Isaya 27 – NEN & NIV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Isaya 27:1-13

Wokovu Kwa Ajili Ya Israeli

127:1 Eze 29:3; Mwa 3:24; Hes 3:15; Ufu 12:9; Isa 2:11; Kum 32:41; Ay 26:13; Za 68:30; Isa 28:5; 31:8; 34:6; 66:16; Eze 21:3; Ay 3:8Katika siku ile,

Bwana ataadhibu kwa upanga wake,

upanga wake mkali, mkubwa na wenye nguvu,

ataadhibu Lewiathani27:1 Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa. yule nyoka apitaye kwa mwendo laini,

Lewiathani yule nyoka mwenye kujipinda;

atamuua joka huyo mkubwa sana wa baharini.

227:2 Yer 2:21; Isa 24:21; 5:1Katika siku ile:

“Imbeni kuhusu shamba la mizabibu lililozaa:

327:3 Isa 58:11; Za 91:4; Yn 6:39; Isa 5:2Mimi, Bwana, ninalitunza,

nalinyweshea maji mfululizo.

Ninalichunga usiku na mchana

ili mtu yeyote asije akalidhuru.

427:4 Isa 10:17; Mt 3:12; 2Sam 23:6; Ebr 6:8Mimi sijakasirika.

Licha pangekuwepo michongoma na miiba kunikabili!

Ningepambana dhidi yake katika vita,

ningeliichoma moto yote.

527:5 Isa 25:4; Efe 2:12-14; Ay 22:21; Za 119:165; Rum 5:1; 2Kor 5:20Au niwaache waje kwangu kwa ajili ya kupata kimbilio,

wao na wafanye amani nami,

naam, wafanye amani nami.”

627:6 Mwa 40:10; Hos 14:5-8; Za 72:16; 2Fal 19:30; Eze 17:23; 36:8; Isa 11:1Katika siku zijazo, Yakobo atatia mizizi,

Israeli atatoa chipukizi na kuchanua maua,

naye atajaza ulimwengu wote kwa matunda.

727:7 Isa 10:26; 37:36-38Je, Bwana amempiga

vile alivyowapiga wale waliompiga?

Je, yeye ameuawa

vile walivyouawa wale waliomuua yeye?

827:8 Isa 49:14; Yer 10:24; Ay 23:6; Isa 54:7; Mwa 41:6; Isa 50:1Kwa vita na kwa kumfukuza unapingana naye:

kwa mshindo wake mkali anamfukuza,

kama siku ile uvumapo upepo wa mashariki.

927:9 Kut 34:13; Rum 11:27; Za 78:38; Kut 23:24; 2Nya 14:5; Law 26:30Kwa hili, basi, hatia ya Yakobo itafanyiwa upatanisho,

nalo hili litakuwa matunda ya utimilizo wa kuondolewa kwa dhambi yake:

Wakati atakapoyafanya mawe yote ya madhabahu

kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa vipande vipande,

hakuna nguzo za Ashera au madhabahu za kufukizia uvumba

zitakazobaki zimesimama.

1027:10 Kum 13:16; Isa 17:2; 5:5, 17; Mao 5:18; Yer 26:6; 10:22; Isa 32:14; Mwa 1:2; Kum 13:16; Isa 5:6; 32:14; Yer 10:22; Law 1:4; 5:18; Isa 5:5; 5:17; 17:2Mji ulio na boma umebaki ukiwa,

makao yaliyotelekezwa, yaliyoachwa kama jangwa.

Huko ndama hulisha,

huko hujilaza,

wanakwanyua matawi yake.

1127:11 Kum 32:18, 38; Yer 8:7; 4:22; Isa 9:17; 10:33; Yer 11:16; Isa 33:12; 41:8; 44:21-24Wakati vijiti vyake vimekauka, huvunjwa

nao wanawake huja na kuwasha navyo moto.

Kwa kuwa hili ni taifa lisilo na ufahamu,

kwa hiyo yeye aliyewafanya hana huruma juu yao,

Muumba wao hawaonyeshi fadhili.

1227:12 Mwa 15:18; Kum 30:4; Isa 1:9; Mt 3:12; Isa 21:10; 17:6Katika siku ile Bwana atapura kutoka matiririko ya Mto Frati hadi Kijito cha Misri, nanyi ee Waisraeli, mtakusanywa mmoja mmoja. 1327:13 Hes 10:2; Amu 3:27; Mt 24:31; Isa 10:19; Hos 8:1; Law 25:9; Za 106:47Katika siku ile tarumbeta kubwa italia. Wale waliokuwa wakiangamia katika nchi ya Ashuru, nao wale waliokuwa uhamishoni katika nchi ya Misri watakuja na kumwabudu Bwana katika mlima mtakatifu huko Yerusalemu.

New International Version

Isaiah 27:1-13

Deliverance of Israel

1In that day,

the Lord will punish with his sword—

his fierce, great and powerful sword—

Leviathan the gliding serpent,

Leviathan the coiling serpent;

he will slay the monster of the sea.

2In that day—

“Sing about a fruitful vineyard:

3I, the Lord, watch over it;

I water it continually.

I guard it day and night

so that no one may harm it.

4I am not angry.

If only there were briers and thorns confronting me!

I would march against them in battle;

I would set them all on fire.

5Or else let them come to me for refuge;

let them make peace with me,

yes, let them make peace with me.”

6In days to come Jacob will take root,

Israel will bud and blossom

and fill all the world with fruit.

7Has the Lord struck her

as he struck down those who struck her?

Has she been killed

as those were killed who killed her?

8By warfare27:8 See Septuagint; the meaning of the Hebrew for this word is uncertain. and exile you contend with her—

with his fierce blast he drives her out,

as on a day the east wind blows.

9By this, then, will Jacob’s guilt be atoned for,

and this will be the full fruit of the removal of his sin:

When he makes all the altar stones

to be like limestone crushed to pieces,

no Asherah poles27:9 That is, wooden symbols of the goddess Asherah or incense altars

will be left standing.

10The fortified city stands desolate,

an abandoned settlement, forsaken like the wilderness;

there the calves graze,

there they lie down;

they strip its branches bare.

11When its twigs are dry, they are broken off

and women come and make fires with them.

For this is a people without understanding;

so their Maker has no compassion on them,

and their Creator shows them no favor.

12In that day the Lord will thresh from the flowing Euphrates to the Wadi of Egypt, and you, Israel, will be gathered up one by one. 13And in that day a great trumpet will sound. Those who were perishing in Assyria and those who were exiled in Egypt will come and worship the Lord on the holy mountain in Jerusalem.