha mimi, atakuwa amemkaribisha yeye aliyenituma. Kwa maana yeye aliye mdogo miongoni mwenu, ndiye aliye mkuu kuliko wote.”

499:49 Mk 9:38; Hes 11:28Yohana akasema, “Bwana, tumemwona mtu akitoa pepo wachafu kwa jina lako, nasi tukamzuia, kwa sababu yeye si mmoja wetu.”

509:50 Mt 12:30; Lk 11:23Yesu akasema, “Msimzuie, kwa sababu yeyote ambaye si kinyume nanyi, yu upande wenu.”

Yesu Akataliwa Samaria

519:51 Mk 16:19; Lk 18:31; 19:28Wakati ulipokaribia wa yeye kuchukuliwa mbinguni, alikaza uso wake kwenda Yerusalemu. 529:52 Mt 10:5Akatuma watu wamtangulie, nao wakaenda katika kijiji kimoja cha Samaria kumwandalia kila kitu; 539:53 Yn 4:9; 4:4lakini watu wa kijiji kile hawakumkaribisha kwa sababu alikuwa anakwenda zake Yerusalemu. 549:54 Mt 4:21; 2Fal 10:12Wanafunzi wake, yaani Yakobo na Yohana, walipoona hayo, wakasema: “Bwana, unataka tuagize moto kutoka mbinguni ili uwaangamize?” 55Yesu akageuka na kuwakemea, 569:56 Yn 3:17; 12:27nao wakaenda kijiji kingine.

Gharama Ya Kumfuata Yesu

(Mathayo 8:19-22)

579:57 Mt 8:19Walipokuwa njiani wakienda, mtu mmoja akamwambia Yesu, “Nitakufuata kokote uendako.”

589:58 Mt 8:20Yesu akamjibu, “Mbweha wana mapango, nao ndege wa angani wana viota, lakini Mwana wa Adamu hana mahali pa kulaza kichwa chake.”

599:59 Mt 4:19Yesu akamwambia mtu mwingine, “Nifuate.”

Mtu huyo akamjibu, “Bwana, niruhusu kwanza nikamzike baba yangu.”

609:60 Mt 3:2Yesu akamwambia, “Waache wafu wawazike wafu wao, bali wewe nenda ukautangaze Ufalme wa Mungu.”

619:61 1Fal 19:20Mtu mwingine akamwambia, “Bwana, nitakufuata lakini naomba kwanza nikawaage jamaa yangu.”

62Yesu akamwambia, “Mtu yeyote atiaye mkono wake kulima, kisha akatazama nyuma, hafai kwa Ufalme wa Mungu.”

Habrit Hakhadasha/Haderekh

הבשורה על-פי לוקס 9:1-62

1יום אחד קרא אליו ישוע את שנים־עשר תלמידיו, והעניק להם סמכות וכוח לגרש שדים ולרפא מחלות. 2לאחר מכן שלח אותם לספר לכולם על בוא מלכות האלוהים ולרפא את החולים.

3”אל תיקחו אתכם דבר“, הורה להם ישוע. ”אל תיקחו אתכם מקל הליכה, תרמיל, מזון, כסף ואף לא בגדים להחלפה. 4בכל עיר או כפר התארחו בבית אחד בלבד.

5”אם התושבים לא יקשיבו לדבריכם, צאו מאותה עיר ונערו את העפר מעל רגליכם, כסימן לכך שעשיתם את המוטל עליכם והזהרתם אותם.“

6התלמידים יצאו לדרך, ובעברם מעיר לעיר ומכפר לכפר בישרו את דבר אלוהים וריפאו את החולים.

7כשהגיעו השמועות על כוחו ונפלאותיו של ישוע לאוזני המושל הורדוס, הוא נמלא מבוכה ודאגה, כי היו אנשים שאמרו: ”זהו יוחנן המטביל שקם לתחייה!“ 8או: ”האיש הזה הוא אליהו הנביא!“ היו שאמרו: ”זהו אחד הנביאים שקם לתחייה!“

9”יוחנן?“ תמה הורדוס. ”הרי כרתי את ראשו, אז מיהו האיש שעליו אני שומע ניסים ונפלאות?“ והורדוס חיפש דרך לפגוש את ישוע.

10לאחר שחזרו השליחים ודיווחו לישוע על כל מעשיהם, הוא עזב את הקהל איתם והם הלכו יחד לבית־צידה כדי להיות לבדם. 11אבל ההמונים גילו לאן ישוע הלך והלכו בעקבותיו. ישוע קיבל אותם בחמימות ולימד אותם על מלכות האלוהים. הוא גם ריפא את החולים שביניהם.

12לפנות ערב ניגשו שנים־עשר התלמידים אל ישוע והאיצו בו לשלוח את הקהל אל הכפרים והמשקים שבסביבה כדי לקנות אוכל ולחפש מקום לינה, כי האזור שבו היו היה שומם לגמרי. 13”אתם תאכילו אותם!“ אמר ישוע לתלמידיו.

אך התלמידים אמרו: ”יש לנו רק חמש ככרות לחם ושני דגים. האם אתה רוצה שנלך לקנות אוכל לכל ההמון הזה?“ 14כחמשת־אלפים גברים היו שם (לא כולל נשים וילדים).

”אמרו להם לשבת בשורות של חמישים איש“, הורה ישוע לתלמידיו. 15התלמידים עשו כדבריו והושיבו את הקהל.

16ישוע לקח את חמש ככרות הלחם ואת שני הדגים, הביט לשמים, וביקש מאלוהים שיברך את האוכל. לאחר מכן פרס את הלחם, חתך את הדגים והגיש לתלמידיו שיחלקו לעם. 17כולם אכלו עד ששבעו, וכאשר אספו את הפירורים שנשארו מילאו שנים־עשר סלים.

18יום אחד כשהתפלל ישוע לבדו ורק תלמידיו היו בחברתו, הוא שאל אותם: ”למי חושבים אותי האנשים?“

19”ליוחנן המטביל“, השיבו התלמידים. ”אבל יש החושבים שאתה אליהו הנביא, ואחרים חושבים שאתה אחד מאבותינו הנביאים שקם לתחייה.“

20”למי אתם חושבים אותי?“ המשיך ישוע לשאול.

”אתה משיח אלוהים!“ ענה פטרוס.

21ישוע ציווה עליהם לא לספר זאת לאיש. 22”על בן־האדם לסבול הרבה“, הוסיף ישוע. ”זקני היהודים, ראשי הכוהנים והסופרים ידחו אותו ואף יהרגו אותו, אולם כעבור שלושה ימים יקום לתחייה!“

23לאחר מכן אמר ישוע לכולם: ”מי שרוצה ללכת בעקבותיי חייב להתכחש לעצמו, לוותר על נוחיותו ושאיפותיו, לשאת עמו את צלבו יום־יום ולבוא אחרי. 24כי מי שחפץ להציל את חייו – יאבד אותם, ואילו מי שיוותר על חייו למעני – יציל אותם. 25מה הרוויח אדם שהשיג את העולם כולו אבל הפסיד חיי־נצח?

26”דעו לכם, שכל מי שמתבייש בי ובדברי, הוא יהיה לבושה לבן־האדם כאשר יבוא בכבודו ובכבוד של אביו עם המלאכים הקדושים. 27אני אומר לכם את האמת: בין העומדים פה עתה יש כאלה שלא ימותו לפני שיראו את מלכות האלוהים!“

28כעבור שמונה ימים לקח איתו ישוע את פטרוס, יוחנן ויעקב ועלה על אחד ההרים כדי להתפלל. 29בזמן שישוע התפלל, פניו השתנו ובגדיו הלבינו והבריקו. 30לפתע הופיעו משה רבנו ואליהו הנביא ודיברו איתו. 31הופעתם הייתה מרשימה ומהודרת, והם דיברו עם ישוע על מותו הקרוב בירושלים, שהיה צפוי לפי דבר ה׳.

32בינתיים שקעו פטרוס והאחרים בשינה עמוקה, וכשהתעוררו ראו את כבודו והדרו של ישוע ואת השנים שעמדו לידו. 33כשעמדו אליהו ומשה ללכת קרא פטרוס, בלי לדעת מה הוא אומר: ”רבי, כמה טוב שאנחנו כאן! מדוע לא נקים כאן שלוש סוכות לכבוד – לך, למשה ולאליהו?“

34בעודו מדבר כיסה אותם ענן והם נמלאו פחד. 35ומן הענן קרא קול: ”זהו בני בחירי, שמעו בקולו.“

36לאחר הקול נראה ישוע עומד לבדו. התלמידים לא סיפרו לאיש את אשר ראו אלא חיכו. 37כשירדו מן ההר למחרת, באו אנשים רבים לקראת ישוע, 38ואחד מהם קרא: ”רבי, אני מתחנן לפניך שתביט בבני היחיד. 39שד אוחז בו, הוא גורם לו לצרוח ללא סיבה, משליך אותו על הרצפה ומתיש את כוחו עד שריר נוזל מפיו. השד הזה מדכא את בני מאוד וכמעט שאינו מניח לו לנפשו. 40התחננתי לפני תלמידיך שיגרשו את השד, אבל הם לא יכלו לעשות זאת.“

41”מה עיקש וחסר־אמונה הדור הזה!“ קרא ישוע. ”עד מתי יהיה עלי לסבול אתכם? הביאו אלי את הילד!“

42לפני שהספיק הילד להגיע אל ישוע, השד הפיל אותו ארצה כאשר הוא מפרכס. אולם ישוע גירש ממנו את השד בגערה, ריפא אותו והשיבו לאביו.

43כשראו הנוכחים את הגילוי הזה של כוח אלוהים, נפלה עליהם יראה גדולה.

בעוד הקהל מתפעל ומחליף רשמים על מעשיו הנפלאים, אמר ישוע לתלמידיו: 44”הקשיבו לדברי בתשומת לב: בן־האדם עומד להימסר לידי אנשים.“ 45אולם התלמידים לא הבינו למה התכוון; דבר־מה מנע מבעדם מלהבין והם חששו לשאול אותו למה התכוון.

46בין התלמידים התעורר ויכוח: מיהו החשוב והגדול ביניהם. 47ישוע ידע את מחשבותיהם ולכן קרא לילד קטן, העמידו לידו 48ואמר לתלמידיו: ”מי שמקבל ילד קטן כזה, כאילו מקבל אותי; ומי שמקבל אותי, מקבל למעשה את אבי אשר שלח אותי. הקטן מביניכם – הצנוע והעניו ביותר – הוא הגדול ביניכם!“

49יוחנן תלמידו פנה אליו ואמר: ”רבי, ראינו איש שמגרש שדים בשמך ואמרנו לו לחדול מכך, כי אין הוא שייך לקבוצתנו.“

50”לא הייתם צריכים לומר לו זאת,“ השיב לו ישוע, ”כי מי שאינו נגדכם הוא בעדכם.“

51בהתקרב המועד שבו יילקח לשמים, התכונן ישוע ללכת לירושלים. 52יום אחד הוא שלח לפניו שליחים, כדי שיכינו לו מקום לינה באחד מכפרי השומרונים. 53אולם השומרונים סרבו לתת להם מקום לינה, משום שפניהם של ישוע ותלמידיו היו מועדות לירושלים (לשומרונים היה ויכוח עם היהודים בנוגע לירושלים).

54כשהגיע הדבר לאוזני ישוע ותלמידיו, שאלו יעקב ויוחנן: ”אתה רוצה שנצווה כי תרד אש מהשמים ותשרוף אותם?“ 55אולם ישוע גער בהם, 56והחבורה המשיכה בדרכה אל כפר אחר.

57בדרך אמר מישהו לישוע: ”אדוני, לאן שתלך, אני אלך אחריך!“ 58אולם ישוע השיב לו: ”אל תשכח שאין לי מקום להניח את ראשי. השועלים מתגוררים במחילות האדמה ולציפורים יש קנים, אולם לבן־האדם אין מקום להניח בו את ראשו.“ 59בהזדמנות אחרת אמר ישוע לאיש מסוים: ”בוא אחרי והיה תלמיד שלי.“ האיש הסכים, אולם ביקש לקבור תחילה את אביו.

60”הנח למתים (מבחינה רוחנית) לקבור את המתים שלהם“, אמר לו ישוע. ”ואילו אתה לך להכריז על מלכות האלוהים.“

61איש אחר אמר לישוע: ”אני אלך אחריך, אדוני, אך הרשה לי תחילה ללכת הביתה ולהיפרד מבני משפחתי.“

62אבל ישוע השיב לו: ”השם את ידו על המחרשה ומביט אחריו לא יהיה כשיר למלכות האלוהים.“