Hesabu 23 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Hesabu 23:1-30

Ujumbe Wa Kwanza Wa Balaamu

123:1 Hes 22:40Balaamu akasema, “Nijengee hapa madhabahu saba, mnitayarishie mafahali saba na kondoo dume saba.” 2Balaki akafanya kama Balaamu alivyosema; hao wawili kila mmoja wao akatoa fahali mmoja na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.

323:3 Kum 18:18; Yer 1:9Kisha Balaamu akamwambia Balaki, “Kaa hapa kando ya sadaka yako wakati mimi ninakwenda kando. Huenda Bwana atakuja kukutana nami. Lolote atakalonifunulia, nitakuambia.” Basi akaenda hata mahali peupe palipoinuka.

423:4 Mwa 25:24-26; Kut 22:21; 23:9; Kum 10:19Mungu akakutana naye, kisha Balaamu akasema, “Nimekwisha kutengeneza madhabahu saba, na juu ya kila madhabahu nimetoa sadaka ya fahali mmoja na kondoo dume mmoja.”

523:5 Kut 4:12, 15; Isa 59:21; Hes 22:20; Mit 21:30; Isa 47:12Bwana akaweka ujumbe katika kinywa cha Balaamu na kusema, “Rudi kwa Balaki umpe ujumbe huu.”

623:6 Law 20:24; 1Fal 8:53; Efe 2:14Basi Balaamu akarudi kwa Balaki, akamkuta amesimama kando ya sadaka yake akiwa na wakuu wote wa Moabu. 723:7 Hes 22:5, 6; 24:3-21; Yos 24:9; 2Sam 23:1; 2Fal 5:1; Mwa 24:10; Neh 13:2; Law 15:16; Hes 5:2, 3; 1Kor 5:11, 13Ndipo Balaamu akasema ujumbe wake:

“Balaki amenileta kutoka Aramu,

mfalme wa Moabu kutoka milima ya mashariki.

Akasema, ‘Njoo, unilaanie Yakobo;

njoo unishutumie Israeli.’

823:8 Hes 22:12; Isa 43:13; Yos 24:10; Neh 13:2Nitawezaje kuwalaani,

hao ambao Mungu hajawalaani?

Nitawezaje kuwashutumu

hao ambao Bwana hakuwashutumu?

923:9 Hes 22:41; Kut 33:16; Kum 32:8Kutoka vilele vya miamba ninawaona,

kutoka mahali palipoinuka ninawatazama.

Ninaliona taifa ambalo wanaishi peke yao,

nao hawahesabiwi kama mojawapo ya mataifa.

1023:10 Mwa 13:16; Za 16:3; 116:15Ni nani awezaye kuhesabu mavumbi ya Yakobo,

au kuhesabu robo ya Israeli?

Mimi na nife kifo cha mtu mwenye haki,

na mwisho wangu na uwe kama wao!”

11Balaki akamwambia Balaamu, “Ni nini ulichonitendea? Nimekuleta ulaani adui zangu, lakini wewe badala yake umewabariki!”

12Balaamu akajibu, “Je, hainipasi kusema kile Bwana anachoweka katika kinywa changu?”

Ujumbe Wa Pili Wa Balaamu

13Ndipo Balaki akamwambia, “Twende pamoja mahali pengine ambapo unaweza kuwaona; utawaona baadhi tu wala si wote. Nawe kutoka huko, unilaanie hao.” 1423:14 Isa 1:10-11; Hos 12:11Basi akampeleka kwenye shamba la Sofimu, juu ya kilele cha Mlima Pisga. Pale akajenga madhabahu saba na kutoa sadaka ya fahali na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.

15Balaamu akamwambia Balaki, “Kaa hapa kando ya sadaka yako wakati ninapokwenda kuonana na Mungu kule.”

16Bwana akakutana na Balaamu, akaweka ujumbe katika kinywa chake akasema, “Rudi kwa Balaki umpe ujumbe huu.”

1723:17 1Sam 3:17Basi Balaamu akarudi kwa Balaki, akamkuta amesimama kando ya sadaka yake, akiwa na wakuu wa Moabu. Balaki akamuuliza, “Je, Bwana amesema nini?”

1823:18 Amu 3:20Ndipo Balaamu akasema ujumbe wake:

“Balaki, inuka na usikilize,

nisikie mimi, wewe mwana wa Sipori.

1923:19 1Sam 15:29Mungu si mtu, hata aseme uongo,

wala yeye si mwanadamu, hata ajute.

Je, anasema, kisha asitende?

Je, anaahidi, asitimize?

20Nimepokea agizo kubariki;

amebariki, nami siwezi kubadilisha.

21“Haijaonekana bahati mbaya katika Yakobo,

wala taabu katika Israeli.

Bwana, Mungu wao yu pamoja nao,

nayo sauti kuu ya Mfalme imo katikati yao.

22Mungu aliwatoa kutoka Misri;

wao wana nguvu za nyati.

23Hakuna uchawi dhidi ya Yakobo,

wala hakuna uaguzi dhidi ya Israeli.

Sasa itasemwa kuhusu Yakobo

na Israeli, ‘Tazama yale Mungu aliyotenda!’

24Taifa lainuka kama simba jike;

linajiinua kama simba

ambaye hatulii mpaka amalize kurarua mawindo yake

na kunywa damu ya mawindo yake.”

25Kisha Balaki akamwambia Balaamu, “Usiwalaani kabisa, wala usiwabariki kabisa!”

26Balaamu akajibu, “Je, sikukuambia ni lazima nifanye lolote analosema Bwana?”

Ujumbe Wa Tatu Wa Balaamu

27Basi Balaki akamwambia Balaamu, “Njoo, nikupeleke mahali pengine. Huenda itampendeza Mungu kukuruhusu unilaanie hao watu kutoka mahali hapo.” 28Balaki akamchukua Balaamu juu ya Mlima Peori, unaotazamana na nyika.

29Balaamu akasema, “Nijengee hapa madhabahu saba, uandae mafahali saba na kondoo dume saba kwa ajili yangu.” 30Balaki akafanya kama Balaamu alivyosema, kisha akatoa sadaka ya fahali mmoja na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

民数记 23:1-30

巴兰的预言

1巴兰巴勒说:“你在这里为我筑七座祭坛,预备七头公牛和七只公绵羊。” 2巴勒就照巴兰的话做了。他们二人在每座坛上献上一头公牛和一只公绵羊, 3巴兰巴勒说:“你留在燔祭旁边,我到前面去,也许耶和华会来见我。无论祂有什么指示,我必告诉你。” 4上帝果然向巴兰显现。巴兰对上帝说:“我已经预备了七座祭坛,每座祭坛上献了一头公牛和一只公绵羊。” 5耶和华告诉他当说的话,命他回去转告巴勒6巴兰就回到巴勒那里,看见他和摩押的臣仆们都站在燔祭旁边。 7巴兰吟诗预言说:

巴勒引我出亚兰

摩押王请我出东山,

说,‘来为我咒诅雅各

来斥责以色列!’

8上帝没有咒诅的,

我怎能咒诅?

耶和华没有斥责的,

我怎能斥责?

9我从峰顶观看他们,

从高岗眺望他们,

这独居一方之民,

不与万国同列。

10雅各的子孙多如尘土,

谁能数得清?

谁能数清以色列人的四分之一?

我愿像义人一样死去,

如义人般终此一生。”

11巴勒巴兰说:“你这是做什么?我请你来咒诅我的仇敌,你竟祝福他们!” 12巴兰说:“耶和华让我说的话,我岂能不说?”

巴兰第二次预言

13巴勒说:“请你跟我去另一个地方,那里看不见全部以色列人,只能看见一部分,你要在那里为我咒诅他们。” 14他领巴兰上到毗斯迦山顶的琐腓田,在那里筑了七座祭坛,每座坛上都献了一头公牛和一只公绵羊。 15巴兰巴勒说:“你留在这些燔祭旁边,我到那边去见耶和华。” 16耶和华向巴兰显现,告诉他当说的话,让他转告巴勒17巴兰回到巴勒那里,看见他和摩押的臣仆们都站在燔祭旁边。巴勒问道:“耶和华说了什么?” 18巴兰吟诗预言说:

巴勒啊,要留心听!

西拨的儿子啊,请听我言。

19上帝并非世人,祂不撒谎;

上帝不是凡人,祂不反悔。

祂言出必行,信守承诺。

20我奉命祝福,祂已赐福,

我不能改变。

21雅各的子孙中未见有罪恶,

以色列人中看不见有祸患。

他们的上帝耶和华与他们同在,

他们向自己的君王欢呼。

22上帝把他们带出埃及

23:22 ”有古卷作“他们”。的力量如野牛之角。

23没有邪术能害雅各

没有咒语可伤以色列

时候一到,人们必谈论雅各

谈论以色列,说,‘看啊,

上帝的作为何等伟大!’

24看啊,这民族挺身如母狮,

又像雄狮一跃而起,

不吞掉猎物不罢休,

不喝饱猎物的血不躺卧。”

25巴勒巴兰说:“你可以不咒诅他们,但也不该为他们祝福啊!” 26巴兰回答说:“我不是说过,我必须按耶和华的指示做吗?”

27巴勒说:“来吧,我带你去另一个地方,也许上帝会同意你在那里为我咒诅他们。” 28他领着巴兰登上俯瞰旷野的毗珥山顶。 29巴兰巴勒说:“你在这里为我筑七座祭坛,预备七头公牛和七只公绵羊。” 30巴勒就照巴兰的话在每座祭坛上献了一头公牛和一只公绵羊。