Isaya 15 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Isaya 15:1-9

Unabii Dhidi Ya Moabu

115:1 Hes 21:28; 22:3-6; Kum 23:6; Hes 17:12; Yer 51:58; 48:24; 2Fal 3:25Neno kuhusu Moabu:

Ari iliyo Moabu imeangamizwa:

imeharibiwa kwa usiku mmoja!

Kiri iliyo Moabu imeangamizwa,

imeharibiwa kwa usiku mmoja!

215:2 Yer 48:35; Law 21:5; Ay 1:20; Hes 21:20; Isa 16:12; 2Sam 10:4; Law 13:40Diboni anakwea hadi kwenye hekalu lake,

mpaka mahali pake pa juu ili walie,

Moabu anaombolezea Nebo na Medeba.

Kila kichwa kimenyolewa

na kila ndevu limeondolewa.

315:3 Mao 2:11; Mik 1:8; Isa 3:24; Yos 2:8; Yer 48:38; Isa 14:31; Eze 7:18; Yer 47:2Wamevaa nguo za magunia barabarani,

juu ya mapaa na kwenye viwanja

wote wanaomboleza,

wamelala kifudifudi kwa kulia.

415:4 Hes 32:3; 21:23-25; Yos 13:26Heshboni na Eleale wanalia,

sauti zao zinasikika hadi Yahazi.

Kwa hiyo watu wenye silaha wa Moabu wanapiga kelele,

nayo mioyo yao imezimia.

515:5 Isa 16:11; Yer 48:31; 48:3-5; 4:20; Mwa 13:10; Hes 21:29Moyo wangu unamlilia Moabu;

wakimbizi wake wanakimbilia Soari,

hadi Eglath-Shelishiya.

Wanapanda njia ya kwenda Luhithi,

wanakwenda huku wanalia;

barabarani iendayo Horonaimu

wanaombolezea maangamizi yao.

615:6 Isa 19:5-7; Za 37:2; Hos 4:3; Yer 48:34; Isa 16:8; 33:9; 14:17; Yer 14:5Maji ya Nimrimu yamekauka

na majani yamenyauka;

mimea imekauka wala hakuna

kitu chochote kibichi kilichobaki.

715:7 Isa 30:6; Yer 48:36Kwa hiyo mali waliyoipata na kujiwekea akiba

wamezichukua na kuvuka Bonde la Mierebi.

815:8 Hes 21:16Mwangwi wa kilio chao umefika hadi mpakani mwa Moabu,

kilio chao cha huzuni kimefika hadi Eglaimu,

maombolezo yao hadi Beer-Elimu.

915:9 2Fal 17:25; Eze 25:8-11Maji ya Dimoni yamejaa damu,

lakini bado nitaleta pigo jingine juu ya Dimoni:

simba juu ya wakimbizi wa Moabu

na juu ya wale wanaobaki katika nchi.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

以赛亚书 15:1-9

关于摩押的预言

1以下是关于摩押的预言:

摩押亚珥城必在一夜之间被摧毁,沦为废墟;

摩押基珥城必在一夜之间被摧毁,沦为废墟。

2底本城的人上到神庙,

到他们的丘坛痛哭。

摩押人都剃光头发,

刮掉胡须,

尼波米底巴城哀号。

3他们身披麻衣走在街上,

房顶和广场上都传出号啕大哭的声音。

4希实本人和以利亚利人都哭喊,

声音一直传到雅杂

因此摩押的战士大声喊叫,

胆战心惊。

5我为摩押感到悲哀。

她的人民逃难到琐珥伊基拉·施利施亚

他们上到鲁希斜坡,边走边哭,

在去何罗念的路上为自己的不幸哀哭。

6宁林的河道干涸,

青草枯萎,植被消失,毫无绿色。

7因此,摩押人把自己积存的财物都运过柳树河。

8摩押境内哀声四起,

号啕声传到以基莲

传到比珥·以琳

9底门的河里流的都是血,

但我还要降更多灾难给底门

狮子必吞噬逃出摩押的人和那里的余民。