Luka 13 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Luka 13:1-35

Tubu, La Sivyo Utaangamia

113:1 Mt 27:2Wakati huo huo, kulikuwa na watu waliomwambia Yesu habari za Wagalilaya ambao Pilato aliwaua, na damu ya hao watu akaichanganya na dhabihu yao waliyokuwa wanatoa. 213:2 Yn 9:2-3Yesu akawauliza, “Mnadhani kwamba hawa Wagalilaya ambao walikufa kifo cha namna hiyo walikuwa na dhambi kuwazidi Wagalilaya wengine wote? 313:3 Za 7:12La hasha! Ninyi nanyi msipotubu, mtaangamia vivyo hivyo. 413:4 Yn 9:7-11Au wale watu kumi na wanane waliokufa walipoangukiwa na mnara huko Siloamu: mnadhani wao walikuwa waovu kuliko watu wote waliokuwa wanaishi Yerusalemu? 513:5 Mt 3:2; Mdo 2:38Nawaambia, la hasha! Ninyi nanyi msipotubu, wote mtaangamia vivyo hivyo.”

Mfano Wa Mti Usiozaa Matunda

613:6 Isa 5:2; Mt 21:19Kisha Yesu akawaambia mfano huu: “Mtu mmoja alikuwa na mtini uliopandwa katika shamba lake la mizabibu, akaja ili kutafuta tini kwenye mti huo, lakini hakupata hata moja. 713:7 Mt 3:10Hivyo akamwambia mtunza shamba: ‘Tazama, kwa muda wa miaka mitatu sasa nimekuwa nikija kutafuta matunda kwenye mtini huu, nami sikupata hata moja. Ukate! Kwa nini uendelee kuharibu ardhi?’

813:8 2Pet 3:9, 15“Yule mtunza shamba akamjibu, ‘Bwana, uache tena kwa mwaka mmoja zaidi, nami nitaupalilia na kuuwekea mbolea. 9Kama ukizaa matunda mwaka ujao, vyema, la sivyo uukate.’ ”

Yesu Amponya Mwanamke Kilema Siku Ya Sabato

1013:10 Mt 4:23Basi Yesu alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo siku ya Sabato. 1113:11 Lk 13:16Wakati huo huo akaja mwanamke mmoja aliyekuwa na pepo mchafu, naye alikuwa amepinda mgongo kwa muda wa miaka kumi na minane, wala alikuwa hawezi kunyooka wima. 12Yesu alipomwona, akamwita, akamwambia, “Mwanamke, uwe huru, umepona ugonjwa wako.” 1313:13 Mt 5:23Yesu alipomwekea mikono yake, mara akasimama wima akaanza kumtukuza Mungu.

1413:14 Mt 12:2; Lk 14:3; Kut 20:9; Mk 5:22Lakini kiongozi wa sinagogi akakasirika kwa sababu Yesu alikuwa ameponya mtu siku ya Sabato. Akaambia ule umati wa watu, “Kuna siku sita ambazo watu wanapaswa kufanya kazi. Katika siku hizo, njooni mponywe, lakini si katika siku ya Sabato.”

1513:15 Lk 14:5Lakini Bwana akamjibu, “Enyi wanafiki! Je, kila mmoja wenu hamfungulii ngʼombe wake au punda wake kutoka zizini akampeleka kumnywesha maji siku ya Sabato? 1613:16 Lk 3:8; 19:9; Mt 4:10Je, huyu mwanamke, ambaye ni binti wa Abrahamu, aliyeteswa na Shetani akiwa amemfunga kwa miaka yote hii kumi na minane, hakustahili kufunguliwa kutoka kifungo hicho siku ya Sabato?”

1713:17 Isa 66:5Aliposema haya, wapinzani wake wakaaibika, lakini watu wakafurahi kwa ajili ya mambo ya ajabu aliyoyafanya.

Mfano Wa Punje Ya Haradali

(Mathayo 13:31-32; Marko 4:30-32)

1813:18 Mt 3:2; 13:24Kisha Yesu akauliza, “Ufalme wa Mungu unafanana na nini? Nitaufananisha na nini? 1913:19 Lk 17:6; Mt 13:32Umefanana na punje ya haradali ambayo mtu aliichukua na kuipanda katika shamba lake. Nayo ikakua, ikawa mti nao ndege wa angani wakatengeneza viota vyao kwenye matawi yake.”

Mfano Wa Chachu

(Mathayo 13:33)

20Yesu akauliza tena, “Nitaufananisha Ufalme wa Mungu na nini? 2113:21 1Kor 5:6Unafanana na chachu ambayo mwanamke aliichukua akaichanganya katika kiasi kikubwa cha unga mpaka wote ukaumuka.”

Mlango Mwembamba

(Mathayo 7:13-14, 21-23)

2213:22 Lk 9:51Yesu akapita katika miji na vijiji, akifundisha wakati alisafiri kwenda Yerusalemu. 23Mtu mmoja akamuuliza, “Bwana, ni watu wachache tu watakaookolewa?”

2413:24 Mt 7:13Yesu akawaambia, “Jitahidini sana kuingia kupitia mlango mwembamba, kwa maana nawaambia wengi watajaribu kuingia, lakini hawataweza. 2513:25 Mt 7:23; 25:10-12Wakati mwenye nyumba atakapoondoka na kufunga mlango, mtasimama nje mkibisha mlango na kusema, ‘Bwana! Tufungulie mlango!’

“Lakini yeye atawajibu, ‘Siwajui ninyi, wala mtokako.’

2613:26 Mt 7:22, 23“Ndipo mtamjibu, ‘Tulikula na kunywa pamoja nawe, tena ulifundisha katika mitaa yetu.’

2713:27 Mt 25:41“Lakini yeye atawajibu, ‘Siwajui ninyi, wala mtokako. Ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu!’

2813:28 Mt 8:11-12“Ndipo kutakuwako kilio na kusaga meno, mtakapowaona Abrahamu, Isaki, Yakobo na manabii wote wakiwa katika Ufalme wa Mungu, lakini ninyi mkiwa mmetupwa nje. 2913:29 Mal 1:11; Isa 49:12; 59:19; Za 107:3; Lk 14:15Watu watatoka mashariki na magharibi, kaskazini na kusini, nao wataketi kwenye sehemu walizoandaliwa karamuni katika Ufalme wa Mungu. 3013:30 Mt 19:30Tazama, kunao walio wa mwisho watakaokuwa wa kwanza, nao wa kwanza watakaokuwa wa mwisho.”

Yesu Aomboleza Kwa Ajili Ya Yerusalemu

(Mathayo 23:37-39)

3113:31 Mt 14:1Wakati huo huo baadhi ya Mafarisayo wakamwendea Yesu na kumwambia, “Ondoka hapa uende mahali pengine kwa maana Herode anataka kukuua.”

3213:32 Ebr 2:10Yesu akawajibu, “Nendeni mkamwambie yule mbweha, ‘Ninafukuza pepo wachafu na kuponya wagonjwa leo na kesho, nami siku ya tatu nitaikamilisha kazi yangu.’ 3313:33 Mt 21:11Sina budi kuendelea na safari yangu leo, kesho na kesho kutwa: kwa maana haiwezekani nabii kufa mahali pengine isipokuwa Yerusalemu.

3413:34 Mt 23:37“Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetamani kuwakusanya watoto wako pamoja, kama vile kuku akusanyavyo vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka! 3513:35 Yer 12:17; 25:2; Za 118:26; Mt 21:9Tazama nyumba yenu imeachwa ukiwa. Ninawaambia, hamtaniona tena mpaka wakati ule mtakaposema, ‘Amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana.’ ”

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

路加福音 13:1-35

不悔改的下场

1这时,有人把加利利人献祭时被彼拉多屠杀的事告诉了耶稣。

2耶稣说:“你们以为这些人被杀,是因为他们的罪比其他加利利人的罪更重吗? 3不!我告诉你们,你们若不悔改,同样也必灭亡。 4西罗亚楼倒塌时曾压死了十八个人。你们以为他们比耶路撒冷其他人更有罪吗? 5不!我告诉你们,你们若不悔改,同样也必灭亡。”

6于是,耶稣说了一个比喻:“有人在葡萄园里种了一棵无花果树,他去树那里找果子,却找不到。 7他对园丁说,‘三年来,我一直盼望它结果子,它却一个也没结。把它砍了,免得白占土地。’

8“园丁请求说,‘主人,再留它一年吧!让我在它四周松土、施肥, 9明年如果结了果子就留它,否则再砍掉它。’”

治好驼背妇人

10有个安息日,耶稣在会堂里讲道。 11那里有个妇人被邪灵缠身十八年,腰弯得很厉害,无法站直。 12耶稣看见她,便叫她过来,说:“妇人,你再不会被疾病缠身了!” 13耶稣双手按在她身上,她的腰立刻直了,便颂赞上帝。

14会堂主管看到耶稣在安息日为人治病,十分恼怒,就对众人说:“一周有六天可以工作,求医应当在这六天之内,不可在安息日!”

15主说:“你们这些伪君子,莫非你们在安息日不解开棚里的牛和驴,带它们去喝水吗? 16这妇人身为亚伯拉罕的女儿,受撒旦的捆绑十八年,难道不该在安息日为她解开捆索吗?” 17反对祂的人听了这番话后,都非常羞愧,众人却为耶稣的奇妙作为高兴欢喜。

上帝国的比喻

18耶稣继续说:“上帝的国好像什么呢?我该把上帝的国比作什么呢? 19上帝的国就像一粒芥菜种,有人把它种在园里,它长成了一棵树,连飞鸟也来栖息在它的树枝上。”

20耶稣又说:“我该把上帝的国比作什么呢? 21上帝的国就像面酵,妇人拿来掺在三斗面里,使整团面都发起来。”

努力进窄门

22耶稣继续前往耶路撒冷,沿途在各城镇教导人。 23有人问祂:“主啊,得救的人是否很少呢?”耶稣对他们说:

24“你们要努力进窄门,因为我告诉你们,将来有许多人想要进却进不去。 25当主人起来把门关闭之后,你们才站在外面叩门哀求,说,‘主啊,给我们开门吧!’主人必说,‘我不认识你们,你们是从哪里来的?’

26“那时,你们必说,‘我们不是在一起用过餐吗?你不是在街上教导过我们吗?’

27“主人必说,‘我告诉你们,我不认识你们,也不知道你们是从哪里来的。你们这些作恶的人,走开!’

28“当你们看见亚伯拉罕以撒雅各和众先知在上帝的国,自己却被丢在门外,必要在那里哀哭切齿。 29那时人们会从东西南北来参加上帝国的宴席。 30看啊,有些殿后的将要为首,有些为首的将要殿后。”

为耶路撒冷哀伤

31那时,有几个法利赛人来告诉耶稣,说:“快离开这里吧,希律要杀你!”

32耶稣说:“你们去告诉那个狐狸,‘今天和明天,我要继续赶鬼治病,到第三天,我的任务就完成了。’ 33无论如何,今天、明天和后天我必须继续前行,因为先知不能死在耶路撒冷以外的地方。

34耶路撒冷啊,耶路撒冷啊!你常杀害先知,又用石头打死派到你那里的使者。我多次想要招聚你的儿女,像母鸡将小鸡招聚在翅膀底下,可是你们却不肯。 35看啊!你们的家园将一片荒凉。我告诉你们,在你们说‘奉主名来的当受称颂’之前,你们再也见不到我了。”