Kumbukumbu 32 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Kumbukumbu 32:1-52

132:1 Za 49:1; Mik 1:2; Yer 2:12; Kum 4:26; Isa 1:2Sikilizeni, enyi mbingu, nami nitasema;

sikia, ee nchi, maneno ya kinywa changu.

232:2 2Sam 23:4; Za 107:20; Isa 9:8; 55:11; Mik 5:7; Za 65:10; 68:9; 72:8; 147:8Mafundisho yangu na yanyeshe kama mvua,

na maneno yangu na yashuke kama umande,

kama manyunyu juu ya majani mabichi,

kama mvua tele juu ya mimea myororo.

332:3 Za 118:17; 145:6; Kut 33:16-19; 34:4-6; Kum 3:24Nitalitangaza jina la Bwana.

Naam, sifuni ukuu wa Mungu wetu!

432:4 Mwa 49:24; 2Sam 22:31; Za 18:30; 19:7; Kum 4:35; Za 92:15; Mwa 18:25Yeye ni Mwamba, kazi zake ni kamilifu,

njia zake zote ni haki.

Mungu mwaminifu ambaye hakosei,

yeye ni mnyofu na mwenye haki.

532:5 Kum 31:29; Mt 17:17; Lk 9:41; Mdo 2:40Wamefanya mambo ya upotovu mbele zake;

kwa aibu yao, wao si watoto wake tena,

lakini ni kizazi kilicho kiovu na kilichopotoka.

632:6 Za 116:12; 94:8; Yer 5:21; Kut 4:22; 2Sam 7:24; Isa 63:16Je, hii ndiyo njia ya kumlipa Bwana,

enyi watu wajinga na wasio na busara?

Je, yeye siye Baba yenu, Muumba wenu,

aliyewafanya ninyi na kuwaumba?

732:7 Za 44:1; 74:2; 74:2; 77:5; Isa 51:9; 63:9; Kum 4:32; Yos 8:8; 20:4; Za 78:4; Isa 46:9; Kut 10:2; 13:14; Ay 15:18Kumbuka siku za kale;

tafakari vizazi vya zamani vilivyopita.

Uliza baba yako, naye atakuambia,

wazee wako, nao watakueleza.

832:8 Za 7:8; Mwa 11:8; Mdo 8:1; Za 74:17; Hes 23:9; Kum 33:12; 28; Yer 23:6; Mdo 17:26Aliye Juu Sana alipowapa mataifa urithi wao,

alipogawanya wanadamu wote,

aliweka mipaka kwa ajili ya mataifa

sawasawa na hesabu ya wana wa Israeli.

932:9 Za 16:5; 73:26; 119:57; 142:5; Yer 10:16; Kum 9:29; 1Sam 26:19; 1Fal 8:51-53Kwa kuwa fungu la Bwana ni watu wake,

Yakobo kura yake ya urithi.

1032:10 Kum 1:19; 8:15; Ay 12:24; Za 107:40; 32:10; Yer 31:22; Za 17:8; Mit 7:2; Hos 13:5; Zek 2:8Katika nchi ya jangwa alimkuta,

katika nyika tupu ivumayo upepo.

Alimhifadhi na kumtunza;

akamlinda kama mboni ya jicho lake,

1132:11 Kut 19:4; Za 17:8; 18:10-19; 61:4kama tai avurugaye kiota chake,

na kurukaruka juu ya makinda yake,

ambaye hutanda mabawa yake kuwadaka,

na huwachukua kwenye mabawa yake.

1232:12 Za 106:9; Isa 63:13; Yer 31:32; Kum 4:35; Amu 2:12; Za 18:31; 81:9; Isa 43:12; 45:5Bwana peke yake alimwongoza;

hakuwepo mungu mgeni pamoja naye.

1332:13 Kum 33:29; 2Sam 22:34; Za 18:33; Isa 33:16; 58:14; Eze 36:2; Ebr 3:19; Kum 8:8; 33:24; Ay 29:6Akamfanya apande sehemu zilizoinuka za nchi,

akamlisha kwa mavuno ya mashamba.

Akamlea kwa asali toka mwambani,

na kwa mafuta kutoka mwamba mgumu,

1432:14 Hes 21:33; Za 65:9; 81:16; 147:14; Mwa 49:11kwa jibini na maziwa kutoka makundi ya ngʼombe

na kutoka makundi ya mbuzi,

kwa mafuta ya wana-kondoo na mbuzi,

kwa kondoo dume wazuri wa Bashani,

na kwa ngano nzuri.

Ukanywa damu ya zabibu inayotoa povu.

1532:15 Kum 33:5; 26; Isa 44:2; Kum 31:20; Yer 5:28; Kum 31:16; Isa 1:4, 28; 58:2; 65:11; Yer 15:6; Eze 14:5; Mwa 49:24Yeshuruni32:15 Yeshuruni maana yake ni Yeye aliye mnyofu, yaani Israeli (ona pia Kum 33:26; Isa 44:2). alinenepa na kupiga teke;

alikuwa na chakula tele,

akawa mzito na akapendeza sana.

Akamwacha Mungu aliyemuumba,

na kumkataa Mwamba Mwokozi wake.

1632:16 1Kor 10:22; Kum 31:17; 1Fal 14:9Wakamfanya Mungu kuwa na wivu kwa miungu yao migeni,

na kumkasirisha kwa sanamu zao

za machukizo.

1732:17 Kut 32:8; 22:20; 1Kor 10:20; Kum 28:64; Amu 5:8Wakatoa dhabihu kwa pepo, ambao si Mungu:

miungu wasiyoijua,

miungu iliyojitokeza siku za karibuni,

miungu ambayo baba zenu hawakuiogopa.

1832:18 Amu 3:7; 1Sam 12:9; Za 44:17, 20; 106:21; Yer 2:32; Eze 23:35; Hos 8:14; 13:6Mkamwacha Mwamba, aliyewazaa ninyi;

mkamsahau Mungu aliyewazaa.

1932:19 Law 26:30; Za 78:59; Amo 6:8; Yer 44:21-23; Za 106:40Bwana akaona hili, akawakataa,

kwa sababu alikasirishwa

na wanawe na binti zake.

2032:20 Kum 31:17; Za 4:6; 44:24; Kum 9:23Akasema, “Nitawaficha uso wangu,

nami nione mwisho wao utakuwa nini,

kwa kuwa wao ni kizazi kilichopotoka,

watoto ambao si waaminifu.

2132:21 Hes 25:11; 1Kor 10:22; 1Fal 16:13, 26; 2Fal 17:15; Yer 8:19; Yon 2:8; Rum 10:19; Za 31:6; Yer 2:8; 10:8; 16:19Wamenifanya niwe na wivu

kwa kile ambacho si mungu,

na kunikasirisha kwa sanamu zao

zisizokuwa na thamani.

Nitawafanya wawaonee wivu wale ambao si taifa.

Nitawafanya wakasirishwe

na taifa lile lisilo na ufahamu.

2232:22 Za 7:11; Hes 16:31-35; Za 18:7-8; Yer 15:14; Mao 4:11; Amo 7:4; Law 26:20Kwa maana moto umewashwa kwa hasira yangu,

ule uwakao hadi kwenye vina vya mauti.

Utateketeza dunia pamoja na mazao yake,

na kuwasha moto katika misingi ya milima.

2332:23 Kum 29:21; 2Sam 22:15; Ay 6:4; Za 7:13; 18:14; 45:5; 77:17; 120:4; Isa 5:28; 49:2; Eze 5:16; Hab 3:9-11“Nitalundika majanga juu yao

na kutumia mishale yangu dhidi yao.

2432:24 Mwa 26:1; 41:55; 42:5; 2Sam 24:13; 1Nya 21:12; Kum 28:22; Za 91:6; Mwa 37:20; Ay 20:16; Za 58:4; Yer 8:17; Amo 5:18-19; Mik 7:17; Ay 20:16Nitatuma njaa kali dhidi yao maradhi mabaya,

yateketezayo na tauni ya kufisha;

nitawapelekea meno makali ya wanyama mwitu,

na sumu ya nyoka wale watambaao mavumbini.

2532:25 Isa 24:17; Yer 14:18; Mao 1:20; Eze 7:15; 2Kor 7:5; 2Nya 36:17; Isa 13:18; Yer 4:31; Mao 2:21Barabarani upanga utawakosesha watoto;

nyumbani mwao hofu itatawala.

Vijana wao wa kiume na wa kike wataangamia,

pia watoto wachanga na wazee wenye mvi.

2632:26 Kum 4:27; Hes 14:12; Ay 18:17; Za 34:16; 37:28; 109:15; Isa 14:20Nilisema ningewatawanya

na kufuta kumbukumbu lao

katika mwanadamu.

2732:27 Kum 9:26-28; Za 140:8; Isa 11:13; Yer 40:2-3Lakini nilihofia dhihaka za adui,

adui asije akashindwa kuelewa,

na kusema, ‘Mikono yetu imeshinda;

Bwana hakufanya yote haya.’ ”

2832:28 Isa 1:3; 5:13; 27:11; Yer 8:7Wao ni taifa lisilo na akili,

hakuna busara ndani yao.

2932:29 Kum 5:29; Za 81:13; Isa 47:7; Mao 1:9Laiti wangekuwa na hekima wangefahamu hili,

na kutambua mwisho wao utakuwa aje!

3032:30 Law 26:8; Amu 2:14; 3:8; 4:2; 10:7; 1Sam 12:9; Hes 21:34; 1Sam 23:7; Za 31:18; 44:12; 106:41; Isa 50:1; 54:6Mtu mmoja angewezaje kufukuza elfu moja,

au wawili kufukuza elfu kumi,

kama si kwamba Mwamba wao amewauza,

kama si kwamba Bwana amewaacha?

3132:31 Mwa 49:24; Kut 14:25Kwa kuwa mwamba wao si kama Mwamba wetu,

sawasawa na vile adui zetu wanavyokiri.

3232:32 Yer 23:14; Ay 6:4; 20:16; Kum 29:18Mzabibu wao unatoka kwenye mzabibu wa Sodoma,

na kutoka kwenye mashamba ya Gomora.

Zabibu zake zimejaa sumu,

na vishada vyake vimejaa uchungu.

3332:33 Za 58:4Mvinyo wao ni sumu ya nyoka,

sumu yenye kufisha ya swila.

3432:34 Ay 14:17; Yer 2:22; Hos 13:12“Je, hili sikuliweka akiba

na kulifungia kwenye vyumba vyangu vya hazina?

3532:35 Mwa 4:24; Yer 51:6; Mwa 30:2; Kut 32:34; Za 54:5; Rum 12:19; Ebr 10:30; Za 17:5; 35:6; 37:31; 38:16; 66:9; 73:2; 94:18; 121:3; Mit 4:19; Yer 23:12; Eze 7:8-9Ni juu yangu kulipiza kisasi; nitalipiza.

Wakati utakapowadia, mguu wao utateleza;

siku yao ya maafa ni karibu,

na maangamizo yao yanawajia haraka.”

3632:36 Ebr 10:30; Amo 7:3; Law 26:43-45; Kum 30:1-3; Amu 2:18; Za 90:13; 102:13; 103:13; 106:45; 135:14; Yoe 2:14; 1Fal 14:10; 21:21; 2Fal 9:8Bwana atawahukumu watu wake,

na kuwahurumia watumishi wake

atakapoona nguvu zao zimekwisha

wala hakuna yeyote aliyebaki,

mtumwa au aliye huru.

3732:37 Amu 10:14; Yer 2:28; 11:12Atasema: “Sasa iko wapi miungu yao,

mwamba walioukimbilia,

3832:38 Hes 25:1-2; Yer 11:12; 44:8; 25miungu wale waliokula mafuta ya dhabihu zao

na kunywa mvinyo wa sadaka zao za vinywaji?

Wainuke basi, wawasaidie!

Wawapeni basi ulinzi!

3932:39 Isa 41:4; 43:10; 44:7; 46:4; 48:12; 1Sam 2:6; 2Fal 5:7; Za 68:20; Yn 11:25-26; Kut 15:26; Ay 5:18; 15:11; Za 147:3; Isa 6:10; 19:22; 30:26; 53:5; 57:18; Yer 33:6; Hos 6:1; Mal 4:2; 1Pet 2:24; Ay 9:12; 10:7; Za 7:2; 50:22; Isa 43:13; Dan 4:35; Hos 5:14“Tazama basi, Mimi mwenyewe, Mimi Ndiye!

Hakuna mungu mwingine ila Mimi.

Mimi ninaua na Mimi ninafufua,

Mimi nimejeruhi na Mimi nitaponya,

wala hakuna awezaye kuokoa kutoka mkononi mwangu.

4032:40 Mwa 14:22; 21:23; Ufu 1:18Ninainua mkono wangu kuelekea mbinguni na kusema:

Hakika kama niishivyo milele,

4132:41 Amu 7:20; Za 7:12; 45:3; Isa 27:1; 34:6; 66:16; Yer 12:12; Eze 21:9-10; Za 149:7; Yer 46:10; Neh 1:2; Za 137:8; Yer 25:14; 50:29; 51:24, 56wakati ninapounoa upanga wangu unaometameta

na mkono wangu unapoushika ili kutoa hukumu,

nitalipiza kisasi juu ya adui zangu

na kuwalipiza wale wanaonichukia.

4232:42 2Sam 2:26; Yer 12:12; 44:1; 46:10-14Nitailevya mishale yangu kwa damu,

wakati upanga wangu ukitafuna nyama:

damu ya waliochinjwa pamoja na mateka,

vichwa vya viongozi wa adui.”

4332:43 Za 137:6; Isa 25:9; 65:18; 66:10; Rum 15:10; 2Fal 9:7; Ufu 6:10; Isa 1:24; Yer 9:9; Za 65:3; 79:9Furahini, enyi mataifa, pamoja na watu wake,

kwa kuwa atailipiza damu ya watumishi wake,

atalipiza kisasi juu ya adui zake

na kufanya upatanisho

kwa ajili ya nchi na watu wake.

4432:44 Hes 13:8, 16Mose na Yoshua32:44 Yoshua, yaani Yehoshea kwa Kiebrania, maana yake ni Yehova ni Mwokozi. mwana wa Nuni wakaja, wakanena maneno yote ya wimbo watu wakiwa wanasikia. 45Mose alipomaliza kuyasoma maneno haya yote kwa Israeli wote, 4632:46 Kum 6:6; Yn 1:17; 7:19; Kum 6:7akawaambia, “Yawekeni moyoni maneno yote ambayo nimewatangazia kwa makini siku hii ya leo, ili kwamba mpate kuwaagiza watoto wenu wayatii kwa bidii maneno yote ya sheria hii. 4732:47 Kum 30:20; 33:25; Kut 23:26; Isa 65:22Siyo maneno matupu tu kwenu, bali ni uzima wenu. Kwa hayo mtaishi maisha marefu katika nchi mnayovuka Yordani kuimiliki.”

Mose Aelezwa Kuhusu Kifo Chake

4832:48 Hes 27:12Siku hiyo hiyo Bwana akamwambia Mose, 4932:49 Hes 27:12; 32:3; 22:1; Law 14:34“Kwea katika mapangano ya Mlima Abarimu hadi kilima cha Nebo kilichoko Moabu, ngʼambo ya Yeriko, na uitazame Kanaani, nchi ninayowapa Waisraeli kama milki yao wenyewe. 5032:50 Mwa 25:8; Hes 27:13; 20:22; 29Utafia kwenye mlima huo unaokwea na kukusanyika pamoja na watu wako, kama ndugu yako Aroni alivyofia juu ya Mlima Hori naye akakusanyika kwa watu wake. 5132:51 Eze 47:19; Hes 13:21; 20:11-13; 27:14Hii ni kwa sababu ninyi wawili mlivunja uaminifu nami mbele ya Waisraeli kwenye maji ya Meriba-Kadeshi katika Jangwa la Sini, na kwa sababu hamkuuinua utakatifu wangu miongoni mwa Waisraeli. 5232:52 Kum 34:1-3; 3:27Kwa hiyo, utaiona tu nchi kwa mbali; wewe hutaingia nchi ninayowapa watu wa Israeli.”