Kutoka 15 – NEN & KJV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Kutoka 15:1-27

Wimbo Wa Mose Na Miriamu

115:1 Hes 21:17; Amu 5:3; 2Sam 22:1; 1Nya 16:9; Ay 36:24; Za 59:16; 105:2; Ufu 15:3; Za 13:6; 21:13; 27:6; 61:8; 104:33; 106:12; Isa 12:5-6; 42:10; 44:23; Kum 11:4; Za 76:6; Yer 51:21; Kut 14:27; Yn 2:11Ndipo Mose na Waisraeli wakamwimbia Bwana wimbo huu:

“Nitamwimbia Bwana,

kwa kuwa ametukuzwa sana.

Farasi na mpanda farasi

amewatosa baharini.

215:2 Za 18:1; 59:17; Mwa 45:7; Kut 14:13; Za 18:2, 46; 25:5; 62:2; 118:14; Isa 12:2; 33:2; Yn 2:9; Hab 3:18; Mwa 28:21; Kum 10:21; 2Sam 22:47; Za 22:3; 34:3; 35:27; 99:5; 103:19; 107:32; 108:5; 118:28; 145:11; 148:14; Isa 24:15; Yer 17:14; Dan 4:37Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu;

amekuwa wokovu wangu.

Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu,

Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza.

315:3 Kut 14:14; 3:15; Ufu 19:11Bwana ni shujaa wa vita;

Bwana ndilo jina lake.

415:4 Kut 14:6-7; Yer 51:21Magari ya vita ya Farao na jeshi lake

amewatosa baharini.

Maafisa wa Farao walio bora sana

wamezamishwa katika Bahari ya Shamu.

515:5 Kut 14:28; Neh 9:11Maji yenye kina yamewafunika,

wamezama mpaka vilindini kama jiwe.

615:6 Za 16:11; 17:7; 21:8; 63:8; 74:11; 77:10; 89:13; 118:15; 138:7; Kut 3:20; Ay 40:14; Hes 24:8; 1Sam 2:10; Za 2:9“Mkono wako wa kuume, Ee Bwana

ulitukuka kwa uweza.

Mkono wako wa kuume, Ee Bwana,

ukamponda adui.

715:7 Kum 33:26; Za 150:2; 2:5; 78:49-50; Yer 12:13; 25:38; Kut 24:17; Kum 4:24; 9:3; Za 18:8; 59:13; Ebr 12:29Katika ukuu wa utukufu wako,

ukawaangusha chini wale waliokupinga.

Uliachia hasira yako kali,

ikawateketeza kama kapi.

815:8 Kut 14:21; Za 18:15; Yos 3:13; Za 78:13; Isa 43:16; Kut 14:22; Za 46:2Kwa pumzi ya pua zako

maji yalijilundika.

Mawimbi ya maji yakasimama imara kama ukuta,

vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari.

915:9 Kut 14:5-9; Kum 28:45; Za 7:5; Mao 1:3; Amu 5:30; Isa 9:3; 53:12; Lk 11:22“Adui alijivuna,

‘Nitawafuatia, nitawapata.

Nitagawanya nyara;

nitajishibisha kwa wao.

Nitafuta upanga wangu

na mkono wangu utawaangamiza.’

1015:10 Neh 9:11; Za 32:6; Ay 4:9; 15:30; Isa 11:4; 30:33; 40:7; Za 29:3Lakini ulipuliza kwa pumzi yako,

bahari ikawafunika.

Wakazama kama risasi

kwenye maji makuu.

1115:11 Kut 8:10; Za 77:13; 99:3; 110:3; 4:2; 26:8; Isa 46:5; 35:2; 40:5; Law 19:2; 1Sam 2:2; 1Nya 16:29; Isa 6:3; Ufu 4:8; Kut 3:20“Ni nani miongoni mwa miungu aliye kama wewe, Ee Bwana?

Ni nani kama Wewe:

uliyetukuka katika utakatifu,

utishaye katika utukufu,

ukitenda maajabu?

1215:12 Kut 7:5; Hes 16:32; 26:10; Kum 11:6; Za 106:17Uliunyoosha mkono wako wa kuume

na nchi ikawameza.

1315:13 Neh 9:12; Za 77:20; Kut 6:6; Ay 33:28; Za 71:23; 106:10; Isa 1:27; 41:14; 43:14; 44:22-24; 51:10; 63:9; Tit 2:14; Za 68:16; 76:2; 78:54“Katika upendo wako usiokoma utawaongoza

watu uliowakomboa.

Katika nguvu zako utawaongoza

mpaka makao yako matakatifu.

1415:14 Kut 23:27; Kum 2:25; Yos 2:9; 9:24; 1Sam 4:7; Es 8:17; Za 48:6; 96:9; 99:1; 114:7; Eze 38:20; Isa 13:8; Za 83:7Mataifa watasikia na kutetemeka,

uchungu utawakamata watu wa Ufilisti.

1515:15 Mwa 36:15; Kum 2:4; Hes 22:3; Za 114:7; Yos 2:9, 24Wakuu wa Edomu wataogopa,

viongozi wa Moabu watatetemeka kwa hofu,

watu wa Kanaani watayeyuka,

1615:16 Mwa 35:5; 1Sam 25:37; Za 74:2; 2Pet 2:1-2; Kum 2:4; Yos 2:9vitisho na hofu vitawaangukia.

Kwa nguvu ya mkono wako

watatulia kama jiwe,

mpaka watu wako waishe kupita, Ee Bwana,

mpaka watu uliowanunua wapite.

1715:17 Kut 23:20; 32:34; 33:12; 2Sam 7:10; Za 44:2; 80:8; Isa 5:2; 60:21; Yer 2:21; 11:17; 24:6; Amo 9:15; Kum 33:19; Za 2:6; 3:4; 78:54-68; 133:3; Dan 9:16; Yoe 2:1; Oba 1:16; Sef 3:11; Za 132:13-14; 78:69; 114:2Utawaingiza na kuwapandikiza

juu ya mlima wa urithi wako:

hapo mahali, Ee Bwana, ulipopafanya kuwa makao yako,

mahali patakatifu, Ee Bwana, ulipopajenga kwa mikono yako.

1815:18 Mwa 21:33; Za 9:7; 29:10; 55:19; 66:7; 80:1; 102:12; 145:13; Mao 5:19Bwana atatawala

milele na milele.”

1915:19 Kut 14:28; 14:22Farasi wa Farao, magari yake ya vita na wapanda farasi wake walipoingia baharini, Bwana aliyarudisha maji ya bahari yakawafunika, lakini wana wa Israeli walipita baharini mahali pakavu. 2015:20 Kut 2:4; Hes 12:1; 20:1; 26:59; 1Nya 4:17; 6:3; Amu 4:4; 2Fal 22:14; 2Nya 34:22; Neh 6:14; Isa 8:3; Eze 13:17; Mwa 31:27; 1Sam 18:6; Za 81:2; Isa 30:32; Mwa 4:21; Amu 11:34; 21:21; 2Sam 6:8-16; Za 30:11; 149:3; Wim 6:13; Yer 31:4, 13Kisha Miriamu yule nabii mke, ndugu yake Aroni, akachukua matari mkononi mwake na wanawake wote wakamfuata na matari yao wakicheza. 2115:21 1Sam 18:17; Amo 2:15; Hag 2:22; Kut 14:27; 15:1Miriamu akawaimbia:

“Mwimbieni Bwana,

kwa maana ametukuka sana.

Farasi na mpanda farasi

amewatosa baharini.”

Maji Ya Mara Na Elimu

2215:22 Za 78:52; Mwa 16:7; Kut 17:1-3; Hes 20:2-5; 33:14; Za 107:5Kisha Mose akawaongoza Israeli kutoka Bahari ya Shamu na kuingia katika Jangwa la Shuri. Kwa siku tatu walisafiri jangwani bila kupata maji. 2315:23 Hes 33:8; Rut 1:20Walipofika Mara, hawakuweza kunywa maji yake kwa sababu yalikuwa machungu. (Ndiyo sababu mahali hapo panaitwa Mara15:23 Mara maana yake ni Chungu.) 2415:24 Kut 14:12; 16:2; Hes 14:2; Yos 9:18; Za 78:18, 42; 106:13, 25; Eze 16:43; Mt 6:31Kwa hiyo watu wakamnungʼunikia Mose, wakisema, “Tunywe nini?”

2515:25 Kut 14:10; 2Fal 2:21; 4:41; Amu 3:4; Ay 23:10; Za 81:7; Isa 48:10Ndipo Mose akamlilia Bwana, naye Bwana akamwonyesha kipande cha mti. Akakitupa ndani ya maji, nayo maji yakawa matamu.

Huko Bwana akawapa amri na sheria na huko akawajaribu. 2615:26 Kut 32:22; Kum 11:13; 15:5; Yer 11:6; Kut 19:5-6; 20:2-7; Kum 7:12, 15; 28:27, 58; 32:39; 1Sam 5:6; Za 30:2; 41:3-4; 103:3; Kut 23:25-26; 2Fal 20:5; Za 25:11; 107:20; Yer 30:17; Hos 11:3Mungu akasema, “Kama mkisikiliza kwa bidii sauti ya Bwana Mungu wenu na kuyafanya yaliyo sawa machoni pake, kama mkiyatii maagizo yake na kuzishika amri zake zote, sitaleta juu yenu ugonjwa wowote niliowaletea Wamisri, kwa kuwa Mimi ndimi Bwana, niwaponyaye.”

2715:27 Hes 33:9Kisha wakafika Elimu, mahali palipokuwa na chemchemi kumi na mbili, na miti sabini ya mitende, wakapiga kambi huko karibu na maji.

King James Version

Exodus 15:1-27

1Then sang Moses and the children of Israel this song unto the LORD, and spake, saying, I will sing unto the LORD, for he hath triumphed gloriously: the horse and his rider hath he thrown into the sea. 2The LORD is my strength and song, and he is become my salvation: he is my God, and I will prepare him an habitation; my father’s God, and I will exalt him. 3The LORD is a man of war: the LORD is his name. 4Pharaoh’s chariots and his host hath he cast into the sea: his chosen captains also are drowned in the Red sea. 5The depths have covered them: they sank into the bottom as a stone. 6Thy right hand, O LORD, is become glorious in power: thy right hand, O LORD, hath dashed in pieces the enemy. 7And in the greatness of thine excellency thou hast overthrown them that rose up against thee: thou sentest forth thy wrath, which consumed them as stubble. 8And with the blast of thy nostrils the waters were gathered together, the floods stood upright as an heap, and the depths were congealed in the heart of the sea. 9The enemy said, I will pursue, I will overtake, I will divide the spoil; my lust shall be satisfied upon them; I will draw my sword, my hand shall destroy them.15.9 destroy: or, repossess 10Thou didst blow with thy wind, the sea covered them: they sank as lead in the mighty waters. 11Who is like unto thee, O LORD, among the gods? who is like thee, glorious in holiness, fearful in praises, doing wonders?15.11 gods: or, mighty ones? 12Thou stretchedst out thy right hand, the earth swallowed them. 13Thou in thy mercy hast led forth the people which thou hast redeemed: thou hast guided them in thy strength unto thy holy habitation. 14The people shall hear, and be afraid: sorrow shall take hold on the inhabitants of Palestina. 15Then the dukes of Edom shall be amazed; the mighty men of Moab, trembling shall take hold upon them; all the inhabitants of Canaan shall melt away. 16Fear and dread shall fall upon them; by the greatness of thine arm they shall be as still as a stone; till thy people pass over, O LORD, till the people pass over, which thou hast purchased. 17Thou shalt bring them in, and plant them in the mountain of thine inheritance, in the place, O LORD, which thou hast made for thee to dwell in, in the Sanctuary, O Lord, which thy hands have established. 18The LORD shall reign for ever and ever. 19For the horse of Pharaoh went in with his chariots and with his horsemen into the sea, and the LORD brought again the waters of the sea upon them; but the children of Israel went on dry land in the midst of the sea.

20¶ And Miriam the prophetess, the sister of Aaron, took a timbrel in her hand; and all the women went out after her with timbrels and with dances. 21And Miriam answered them, Sing ye to the LORD, for he hath triumphed gloriously; the horse and his rider hath he thrown into the sea.

22So Moses brought Israel from the Red sea, and they went out into the wilderness of Shur; and they went three days in the wilderness, and found no water.

23¶ And when they came to Marah, they could not drink of the waters of Marah, for they were bitter: therefore the name of it was called Marah.15.23 Marah: that is Bitterness 24And the people murmured against Moses, saying, What shall we drink? 25And he cried unto the LORD; and the LORD shewed him a tree, which when he had cast into the waters, the waters were made sweet: there he made for them a statute and an ordinance, and there he proved them, 26And said, If thou wilt diligently hearken to the voice of the LORD thy God, and wilt do that which is right in his sight, and wilt give ear to his commandments, and keep all his statutes, I will put none of these diseases upon thee, which I have brought upon the Egyptians: for I am the LORD that healeth thee.

27¶ And they came to Elim, where were twelve wells of water, and threescore and ten palm trees: and they encamped there by the waters.