Hesabu 32 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Hesabu 32:1-42

Makabila Ngʼambo Ya Yordani

(Kumbukumbu 3:12-22)

132:1 Amu 5:16; Hes 21:32; Mwa 31:21; Kut 12:38Kabila la Wareubeni na Wagadi, waliokuwa na makundi makubwa ya ngʼombe, kondoo na mbuzi, waliona kuwa nchi ya Yazeri na nchi ya Gileadi ni nzuri kwa mifugo. 232:2 Law 4:22; Hes 27:2; 2Sam 24:5; Isa 16:8-9Hivyo walimjia Mose, na kuhani Eleazari na viongozi wa jumuiya, na kuwaambia, 332:3 Yos 16:2; 18:13; Hes 21:30; Yos 13:27; Hes 21:25; Isa 15:4; 16:9; Yer 48:34; Yos 13:19; Isa 16:8; Yer 48:32; Hes 33:47“Atarothi, Diboni, Yazeri, Nimra, Heshboni, Eleale, Sebamu, Nebo na Beoni, 432:4 Hes 21:34; Kut 12:38nchi ambayo Bwana ameishinda mbele ya wana wa Israeli, inafaa kwa mifugo, nao watumishi wako wana mifugo. 532:5 Hes 13:29Kama tumepata kibali mbele ya macho yako, nchi hii na ipewe watumishi wako kama milki yetu. Usitufanye tuvuke Yordani.”

6Mose akawaambia Wagadi na Wareubeni, “Je, watu wa nchi yenu watakwenda vitani wakati ninyi mmeketi hapa? 732:7 Hes 13:27–14:4Kwa nini mmewakatisha Waisraeli tamaa wasivuke katika nchi ambayo Bwana amewapa? 832:8 Hes 13:3; Kum 1:19-25; 1:22Hivi ndivyo baba zenu walivyofanya wakati nilipowatuma kutoka Kadesh-Barnea kuipeleleza nchi. 932:9 Hes 13:23; Kum 1:24Baada ya kufika kwenye Bonde la Eshkoli na kuitazama nchi, waliwakatisha tamaa Waisraeli wasiingie katika nchi ambayo Bwana alikuwa amewapa. 1032:10 Hes 11:1; 14:20-23; 14:11; Za 95:11; Eze 20:15; Ebr 3:8-19Siku ile hasira ya Bwana iliwaka naye akaapa kiapo hiki: 1132:11 Kut 30:14; Hes 1:1; 14:23; Kum 1:35; Hes 14:24; 14:28‘Kwa kuwa hawakunifuata kwa moyo wote, hakuna mtu yeyote mwenye miaka ishirini au zaidi ambaye alikuja kutoka Misri atakayeona nchi niliyoahidi kwa kiapo kwa Abrahamu, Isaki na Yakobo; 1232:12 Hes 14:24; Za 63:8; Kum 1:35; Yos 14:8, 9; Ay 4:7; Za 37:29; Mit 11:31hakuna hata mmoja isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, Mkenizi, na Yoshua mwana wa Nuni, kwa sababu walimfuata Bwana kwa moyo wote.’ 1332:13 Kut 4:14; Hes 14:28-35; 26:64, 65Hasira ya Bwana iliwaka dhidi ya Waisraeli na akawafanya watangetange katika jangwa kwa miaka arobaini, mpaka kizazi chote cha wale waliofanya maovu mbele yake kimeangamia.

1432:14 Kum 1:34; Za 78:59“Nanyi mko hapa, uzao wa wenye dhambi, mkisimamia mahali pa baba zenu na mkimfanya Bwana kuwakasirikia Waisraeli hata zaidi. 1532:15 Kum 30:17-18; 2Nya 7:20; Yos 22:16, 18; 2Nya 15:2Kama mkigeuka na mkiacha kumfuata, atawaacha tena watu hawa wote jangwani, na mtakuwa sababu ya maangamizi yao.”

1632:16 1Sam 24:3; Za 50:9; 78:70; Kut 12:38; Kum 3:19Ndipo wakamjia Mose na kumwambia, “Tungalitaka kujenga mazizi hapa kwa ajili ya mifugo yetu na miji kwa ajili ya wanawake wetu na watoto. 1732:17 Kum 3:18; Yos 4:12, 13; Hes 22:4; Kum 3:20Lakini sisi tuko tayari kuchukua silaha zetu na kutangulia mbele ya Waisraeli mpaka tutakapowaleta mahali pao. Wakati huo wanawake wetu na watoto wataishi katika miji yenye ngome, kwa ajili ya ulinzi dhidi ya wenyeji wa nchi. 1832:18 Yos 22:1-4Hatutarudi nyumbani mwetu mpaka kila Mwisraeli apokee urithi wake. 1932:19 Hes 21:33; Yos 12:1; 22:7Hatutapokea urithi wowote pamoja nao ngʼambo ya Yordani, kwa sababu urithi wetu umekuja kwetu upande wa mashariki ya Yordani.”

2032:20 Kum 3:18; Yos 4:12-13Kisha Mose akawaambia, “Kama mtafanya jambo hili, kama mtajivika silaha mbele za Bwana kwa ajili ya vita, 21na kama ninyi nyote mtakwenda mmejivika silaha ngʼambo ya Yordani mbele za Bwana mpaka awe amewafukuza adui zake mbele zake, 2232:22 Yos 22:4; Law 14:34; Kum 3:18-20hadi wakati nchi itakapokuwa imeshindwa mbele za Bwana, ndipo mtaweza kurudi na kuwa huru kutoka masharti yenu kwa Bwana na Israeli. Nayo nchi hii itakuwa milki yenu mbele za Bwana.

2332:23 Mwa 4:7; Isa 3:9; Mwa 44:16; Za 140:11; Mit 13:21; Isa 59:12; Rum 2:9“Lakini mkishindwa kufanya hili, mtakuwa mnatenda dhambi dhidi ya Bwana; nanyi kuweni na hakika kuwa dhambi yenu itawapata. 2432:24 Hes 30:2; 32:16, 34Jengeni miji kwa ajili ya wanawake na watoto wenu, na mazizi kwa ajili ya mbuzi na kondoo zenu, lakini fanyeni yale mliyoahidi.”

2532:25 Yos 1:16; 22:2Wagadi na Wareubeni wakamwambia Mose, “Sisi watumishi wako tutafanya kama bwana wetu anavyotuagiza. 2632:26 Yos 1:14; 12:2; 22:9; 2Sam 2:9; 1Nya 5:9Watoto na wake zetu, makundi ya mbuzi na kondoo, na makundi ya ngʼombe zetu, watabaki hapa katika miji ya Gileadi. 2732:27 Yos 4:12Lakini watumishi wenu, kila mwanaume aliyevaa silaha za vita, watavuka ngʼambo kupigana mbele za Bwana, sawa kama bwana wetu anavyosema.”

2832:28 Kum 3:18; Yos 1:13; Hes 11:28; 1:16Kisha Mose akatoa amri kuhusu wao kwa kuhani Eleazari, na Yoshua mwana wa Nuni na viongozi wa jamaa za makabila ya Waisraeli. 2932:29 Hes 22:4Mose akawaambia, “Ikiwa Wagadi na Wareubeni, kila mwanaume aliyevaa silaha za vita, atavuka Yordani pamoja nanyi mbele za Bwana, basi wakati mtakapoishinda nchi iliyoko mbele yenu, wapeni nchi ya Gileadi kama milki yao. 30Lakini kama hawatavuka pamoja nanyi wakiwa wamevaa silaha za vita, lazima wakubali kupokea milki yao pamoja nanyi katika nchi ya Kanaani.”

31Wagadi na Wareubeni wakajibu, “Watumishi wako watafanya lile Bwana alilosema. 3232:32 Yos 12:6Tutavuka mbele za Bwana kuingia Kanaani tukiwa tumevaa silaha za vita, lakini mali tutakayoirithi itakuwa ngʼambo hii ya Yordani.”

3332:33 Yos 13:24-28; 1Sam 13:7; Yos 1:12; Hes 21:21; Kum 2:26; Yos 12:5; Hes 21:24; 34:24; Kum 2:36; Yos 12:6Kisha Mose akawapa Wagadi, Wareubeni, na nusu ya kabila la Manase mwana wa Yosefu ufalme wa Sihoni mfalme wa Waamori, na ufalme wa Ogu mfalme wa Bashani, nchi yote pamoja na miji yake, na nchi inayowazunguka.

3432:34 Kum 2:36; 3:13; 4:48; Yos 12:2; 13:9; Amu 11:26; 1Sam 30:28; 1Nya 5:8; Yer 48:19; Hes 33:45Wagadi wakajenga Diboni, Atarothi, Aroeri, 3532:35 Amu 8:11Atroth-Shofani, Yazeri, Yogbeha, 36Beth-Nimra na Beth-Harani kama miji iliyozungushiwa ngome, tena wakajenga mazizi kwa ajili ya makundi yao ya mbuzi na kondoo. 3732:37 Hes 21:25; Yos 13; 19; 1Nya 6:76; Yer 48:1; Eze 25:9Nao Wareubeni wakajenga upya miji ya Heshboni, Eleale na Kiriathaimu, 3832:38 Isa 15:2; 46:1; Yer 48:1, 22; Hes 32:3; Kut 23:13pia Nebo na Baal-Meoni (majina ya hiyo miji yalibadilishwa) na Sibma. Miji waliyoijenga upya waliipa majina.

3932:39 Mwa 50:23; Hes 26:29; Kum 2:36; Mwa 10:16; Yos 17:1Wazao wa Makiri mwana wa Manase walikwenda Gileadi, wakaiteka nchi na kuwafukuza Waamori waliokuwa huko. 4032:40 Mwa 50:23; Kum 3:15Kwa hiyo Mose akawapa Wamakiri, wazao wa Manase, nchi ya Gileadi, nao wakakaa huko. 4132:41 Kum 3:14; Yos 13:30; Amu 10:4; 1Nya 2:23Yairi, mzao wa Manase, akateka makao yao, akayaita Hawoth-Yairi. 4232:42 1Nya 2:23; Amu 8:11; 1Sam 15:12; 2Sam 18:18Naye Noba akateka Kenathi na makao yaliyoizunguka, akayaita Noba kwa jina lake.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

民数记 32:1-42

约旦河东的支派

1吕便迦得的子孙有许多牲畜,他们见雅谢基列适于放牧, 2就来见摩西以利亚撒祭司和会众的首领,说: 3亚大录底本雅谢宁拉希实本以利亚利示班尼波比稳—— 4这些耶和华为以色列会众攻取的地方适于放牧,而仆人们有许多牲畜。 5如果你们恩待我们,请将这些地方赐给我们作产业,别让我们过约旦河了。”

6摩西对他们说:“难道你们要坐在这里,让其他同胞去打仗吗? 7你们为何使以色列人军心动摇,不敢进入耶和华所赐之地? 8从前我在加低斯·巴尼亚派你们的祖先去打探那地方的时候,他们就是这样。 9他们到以实各谷打探那地方,回来后竟动摇军心,使以色列人不敢进入耶和华所赐之地。 10那天耶和华发怒,起誓说, 11‘从埃及出来、二十岁以上的人都看不到我起誓要赐给亚伯拉罕以撒雅各的土地,因为他们没有全心全意地跟从我; 12只有基尼洗耶孚尼的儿子迦勒的儿子约书亚可以看到,因为他们全心全意地跟从我。’ 13耶和华向以色列人发怒,使他们在旷野漂泊了四十年,直到在耶和华面前作恶的那一代都死了。

14“现在,你们这群罪人的后代竟然重蹈前人的覆辙,加剧耶和华的怒气。 15如果你们离弃祂,祂必再次把以色列人丢弃在旷野,这样你们就毁了整个民族。”

16他们上前对摩西说:“我们要在这里为牲畜建围栏,为家眷筑城邑, 17让他们留在坚固的城内,免受当地居民的威胁。然后我们必拿起兵器率先上阵,直到帮其他以色列同胞夺取他们的土地。 18在其他同胞占领各自的产业之前,我们决不回家。 19但我们不会跟他们在约旦河西岸分土地,我们只想要约旦河东岸之地作产业。” 20摩西说:“如果你们信守承诺,拿起兵器在耶和华面前出战, 21你们全军就要在耶和华面前渡过约旦河,直到祂赶走祂面前的仇敌, 22征服那地方。之后,你们才可以回家,才算在耶和华和以色列人面前尽了自己的责任,这地方就在耶和华面前归给你们作产业。 23但如果你们不守承诺,就是得罪耶和华,必难逃惩罚。 24你们现在去为家人筑城邑,为牛羊建围栏吧,但别忘了信守承诺。” 25迦得吕便的子孙对摩西说:“仆人们一定遵命而行。 26我们的妻子、孩子、牛羊等牲畜都会留在基列的各城。 27仆人当中所有能上阵打仗的人都会照你的吩咐在耶和华面前过河作战。”

28于是,摩西以利亚撒祭司、的儿子约书亚以色列各支派的族长说: 29“如果迦得吕便子孙中所有能上阵打仗的人,在耶和华面前跟你们一同过河作战,你们征服那片土地以后就要把基列给他们作产业。 30如果他们不带着兵器跟你们一起过河作战,就只能在迦南与你们同分产业。” 31迦得吕便的子孙再次说:“凡耶和华所吩咐的,仆人们一定照办。 32我们一定带着兵器在耶和华面前过河,前往迦南,但我们要拥有约旦河东之地作产业。”

33摩西就把亚摩利西宏巴珊的国土及周围的城邑都给了迦得的子孙、吕便的子孙和约瑟儿子玛拿西的半个支派。 34迦得的子孙重建了底本亚他录亚罗珥35亚他录·朔反雅谢约比哈36伯·宁拉伯·哈兰,使之成为坚固的城池,并建了羊圈。 37吕便的子孙重建了希实本以利亚利基列亭38尼波巴力·免西比玛。他们为重建的城邑起了新名字,如尼波巴力·免39玛拿西之子玛吉的子孙占领了基列,赶走了那里的亚摩利人。 40摩西就把基列赐给玛拿西的儿子玛吉,作他的居所。 41玛拿西的子孙雅珥占领了基列的村庄,将它们改名为哈倭特·雅珥42挪巴占领了基纳及其周围的村庄,就按自己的名字称基纳挪巴