Kutoka 6 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Kutoka 6:1-30

16:1 Kut 3:20; 11:1; 12:31-39; Kum 5:15Kisha Bwana akamwambia Mose, “Sasa utaona kitu nitakachomfanyia Farao: Kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawaachia watu waende; kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawafukuza waondoke nchini mwake.”

26:2 Kut 3:14-15; 7:5; 8:22; 10:2; 12:12; 14:4, 18; 16:12; Law 11:44; 18:21; 20:7; Isa 41:20; 43:11; 49:23; 60:16; Eze 13:9; 25:17; 36:38; 37:6, 13; Yoe 2:27Pia Mungu akamwambia Mose, “Mimi ndimi Bwana. 36:3 Mwa 7:1; 2Sam 7:26; Za 48:10; 61:5; 68:4; 83:18; 99:3; Isa 52:6; Kut 3:14, 15; Yn 8:58Nilimtokea Abrahamu, Isaki na Yakobo kama Mungu Mwenyezi,6:3 Mungu Mwenyezi hapa ni jina la Kiebrania, El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote). ingawa sikuwajulisha Jina langu, Yehova, Mimi mwenyewe sikujitambulisha kwao. 46:4 Mwa 6:18; 12:7; 15:18; 17:8; Mdo 7:5; Rum 4:13; Gal 3:16; Ebr 11:8-10Pia niliweka Agano langu nao kuwapa nchi ya Kanaani, ambako waliishi kama wageni. 56:5 Kut 2:23; Mdo 7:34; Mwa 9:15Zaidi ya hayo, nimesikia kilio cha huzuni cha Waisraeli ambao Wamisri wamewatia utumwani, nami nimelikumbuka Agano langu.

66:6 Kut 3:8, 19-20; 12:17, 51; 15:13; 16:6; 20:2; 29:46; Law 22:33; 26:13; Kum 6:12; 7:8; 9:26; Za 9:16; 19:14; 34:22; 74:2; 77:15; 81:10; 105:27; 136:11; Yer 2:6; 15:21; 31:11; 50:34; Hos 13:4; Amo 2:10; Mik 6:4; 1Nya 17:21; Isa 29:22; 35:9; 44:23; 48:20; Mdo 13:17“Kwa hiyo, waambie Waisraeli: ‘Mimi ndimi Bwana, nami nitawatoa mtoke katika kongwa la Wamisri. Nitawaweka huru mtoke kuwa watumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyooshwa pamoja na matendo makuu ya hukumu. 76:7 Mwa 17:7; Kut 34:9; Eze 11:19-20; 39:6; Rum 9:4; 1Fal 20:13, 28; Isa 43:10; Yoe 3:17Nitawatwaa mwe watu wangu mwenyewe, nami nitakuwa Mungu wenu. Ndipo mtajua kuwa mimi ndimi Bwana Mungu wenu, niliyewatoa chini ya kongwa la Wamisri. 86:8 Mwa 12:7; 14:22; Kut 3:8; Yer 11:5; Eze 20:6; Ufu 10:5-6; Za 136:21-22; Law 18:21Nami nitawaleta mpaka nchi niliyoapa kwa mkono ulioinuliwa kumpa Abrahamu, Isaki na Yakobo. Nitawapa iwe milki yenu. Mimi ndimi Bwana.’ ”

96:9 Mwa 34:30; Kut 2:23Mose akawaarifu Waisraeli jambo hili, lakini hawakumsikiliza kwa sababu ya maumivu makuu ya moyoni na utumwa wa kikatili.

10Ndipo Bwana akamwambia Mose, 116:11 Kut 3:18“Nenda, mwambie Farao mfalme wa Misri awaachie Waisraeli waondoke nchini mwake.”

126:12 Kut 3:18; 4:10Lakini Mose akamwambia Bwana, “Ikiwa Waisraeli hawatanisikiliza, kwa nini yeye Farao anisikilize mimi, ambaye huzungumza kwa kigugumizi?”

Orodha Ya Jamaa Ya Mose Na Aroni

136:13 Kut 3:10Ndipo Bwana akanena na Mose na Aroni kuhusu Waisraeli na Farao mfalme wa Misri, naye akawaamuru wawatoe Waisraeli kutoka Misri.

146:14 Kut 13:3; Hes 1:1; 26:4; Mwa 29:32Hawa walikuwa wakuu wa jamaa zao:

Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Israeli walikuwa Hanoki, Palu, Hesroni na Karmi. Hawa walikuwa ndio koo za Reubeni.

156:15 Mwa 29:33Wana wa Simeoni walikuwa Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Sohari na Shauli mwana wa mwanamke Mkanaani. Hawa walikuwa ndio koo za Simeoni.

166:16 Mwa 29:34; 46:11; Hes 3:17; Yos 21:7; 1Nya 6:1, 16Haya ndiyo majina ya wana wa Lawi kufuatana na orodha zao: Gershoni, Kohathi na Merari. Lawi aliishi miaka 137.

176:17 Hes 3:18; 1Nya 6:17Wana wa Gershoni kwa koo, walikuwa Libni na Shimei.

186:18 Hes 3:19, 27; 1Nya 6:18; 23:12Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli. Kohathi aliishi miaka 133.

196:19 1Nya 6:19; 23:21; Hes 3:20, 33Wana wa Merari walikuwa Mahli na Mushi.

Hizi ndizo zilizokuwa koo za Lawi kufuatana na orodha zao.

206:20 Kut 2:1-2; 1Nya 23:13; Hes 26:59Amramu akamwoa Yokebedi, shangazi yake, ambaye alimzalia Aroni na Mose. Amramu aliishi miaka 137.

216:21 1Nya 6:38Wana wa Ishari walikuwa Kora, Nefegi na Zikri.

226:22 Law 10:4; Hes 3:30; 2Nya 29:13Wana wa Uzieli walikuwa Mishaeli, Elisafani na Sithri.

236:23 Rut 4:19-20; 1Nya 2:10; 6:3; 24:1; Hes 2:3; 3:2, 32; 4:28; 16:37-39; 26:60; Kum 10:6; Kut 24:1; Law 10:1-6; 10:12-16Aroni akamwoa Elisheba binti wa Aminadabu ndugu yake Nashoni, naye akamzalia Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.

246:24 Hes 16:1; 1Nya 6:22, 37Wana wa Kora walikuwa Asiri, Elikana na Abiasafu. Hawa walikuwa ndio koo za Kora.

256:25 Hes 25:7; 31:6; Yos 24:33; Za 106:30Eleazari mwana wa Aroni akamwoa mmoja wa binti za Putieli, naye akamzalia Finehasi.

Hawa walikuwa ndio wakuu wa jamaa za Walawi, ukoo kwa ukoo.

266:26 Kut 3:10; 7:4; 12:17, 41, 51Hawa walikuwa Aroni na Mose wale wale ambao Bwana aliwaambia, “Watoeni Waisraeli katika nchi ya Misri kwa vikosi vyao.” 27Ndio hao hao waliozungumza na Farao mfalme wa Misri kuhusu kuwatoa Waisraeli Misri. Ilikuwa ni huyo Mose na huyo Aroni.

Aroni Kuzungumza Badala Ya Mose

28Bwana aliponena na Mose huko Misri, 29akamwambia, “Mimi ndimi Bwana. Mwambie Farao mfalme wa Misri kila kitu nikuambiacho.”

306:30 Kut 3:11Lakini Mose akamwambia Bwana, “Kwa kuwa mimi huzungumza kwa kigugumizi, Farao atanisikiliza mimi?”