Isaya 14 – NEN & NIVUK

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Isaya 14:1-32

Yuda Kufanywa Upya

114:1 Isa 54:7-8; Zek 10:6; Mwa 18:19; Eze 47:22; Efe 2:12-19; Kut 12:43; Eze 47:22; Zek 8:22-23; Isa 11:10; Yer 3:18; Zek 2:12Bwana atamhurumia Yakobo,

atamchagua Israeli tena,

na kuwakalisha katika nchi yao wenyewe.

Wageni wataungana nao

na kujiunga na nyumba ya Yakobo.

214:2 Isa 11:12; 26:15; 49:7; 49:23; 54:3; 60:9; Sef 3:19; Zek 2:9; Za 49:14Mataifa watawachukua

na kuwaleta mahali pao wenyewe.

Nayo nyumba ya Israeli itamiliki mataifa

kama watumishi na wajakazi katika nchi ya Bwana.

Watawafanya watekaji wao kuwa mateka,

na kutawala juu ya wale waliowaonea.

314:3 Isa 11:10-12; Ay 3:17; Kut 1:14Katika siku Bwana atakapokuondolea mateso, udhia na utumwa wa kikatili, 414:4 Hab 2:6; Mik 2:4; Isa 13:19; 9:4utaichukua dhihaka hii dhidi ya mfalme wa Babeli:

Tazama jinsi mtesi alivyofikia mwisho!

Tazama jinsi ghadhabu yake kali ilivyokoma!

514:5 Isa 10:15; Za 125:3; 110:2Bwana amevunja fimbo ya mwovu,

fimbo ya utawala ya watawala,

614:6 2Fal 15:29; Isa 10:14; Za 47:3; Isa 47:6ambayo kwa hasira waliyapiga mataifa

kwa mapigo yasiyo na kikomo,

nao kwa ghadhabu kali waliwatiisha mataifa

kwa jeuri pasipo huruma.

714:7 Za 126:1-3; Hes 6:26; Yer 50:34; Zek 1:11Nchi zote ziko kwenye mapumziko na kwenye amani,

wanabubujika kwa kuimba.

814:8 1Nya 16:33; Za 65:13; Eze 31:16; 2Fal 19:23; Isa 37:24Hata misunobari na mierezi ya Lebanoni

inashangilia mbele yako na kusema,

“Basi kwa sababu umeangushwa chini,

hakuna mkata miti atakayekuja kutukata.”

914:9 Mit 30:16; Eze 32:21; Ay 26:5; Zek 10:3; Ay 3:14Kuzimu kote kumetaharuki

kukulaki unapokuja,

kunaamsha roho za waliokufa ili kukupokea,

wote waliokuwa viongozi katika ulimwengu,

kunawafanya wainuke kwenye viti vyao vya kifalme:

wale wote waliokuwa wafalme juu ya mataifa.

1014:10 Eze 26:20; 32:21Wote wataitikia,

watakuambia,

“Wewe pia umekuwa dhaifu, kama sisi tulivyo;

wewe umekuwa kama sisi.”

1114:11 Ay 7:5; 24:20; Hes 16:30; Mit 30:16; Isa 5:12; Eze 26:13; Amo 6:5; Ay 21:26Majivuno yako yote yameshushwa mpaka kuzimu,

pamoja na kelele ya vinubi vyako,

mafunza yametanda chini yako,

na minyoo imekufunika.

1214:12 Isa 34:4; 2Pet 1:19; Ufu 2:28; Lk 10:18; Eze 26:17; Ufu 2:28Tazama jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni,

ewe nyota ya asubuhi, mwana wa mapambazuko!

Umetupwa chini duniani,

wewe uliyepata kuangusha mataifa!

1314:13 Mt 11:23; Eze 28:2; 2The 2:4; Dan 8:10; 5:23; Isa 37:24Ulisema moyoni mwako,

“Nitapanda juu hadi mbinguni,

nitakiinua kiti changu cha enzi

juu ya nyota za Mungu,

nitaketi nimetawazwa

juu ya mlima wa kusanyiko,

kwenye vimo vya juu sana vya Mlima Mtakatifu.

1414:14 Hes 24:16; 2The 2:4; Ay 20:6; Isa 47:8; Yer 50:29; Dan 11:38; Isa 10:13Nitapaa juu kupita mawingu,

nitajifanya kama Yeye Aliye Juu Sana.”

1514:15 Mt 11:23; Lk 10:15; Mdo 12:23; Isa 13:6; 47:11; Ay 21:13; Eze 31:16Lakini umeshushwa chini hadi kuzimu,

hadi kwenye vina vya shimo.

1614:16 Yer 50:23; Ufu 18:18; Isa 2:19; 13:13; Yoe 3:16Wale wanaokuona wanakukazia macho,

wanatafakari hatima yako:

“Je, huyu ndiye yule aliyetikisa dunia

na kufanya falme zitetemeke,

1714:17 Isa 15:6; Za 52:7; 2Fal 15:29; Kut 7:14; Yer 50:33; Ufu 18:18yule aliyeifanya dunia kuwa jangwa,

aliyeipindua miji yake,

na ambaye hakuwaachia mateka wake

waende nyumbani?”

1814:18 Ay 21:32Wafalme wote wa mataifa wamelala kwa heshima

kila mmoja katika kaburi lake.

1914:19 Isa 22:16-18; Yer 36:30; Isa 34:3; 13:15; Yer 8:1; 41:7-9Lakini wewe umetupwa nje ya kaburi lako

kama tawi lililokataliwa,

umefunikwa na waliouawa

pamoja na wale waliochomwa kwa upanga,

wale washukao mpaka

kwenye mawe ya shimo.

Kama mzoga uliokanyagwa chini ya nyayo,

2014:20 Ay 18:19; Kum 32:16; Za 21:10; 1Fal 21:19Hutajumuika nao kwenye mazishi,

kwa kuwa umeharibu nchi yako

na kuwaua watu wako.

Mzao wa mwovu

hatatajwa tena kamwe.

2114:21 Mwa 9:25; Kut 20:5; Hes 16:27; Law 26:39Andaa mahali pa kuwachinjia wanawe

kwa ajili ya dhambi za baba zao,

wasije wakainuka ili kuirithi nchi

na kuijaza dunia kwa miji yao.

2214:22 2Sam 18:18; 1Fal 14:10; Za 94:16; Ay 18:17-19; Isa 13:18; Za 109:13Bwana Mwenye Nguvu Zote asema,

“Nitainuka dhidi yao,

nitalikatilia mbali jina lake kutoka Babeli pamoja na watu wake walionusurika,

watoto wake na wazao wake,”

asema Bwana.

2314:23 Law 11:16-18; Sef 2:14; Isa 34:11-15; Yer 25:12; 50:3; 51:62“Nitaifanya kuwa mahali pa bundi,

na kuwa nchi ya matope;

nitaifagia kwa ufagio wa maangamizi,”

asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

Unabii Dhidi Ya Ashuru

2414:24 Isa 62:8; Eze 12:25; Mdo 4:28; Isa 45:23; 23:8-9; Dan 4:35; Isa 46:10-11Bwana Mwenye Nguvu Zote ameapa,

“Hakika, kama vile nilivyopanga, ndivyo itakavyokuwa,

nami kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyosimama.

2514:25 Isa 37:36-37; 10:27; 9:4Nitamponda Mwashuru katika nchi yangu,

juu ya milima yangu nitawakanyagia chini.

Nira yake itaondolewa kutoka kwa watu wangu,

nao mzigo wake utaondolewa kutoka mabegani mwao.”

2614:26 Kut 15:12; Ay 30:21; Isa 23:9Huu ndio mpango uliokusudiwa kwa ajili ya ulimwengu wote,

huu ni mkono ulionyooshwa juu ya mataifa yote.

2714:27 2Nya 20:6; Ay 40:8; Dan 4:35; Yer 49:20; Kut 14:21Kwa kuwa Bwana Mwenye Nguvu Zote amekusudia,

ni nani awezaye kumzuia?

Mkono wake umenyooshwa,

ni nani awezaye kuurudisha?

Unabii Dhidi Ya Wafilisti

28Neno hili lilikuja mwaka ule Mfalme Ahazi alipofariki:

2914:29 Yos 13:3; Isa 11:8; Kum 8:15; 2Nya 26:6Msifurahi, enyi Wafilisti wote,

kwamba fimbo iliyowapiga imevunjika;

kutoka mzizi wa huyo nyoka

atachipuka nyoka mwenye sumu kali,

uzao wake utakuwa joka lirukalo,

lenye sumu kali.

3014:30 Isa 3:15; 25:4; 7:21-22; 8:21; 9:20; Sef 2:5Maskini kuliko maskini wote watapata malisho,

nao wahitaji watalala salama.

Lakini mzizi wako nitauangamiza kwa njaa,

nayo njaa itawaua walionusurika.

3114:31 Isa 3:26; Yer 47:2; Eze 32:30; Isa 13:6; 41:25; Mwa 10:14; Yer 13:20; 46:20-24Piga yowe, ee lango! Bweka, ee mji!

Yeyukeni, enyi Wafilisti wote!

Wingu la moshi linakuja toka kaskazini,

wala hakuna atakayechelewa katika safu zake.

3214:32 Za 51:18; Isa 37:9; Yak 2:5; Za 87:2; Isa 28:16; 44:28; 4:6Ni jibu gani litakalotolewa

kwa wajumbe wa taifa hilo?

Bwana ameifanya imara Sayuni,

nako ndani yake watu wake walioonewa watapata kimbilio.”

New International Version – UK

Isaiah 14:1-32

1The Lord will have compassion on Jacob;

once again he will choose Israel

and will settle them in their own land.

Foreigners will join them

and unite with the descendants of Jacob.

2Nations will take them

and bring them to their own place.

And Israel will take possession of the nations

and make them male and female servants in the Lord’s land.

They will make captives of their captors

and rule over their oppressors.

3On the day the Lord gives you relief from your suffering and turmoil and from the harsh labour forced on you, 4you will take up this taunt against the king of Babylon:

How the oppressor has come to an end!

How his fury14:4 Dead Sea Scrolls, Septuagint and Syriac; the meaning of the word in the Masoretic Text is uncertain. has ended!

5The Lord has broken the rod of the wicked,

the sceptre of the rulers,

6which in anger struck down peoples

with unceasing blows,

and in fury subdued nations

with relentless aggression.

7All the lands are at rest and at peace;

they break into singing.

8Even the junipers and the cedars of Lebanon

gloat over you and say,

‘Now that you have been laid low,

no-one comes to cut us down.’

9The realm of the dead below is all astir

to meet you at your coming;

it rouses the spirits of the departed to greet you –

all those who were leaders in the world;

it makes them rise from their thrones –

all those who were kings over the nations.

10They will all respond,

they will say to you,

‘You also have become weak, as we are;

you have become like us.’

11All your pomp has been brought down to the grave,

along with the noise of your harps;

maggots are spread out beneath you

and worms cover you.

12How you have fallen from heaven,

morning star, son of the dawn!

You have been cast down to the earth,

you who once laid low the nations!

13You said in your heart,

‘I will ascend to the heavens;

I will raise my throne

above the stars of God;

I will sit enthroned on the mount of assembly,

on the utmost heights of Mount Zaphon.14:13 Or of the north; Zaphon was the most sacred mountain of the Canaanites.

14I will ascend above the tops of the clouds;

I will make myself like the Most High.’

15But you are brought down to the realm of the dead,

to the depths of the pit.

16Those who see you stare at you,

they ponder your fate:

‘Is this the man who shook the earth

and made kingdoms tremble,

17the man who made the world a wilderness,

who overthrew its cities

and would not let his captives go home?’

18All the kings of the nations lie in state,

each in his own tomb.

19But you are cast out of your tomb

like a rejected branch;

you are covered with the slain,

with those pierced by the sword,

those who descend to the stones of the pit.

Like a corpse trampled underfoot,

20you will not join them in burial,

for you have destroyed your land

and killed your people.

Let the offspring of the wicked

never be mentioned again.

21Prepare a place to slaughter his children

for the sins of their ancestors;

they are not to rise to inherit the land

and cover the earth with their cities.

22‘I will rise up against them,’

declares the Lord Almighty.

‘I will wipe out Babylon’s name and survivors,

her offspring and descendants,’

declares the Lord.

23‘I will turn her into a place for owls

and into swampland;

I will sweep her with the broom of destruction,’

declares the Lord Almighty.

24The Lord Almighty has sworn,

‘Surely, as I have planned, so it will be,

and as I have purposed, so it will happen.

25I will crush the Assyrian in my land;

on my mountains I will trample him down.

His yoke will be taken from my people,

and his burden removed from their shoulders.’

26This is the plan determined for the whole world;

this is the hand stretched out over all nations.

27For the Lord Almighty has purposed, and who can thwart him?

His hand is stretched out, and who can turn it back?

A prophecy against the Philistines

28This prophecy came in the year King Ahaz died:

29Do not rejoice, all you Philistines,

that the rod that struck you is broken;

from the root of that snake will spring up a viper,

its fruit will be a darting, venomous serpent.

30The poorest of the poor will find pasture,

and the needy will lie down in safety.

But your root I will destroy by famine;

it will slay your survivors.

31Wail, you gate! Howl, you city!

Melt away, all you Philistines!

A cloud of smoke comes from the north,

and there is not a straggler in its ranks.

32What answer shall be given

to the envoys of that nation?

‘The Lord has established Zion,

and in her his afflicted people will find refuge.’