Kutoka 25 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Kutoka 25:1-40

Sadaka Kwa Ajili Ya Maskani Ya Mungu

(Kutoka 35:4-9)

125:1 Kut 35:21, 29; 36:2; 2Fal 12:4; 1Nya 29:5, 9; 2Nya 24:10; 29:31; Ezr 2:68; Neh 7:70; 2Kor 8:11; 9:7Bwana akamwambia Mose, 2“Waambie Waisraeli waniletee sadaka. Utapokea sadaka kwa niaba yangu kutoka kwa kila mtu ambaye moyo wake wapenda kutoa. 3Hizi ndizo sadaka utakazozipokea kutoka kwao: dhahabu, fedha na shaba; 425:4 Kut 28:4-8nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu, pamoja na kitani safi; singa za mbuzi; 525:5 Hes 4:6-10; Kum 10:3ngozi za kondoo dume zilizopakwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo;25:5 Pomboo hapa ina maana ya mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili. mbao za mshita; 625:6 Kut 27:20; 30:22-32; 35:28; 39:37; Hes 4:16; Kut 30:11; Law 16:12; Hes 7:14; 2Nya 13:11mafuta ya zeituni kwa ajili ya taa; vikolezi kwa ajili ya mafuta ya upako, pamoja na uvumba wa harufu nzuri; 725:7 Kut 28:4-14; 29:5; Amu 8:27; Hos 3:4; Law 8:8; Kut 28:15-30na vito vya shohamu na vito vingine vya thamani vya kuweka kwenye kisibau na kile kifuko cha kifuani.

825:8 Kut 36:1-5; Law 4:6; 10:4-7; 21:12; 23; Hes 3:28; Ebr 9:1-2; Law 26:11-12; Hes 5:3; Kum 12:11; 1Fal 6:13; Zek 2:10; 2Kor 7:16; Ufu 21:3“Kisha uwaamuru wanitengenezee mahali patakatifu, nami nitakaa miongoni mwao. 925:9 Kut 26:30; 27:8; 31:11; 39:42-43; 1Nya 28:11, 19; Mdo 7:44; Ebr 8:5; Hes 8:4Tengeneza hema hili na vyombo vyake vyote sawasawa na kielelezo nitakachokuonyesha.

Sanduku La Agano

(Kutoka 37:1-9)

1025:10 Kum 10:1-5; 1Fal 6:19; Ebr 9:4“Nao watatengeneza Sanduku la mbao za mshita, lenye urefu wa dhiraa mbili na nusu,25:10 Dhiraa mbili na nusu ni sawa na sentimita 112.5. upana wa dhiraa moja na nusu,25:10 Dhiraa moja na nusu ni sawa na sentimita 67.5. na kimo cha dhiraa moja na nusu. 1125:11 Kut 30:3-4Utalifunika hilo Sanduku kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulifanyia ukingo wa dhahabu juu yake kulizunguka. 12Utalisubu kwa pete nne za dhahabu na kuzifungia kwenye miguu yake minne, pete mbili kwa upande mmoja na pete mbili kwa upande mwingine. 1325:13 Kut 27:6; 30:5; 37:28Kisha utatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuzifunika kwa dhahabu. 1425:14 Kut 27:7; 40:20; 1Nya 15:15Utaiingiza hiyo mipiko kwenye zile pete katika pande mbili za Sanduku ili kulibeba. 1525:15 1Fal 8:8Hiyo mipiko itabakia daima katika hizo pete za hilo Sanduku; haitaondolewa. 1625:16 Kut 16:34; 1Fal 8:8; Kum 31:26Kisha weka ndani ya hilo Sanduku ule Ushuhuda nitakaokupa.

1725:17 Law 16:13; Rum 3:25“Tengeneza kifuniko cha upatanisho cha dhahabu safi, chenye urefu wa dhiraa mbili na nusu, na upana wa dhiraa moja na nusu. 1825:18 Kut 26:1, 35; 1Fal 6:23-27; 2Nya 3:10-13; Ebr 9:5Tengeneza makerubi wawili wa dhahabu iliyofuliwa katika miisho ya hicho kifuniko. 19Tengeneza kerubi mmoja kwenye mwisho mmoja, na kerubi mwingine kwenye mwisho mwingine; watengeneze makerubi hao wawe kitu kimoja na hicho kifuniko katika miisho hiyo miwili. 2025:20 Mwa 3:24; Kut 37:9; 1Fal 8:7; 1Nya 28:18; Ebr 9:5Makerubi hao watakuwa wametandaza mabawa kuelekea juu, yakitia kivuli hicho kifuniko. Makerubi hao wataelekeana, wakitazama hicho kifuniko. 2125:21 Kut 26:34; 40:20; Kum 10:5; Kut 16:34; Ebr 9:4Weka huo Ushuhuda nitakaokupa ndani ya hilo Sanduku la Agano, na uweke hicho kifuniko juu ya hilo Sanduku. 2225:22 Hes 7:89; 1Sam 4; 4; 2Sam 6:2; 22:11; 2Fal 19:15; 1Nya 13:6; 28:18; Za 18:10; Isa 37:16; Kut 19:3; 29:42; 30:6, 36; Law 16:2; Hes 17:4Hapo juu ya hicho kifuniko, kati ya hao makerubi wawili walioko juu ya hilo Sanduku la Ushuhuda, hapo ndipo nitakapokutana nawe na kukupa maagizo yangu kwa ajili ya Waisraeli.

Meza Ya Mikate Ya Wonyesho

(Kutoka 37:10-16)

2325:23 Yer 3:16; Kut 26:35; 40:4, 22; Law 24:6; Hes 3:31; 1Fal 7:48; 1Nya 28:16; 2Nya 4:8, 19; Eze 41:22; 44:16; Ebr 9:2“Tengeneza meza ya mbao za mshita yenye urefu wa dhiraa mbili,25:23 Dhiraa mbili ni sawa na sentimita 90. upana wa dhiraa moja, na kimo cha dhiraa moja na nusu. 24Ifunike kwa dhahabu safi, na kuitengenezea ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote. 25Kisha tengeneza upapi wenye upana wa nyanda nne,25:25 Nyanda nne ni sawa na sentimita 8. na ufanyie ule upapi ukingo wa dhahabu kuuzunguka pande zote. 26Tengeneza pete nne za dhahabu kwa ajili ya meza hiyo, na uzifungie kwenye pembe nne, pale penye miguu yake minne. 27Pete hizo zitakuwa karibu na ukingo ule ili kuishikilia ile mipiko itakayotumika kuibebea hiyo meza. 28Tengeneza mipiko hiyo kwa mbao za mshita, uifunike na dhahabu, uitumie kubeba hiyo meza. 2925:29 Hes 4:7Tengeneza sahani zake na masinia yake kwa dhahabu safi, pamoja na bilauri na bakuli zake kwa ajili ya kumiminia sadaka. 3025:30 Kut 35:13; 39:36; 40:4, 23; Law 24:5-9; Hes 4:7; 1Sam 21:4-6; 1Fal 7:48; 1Nya 23:29Utaweka mikate ya Wonyesho juu ya meza hii iwe mbele yangu daima.

Kinara Cha Taa

(Kutoka 37:17-24)

3125:31 Kut 26:35; 31:8; 35:14; 39:37; Law 24:4; Hes 3:31; 1Fal 7:49; 2Nya 4:7; Zek 4:2; Ebr 9:2; Ufu 1:12“Tengeneza kinara cha taa cha dhahabu safi iliyofuliwa vizuri katika kitako chake na ufito wake; vikombe vyake vinavyofanana na ua, matovu yake na maua yake viwe kitu kimoja. 3225:32 Hes 8:4; Kut 37:18, 19Matawi sita yatatokeza kuanzia ule ufito wa katikati wa kinara cha taa: matawi matatu upande mmoja na matatu upande mwingine. 33Vikombe vitatu vya mfano wa maua ya mlozi yenye matovu na maua vitakuwa katika tawi moja, vikombe vitatu katika tawi jingine, na vivyo hivyo kwa matawi yote sita yanayotokeza kwenye kile kinara cha taa. 34Juu ya kinara chenyewe vitakuwepo vikombe vinne vya mfano wa maua ya mlozi yakiwa na matovu yake na maua yake. 35Tovu moja litakuwa chini ya jozi ya kwanza ya matawi yaliyotokeza kwenye kinara cha taa, tovu la pili chini ya jozi ya pili, nalo tovu la tatu chini ya jozi ya tatu, yaani matawi sita kwa jumla. 3625:36 Hes 8:4Matovu na matawi yote yatakuwa kitu kimoja na kile kinara cha taa, yakifuliwa kwa dhahabu safi.

3725:37 Kut 27:21; 30:8; Law 24:3-4; Hes 8:2; 1Sam 3:3; 2Nya 13:11; Ufu 1:12“Kisha tengeneza taa zake saba na uziweke juu ya kinara hicho ili ziangaze mbele yake. 3825:38 Hes 4:9Mikasi ya kusawazishia tambi, pamoja na masinia, zote zitakuwa za dhahabu safi. 39Utatumia talanta moja25:39 Talanta moja ya dhahabu ni sawa na kilo 34. ya dhahabu safi kutengeneza hicho kinara na vifaa vyake vyote. 4025:40 Hes 8:4; Mdo 7:44; Ebr 8:5; Kut 26:30; 1Nya 28:11, 19Hakikisha kuwa umevitengeneza sawasawa na ule mfano ulioonyeshwa kule mlimani.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

出埃及记 25:1-40

奉献的条例

1耶和华对摩西说: 2“你去告诉以色列百姓要献礼物给我。你们要为我收下所有甘愿献上的礼物。 3你们要收的礼物是金,银,铜, 4细麻线,山羊毛,蓝色、紫色和朱红色的线, 5染成红色的公羊皮,海狗皮,皂荚木, 6灯油,制作膏油和香的香料, 7用来镶嵌在以弗得和胸牌上的红玛瑙及其他宝石。 8要为我造一座圣所,我好住在他们中间。 9你们要照我的指示去造圣幕和里面各样的器具。

造约柜的条例

10“要用皂荚木做一个柜,长一点一米,宽六十六厘米,高六十六厘米, 11里外都要包上纯金,要用金子镶柜边。 12再造四个金环,安在柜的四个脚上,每边两个环。 13用皂荚木造两根横杠,外面要包上金, 14然后把横杠穿过柜旁的金环,便于抬柜。 15横杠穿进环以后,不可再抽出来。 16把我将要赐给你的两块约版放在柜里。 17要用纯金造一个施恩25:17 施恩”或译“赎罪”。座,长一点一米,宽六十六厘米。 18用纯金在施恩座的两端打造两个基路伯天使, 19跟施恩座连在一起,一端一个。 20两个基路伯天使要面对面朝向施恩座,向上展开翅膀,遮盖施恩座。 21要把施恩座放在柜上面,把我赐给你的约版放在柜里。 22我就在那里跟你会面,从两个基路伯天使中间的施恩座上,把要传给以色列百姓的一切诫命告诉你。

造供桌的条例

23“要用皂荚木造一张桌子,长八十八厘米,宽四十四厘米,高六十六厘米。 24整张桌子都要包上纯金,四周镶上金边, 25在桌子四周造一个八厘米宽的外框,上面也镶上金边。 26要造四个金环,安在桌子四角的桌腿上, 27金环要靠近外框,以便穿横杠抬桌子。 28两根横杠要用皂荚木制作,外面包金,用来抬桌子。 29你们要用纯金造桌子上的盘、碟和献酒用的杯和瓶。 30桌子上要一直摆着供饼,献在我面前。

造灯台的条例

31“要用纯金造一个灯台,灯台的灯座、灯柱、油杯、花瓣和花苞要用一块纯金打造。 32灯台的两边要各伸出三个分枝,共六个分枝。 33每个分枝要伸出三个杏花形状、有花瓣和花苞的杯,六个分枝都是这样。 34灯台上要有四个杏花形状、有花瓣和花苞的杯。 35灯台上每一对分枝的相连处要有花苞,三对都是这样。 36整座灯台,包括一切装饰,都要用一块纯金打造。 37此外,要为灯台造七个灯盏,放在灯台上面,照亮前面的地方。 38灯台用的灯剪和灯花盘都要用纯金造。 39造整座灯台和灯台的器具要用三十四公斤纯金。 40你务要照着在山上指示你的样式造这些器具。