Luka 22 – NEN & KLB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Luka 22:1-71

Yuda Akubali Kumsaliti Yesu

(Mathayo 26:14-16; Marko 14:10-11)

122:1 Yn 11:55Wakati huu Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, iitwayo Pasaka, ilikuwa imekaribia. 222:2 Mt 12:14Viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walikuwa wanatafuta njia ya kumuua Yesu, kwa sababu waliwaogopa watu. 322:3 Mt 4:10; Mk 14:10, 1122:3 Mt 4:10; Yn 13:2; Mt 10:4Shetani akamwingia Yuda, aliyeitwa Iskariote, mmoja wa wale Kumi na Wawili. 422:4 Mdo 4:1; 5:24Yuda akaenda kwa viongozi wa makuhani na kwa maafisa wa walinzi wa Hekalu, akazungumza nao jinsi ambavyo angeweza kumsaliti Yesu. 522:5 Zek 11:12Wakafurahi na wakakubaliana kumpa fedha. 6Naye akakubali, akaanza kutafuta wakati uliofaa wa kumsaliti Yesu kwao, wakati ambapo hakuna umati wa watu.

Maandalizi Ya Pasaka

(Mathayo 26:17-25; Marko 14:12-21; Yohana 13:21-30)

722:7 Kum 16:5-8; Mk 4:12Basi ikawadia siku ya Mikate Isiyotiwa Chachu, siku ambayo mwana-kondoo wa Pasaka huchinjwa. 822:8 Mdo 3:1, 11; 4:13-19Hivyo Yesu akawatuma Petro na Yohana, akisema, “Nendeni mkatuandalie chakula cha Pasaka ili tuweze kuila.”

9Wakamuuliza, “Unataka tukuandalie wapi?”

10Yesu akawaambia, “Tazameni, mtakapokuwa mkiingia mjini, mtakutana na mwanaume amebeba mtungi wa maji. Mfuateni mpaka kwenye nyumba atakayoingia. 11Nanyi mwambieni mwenye nyumba, ‘Mwalimu anauliza: Kiko wapi chumba cha wageni, ambamo mimi na wanafunzi wangu tutakula Pasaka?’ 12Atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani, kikiwa kimepambwa vizuri. Andaeni humo.”

1322:13 Lk 19:32Wakaenda, nao wakakuta kila kitu kama Yesu alivyowaambia. Hivyo wakaiandaa Pasaka.

Kuanzishwa Kwa Meza Ya Bwana

(Mathayo 26:31-35; Marko 14:27-31; Yohana 13:36-38)

1422:14 Mk 6:30; Mt 26:20; Mk 14:17-18Wakati ulipowadia, Yesu akaketi mezani pamoja na wale mitume wake. 1522:15 Mt 16:21Kisha akawaambia, “Nimetamani sana kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu. 1622:16 Lk 14:15; Ufu 19:9Kwa maana, nawaambia, sitaila tena Pasaka mpaka itakapotimizwa katika Ufalme wa Mungu.”

17Akiisha kukichukua kikombe, akashukuru, akasema, “Chukueni hiki mnywe wote. 1822:18 Mt 26:29; Mk 14:29Kwa maana nawaambia tangu sasa sitakunywa tena katika uzao wa mzabibu, hadi Ufalme wa Mungu utakapokuja.”

1922:19 Mt 14:19Kisha akachukua mkate, akashukuru, akaumega, na kuwapa, akisema, “Huu ni mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.”

2022:20 Zek 9:11; 2Kor 3:6Vivyo hivyo baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, imwagikayo kwa ajili yenu. 2122:21 Za 41:9Lakini mkono wake huyo atakayenisaliti uko hapa mezani pamoja nami. 2222:22 Mt 8:20; Mdo 2:23; 4:29Mwana wa Adamu anaenda zake kama ilivyokusudiwa. Lakini ole wake mtu huyo amsalitiye.” 2322:23 Mt 26:22; Yn 13:22, 25Wakaanza kuulizana wenyewe ni nani miongoni mwao angeweza kufanya jambo hilo.

Mabishano Kuhusu Ukuu

2422:24 Mk 9:34; Lk 9:46Pia yakazuka mabishano katikati ya wanafunzi kwamba ni nani aliyeonekana kuwa mkuu kuliko wote miongoni mwao. 25Yesu akawaambia, “Wafalme na watu wa Mataifa huwatawala watu kwa nguvu. Nao wenye mamlaka juu yao hujiita ‘Wafadhili.’ 2622:26 1Pet 5:5; Mk 9:35; Lk 12:37Lakini ninyi msifanane nao. Bali yeye aliye mkuu kuliko wote miongoni mwenu, inampasa kuwa kama yeye aliye mdogo wa wote, naye atawalaye na awe kama yeye ahudumuye. 2722:27 Mt 20:28; Lk 12:37Kwani ni nani aliye mkuu? Ni yule aketiye mezani au ni yule ahudumuye? Si ni yule aliyekaa mezani? Lakini mimi niko miongoni mwenu kama yule ahudumuye. 2822:28 Ebr 4:15Ninyi mmekuwa pamoja nami katika majaribu yangu. 2922:29 Mt 25:34; 2Tim 2:12Nami kama Baba yangu alivyonipa ufalme, kadhalika mimi nami ninawapa ninyi, 30ili mpate kula na kunywa mezani pangu katika karamu ya ufalme wangu, na kukaa katika viti vya enzi, mkihukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.”

Yesu Atabiri Kuwa Petro Atamkana

3122:31 Ay 16:12; Amo 9:9Yesu akasema, “Simoni, Simoni, sikiliza, Shetani ameomba kuwapepeta ninyi wote kama ngano. 3222:32 Yn 17:9-15; Rum 8:34; Yn 21:15-17Lakini nimekuombea wewe Simoni ili imani yako isishindwe, nawe ukiisha kunirudia, uwaimarishe ndugu zako.”

3322:33 Yn 11:16Petro akajibu, “Bwana, niko tayari kwenda pamoja nawe gerezani na hata kifoni.”

3422:34 Mt 26:34; Mk 14:30; Yn 13:38Yesu akamjibu, “Ninakuambia Petro, kabla jogoo hajawika usiku wa leo, utakana mara tatu kwamba hunijui mimi.”

Mfuko, Mkoba Na Upanga

3522:35 Mt 10:9-10; Lk 9:3Kisha Yesu akawauliza, “Nilipowatuma bila mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu chochote?”

Wakajibu, “La, hatukupungukiwa na kitu chochote.”

36Akawaambia, “Lakini sasa, aliye na mfuko na auchukue, na aliye na mkoba vivyo hivyo. Naye asiye na upanga, auze joho lake anunue mmoja. 3722:37 Isa 53:12Kwa sababu, nawaambia, andiko hili lazima litimizwe juu yangu, kwamba, ‘Alihesabiwa pamoja na wakosaji’; kwa kweli yaliyoandikwa kunihusu mimi hayana budi kutimizwa.”

38Wanafunzi wake wakamwambia, “Bwana, tazama hapa kuna panga mbili.”

Akawajibu, “Inatosha.”

Yesu Aomba Kwenye Mlima Wa Mizeituni

(Mathayo 26:36-46; Marko 14:32-42)

3922:39 Lk 21:37; Mt 21:1Yesu akatoka, akaenda kwenye Mlima wa Mizeituni kama ilivyokuwa kawaida yake, nao wanafunzi wake wakamfuata. 4022:40 Mt 6:13; 26:41; Mk 14:38Walipofika huko, akawaambia wanafunzi wake, “Ombeni, msije mkaingia majaribuni.” 4122:41 Lk 18:11Akajitenga nao kama umbali wa kutupa jiwe, akapiga magoti, akaomba 4222:42 Mt 20:22; 26:39akisema, “Baba, kama ni mapenzi yako, niondolee kikombe hiki. Lakini si kama nipendavyo, bali mapenzi yako yatendeke.” 4322:43 Mt 4:11; 1:13Malaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu. 4422:44 Yn 12:27Naye akiwa katika maumivu makuu, akaomba kwa bidii, nalo jasho lake likawa kama matone ya damu yakidondoka ardhini.

45Baada ya kuomba, akawarudia wanafunzi wake akawakuta wamelala, wakiwa wamechoka kutokana na huzuni. 4622:46 Lk 22:40Naye akawauliza, “Mbona mmelala? Amkeni, mwombe ili msije mkaingia majaribuni.”

Yesu Akamatwa

(Mathayo 26:47-56; Marko 14:43-50; Yohana 18:3-11)

4722:47 Mt 26:47-57; Mk 14:43-49; Yn 18:2-11Yesu alipokuwa bado anazungumza, umati mkubwa wa watu ukaja. Uliongozwa na Yuda, ambaye alikuwa mmoja wa wale wanafunzi Kumi na Wawili. Akamkaribia Yesu ili ambusu. 48Lakini Yesu akamwambia, “Yuda, je, unamsaliti Mwana wa Adamu kwa busu?”

49Wafuasi wa Yesu walipoona yale yaliyokuwa yanakaribia kutokea, wakasema, “Bwana, tuwakatekate kwa panga zetu?” 5022:50 Mt 26:51; Mk 14:47; Yn 18:10Mmoja wao akampiga mtumishi wa kuhani mkuu kwa upanga, akamkata sikio la kuume.

51Lakini Yesu akasema, “Acheni!” Akaligusa lile sikio la yule mtu na kumponya.

5222:52 Mt 26:55; Mk 14:14-48Kisha Yesu akawaambia wale viongozi wa makuhani, maafisa wa walinzi wa Hekalu, pamoja na wazee waliokuwa wamekuja kumkamata, “Mmekuja na panga na marungu, kana kwamba mimi ni mnyangʼanyi? 5322:53 Mt 26:55; Yn 12:27; Mt 8:12; Yn 3:20Siku kwa siku nilikuwa pamoja nanyi Hekaluni lakini hamkunikamata. Lakini hii ni saa yenu, wakati giza linatawala!”

Petro Amkana Yesu

(Mathayo 26:57-75; Marko 14:53-72; Yohana 18:12-27)

5422:54 Mt 26:57; Mk 14:53; Mt 26:58; Yn 18:15Kisha wakamkamata Yesu, wakamchukua, wakaenda naye mpaka nyumbani kwa kuhani mkuu. Lakini Petro akafuata kwa mbali. 5522:55 Mt 26:69; Mk 14:66Walipokwisha kuwasha moto katikati ya ua na kuketi pamoja, Petro naye akaketi pamoja nao. 56Mtumishi mmoja wa kike akamwona kwa mwanga wa moto akiwa ameketi pale. Akamtazama sana, akasema, “Huyu mtu pia alikuwa pamoja na Yesu!”

57Lakini Petro akakana, akasema, “Ewe mwanamke, hata simjui!”

5822:58 Mt 26:71; Mk 14:69; Yn 18:26Baadaye kidogo, mtu mwingine alimwona Petro akasema, “Wewe pia ni mmoja wao!” Petro akajibu, “Wewe mtu, mimi sio mmoja wao!”

5922:59 Lk 23:6Baada ya muda wa kama saa moja hivi, mtu mwingine akazidi kusisitiza, “Kwa hakika huyu mtu naye alikuwa pamoja na Yesu, kwa maana yeye pia ni Mgalilaya.”

60Petro akajibu, “Wewe mtu, mimi sijui unalosema!” Wakati huo huo, akiwa bado anazungumza, jogoo akawika. 6122:61 Lk 7:13Naye Bwana akageuka, akamtazama Petro. Ndipo Petro akakumbuka lile neno ambalo Bwana alimwambia: “Kabla jogoo hajawika leo, utanikana mara tatu.” 62Naye akaenda nje, akalia kwa majonzi.

Walinzi Wamdhihaki Yesu Na Kumpiga

(Mathayo 26:67-68; Marko 14:65)

6322:63 Mt 26:67, 68; Mk 14:6522:63 Mt 26:67, 68; Mk 14:65Watu waliokuwa wanamlinda Yesu wakaanza kumdhihaki na kumpiga. 64Wakamfunga kitambaa machoni na kumuuliza, “Tabiri! Tuambie ni nani aliyekupiga?” 6522:65 Mt 16:21Wakaendelea kumtukana kwa matusi mengi.

Yesu Apelekwa Mbele Ya Baraza

(Mathayo 26:59-66; Marko 14:55-64; Yohana 18:28-38)

6622:66 Mt 5:22; 27:1; Mk 15:1; Mdo 4:26; 22:5Kulipopambazuka, baraza la wazee wa watu,22:66 Baraza la wazee hapa ina maana ya Sanhedrin ambalo lilikuwa ndilo Baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi, lililoundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu. yaani viongozi wa makuhani na walimu wa sheria, wakakutana pamoja, naye Yesu akaletwa mbele yao. 6722:67 Mt 26:63; Mk 14:61Wakamwambia, “Kama wewe ndiye Kristo,22:67 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. tuambie.”

Yesu akawajibu, “Hata nikiwaambia hamtaamini. 6822:68 Lk 20:3-8Nami nikiwauliza swali, hamtanijibu. 6922:69 Mk 16:19Lakini kuanzia sasa, Mwana wa Adamu ataketi mkono wa kuume wa Mungu Mwenye Nguvu.”

7022:70 Mt 26:65; 27:11; Lk 23:3Wote wakauliza, “Wewe basi ndiwe Mwana wa Mungu?”

Yeye akawajibu, “Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye.”

7122:71 Mt 26:65; Mk 14:62Kisha wakasema, “Tuna haja gani tena ya ushahidi zaidi? Tumesikia wenyewe kutoka kinywani mwake.”

Korean Living Bible

누가복음 22:1-71

예수님을 죽이려는 음모

1누룩 넣지 않은 빵을 먹는 22:1 또는 ‘무교절’명절인 22:1 이집트의 노예 생활에서 해 방된 유대인의 기념일.유월절이 다가왔다.

2대제사장들과 율법학자들은 백성들을 두려워하여 어떻게 하면 예수님을 아무 탈없이 죽일 수 있을까 하고 의논하고 있었다.

3그때 열두 제자 중 하나인 가룟 유다에게 사탄이 들어갔다.

4유다가 대제사장들과 성전 경비병들에게 가서 예수님을 팔아 넘길 방법을 의논하자

5그들이 기뻐하며 돈을 주기로 약속하였다.

6그래서 유다는 그들의 뜻에 따르기로 하고 사람들이 없을 때 예수님을 넘겨 줄 기회를 찾기 시작했다.

7누룩 넣지 않은 빵을 먹는 명절인 무교절이 되었는데 이 날은 유월절에 쓸 어린 양을 잡는 날이었다.

8예수님은 베드로와 요한을 보내시며 “가서 우리가 먹을 유월절 음식을 준비하여라” 하셨다.

9그들이 “어디다 마련할까요?” 하고 묻자

10예수님은 이렇게 말씀하셨다. “성 안에 들어가면 물통을 가지고 가는 사람을 만날 것이다. 그가 들어가는 집으로 따라 들어가거라.

11그리고 그 집 주인에게 ‘우리 선생님이 제자들과 함께 유월절 음식을 먹을 방을 알아보라고 하셨습니다’ 하여라.

12그러면 잘 준비된 이층 넓은 방으로 안내할 것이다. 거기서 준비하도록 하라.”

13제자들이 가 보니 예수님이 말씀 하신 그대로였다. 그래서 그들은 거기서 유월절 음식을 준비하였다.

최후의 만찬

14시간이 되자 예수님은 사도들과 함께 식탁에 앉으시고

15그들에게 이렇게 말씀하셨다. “내가 고난을 당하기 전에 너희와 함께 이 유월절 음식 먹기를 무척 원하였다.

16내가 너희에게 말하지만 22:16 원문에는 그냥 ‘유월절이’유월절의 의미가 하나님의 나라에서 성취될 때까지 내가 다시는 이 음식을 먹지 않을 것이다.”

17그러고서 예수님은 잔을 들어 감사 기도를 드리신 후 말씀하셨다. “너희는 이것을 가져다가 너희끼리 나누어 마셔라.

18나는 이제부터 하나님의 나라가 올 때까지 포도나무에서 난 것을 다시 마시지 않을 것이다.”

19예수님은 또 빵을 들어 감사 기도를 드리고 떼어서 제자들에게 주시며 “이것은 너희를 위해 주는 내 몸이다. 너희는 이것을 행하여 나를 기념하라” 하고 말씀하셨다.

20그리고 예수님은 저녁을 잡수신 후에 마찬가지로 잔을 들고 이렇게 말씀하셨다. “이 잔은 너희를 위해 흘릴 내 피로 세우는 새 계약이다.

21그러나 나를 파는 사람의 손이 내 손과 함께 식탁 위에 있다.

2222:22 원문에는 ‘인자는 이미 작정된 대로 가거니와’ 나는 하나님이 정하신 대로 죽지만 나를 파는 사람에게는 불행이 닥칠 것이다.”

23그러자 제자들은 그들 가운데 이런 짓을 할 사람이 누구겠느냐고 서로 물었다.

24제자들 사이에 누가 가장 위대하냐고 하는 문제로 말다툼이 생겼다.

25그래서 예수님이 그들에게 말씀하셨다. “세상의 왕들은 권력으로 자기 백성을 다스리고 직권을 행사하는 사람들은 자기들을 ‘은인’ 이라고 부른다.

26그러나 너희는 그렇게 해서는 안 된다. 너희 가운데 가장 22:26 또는 ‘큰 자’나은 사람은 제일 나이 어린 사람과 같아야 하고 지도자는 종과 같아야 한다.

27식탁에 앉아서 먹는 사람과 심부름하는 사람 중에 누가 더 지위가 높으냐? 식탁에 앉아 먹는 사람이 아니냐? 그러나 나는 섬기는 자로 너희 가운데 있다.

28너희가 항상 나와 같이 있으면서 내가 당한 시험을 함께 받았으므로

29내 아버지께서 내게 나라를 주신 것처럼 나도 너희에게 나라를 주어

30너희가 내 나라에서 내 식탁에 앉아 먹고 마시며 보좌에 앉아 이스라엘의 열두 지파를 다스리게 하겠다.

31“시몬아, 시몬아, 사탄이 너희를 밀 까부르듯 하겠다고 요구하였다.

32그러나 네 믿음이 완전히 사라지지 않도록 내가 너를 위해 기도하였다. 너는 뉘우치고 돌아온 후에 네 형제들을 굳세게 하여라.”

33그때 베드로가 “주님, 나는 주님과 함께 감옥에도, 사형장에도 갈 준비가 되어 있습니다” 하자

34예수님은 “베드로야, 내가 분명히 너에게 말하지만 오늘 밤 닭 울기 전에 네가 세 번이나 나를 모른다고 말할 것이다” 하고 말씀하셨다.

35그러고 나서 예수님이 제자들에게 “내가 너희를 지갑이나 가방이나 신도 없이 보냈을 때 부족한 것이 있었느냐?” 하고 물으시자 제자들은 “없었습니다” 하고 대답하였다.

36그래서 예수님은 다시 말씀하셨다. “그러나 이제는 지갑이나 가방이 있는 사람은 가지고 다니고 칼이 없는 사람은 겉옷을 팔아서 칼을 사라.

37내가 너희에게 말하지만 22:37 사53:12‘그가 범죄자처럼 되었다’ 라고 기록된 말이 내게 이루어져야 한다. 사실 내게 관한 일은 이루어져 가고 있다.”

38그때 제자들이 “주님, 여기 칼 두 자루가 있습니다” 하자 예수님은 “그것이면 충분하다” 하고 말씀하셨다.

예수님이 체포되심

39예수님이 습관대로 감람산에 가시자 제자들도 따라갔다.

40예수님은 그 곳에 도착하셔서 제자들에게 “시험에 들지 않게 기도하라” 하시고

41그들을 떠나 돌을 던지면 닿을 정도 떨어진 곳으로 가셔서 무릎을 꿇고 이렇게 기도하셨다.

42“아버지, 아버지께서 원하신다면 이 고난의 잔을 내게서 거두어 주십시오. 그러나 내 뜻대로 마시고 아버지의 뜻대로 하십시오.”

43그러자 한 천사가 하늘에서 나타나 예수님께 힘을 북돋아 주었다.

44예수님이 괴로워 몸부림치시며 더욱 간절히 기도하시자 땀이 핏방울같이 되어 땅에 떨어졌다.

45예수님은 기도하시던 자리에서 일어나 제자들에게 돌아가 그들이 슬픔에 지쳐 잠든 것을 보시고

46“왜 잠만 자느냐? 시험에 들지 않도록 일어나 기도하여라” 하고 말씀하셨다.

47예수님의 말씀이 미처 끝나기도 전에 한 떼의 군중이 열두 제자 중 하나인 유다를 앞세우고 나타났다. 유다가 예수님께 가까이 와서 입을 맞추려고 하였으나

48예수님은 그에게 “유다야, 네가 입맞춤으로 22:48 원문에는 ‘인자’ (사람의아들)나를 파느냐?” 하고 말씀하셨다.

49함께 있던 제자들은 되어가는 일을 보고 예수님께 “주님, 칼로 쳐 버릴까요?” 하고 물었다.

50그러고는 그들 중 한 사람이 대제사장의 종의 오른쪽 귀를 쳐서 잘라 버렸다.

51그러나 예수님은 22:51 또는 ‘이것까지 허용하여라’“그만두어라. 이만하면 됐다” 하시고 그 사람의 귀를 만져 고쳐 주셨다.

52그리고 예수님은 자기를 잡으러 온 대제사장들과 성전 경비병들과 장로들에게 말씀하셨다. “내가 마치 강도라도 되는 것처럼 너희가 칼과 몽둥이를 들고 나왔느냐?

53내가 날마다 너희와 함께 성전에 있을 때는 너희가 나를 잡지 않았다. 그러나 이제는 너희 때이며 22:53 원문에는 ‘어두움의 권세로다’어두움의 권세가 기세를 부릴 때이다.”

베드로가 주님을 부인함

54그들이 예수님을 잡아 대제사장의 집으로 끌고 들어가자 베드로도 멀찍이 뒤따라갔다.

55사람들이 뜰 한가운데 불을 피우고 둘러앉아 있을 때 베드로는 그들 틈에 끼어 앉았다.

56그때 여종 하나가 앉아서 불을 쬐고 있는 베드로를 유심히 보더니 “이 사람도 그와 한패예요” 하였다.

57그러나 베드로는 “이 여자야, 나는 그를 모른다” 하고 딱 잡아떼었다.

58조금 후에 또 어떤 사람이 베드로를 보고 “당신도 그들과 한패지요?” 하자 베드로는 “이 사람아, 나는 아니야” 하고 말하였다.

59한 시간쯤 지난 뒤 또 다른 사람이 “이 사람이 갈릴리 사람인 걸 보니 틀림없이 그들과 한패요” 하자

60베드로는 “여보시오, 나는 당신이 무슨 말을 하는지 도무지 모르겠소” 하고 대답하였다. 베드로의 말이 미처 끝나기도 전에 닭이 곧 울었다.

61주님께서 몸을 돌이켜 베드로를 보시자 그는 “오늘 밤 닭 울기 전에 네가 세 번이나 나를 모른다고 말할 것이다” 라고 하신 주님의 말씀이 생각나서

62밖으로 나가 한없이 울었다.

63예수님을 지키던 사람들은 그분을 조롱하고 때리며

64눈을 가리고 “너를 때리는 사람이 누구냐? 알아맞혀 보아라” 하면서

65예수님께 갖은 모욕을 다 하였다.

66날이 밝자 대제사장들과 율법학자들과 장로들이 22:66 헬 ‘수네드리온’ (공회)의회를 열어 예수님을 의원들 앞에 세우고

67“네가 그리스도라면 우리에게 말하라” 하였다. 그래서 예수님은 이렇게 말씀하셨다. “내가 말하여도 너희가 믿지 않을 것이며

68내가 물어도 너희가 대답하지 않을 것이다.

69그러나 이제부터는 22:69 원문에는 ‘인자가 하나님의 권능의 우 편에 앉아 있으리라’내가 전능하신 하나님의 오른편에 앉을 것이다.”

70“그렇다면 네가 하나님의 아들이냐?” 하고 그들이 묻자 예수님은 “그렇다” 하고 대답하셨다.

71그러자 그들은 “이 이상 무슨 증거가 더 필요하겠는가? 우리는 22:71 원문에는 ‘그가’이 사람이 직접 하는 말을 다 들었다” 하고 외쳤다.