Hesabu 22 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Hesabu 22:1-41

Balaki Anamwita Balaamu

122:1 Hes 22:11; 13:29; Yos 2:7; Hes 31:12; 33:48; Kum 32:49; Yos 2:1Kisha Waisraeli wakasafiri katika tambarare za Moabu na kupiga kambi kando ya Mto Yordani, ngʼambo ya Yeriko.

222:2 Hes 23:1-3; Yos 24:9; Amu 11:25; Mik 6:5; Ufu 2:14Basi Balaki mwana wa Sipori, aliona mambo yale yote ambayo Israeli aliwatendea Waamori, 322:3 Kut 15:15Moabu aliogopa, kwa kuwa walikuwepo watu wengi sana. Hakika, Moabu alijawa na hofu kubwa kwa sababu ya Waisraeli.

422:4 Mwa 19:37; 25:2; Hes 32:17; 18:29; Ay 5:25; Za 72:16Wamoabu wakawaambia wazee wa Midiani, “Umati huu wa watu unakwenda kuramba kila kitu kinachotuzunguka, kama maksai arambavyo majani ya shambani.”

Kwa hiyo Balaki mwana wa Sipori, ambaye alikuwa mfalme wa Moabu wakati huo, 522:5 Hes 24:25; 31:8; Kum 23:4; Yos 13:22; Neh 13:2; Mik 6:5; 2Pet 2:15; Mwa 2:14; Kut 13:3akatuma wajumbe kwenda kumwita Balaamu mwana wa Beori, ambaye alikuwa huko Pethori, karibu na Mto Frati, katika nchi yake ya kuzaliwa. Balaki akasema:

“Taifa limekuja kutoka Misri, nao wamefunika uso wa nchi, nao wametua karibu nami. 622:6 Hes 23:17; 24:9, 10Sasa uje kuwalaani watu hawa, kwa kuwa wana nguvu sana kuniliko. Kisha huenda nikaweza kuwashinda na kuwatoa nje ya nchi. Kwa kuwa ninajua kwamba, wale unaowabariki wanabarikiwa na wale unaowalaani wanalaaniwa.”

722:7 Mwa 30:27Wazee wa Moabu na wa Midiani wakaondoka, wakiwa wamechukua ada ya uaguzi. Walipokwenda kwa Balaamu, wakamweleza kile Balaki alikuwa amesema.

8Balaamu akawaambia, “Mlale hapa usiku huu, nami nitawaletea jibu lile Bwana atakalonipa.” Kwa hiyo wakuu wa Moabu wakakaa naye.

922:9 Mwa 20:3; Hes 23:5; 24:4Mungu akamjia Balaamu na kumuuliza, “Watu gani hawa walio pamoja nawe?”

10Balaamu akamwambia Mungu, “Balaki mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu, alinipelekea ujumbe huu: 11‘Taifa ambalo limekuja kutoka Misri limefunika uso wa nchi. Sasa uje unilaanie hao watu. Kisha huenda nitaweza kupigana nao na kuwafukuza.’ ”

1222:12 Mwa 12:2Lakini Bwana akamwambia Balaamu, “Usiende pamoja nao. Hupaswi kulaani watu hao, kwa kuwa wamebarikiwa.”

13Asubuhi iliyofuata Balaamu akaamka, akawaambia wakuu wa Balaki, “Rudini katika nchi yenu, kwa kuwa Bwana amenikataza nisiende pamoja nanyi.”

14Kwa hiyo wakuu wa Moabu wakarudi kwa Balaki na kumwambia, “Balaamu amekataa kuja pamoja nasi.”

15Kisha Balaki akatuma wakuu wengine, wengi zaidi na wanaoheshimiwa zaidi kuliko wale wa kwanza. 16Wakafika kwa Balaamu na kumwambia:

“Balaki mwana wa Sipori amesema hivi: Usiruhusu kitu chochote kikuzuie kuja kwangu, 1722:17 Hes 24:11kwa sababu nitakulipa vizuri sana na kufanya lolote usemalo. Njoo unilaanie watu hawa.”

1822:18 Hes 22:37; 23:12, 26; 24:13; 1Fal 22:14; 2Nya 18:13; Yer 42:4Lakini Balaamu akawajibu, “Hata kama Balaki angenipa jumba lake la kifalme likiwa limejazwa fedha na dhahabu, singeweza kufanya kitu chochote kikubwa au kidogo ili kutenda kitu nje ya agizo la Bwana Mungu wangu. 19Mlale hapa usiku huu kama wale wengine walivyofanya, nami nitatafuta ni nini kingine Bwana atakachoniambia.”

2022:20 Mwa 20:3; Hes 23:5; 24; 13; 2Nya 18:13Usiku ule Bwana akamjia Balaamu na kumwambia, “Kwa kuwa watu hawa wamekuja kukuita wewe, nenda nao, lakini ufanye tu lile nitakalokuambia.”

Punda Wa Balaamu

21Balaamu akaamka asubuhi, akatandika punda wake akaenda pamoja na wakuu wa Moabu. 2222:22 Kut 4:14; Mwa 16:7; Amu 13:3, 6, 13Lakini Mungu alikasirika sana alipokwenda, naye malaika wa Bwana akasimama barabarani kumpinga. Balaamu alikuwa amepanda punda wake, na watumishi wake wawili walikuwa pamoja naye. 2322:23 Yos 5:13Wakati punda alipomwona malaika wa Bwana akiwa amesimama barabarani akiwa na upanga uliofutwa mkononi mwake, punda akageukia upande kuelekea shambani. Balaamu akampiga ili amrudishe barabarani.

24Ndipo malaika wa Bwana akasimama katika njia nyembamba iliyo kati ya mashamba mawili ya mizabibu, yakiwa na kuta pande zote mbili. 25Punda alipomwona malaika wa Bwana, alijisukumiza karibu na ukuta, na kugandamiza mguu wa Balaamu ukutani. Ndipo Balaamu akampiga tena punda.

26Kisha malaika wa Bwana akaendelea mbele na kusimama mahali pembamba ambapo hapakuwepo nafasi ya kugeuka, upande wa kulia wala wa kushoto. 2722:27 Hes 11:1; Yak 1:19Punda alipomwona malaika wa Bwana, alilala chini Balaamu angali amempanda, naye Balaamu akakasirika na kumpiga kwa fimbo yake. 2822:28 2Pet 2:16Kisha Bwana akakifungua kinywa cha punda, akamwambia Balaamu, “Nimekutendea nini kinachokufanya unipige mara hizi tatu?”

2922:29 Kum 25:4; Mit 12:10; 27:23-27; Mt 15:19Balaamu akamjibu punda, “Umenifanya mjinga! Kama ningelikuwa na upanga mkononi mwangu, ningelikuua sasa hivi.”

30Punda akamwambia Balaamu, “Je, mimi si punda wako mwenyewe, ambaye umenipanda siku zote, hadi leo? Je, nimekuwa na tabia ya kufanya hivi kwako?”

Akajibu, “Hapana.”

3122:31 Mwa 21:19Kisha Bwana akafungua macho ya Balaamu, naye akamwona malaika wa Bwana amesimama barabarani akiwa ameufuta upanga wake. Balaamu akainama, akaanguka kifudifudi.

32Malaika wa Bwana akamuuliza Balaamu, “Kwa nini umempiga punda wako mara tatu hizi? Nimekuja kukuzuia kwa sababu njia yako imepotoka mbele yangu. 33Punda aliniona na kunikwepa mara hizi tatu. Kama punda hangenikwepa, hakika ningekuwa nimeshakuua sasa, lakini ningemwacha punda hai.”

3422:34 Mwa 39:9; Hes 14:40; 1Sam 15:24; 2Sam 12:13; 24:10; Ay 33:27; Za 51:4Balaamu akamwambia malaika wa Bwana, “Nimetenda dhambi. Sikutambua kuwa umesimama barabarani kunizuia. Basi kama haikupendezi, nitarudi.”

35Malaika wa Bwana akamwambia Balaamu, “Uende na watu hao, lakini useme tu lile nikuambialo.” Kwa hiyo Balaamu akaenda na wale wakuu wa Balaki.

3622:36 Hes 21:13Balaki aliposikia kuwa Balaamu anakuja, akatoka kumlaki katika mji wa Moabu, katika mpaka wa Arnoni, ukingoni mwa nchi yake. 37Balaki akamwambia Balaamu, “Je, sikukupelekea jumbe za haraka? Kwa nini hukuja kwangu? Hivi kweli mimi siwezi kukulipa?”

3822:38 Hes 23:5Balaamu akajibu, “Vema, sasa nimekuja kwako. Lakini kwani nina uwezo wa kusema tu chochote? Ni lazima niseme tu kile ambacho Mungu ataweka kinywani mwangu.”

39Kisha Balaamu alikwenda na Balaki mpaka Kiriath-Husothi. 4022:40 Hes 23:1; Eze 45:25Balaki akatoa dhabihu ya ngʼombe na kondoo; baadhi yake akampa Balaamu na wakuu waliokuwa pamoja naye. 4122:41 Hes 21:28; 23:13Asubuhi iliyofuata Balaki akamchukua Balaamu mpaka Bamoth-Baali, na kutoka huko Balaamu akawaona baadhi ya watu.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

民數記 22:1-41

摩押王召巴蘭

1以色列人繼續前行,抵達約旦河東岸的摩押平原,在耶利哥對面安營。 2西撥的兒子摩押巴勒及其人民得知以色列人殺敗了亞摩利人, 3又見他們人多勢眾,都驚恐萬狀, 4米甸的長老說:「這群人將吞掉我們周圍的一切,如同牛吃光田間的草一樣。」那時,西撥的兒子巴勒摩押王。 5他差遣使者到幼發拉底河附近的毗奪——比珥的兒子巴蘭的家鄉,去召巴蘭。他讓使者帶去的信息是:「有一個民族從埃及鋪天蓋地而來,就住在我對面。 6他們比我強大,求你為我咒詛他們。這樣,我也許就能擊敗他們,把他們趕走。我知道你祝福誰,誰就蒙福;你咒詛誰,誰就遭禍。」

7摩押米甸的長老們帶著占卜的禮金去見巴蘭,把巴勒的話轉告他。 8巴蘭說:「你們今夜住在這裡,我必照耶和華的旨意回覆你們。」摩押的使臣就在巴蘭那裡住下。 9晚上,上帝來問巴蘭:「住在你這裡的是誰?」 10巴蘭回答說:「他們是摩押西撥的兒子巴勒派來的使臣, 11前來告訴我說,『有一個民族從埃及鋪天蓋地而來。請你去咒詛那民族,這樣巴勒王或許能擊敗他們,把他們趕走。』」 12上帝對巴蘭說:「你不可跟他們去,也不可咒詛那民族,因為那民族是蒙福的。」

13第二天清早,巴蘭巴勒的使臣說:「你們回去吧,耶和華不准我跟你們去。」 14摩押的使臣回去對巴勒說:「巴蘭不肯跟我們來。」 15巴勒又派去更多、更尊貴的使臣。 16他們到了巴蘭那裡,對他說:「西撥的兒子巴勒請你務必去一趟, 17他必有重賞。你要什麼都可以,只求你去為他咒詛那民族。」 18巴蘭回答說:「巴勒就是把他滿屋的金銀都給我,我也不能在任何事上違背我的上帝耶和華的命令。 19你們可以在這裡過夜,看看耶和華對我還有什麼吩咐。」 20當夜,上帝來對巴蘭說:「這些人既然來請你,你就跟他們去吧,但你只可照我說的做。」 21巴蘭清早起來,備好驢,跟摩押的使臣去了。

上帝攔阻巴蘭

22巴蘭這一去,激怒了上帝。巴蘭騎著驢,帶著兩個僕人正走在途中,耶和華的天使攔住他的去路。 23驢看見耶和華的天使持刀攔在路上,就離開大路,跑進田間。巴蘭鞭打牠,要牠回到路上。 24耶和華的天使又站在葡萄園之間的一條窄路上,兩邊都是牆。 25驢看見耶和華的天使,就靠著牆邊走,將巴蘭的腳擠傷了。巴蘭又鞭打牠。 26耶和華的天使又走到前面,站在狹窄之處,兩邊都無側身通過的餘地。 27驢看見耶和華的天使,就臥在地上,巴蘭大怒,便用杖打牠。 28耶和華使驢開口對巴蘭說:「我做錯了什麼,你竟打我三次!」 29巴蘭說:「因為你戲弄我。如果我手中有刀,早就把你宰了!」 30驢對巴蘭說:「我是你從小就騎的驢,我可曾這樣對你?」巴蘭說:「沒有。」

31那時,耶和華開了巴蘭的眼,他才看見耶和華的天使持刀攔在路上,便俯伏在地。 32耶和華的天使對他說:「你為何三次打你的驢?我特意來阻擋你,因為你走的路在我眼中是邪路。 33你的驢看見我,一連躲避了三次,驢若沒有躲開,我早已殺了你,只放過驢。」 34巴蘭對耶和華的天使說:「我有罪了,我不知道是你攔在路上。如果你反對我去,我就回去。」 35耶和華的天使說:「跟這些人去吧,但你只許按我的指示說話。」於是,巴蘭巴勒的使臣去了。

36巴勒聽見巴蘭來了,就來到邊界盡頭、亞嫩河邊的摩押城迎接他。 37巴勒巴蘭說:「上次派人請你,你為何不肯來?難道我不能給你重賞嗎?」 38巴蘭說:「現在我已經來了,但我不能隨便發言,只能按上帝的指示說話。」 39巴蘭巴勒一同來到基列·胡瑣40巴勒宰牛殺羊賞給巴蘭和隨行的臣僕。 41次日清晨,巴勒巴蘭上到巴力巴末22·41 巴力巴末」希伯來文是「巴力的高崗」之意。,從那裡可以看到一部分以色列人。