Luka 6 – NEN & KJV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Luka 6:1-49

Bwana Wa Sabato

(Mathayo 12:1-8; Marko 2:23-28)

16:1 Kum 23:25Ikawa siku moja ya Sabato Yesu alikuwa akipita katika mashamba ya nafaka, nao wanafunzi wake wakaanza kuvunja masuke ya nafaka, wakayafikicha kwa mikono yao na kula punje zake. 26:2 Mt 12:2Baadhi ya Mafarisayo wakawauliza, “Mbona mnafanya mambo yasiyo halali kufanywa siku ya Sabato?”

36:3 1Sam 21:6Yesu akawajibu, “Je, ninyi hamjasoma kamwe alivyofanya Daudi wakati yeye na wenzake walikuwa na njaa? 46:4 Law 24:5-9Aliingia ndani ya nyumba ya Mungu, akaichukua na kuila ile mikate iliyowekwa wakfu, ambayo ni halali kuliwa na makuhani peke yao. Naye pia akawapa wenzake.” 56:5 Mt 8:20Yesu akawaambia, “Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.”

Mtu Aliyepooza Mkono Aponywa

(Mathayo 12:9-14; Marko 3:1-6)

66:6 Lk 6:1; Mt 12:9; Mk 3:1; Lk 13:14; 14:3; Yn 9:16Ikawa siku nyingine ya Sabato, Yesu aliingia ndani ya sinagogi na akawa anafundisha. Huko palikuwa na mtu ambaye mkono wake wa kuume ulikuwa umepooza. 76:7 Mt 9:4Mafarisayo na walimu wa sheria walikuwa wakitafuta sababu ya kumshtaki Yesu. Kwa hivyo wakawa wanamwangalia sana ili waone kama ataponya katika siku ya Sabato. 86:8 Mt 9:4Lakini Yesu alijua mawazo yao, hivyo akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, “Inuka usimame mbele ya watu wote.” Hivyo yule mtu akainuka, akasimama mbele yao wote.

9Ndipo Yesu akawaambia wale walimu wa sheria na Mafarisayo, “Nawauliza ninyi, ni lipi lililo halali siku ya Sabato? Ni kutenda mema au kutenda mabaya? Ni kuokoa maisha au kuyaangamiza?”

106:10 Mt 13:47Akawatazama watu wote waliokuwepo, kisha akamwambia yule aliyepooza mkono, “Nyoosha mkono wako!” Akaunyoosha na mkono wake ukaponywa kabisa. 116:11 Yn 5:18Wale wakuu wakakasirika sana, wakashauriana wao kwa wao ni nini watakachomtendea Yesu.

Yesu Achagua Mitume Kumi Na Wawili

(Mathayo 10:1-4; Marko 3:13-19)

126:12 Lk 3:21Ikawa katika siku hizo Yesu alikwenda mlimani kuomba, akakesha usiku kucha akimwomba Mungu. 136:13 Mk 6:30Kulipopambazuka, akawaita wanafunzi wake, naye akachagua kumi na wawili, ambao pia aliwaita mitume: 146:14 Yn 1:42Simoni aliyemwita Petro, Andrea nduguye, Yakobo, Yohana, Filipo, Bartholomayo, 156:15 Mt 9:9Mathayo, Tomaso, Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni aliyeitwa Zelote, 16Yuda mwana wa Yakobo, na Yuda Iskariote ambaye alikuwa msaliti.

Yesu Aponya Wengi

(Mathayo 4:23-25)

176:17 Mt 11:21; Mk 3:7-8; Mt 4:23; 5:1; Mk 3:7-12Akashuka pamoja nao, akasimama mahali penye uwanja tambarare. Hapo palikuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wake na umati mkubwa wa watu kutoka sehemu zote za Uyahudi, kutoka Yerusalemu, na kutoka pwani ya Tiro na Sidoni. 186:18 Mt 4:23; 5:1; Mk 3:7-12Walikuwa wamekuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. Wale waliokuwa wakiteswa na pepo wachafu akawaponya. 196:19 Mt 9:20; 14:36; Mk 5:30; Mt 4:23; 5:1; Mk 3:7-12Watu wote walikuwa wanajitahidi kumgusa kwa sababu nguvu zilikuwa zikimtoka na kuwaponya wote.

Baraka Na Ole

(Mathayo 5:1-12)

206:20 Mt 25:34Akawatazama wanafunzi wake, akasema:

“Mmebarikiwa ninyi mlio maskini,

kwa sababu Ufalme wa Mungu ni wenu.

216:21 Isa 55:1; 61:2-3; Ufu 7:17Mmebarikiwa ninyi mlio na njaa sasa,

kwa sababu mtashibishwa.

Mmebarikiwa ninyi mnaolia sasa,

kwa sababu mtacheka.

226:22 Yn 9:22; 16:2; 15:21; Isa 51:7; Yn 15:19; 16:2Mmebarikiwa ninyi, watu watakapowachukia,

watakapowatenga na kuwatukana

na kulikataa jina lenu kama neno ovu,

kwa ajili ya Mwana wa Adamu.

236:23 Mt 5:21; 5:12; Mdo 5:41; Kol 1:24; Yak 1:2; Mdo 7:51“Furahini na kurukaruka kwa shangwe, kwa sababu thawabu yenu ni kubwa mbinguni, kwa kuwa hivyo ndivyo baba zao walivyowatenda manabii.

246:24 Yak 5:1; Lk 16:25; Amo 6:1; Yak 5:1; Lk 12:21; Mt 6:2, 5, 16; Lk 16:25“Lakini ole wenu ninyi mlio matajiri,

kwa sababu mmekwisha kupokea faraja yenu.

256:25 Isa 65:13; Mit 14:13; Isa 65:13; Mit 14; 13Ole wenu ninyi mlioshiba sasa,

maana mtaona njaa.

Ole wenu ninyi mnaocheka sasa,

maana mtaomboleza na kulia.

266:26 Mt 7:15; Yn 15:19; 1Yn 4:5Ole wenu watu watakapowasifu,

kwani ndivyo baba zao walivyowasifu

manabii wa uongo.

Wapendeni Adui Zenu

(Mathayo 5:38-48)

276:27 Mt 5:44; Rum 12:20; Kut 23:4; Mt 5:44; Lk 6:35; Rum 12:20“Lakini nawaambia ninyi mnaonisikia: Wapendeni adui zenu. Watendeeni mema wanaowachukia. 286:28 Lk 23:34; Mdo 7:60Wabarikini wale wanaowalaani, waombeeni wale wanaowatendea mabaya. 296:29 Mt 5:39; 1Kor 6:7Kama mtu akikupiga shavu moja, mgeuzie na la pili pia. Mtu akikunyangʼanya koti lako, usimzuie kuchukua joho pia. 306:30 Kum 15:7-10; Mt 21:36Mpe kila akuombaye, na kama mtu akichukua mali yako usitake akurudishie. 316:31 Mt 7:12Watendeeni wengine kama ambavyo mngetaka wawatendee ninyi.

326:32 Mt 5:42-46“Kama mkiwapenda tu wale wanaowapenda, mwapata sifa gani? Hata ‘wenye dhambi’ huwapenda wale wawapendao. 33Tena mkiwatendea mema wale tu wanaowatendea ninyi mema, mwapata sifa gani? Hata ‘wenye dhambi’ hufanya vivyo hivyo. 346:34 Mt 5:42Tena mnapowakopesha wale tu mnaotegemea wawalipe, mwapata sifa gani? Hata ‘wenye dhambi’ huwakopesha ‘wenye dhambi’ wenzao wakitarajia kulipwa mali yao yote. 356:35 Rum 8:14; Mk 5:7Lakini wapendeni adui zenu, watendeeni mema, wakopesheni bila kutegemea kurudishiwa mlichokopesha. Ndipo thawabu yenu itakapokuwa kubwa, nanyi mtakuwa wana wa Aliye Juu Sana, kwa sababu yeye ni mwema kwa watu wasio na shukrani na kwa wale waovu. 366:36 Yak 2:13; 1Pet 1:17; 1Yn 3:1Kuweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.

Kuwahukumu Wengine

(Mathayo 7:1-5)

376:37 Mt 7:1; 6:14“Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa. Msilaumu, nanyi hamtalaumiwa. Sameheni, nanyi mtasamehewa. 386:38 Za 79:12; Isa 65:6-7; Mk 4:24Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa. Kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa.”

396:39 Mt 15:14 Pia akawapa mfano akasema, “Je, kipofu aweza kumwongoza kipofu? Je, wote wawili hawatatumbukia shimoni? 406:40 Mt 10:24; Yn 3:16Mwanafunzi hawezi kumzidi mwalimu wake, ila yule aliyehitimu aweza kuwa kama mwalimu wake.

416:41 Mt 7:3“Mbona unatazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, wala huoni boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? 426:42 Mt 18:17Utawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu yangu, acha nitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako,’ wakati wewe mwenyewe huoni boriti iliyo ndani ya jicho lako? Ewe mnafiki, ondoa boriti ndani ya jicho lako kwanza, ndipo utaweza kuona dhahiri jinsi ya kuondoa kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako.

Mti Na Mazao Yake

(Mathayo 7:16-20; Marko 12:33-35)

436:43 Mt 7:16, 17“Hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala hakuna mti mbaya uzaao matunda mazuri. 446:44 Mt 12:33Kila mti hujulikana kwa matunda yake. Kwa maana watu hawachumi tini kwenye miiba, wala zabibu kwenye michongoma. 456:45 Mt 4:23; Mk 7:20Vivyo hivyo mtu mwema hutoa mambo mema kutoka kwenye hazina ya moyo wake, naye mtu mwovu hutoa mambo maovu kutoka kwenye hazina ya moyo wake. Kwa kuwa mtu hunena kwa kinywa chake yale yaliyoujaza moyo wake.

Mjenzi Mwenye Busara Na Mjenzi Mpumbavu

(Mathayo 7:24-27)

466:46 Mal 1:6; Mt 7:21“Kwa nini mnaniita, ‘Bwana, Bwana,’ nanyi hamfanyi ninayowaambia? 476:47 Lk 11:28; Yak 1:22-25; Mt 8:9-13Nitawaonyesha jinsi alivyo mtu yule anayekuja kwangu na kusikia maneno yangu na kuyatenda. 48Yeye ni kama mtu aliyejenga nyumba, akachimba chini sana, na kuweka msingi kwenye mwamba. Mafuriko yalipokuja, maji ya ghafula yaliipiga ile nyumba, lakini haikutikisika, kwa sababu ilikuwa imejengwa vizuri. 49Lakini yeye anayesikia maneno yangu wala asiyatende, ni kama mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi bila kuweka msingi. Mafuriko yalipoikumba nyumba ile, ikaanguka mara na kubomoka kabisa.”

King James Version

Luke 6:1-49

1And it came to pass on the second sabbath after the first, that he went through the corn fields; and his disciples plucked the ears of corn, and did eat, rubbing them in their hands. 2And certain of the Pharisees said unto them, Why do ye that which is not lawful to do on the sabbath days? 3And Jesus answering them said, Have ye not read so much as this, what David did, when himself was an hungred, and they which were with him; 4How he went into the house of God, and did take and eat the shewbread, and gave also to them that were with him; which it is not lawful to eat but for the priests alone? 5And he said unto them, That the Son of man is Lord also of the sabbath. 6And it came to pass also on another sabbath, that he entered into the synagogue and taught: and there was a man whose right hand was withered. 7And the scribes and Pharisees watched him, whether he would heal on the sabbath day; that they might find an accusation against him. 8But he knew their thoughts, and said to the man which had the withered hand, Rise up, and stand forth in the midst. And he arose and stood forth. 9Then said Jesus unto them, I will ask you one thing; Is it lawful on the sabbath days to do good, or to do evil? to save life, or to destroy it? 10And looking round about upon them all, he said unto the man, Stretch forth thy hand. And he did so: and his hand was restored whole as the other. 11And they were filled with madness; and communed one with another what they might do to Jesus. 12And it came to pass in those days, that he went out into a mountain to pray, and continued all night in prayer to God.

13¶ And when it was day, he called unto him his disciples: and of them he chose twelve, whom also he named apostles; 14Simon, (whom he also named Peter,) and Andrew his brother, James and John, Philip and Bartholomew, 15Matthew and Thomas, James the son of Alphæus, and Simon called Zelotes, 16And Judas the brother of James, and Judas Iscariot, which also was the traitor.

17¶ And he came down with them, and stood in the plain, and the company of his disciples, and a great multitude of people out of all Judæa and Jerusalem, and from the sea coast of Tyre and Sidon, which came to hear him, and to be healed of their diseases; 18And they that were vexed with unclean spirits: and they were healed. 19And the whole multitude sought to touch him: for there went virtue out of him, and healed them all.

20¶ And he lifted up his eyes on his disciples, and said, Blessed be ye poor: for yours is the kingdom of God. 21Blessed are ye that hunger now: for ye shall be filled. Blessed are ye that weep now: for ye shall laugh. 22Blessed are ye, when men shall hate you, and when they shall separate you from their company, and shall reproach you, and cast out your name as evil, for the Son of man’s sake. 23Rejoice ye in that day, and leap for joy: for, behold, your reward is great in heaven: for in the like manner did their fathers unto the prophets. 24But woe unto you that are rich! for ye have received your consolation. 25Woe unto you that are full! for ye shall hunger. Woe unto you that laugh now! for ye shall mourn and weep. 26Woe unto you, when all men shall speak well of you! for so did their fathers to the false prophets.

27¶ But I say unto you which hear, Love your enemies, do good to them which hate you, 28Bless them that curse you, and pray for them which despitefully use you. 29And unto him that smiteth thee on the one cheek offer also the other; and him that taketh away thy cloke forbid not to take thy coat also. 30Give to every man that asketh of thee; and of him that taketh away thy goods ask them not again. 31And as ye would that men should do to you, do ye also to them likewise. 32For if ye love them which love you, what thank have ye? for sinners also love those that love them. 33And if ye do good to them which do good to you, what thank have ye? for sinners also do even the same. 34And if ye lend to them of whom ye hope to receive, what thank have ye? for sinners also lend to sinners, to receive as much again. 35But love ye your enemies, and do good, and lend, hoping for nothing again; and your reward shall be great, and ye shall be the children of the Highest: for he is kind unto the unthankful and to the evil. 36Be ye therefore merciful, as your Father also is merciful. 37Judge not, and ye shall not be judged: condemn not, and ye shall not be condemned: forgive, and ye shall be forgiven: 38Give, and it shall be given unto you; good measure, pressed down, and shaken together, and running over, shall men give into your bosom. For with the same measure that ye mete withal it shall be measured to you again. 39And he spake a parable unto them, Can the blind lead the blind? shall they not both fall into the ditch? 40The disciple is not above his master: but every one that is perfect shall be as his master. 41And why beholdest thou the mote that is in thy brother’s eye, but perceivest not the beam that is in thine own eye? 42Either how canst thou say to thy brother, Brother, let me pull out the mote that is in thine eye, when thou thyself beholdest not the beam that is in thine own eye? Thou hypocrite, cast out first the beam out of thine own eye, and then shalt thou see clearly to pull out the mote that is in thy brother’s eye. 43For a good tree bringeth not forth corrupt fruit; neither doth a corrupt tree bring forth good fruit. 44For every tree is known by his own fruit. For of thorns men do not gather figs, nor of a bramble bush gather they grapes. 45A good man out of the good treasure of his heart bringeth forth that which is good; and an evil man out of the evil treasure of his heart bringeth forth that which is evil: for of the abundance of the heart his mouth speaketh.

46¶ And why call ye me, Lord, Lord, and do not the things which I say? 47Whosoever cometh to me, and heareth my sayings, and doeth them, I will shew you to whom he is like: 48He is like a man which built an house, and digged deep, and laid the foundation on a rock: and when the flood arose, the stream beat vehemently upon that house, and could not shake it: for it was founded upon a rock. 49But he that heareth, and doeth not, is like a man that without a foundation built an house upon the earth; against which the stream did beat vehemently, and immediately it fell; and the ruin of that house was great.