Kutoka 2 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Kutoka 2:1-25

Kuzaliwa Kwa Mose

12:1 Mwa 29:34; Kut 6:20; Hes 26:29Basi mtu mmoja wa nyumba ya Lawi akaoa mwanamke Mlawi, 22:2 Mwa 39:6; Ebr 11:23naye mwanamke huyo akapata mimba, akazaa mtoto wa kiume. Alipoona mtoto huyo ni mzuri, akamficha kwa miezi mitatu. 32:3 Isa 18:2; Mwa 6:14; 41:2; Ay 8:11; Mdo 7:21Lakini alipoona hawezi kumficha zaidi, akamtengenezea kisafina cha mafunjo, akakipaka lami. Kisha akamweka huyo mtoto ndani yake, akakificha katikati ya matete kando ya ukingo wa Mto Naili. 42:4 Kut 15:20Dada ya huyo mtoto akasimama mbali ili kuona kitakachompata mtoto.

52:5 Kut 7:15; 8:20Ndipo binti Farao akateremka mtoni Naili kuoga, nao wahudumu wake wakawa wanatembea ukingoni mwa mto. Binti mfalme akaona kisafina katikati ya manyasi, akamtuma mmoja wa watumwa wake wa kike kukichukua. 6Alifungua kisafina akaona mtoto ndani yake. Mtoto alikuwa akilia, akamhurumia. Akasema, “Huyu ni mmoja wa watoto wa Kiebrania.”

7Ndipo dada wa huyo mtoto akamuuliza binti Farao, “Je, niende nikakutafutie mmoja wa wanawake wa Kiebrania akulelee huyu mtoto?”

8Binti Farao akamjibu, “Ndiyo, nenda.” Yule msichana akaenda akamleta mama wa mtoto. 9Binti Farao akamwambia, “Mchukue huyu mtoto unisaidie kumlea, nami nitakulipa.” Basi yule mwanamke akamchukua mtoto na kumlea. 102:10 1Sam 1:20; 2Sam 22:17Mtoto alipokua, akampeleka kwa binti Farao, naye akawa mwanawe. Akamwita jina lake Mose akisema, “Nilimtoa kwenye maji.”

Mose Akimbilia Midiani

112:11 Mdo 7:23; Ebr 11:24-26; Kut 1:11Siku moja, baada ya Mose kukua, akaondoka kwenda walikokuwa watu wake, na akachunguza jinsi walivyokuwa wakifanya kazi ngumu. Akamwona Mmisri akimpiga Mwebrania, mmojawapo wa watu wake. 12Mose akatazama huku na huko asione mtu yeyote, akamuua yule Mmisri, akamficha mchangani. 132:13 Mdo 7:26Kesho yake akatoka, akaona Waebrania wawili wakipigana. Akamuuliza yule aliyekosa, “Mbona unampiga Mwebrania mwenzako?”

142:14 Mwa 13:8; Mdo 7:27Yule mtu akamjibu, “Ni nani aliyekufanya mtawala na mwamuzi juu yetu? Je, unataka kuniua kama ulivyomuua yule Mmisri?” Ndipo Mose akaogopa na kuwaza, “Jambo lile nililofanya lazima limefahamika.”

152:15 Kut 4:19; Ebr 11:27; Mwa 31:21Farao aliposikia jambo hili, alijaribu kumuua Mose, lakini Mose akamkimbia Farao na kwenda kuishi katika nchi ya Midiani, akaketi kando ya kisima. 162:16 Kut 3:1; 18:1; Mwa 24:11Kuhani wa Midiani alikuwa na binti saba, nao wakaja kisimani ili kuchota maji na kujaza hori kwa ajili ya kunyweshea mifugo ya baba yao. 172:17 1Sam 30:8; Za 31:2; Mwa 29:10Baadhi ya wachungaji wakaja wakawafukuza hao wasichana. Ndipo Mose akainuka, akawasaidia na kunywesha mifugo yao.

182:18 Kut 3:1; 4:18; 18:5-12; Hes 10:29Hao wasichana waliporudi nyumbani kwa Reueli baba yao, akawauliza, “Imekuwaje leo mmerudi mapema hivyo?”

19Wakamjibu, “Mmisri mmoja alituokoa kutoka mikononi mwa wachungaji. Pia mtu huyo alituchotea maji na kunywesha mifugo.”

202:20 Mwa 18:2-5Akawauliza binti zake, “Yuko wapi? Mbona mmemwacha? Mkaribisheni ale chakula.”

212:21 Kut 4:25; 18:2; Hes 12:1Mose akakubali kukaa kwa huyo mtu, ambaye alimpa Mose binti yake aliyeitwa Sipora amwoe. 222:22 Amu 18:30; Mwa 23:4; Ebr 11:13Sipora alizaa mtoto wa kiume, naye Mose akamwita Gershomu, akisema, “Nimekuwa mgeni katika nchi ya kigeni.”

232:23 Mdo 7:30; Kut 4:19; 1:14; 3:7-9; 6:5; Hes 20:15-16; Kum 26:7; Yak 5:4; Amu 2:18; 1Sam 12:8; Za 5:2; 18:6; 39:12; 81:7Baada ya muda mrefu, mfalme wa Misri akafa. Waisraeli wakalia kwa huzuni katika utumwa wao, walilia na kilio chao cha kutaka msaada kwa ajili ya utumwa kikamfikia Mungu. 242:24 Mwa 8:1; 9:15; 15:15; 17:4; 22:16-18; 26:3; 28:13-15; Kut 32:13; 2Fal 13:23; Za 105:10, 42; Yer 14:21Mungu akasikia kilio chao cha huzuni, akakumbuka Agano alilofanya na Abrahamu pamoja na Isaki na Yakobo. 252:25 Kut 3:7; 4:31; Lk 1:25Kwa hiyo Mungu akawaangalia Waisraeli na kuwahurumia.