Isaya 43 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Isaya 43:1-28

Mwokozi Pekee Wa Israeli

143:1 Mwa 2:7; 32:28; Isa 45:3-4; Kut 6:6; Isa 42:6; 27:11; Ay 19:25Lakini sasa hili ndilo asemalo Bwana,

yeye aliyekuumba, ee Yakobo,

yeye aliyekuhuluku, ee Israeli:

“Usiogope kwa maana nimekukomboa,

nimekuita wewe kwa jina lako, wewe u wangu.

243:2 Mwa 26:3; Kum 31:6-8; Isa 30:27; 8:7; Dan 3:25-27; Kut 14:22; Isa 29:6Unapopita kwenye maji makuu,

nitakuwa pamoja nawe,

unapopita katika mito ya maji,

hayatakugharikisha.

Utakapopita katika moto,

hutaungua,

miali ya moto haitakuunguza.

343:3 Mit 21:18; Kut 30:2; Isa 20:3; Mwa 10:7; Eze 29:20; Za 68:31; Amu 2:18; Kut 14:30Kwa kuwa Mimi ndimi Bwana, Mungu wako,

yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, Mwokozi wako.

Ninaitoa Misri kuwa fidia yako,

Kushi na Seba badala yako.

443:4 Isa 63:9; Ufu 3:9; Kut 19:5-6; Isa 49:5Kwa kuwa wewe ni wa thamani na wa kuheshimiwa machoni pangu,

nami kwa kuwa ninakupenda,

nitatoa watu badala yako

na mataifa badala ya maisha yako.

543:5 Isa 44:2; Mwa 21:22; Kut 14:22; Mdo 18:10; Yer 30:10-11; Mt 8:11; Zek 8:7; Isa 24:14Usiogope, kwa kuwa mimi nipo pamoja nawe,

nitawaleta watoto wako kutoka mashariki,

na kukukusanya kutoka magharibi.

643:6 Eze 16:61; 2Kor 6:18; Eze 36:24; Yer 23:8; Kum 30:4; Isa 60:4; 11:12Nitaiambia kaskazini, ‘Watoe!’

nayo kusini, ‘Usiwazuie.’

Walete wana wangu kutoka mbali,

na binti zangu kutoka miisho ya dunia:

743:7 Yak 2:7; Isa 29:23; Yer 15:16; Efe 2:10; Isa 56:5; 62:2; 63:19; Za 89:9kila mmoja ambaye ameitwa kwa Jina langu,

niliyemuumba kwa utukufu wangu,

niliyemhuluku na kumfanya.”

843:8 Isa 6:9-10; 42:20; Eze 12:2Uwaongoze wale wenye macho lakini hawaoni,

wenye masikio lakini hawasikii.

943:9 Isa 45:20; 48:14; 41:26Mataifa yote yanakutanika pamoja,

na makabila yanakusanyika.

Ni nani miongoni mwao aliyetangulia kutuambia haya,

na kututangazia mambo yaliyopita?

Walete mashahidi wao ili kuwathibitisha kuwa walikuwa sahihi,

ili wengine waweze kusikia, waseme, “Ni kweli.”

1043:10 Isa 41:8-9; 19:21; Za 86:10; Yer 14:22; Yos 24:22; Kum 4:35; Isa 45:5-6, 14“Ninyi ni mashahidi wangu,” asema Bwana,

“na mtumishi wangu niliyemchagua,

ili mpate kunijua na kuniamini,

na kutambua kwamba Mimi ndiye.

Kabla yangu hakuna mungu aliyefanyizwa,

wala hatakuwepo mwingine baada yangu.

1143:11 Isa 42:8; Za 18:31; Isa 25:9; 63:4; Kut 6:2Mimi, naam mimi, ndimi Bwana,

zaidi yangu hakuna mwokozi.

1243:12 Kum 32:16; Za 81:9; Isa 44:8Nimedhihirisha, kuokoa na kutangaza:

Mimi, wala si mungu mgeni katikati yenu.

Ninyi ni mashahidi wangu,” asema Bwana,

“kwamba Mimi ndimi Mungu.

1343:13 Hes 23:8; Ay 9:12; Za 90:2; Mit 8:23; Kum 32:39; Isa 48:12Naam, tangu siku za kale, Mimi ndiye.

Hakuna hata mmoja awezaye kuokoa

kutoka mkononi wangu.

Mimi ninapotenda,

ni nani awezaye kutangua?”

Huruma Za Mungu, Na Kukosa Uaminifu Kwa Israeli

1443:14 Isa 13:14-15; 23:13; Kut 15:13; Ay 19:25; Isa 41:20Hili ndilo Bwana asemalo,

Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli:

“Kwa ajili yenu nitatumana Babeli

na kuwaleta Wakaldayo wote kama wakimbizi,

katika meli walizozionea fahari.

1543:15 Isa 42:8; 27:11; 45:11; 41:21Mimi ndimi Bwana, yeye Aliye Mtakatifu wako,

Muumba wa Israeli, Mfalme wako.”

1643:16 Kut 14:29; Za 77:19; Kut 15:8; Isa 11:15Hili ndilo asemalo Bwana,

yeye aliyefanya njia baharini,

mahali pa kupita kwenye maji mengi,

1743:17 Za 118:12; Kut 14:4-9, 22; Za 76:5-6; Ay 13:25; Yer 51:21; Eze 38:4aliyeyakokota magari ya vita na farasi,

jeshi pamoja na askari wa msaada,

nao wakalala huko, wala hawatainuka tena kamwe,

wakakomeshwa, na wakazimika kama utambi:

1843:18 Isa 41:22“Msiyakumbuke mambo yaliyopita,

wala msiyatafakari mambo ya zamani.

1943:19 Hes 20:11; Yer 23:8-9; Ufu 21:5; Isa 40:3; 41:22; Yer 16:14-15; 2Kor 5:17; Isa 35:7Tazama, nitafanya jambo jipya!

Sasa litachipuka, je, hamtalitambua?

Nitafanya njia jangwani

na vijito vya maji katika nchi kame.

2043:20 Hes 20:8; Isa 48:21; 41:17; Za 148:10; Isa 13:22Wanyama wa mwituni wataniheshimu,

mbweha na bundi,

kwa sababu ninawapatia maji jangwani,

na vijito katika nchi kame,

ili kuwapa watu wangu maji, wale niliowachagua,

2143:21 Za 66:2; 1Pet 2:9; Mwa 2:7; Mal 3:17; Za 102:18watu wale niliowaumba kwa ajili yangu,

ili wapate kutangaza sifa zangu.

22“Hata hivyo hukuniita mimi, ee Yakobo,

hujajitaabisha kwa ajili yangu, ee Israeli.

2343:23 Zek 7:5-6; Kut 30:35; Yer 7:22; Amo 5:25; Kut 29:41; Mik 6:3; Mal 1:12-13Hujaniletea kondoo kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa,

wala kuniheshimu kwa dhabihu zako.

Sikukulemea kwa sadaka za nafaka

wala kukuchosha kwa kuhitaji uvumba.

2443:24 Kut 30:23; Mal 2:17; Isa 7:13; Yer 8:21; Law 3:9; Yer 44:22Hukuninunulia uvumba wowote wenye manukato,

wala hukunipa kwa ukarimu

mafuta ya wanyama wa dhabihu zako.

Lakini umenilemea kwa dhambi zako,

na kunitaabisha kwa makosa yako.

2543:25 2Sam 12:13; Lk 5:21; Eze 20:44; Yer 31:34; Ay 7:21; 2Nya 6:21; Isa 64:9“Mimi, naam mimi, ndimi nizifutaye dhambi zako,

kwa ajili yangu mwenyewe,

wala sizikumbuki dhambi zako tena.

2643:26 Isa 1:18; 41:1; 49:25; 50:8Tafakari mambo yaliyopita,

njoo na tuhojiane,

leta shauri lako uweze kupewa haki yako.

2743:27 Rum 5:12; Isa 28:7; Yer 5:31; Mwa 12:18; Isa 9:15; 24:20Baba yako wa kwanza alitenda dhambi,

wasemaji wako wameasi dhidi yangu.

2843:28 Eze 5:15; Za 39:8; Hes 5:27; Kum 13:15; Isa 42:24; Zek 5:3; Yer 24:9Kwa hiyo nitawaaibisha wakuu wa Hekalu lako,

nami nitamtoa Yakobo aangamizwe,

na Israeli adhihakiwe.