Isaya 4 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Isaya 4:1-6

14:1 Mwa 30:23; 2The 3:12; Isa 13:12; 32:9; 2:11Katika siku ile wanawake saba

watamshika mwanaume mmoja

wakisema, “Tutakula chakula chetu wenyewe

na kuvaa nguo zetu wenyewe,

ila wewe uturuhusu tu tuitwe kwa jina lako.

Utuondolee aibu yetu!”

Tawi La Bwana

24:2 Zek 6:12; Yer 23:5; Eze 36:8; 17:22; Za 72:16; Isa 11:1-5; 52:13; Yer 33:15-16; Isa 2:11; Yer 23:6; Zek 3:8Katika siku ile Tawi la Bwana litakuwa zuri na lenye utukufu, nalo tunda la nchi litakuwa fahari na utukufu wa wale Waisraeli watakaonusurika. 34:3 Mao 1:17; Sef 3:13; Rum 11:5; Za 56:8; Lk 10:20; Isa 1:26; Kut 19:6; Yoe 3:1-7Wale watakaoachwa Sayuni, watakaobaki Yerusalemu, wataitwa watakatifu, wale wote ambao wameorodheshwa miongoni mwa walio hai huko Yerusalemu. 44:4 Zek 13:9; Isa 3:24; 28:6; 30:30; Mt 3:11; Ufu 7:15Bwana atausafisha uchafu wa wanawake wa Sayuni, atatakasa madoa ya damu kutoka Yerusalemu kwa Roho ya hukumu na Roho ya moto. 54:5 Isa 58:8; Kut 13:21-22; Isa 41:20; 65:18; Ufu 14:1; Isa 35:2; Za 18:11; Ufu 7:15Kisha Bwana ataumba juu ya Mlima wote wa Sayuni, na juu ya wale wote wanaokusanyika hapo, wingu la moshi wakati wa mchana, na kungʼaa kwa miali ya moto wakati wa usiku, nako juu ya huo utukufu wote kutatanda kifuniko cha ulinzi. 64:6 Law 23:34-43; Isa 25:4; 30:2; 57:13; 8:14; Za 27:5; 55:8; Eze 11:16; Isa 14:32Utakuwa sitara na kivuli kutokana na joto la mchana, na kuwa mahali pa kujificha kutokana na dhoruba na mvua.