Hesabu 26 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Hesabu 26:1-65

Kuhesabiwa Watu Mara Ya Pili

126:1 Hes 14:37; 25:8Baada ya hiyo tauni, Bwana akamwambia Mose na Eleazari mwana wa kuhani Aroni, 226:2 Kut 30:11-16; Hes 1:3; Kut 38:25“Hesabu jumuiya yote ya Kiisraeli kwa jamaa zao, wale wote wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, ambao wanaweza kutumika katika jeshi la Israeli.” 326:3 Hes 33:48; Yos 13:22; Hes 22:1; Kum 4:46-49Hivyo Mose na kuhani Eleazari wakazungumza na watu kwenye nchi tambarare ya Moabu, ngʼambo ya Yordani kutokea Yeriko, wakasema, 426:4 Kut 6:14; 13:3“Hesabuni wanaume wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, kama Bwana alivyomwagiza Mose.”

Hawa ndio Waisraeli waliotoka Misri:

526:5 Hes 1:20; Mwa 46:8, 9; 1Nya 5:3; Ufu 7:5Wazao wa Reubeni, mwana mzaliwa wa kwanza wa Israeli, walikuwa:

kutoka kwa Hanoki, ukoo wa Wahanoki;

kutoka kwa Palu, ukoo wa Wapalu;

626:6 1Nya 5:3; Mwa 46:9kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahesroni;

kutoka kwa Karmi, ukoo wa Wakarmi.

7Hizi zilikuwa ndizo koo za Reubeni; wale waliohesabiwa walikuwa 43,730.

8Mwana wa Palu alikuwa Eliabu, 926:9 Hes 16:1; 1:16; 16:2; Isa 65:16; Kum 11:6; Hes 27:3; 16:1, 2nao wana wa Eliabu walikuwa Nemueli, Dathani na Abiramu. Hawa wawili Dathani na Abiramu ndio walikuwa maafisa wa jumuiya ambao walimwasi Mose na Aroni, na walikuwa miongoni mwa wafuasi wa Kora wakati walimwasi Bwana. 1026:10 Kut 15:12; Hes 16:35, 38; Kut 3:12; Ay 31:3; Za 145:20; Yer 29:22; 2Pet 2:6; Yud 7Ardhi ilifunua kinywa chake na kuwameza pamoja na Kora, ambaye wafuasi wake walikufa wakati moto ulipowateketeza wanaume 250. Nao walikuwa kama alama ya onyo. 1126:11 Kut 6:24; Hes 16:33; Kum 5:9; 24:16; 2Fal 14:6; 2Nya 25:4; Eze 18:20Pamoja na hayo, hao ukoo wa Kora hawakufa.

1226:12 Mwa 46:10; 1Nya 4:24; Kut 6:15Wazao wa Simeoni kwa koo zao walikuwa:

kutoka kwa Nemueli, ukoo wa Wanemueli;

kutoka kwa Yamini, ukoo wa Wayamini;

kutoka wa Yakini, ukoo wa Wayakini;

1326:13 Mwa 46:10kutoka kwa Zera, ukoo wa Wazera;

kutoka kwa Shauli, ukoo wa Washauli.

1426:14 Mwa 46:10; Hes 1:23Hizi ndizo koo za Simeoni; walikuwa 22,200.

1526:15 Mwa 46:16Wazao wa Gadi kwa koo zao walikuwa:

kutoka kwa Sifoni, ukoo wa Wasifoni;

kutoka kwa Hagi, ukoo wa Wahagi;

kutoka kwa Shuni, ukoo wa Washuni;

16kutoka kwa Ozni, ukoo wa Waozni;

kutoka kwa Eri, ukoo wa Waeri;

1726:17 Mwa 46:16kutoka kwa Arodi, ukoo wa Waarodi;

kutoka kwa Areli, ukoo wa Waareli.

1826:18 Mwa 30:11; Hes 1:25; Yos 13:24-28Hizi ndizo zilizokuwa koo za Gadi; wale waliohesabiwa walikuwa 40,500.

1926:19 Mwa 38:3; 38:4; 38:7; 46:12; 1Nya 2:3Eri na Onani walikuwa wana wa Yuda, lakini walifia huko Kanaani.

2026:20 Mwa 38:5; 38:29; Yos 7:17Wazao wa Yuda kwa koo zao walikuwa:

kutoka kwa Shela, ukoo wa Washela;

kutoka kwa Peresi, ukoo wa Waperesi;

kutoka kwa Zera, ukoo wa Wazera.

2126:21 Mwa 38:29; Rut 4:19; 1Fal 2:9Wazao wa Peresi walikuwa:

kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahesroni;

kutoka kwa Hamuli, ukoo wa Wahamuli.

2226:22 Hes 1:27Hizi ndizo zilizokuwa koo za Yuda; wale waliohesabiwa walikuwa 76,500.

2326:23 Mwa 46:13; 49:14Wazao wa Isakari kwa koo zao walikuwa:

kutoka kwa Tola, ukoo wa Watola;

kutoka kwa Puva, ukoo wa Wapuva;

2426:24 Mwa 46:13kutoka kwa Yashubu, ukoo wa Wayashubu;

kutoka kwa Shimroni, ukoo wa Washimroni.

2526:25 Mwa 30:18Hizi ndizo zilizokuwa koo za Isakari; wale waliohesabiwa walikuwa 64,300.

2626:26 Hes 1:30; Mwa 46:14; 49:13Wazao wa Zabuloni kwa koo zao walikuwa:

kutoka kwa Seredi, ukoo wa Waseredi;

kutoka kwa Eloni, ukoo wa Waeloni;

kutoka kwa Yaleeli, ukoo wa Wayaleeli.

2726:27 Mwa 30:20Hizi ndizo zilizokuwa koo za Zabuloni, wale waliohesabiwa walikuwa 60,500.

2826:28 Hes 1:32; 36:1; Mwa 41:52; 46:20; 48:3Wazao wa Yosefu kwa koo zao kutoka kwa Manase na kwa Efraimu walikuwa:

2926:29 Hes 1:34; Mwa 50:23; Amu 11:1; Hes 32:39Wazao wa Manase:

kutoka kwa Makiri, ukoo wa Wamakiri (Makiri alikuwa baba wa Gileadi);

kutoka kwa Gileadi, ukoo wa Wagileadi.

3026:30 Hes 27:1; 36:1; 1Nya 7:14; Yos 17:2; Amu 6:11; 8:2Hawa ndio waliokuwa wazao wa Gileadi:

kutoka kwa Iezeri, ukoo wa Waiezeri;

kutoka kwa Heleki, ukoo wa Waheleki;

31kutoka kwa Asirieli, ukoo wa Waasirieli;

kutoka kwa Shekemu, ukoo wa Washekemu;

32kutoka kwa Shemida, ukoo wa Washemida;

kutoka kwa Heferi, ukoo wa Waheferi.

3326:33 Hes 27:1; 36:2; Yos 17:3; 1Nya 7:15; Hes 27:3; 36:11(Selofehadi mwana wa Heferi hakuzaa wana, bali alikuwa na watoto wa kike tu, ambao majina yao yalikuwa Mahla, Noa, Hogla, Milka na Tirsa.)

3426:34 Hes 1:35Hizi ndizo zilizokuwa koo za Manase; wale waliohesabiwa walikuwa 52,700.

3526:35 Hes 1:32; 1Nya 7:20Hawa walikuwa wazao wa Efraimu kwa koo zao:

kutoka kwa Shuthela, ukoo wa Washuthela;

kutoka kwa Bekeri, ukoo wa Wabekeri;

kutoka kwa Tahani, ukoo wa Watahani;

36Hawa ndio walikuwa wazao wa Shuthela:

kutoka kwa Erani, ukoo wa Waerani.

3726:37 Hes 1:33; Kum 33:13-17Hizi ndizo zilizokuwa koo za Efraimu; wale waliohesabiwa walikuwa 32,500.

Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yosefu kwa koo zao.

3826:38 Mwa 46:21; Hes 1:36; 1Nya 8:40Wazao wa Benyamini kwa koo zao walikuwa:

kutoka kwa Bela, ukoo wa Wabela;

kutoka kwa Ashbeli, ukoo wa Waashbeli;

kutoka kwa Ahiramu, ukoo wa Waahiramu;

3926:39 Mwa 46:21; 1Nya 7:12kutoka kwa Shufamu, ukoo wa Washufamu;

kutoka kwa Hufamu, ukoo wa Wahufamu.

4026:40 Mwa 46:21; 1Nya 8:3Wazao wa Bela kutoka kwa Ardi na Naamani walikuwa:

kutoka kwa Ardi, ukoo wa Waardi;

kutoka kwa Naamani, ukoo wa Wanaamani.

4126:41 Hes 1:37Hizi ndizo zilizokuwa koo za Benyamini; wale waliohesabiwa walikuwa 45,600.

4226:42 Hes 1:38, 39; Amu 18:19; Mwa 46:23; 49:16; Kum 33:22Hawa ndio waliokuwa wazao wa Dani kwa koo zao:

kutoka kwa Shuhamu, ukoo wa Washuhamu.

Hizi ndizo zilizokuwa koo za Dani: 43Wote walikuwa koo za Washuhamu; wale waliohesabiwa walikuwa 64,400.

4426:44 Hes 1:40; 26:47; 1:41Wazao wa Asheri kwa koo zao walikuwa:

kutoka kwa Imna, ukoo wa Waimna;

kutoka kwa Ishvi, ukoo wa Waishvi;

kutoka kwa Beria, ukoo wa Waberia;

45kutoka kwa wazao wa Beria:

kutoka kwa Heberi, ukoo wa Waheberi;

kutoka kwa Malkieli, ukoo wa Wamalkieli.

46(Asheri alikuwa na binti aliyeitwa Sera.)

47Hizi ndizo zilizokuwa koo za Asheri; wale waliohesabiwa walikuwa 53,400.

4826:48 Mwa 30:8; 46:24; 1Nya 7:13Wazao wa Naftali kwa koo zao walikuwa:

kutoka kwa Yaseeli, ukoo wa Wayaseeli;

kutoka kwa Guni, ukoo wa Waguni;

4926:49 1Nya 7:13kutoka kwa Yeseri, ukoo wa Wayeseri;

kutoka kwa Shilemu, ukoo wa Washilemu.

5026:50 Hes 1:42, 43Hizi ndizo zilizokuwa koo za Naftali; wale waliohesabiwa walikuwa 45,400.

5126:51 Kut 12:37; Hes 1:46; 2:32Jumla ya hesabu ya wanaume wa Israeli ilikuwa 601,730.

52Bwana akamwambia Mose, 5326:53 Yos 11:23; 14:1; Eze 45:8“Watagawiwa nchi kama urithi kwa kulingana na hesabu ya majina. 5426:54 Hes 33:54; 35:8Kundi kubwa zaidi lipe urithi mkubwa zaidi, na kundi dogo zaidi lipewe urithi mdogo zaidi; kila kundi litapokea urithi wake kulingana na hesabu ya wale walioorodheshwa. 5526:55 Hes 34:13; Yos 11:23; 14:2Hakikisha kuwa nchi inagawanywa kwa kura. Kile kitakachorithiwa na kila kikundi kitakuwa kwa kulingana na majina ya kabila la babu yao. 56Kila urithi utagawanywa kwa kura miongoni mwa makundi makubwa na madogo.”

5726:57 Mwa 46:11; Kut 6:16; 1Nya 6:16Hawa walikuwa Walawi ambao walihesabiwa kwa koo zao:

kutoka kwa Gershoni, ukoo wa Wagershoni;

kutoka kwa Kohathi, ukoo wa Wakohathi;

kutoka kwa Merari, ukoo wa Wamerari.

5826:58 Kut 6:20Hizi pia zilikuwa koo za Walawi:

ukoo wa Walibni;

ukoo wa Wahebroni;

ukoo wa Wamahli;

ukoo wa Wamushi;

ukoo wa wana wa Kora.

(Kohathi alikuwa baba aliyemzaa Amramu; 5926:59 Kut 2:1; 6:20; 2:4; 15:20jina la mke wa Amramu ni Yokebedi, naye pia alikuwa mzao wa Lawi, ambaye alizaliwa kwa Walawi nchini Misri. Alimzalia Amramu: Aroni, Mose na dada yao Miriamu. 6026:60 Kut 6:23Aroni alikuwa baba yake Nadabu na Abihu, Eleazari na Ithamari. 6126:61 Law 10:1-2; Hes 3:4; 1Nya 24; 2Lakini Nadabu na Abihu walikufa wakati walitoa sadaka mbele za Bwana kwa moto usioruhusiwa.)

6226:62 Hes 3:39; 1:47; 18:23; 2:33; 18:20-24; 35:2-8; Kum 14:27-29Wanaume wote wa Walawi wa umri wa mwezi mmoja na zaidi walikuwa 23,000. Wao hawakuhesabiwa pamoja na Waisraeli wengine kwa sababu hawakupokea urithi miongoni mwao.

6326:63 Hes 1:19; 22:1Hawa ndio walioorodheshwa na Mose na kuhani Eleazari wakati waliwahesabu Waisraeli kwenye nchi tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ngʼambo ya Yeriko. 6426:64 Hes 14:29; 1:44; 1:1; Kum 2:14, 15Hakuna hata mmoja wao aliyekuwa miongoni mwa wale waliohesabiwa na Mose na kuhani Aroni wakati waliwahesabu Waisraeli katika Jangwa la Sinai. 6526:65 Hes 14:18; 1Kor 10:5; Hes 13:6; 11:28; Za 90:3-8; Rum 11:22; Kum 32:49-50; Yos 14:10; Hes 14:18, 30; Ebr 3:17, 18; Yud 5Kwa maana Bwana alikuwa amewaambia hao Waisraeli hakika wangekufa huko jangwani, wala hakuna mmoja wao aliyeachwa, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune na Yoshua mwana wa Nuni.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

民数记 26:1-65

第二次人口统计

1瘟疫过后,耶和华对摩西亚伦祭司的儿子以利亚撒说: 2“你们要统计以色列全体会众,按宗族登记所有二十岁以上、有作战能力的男子。” 3摩西以利亚撒祭司就在约旦河边、耶利哥对面的摩押平原对以色列人说: 4“你们要按照耶和华的吩咐统计二十岁以上的男子。”

以下是从埃及出来的以色列人。

5以色列的长子是吕便吕便的子孙有哈诺族、法路族、 6希斯伦族和迦米族, 7共登记了四万三千七百三十人。 8法路的儿子是以利押9以利押的儿子是尼姆利大坍亚比兰大坍亚比兰原是会众所推选的首领,他们与可拉一伙一起反叛摩西亚伦,反叛耶和华, 10以致大地裂开将他们全部吞了下去,当时大火还烧灭了二百五十人——成了后人的警戒。 11然而,可拉的子孙没有被灭绝。

12西缅的子孙有尼姆利族、雅悯族、雅斤族、 13谢拉族和扫罗族, 14共登记了两万二千二百人。

15迦得的子孙有洗分族、哈基族、书尼族、 16阿斯尼族、以利族、 17亚律族和亚列利族, 18共登记了四万零五百人。

19犹大的儿子俄南死在迦南20犹大的子孙有示拉族、法勒斯族、谢拉族。 21法勒斯的子孙有希斯伦族和哈姆勒族。 22这些是犹大各宗族,共登记了七万六千五百人。

23以萨迦的子孙有陀拉族、普瓦族、 24雅述族和伸仑族, 25共登记了六万四千三百人。

26西布伦的子孙有西烈族、以伦族和雅利族, 27共登记了六万零五百人。

28约瑟的儿子有玛拿西以法莲29玛拿西的子孙有玛吉族和基列族。基列玛吉的儿子。 30基列的子孙有伊以谢族、希勒族、 31亚斯烈族、示剑族、 32示米大族和希弗族。 33希弗的儿子西罗非哈没有儿子,只有女儿玛拉挪阿曷拉密迦得撒34这些是玛拿西各宗族,共登记了五万二千七百人。

35以法莲的子孙有书提拉族、比结族和他罕族。 36书提拉的子孙有以兰族。 37这些是以法莲各宗族,共登记了三万二千五百人,都是约瑟的子孙。

38便雅悯的子孙有比拉族、亚实别族、亚希兰族、 39书反族和户反族。 40比拉的子孙有亚勒族和乃幔族。 41这些是便雅悯各宗族,共登记了四万五千六百人。

42的子孙有书含族, 43共登记了六万四千四百人。

44亚设的子孙有音拿族、亦施韦族和比利亚族。 45比利亚的子孙有希别族和玛结族。 46亚设的女儿名叫西拉47这些是亚设各宗族,共登记了五万三千四百人。

48拿弗他利的子孙有雅薛族、沽尼族、 49耶色族和示冷族, 50共登记了四万五千四百人。

51登记的以色列男子共有六十万一千七百三十人。

52耶和华对摩西说: 53“你要按着各支派登记的人数把土地分给他们作产业; 54人数多的多分产业,人数少的少分产业,要按登记的人数分配。 55以色列人要按各自的支派抽签分地,承受产业。 56无论大小支派,都要用抽签的方法分配产业。”

57利未的子孙有革顺族、哥辖族和米拉利族。 58立尼族、希伯仑族、玛利族、姆示族和可拉族也是利未的子孙。哥辖暗兰59暗兰的妻子叫约基别,是利未女子,出生在埃及。她给暗兰生了亚伦摩西和他们的姐姐米利暗60亚伦拿答亚比户以利亚撒以他玛61拿答亚比户因用凡火向耶和华献祭而被击杀。 62利未人中一个月以上的男性共登记了两万三千人,他们的人数没有登记在以色列人中,因为他们在以色列人中不分产业。

63以上是摩西以利亚撒祭司在约旦河边、耶利哥对面的摩押平原统计的人数, 64其中没有一个是摩西和祭司亚伦从前在西奈旷野登记的人。 65因为耶和华说过,那批人都要死在旷野。果然,除了耶孚尼的儿子迦勒的儿子约书亚以外,上次登记的人无一存活。