Hesabu 16 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Hesabu 16:1-50

Kora, Dathani Na Abiramu

116:1 Kut 6:24; Yud 11; Za 106:17; Hes 26:8; Kum 11:6Kora mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, pamoja na baadhi ya Wareubeni, yaani Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu, na Oni mwana wa Pelethi, wakachukua baadhi ya watu, 216:2 Hes 27:3; 1:16; 26:9wakainuka dhidi ya Mose. Pamoja nao walikuwepo wanaume wa Kiisraeli 250, watu waliojulikana, viongozi wa jumuiya waliokuwa wameteuliwa kuwa wakuu wa kusanyiko. 316:3 Za 106:16; Kut 19:6; Hes 14:14; 12:2Wakaja kama kikundi kuwapinga Mose na Aroni, wakawaambia, “Ninyi mmejitukuza sana! Kusanyiko hili lote ni takatifu, kila mmoja wao, naye Bwana yu pamoja nao. Kwa nini basi mmejitukuza wenyewe juu ya kusanyiko la Bwana?”

416:4 Hes 14:2; 20:6Mose aliposikia jambo hili, akaanguka kifudifudi. 516:5 Law 10:3; 2Tim 2:19; Yer 30:21; Hes 17:5; Za 65:4; 105:26; Yer 50:44; Law 21:6-12; Kut 28:1; 1Sam 2:28; Eze 40:46Kisha akamwambia Kora na wafuasi wake wote: “Asubuhi Bwana ataonyesha ni nani aliye wake na ni nani aliye mtakatifu, tena atamtaka mtu huyo aje kwake. Mtu yule ambaye atamchagua atamfanya kuja karibu naye. 616:6 Law 10:1; Ufu 8:3Wewe Kora na wafuasi wako wote mtafanya hivi: Chukueni vyetezo, 716:7 Law 10:1; Kut 30:9kesho wekeni moto na uvumba kwenye hivyo vyetezo mbele za Bwana. Mtu ambaye Bwana atamchagua atakuwa ndiye mtakatifu. Ninyi Walawi mmejitukuza sana!”

8Pia Mose akamwambia Kora, “Enyi Walawi! Sasa nisikilizeni. 916:9 Mwa 30:15; Hes 3:6; Kum 10:8; 17:12; 21:5; 1Sam 2:11; Za 134:1; Eze 44:11; 1Sam 18:23; Isa 7:13Haiwatoshi ninyi kwamba Mungu wa Israeli amewateua ninyi kutoka kusanyiko lote la Kiisraeli, na kuwaleta karibu naye mpate kufanya kazi kwenye Maskani ya Bwana, na kusimama mbele ya kusanyiko ili kuwahudumia? 1016:10 Hes 3:10; 18:7; Amu 17:5, 12Amekuleta wewe na ndugu zako Walawi mwe karibu naye, lakini sasa unajaribu kupata na ukuhani pia. 1116:11 1Kor 10:10; Kut 16:7-8; 1Kor 3:5Wewe na wafuasi wako wote mmekusanyika pamoja kinyume cha Bwana. Aroni ni nani kwamba ninyi mnungʼunike dhidi yake?”

12Kisha Mose akawaita Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu. Lakini wao wakasema, “Sisi hatuji! 1316:13 Hes 13:27; 14:2; Mwa 13:8; Mdo 7:27, 35; Kut 2:14; Mdo 7:27, 35Haitoshi tu kwamba wewe umetuleta kutoka nchi itiririkayo maziwa na asali ili kutuua sisi jangwani? Nawe sasa pia unataka kuwa mkuu juu yetu? 1416:14 Law 20:24; Kut 22:5; 23:11; Hes 20:5; 1Fal 4:25; Neh 13:15; Za 105:33; Yer 5:17; Hos 2:12; Yoe 2:22; Hag 2:19; Zek 3:10; Amu 16:21; 1Sam 2:11Zaidi ya hayo, hujatuingiza katika nchi inayotiririka maziwa na asali, wala hujatupa urithi wa mashamba na mashamba ya mizabibu. Je, utayangʼoa macho ya watu hawa? Hapana, sisi hatuji!”

1516:15 Kut 4:14; 1Sam 12:3; Mdo 20:33; 2Kor 7:2Ndipo Mose akakasirika sana na kumwambia Bwana, “Usiikubali sadaka yao. Mimi sikuchukua chochote, hata punda kutoka kwao, wala sijamkosea hata mmoja wao.”

16Mose akamwambia Kora, “Wewe na wafuasi wako wote kesho mtatokea mbele za Bwana: yaani wewe na hao wenzako, pamoja na Aroni. 1716:17 Eze 8:11Kila mtu atachukua chetezo chake na kuweka uvumba ndani yake, vyetezo 250 kwa jumla, na kukileta mbele za Bwana. Wewe na Aroni mtaleta vyetezo vyenu pia.” 18Kwa hiyo kila mtu akachukua chetezo chake, akaweka moto na uvumba ndani yake, na kusimama pamoja na Mose na Aroni kwenye mlango wa Hema la Kukutania. 1916:19 Hes 14:10; 20:2, 6; Kut 16:7; Law 9:6, 23Kora alipokuwa amekusanya wafuasi wake wote kuwapinga Mose na Aroni kwenye mlango wa Hema la Kukutania, utukufu wa Bwana ukatokea kwa kusanyiko lote. 20Bwana akamwambia Mose na Aroni, 2116:21 Mwa 19:14; Kut 32:10; Yer 51:6; Mdo 2:40; Ufu 18:4; Za 73:19“Jitengeni kutoka kwenye kusanyiko hili ili nipate kuwaangamiza mara moja.”

2216:22 Hes 14:5; 27:16; Ay 12:10; 21:20; 27:8; 33:4; 34:14; Yer 32:27; Eze 18:4; Ebr 12:9; Mwa 18:23Lakini Mose na Aroni wakaanguka kufudifudi na kulia kwa sauti, wakasema, “Ee Mungu, Mungu wa roho za wanadamu wote, utakuwa na hasira na kusanyiko lote wakati ni mtu mmoja tu ametenda dhambi?”

23Ndipo Bwana akamwambia Mose, 24“Liambie kusanyiko, ‘Ondokeni hapo karibu na mahema ya Kora, Dathani na Abiramu.’ ”

2516:25 Kut 19:7Mose akainuka na kuwaendea Dathani na Abiramu, nao wazee wa Israeli wakafuatana naye. 2616:26 Isa 52:11; Mwa 19:15; Yer 51:6; Mwa 19:12; Mdo 2:40; 2Kor 6:17; Ufu 18:4Mose akalionya kusanyiko, “Sogeeni nyuma mbali na mahema ya hawa watu waovu! Msiguse kitu chochote kilicho mali yao, la sivyo mtafagiliwa mbali kwa sababu ya dhambi zao zote.” 2716:27 Yos 7:24; Isa 13:16; 14:21; Kut 33:8; Ay 9:4; Mit 16:18Hivyo wakaondoka karibu na mahema ya Kora, Dathani na Abiramu. Dathani na Abiramu walikuwa wametoka nje, nao walikuwa wamesimama pamoja na wake zao, watoto wao na wale wanyonyao kwenye mlango wa mahema yao.

2816:28 1Fal 18:36; Kut 3:12; Yn 5:36; 6:38; Kum 18:22; Zek 2:9; Yer 23:16; Eze 13:17Ndipo Mose akasema, “Hivi ndivyo mtakavyojua kuwa Bwana amenituma kufanya mambo haya, na kwamba halikuwa wazo langu. 2916:29 Hes 24:13; Ay 31:2; Mhu 3:19; Isa 10:3; Yer 5:9; Mao 4:22Ikiwa watu hawa watakufa kifo cha kawaida na kupatwa na yale ya kawaida yanayowapata wanadamu, basi Bwana hakunituma mimi. 3016:30 Za 9:17; 16:10; 55:15; 141:7; Isa 5:14; 14:11; 38:18; Mwa 37:35; 1Sam 2:6; Ay 5:26; 21:13; Hes 14:11; Eze 26:20Lakini ikiwa Bwana ataleta jambo jipya kabisa, ardhi ikifunua kinywa chake na kuwameza wao, pamoja na kila kitu kilicho mali yao, nao washuke chini kaburini16:30 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. wakiwa hai, ndipo mtafahamu kuwa watu hawa wamemdharau Bwana.”

3116:31 Isa 64:1-2; Eze 47:1-2; Mik 1:3-4; Zek 14:4Mara Mose alipomaliza kusema haya yote, ardhi iliyokuwa chini yao ikapasuka, 3216:32 Kut 15:12; Za 10:17; 1Nya 6:22nchi ikafunua kinywa chake na kuwameza wao, pamoja na jamaa zao, na watu wote wa Kora na mali zao zote. 3316:33 Mhu 9:10Wakashuka chini kaburini wakiwa hai, pamoja na kila kitu walichokuwa nacho; nchi ikajifunika juu yao, nao wakaangamia wakatoweka kutoka kusanyiko. 34Kutoka kilio chao, Waisraeli wote waliowazunguka walikimbia, wakipaza sauti, “Nchi inatumeza na sisi pia!”

3516:35 Hes 11:1-3; 26:10; Ufu 11:5; Law 10:2; Za 106:18Moto ukaja kutoka kwa Bwana, ukawateketeza wale watu 250 waliokuwa wakifukiza uvumba.

36Bwana akamwambia Mose, 3716:37 Kut 6:23“Mwambie Eleazari mwana wa kuhani Aroni, atoe vyetezo kwenye mabaki ya moto na kutawanya makaa mbali kiasi, kwa maana vyetezo ni vitakatifu: 3816:38 Law 10:1; Mit 20:2; Kut 20:24; 38:1-7; Hes 26:10; Kum 28:46; Yer 44:29; Eze 14:8; 2Pet 2:6vyetezo vya watu waliofanya dhambi iliyowagharimu maisha yao. Fua vyetezo hivyo kuwa bamba ili kufunika madhabahu, kwa maana vimeletwa mbele za Bwana na vimekuwa vitakatifu. Navyo viwe ishara kwa Waisraeli.”

3916:39 2Nya 26:18; Law 20:14Hivyo kuhani Eleazari akavikusanya vile vyetezo vya shaba vilivyoletwa na wale waliokuwa wameteketezwa kwa moto, naye akavifua kufunika madhabahu, 4016:40 Kut 30:1, 9; Isa 1:13; 66:3; Yer 41:5; 44:3; 2Nya 26:18; Hes 3:10kama vile Bwana alivyomwelekeza kupitia Mose. Hili lilikuwa kuwakumbusha Waisraeli kwamba hakuna mtu hata mmoja, isipokuwa mzao wa Aroni, awezaye kuja kufukiza uvumba mbele za Bwana, la sivyo, angekuwa kama Kora na wafuasi wake.

4116:41 Hes 14:2; Za 106:13; Mdo 21:28Siku iliyofuata jumuiya yote ya Kiisraeli wakanungʼunika dhidi ya Mose na Aroni, wakisema, “Mmewaua watu wa Bwana.”

4216:42 Kut 16:7; Hes 14:10; 20:6; Law 9:23Lakini wakati kusanyiko lilipokusanyika kupingana na Mose na Aroni, nalo likageuka kuelekea Hema la Kukutania, ghafula wingu likafunika Hema, nao utukufu wa Bwana ukatokea. 43Ndipo Mose na Aroni wakaenda mbele ya Hema la Kukutania, 44naye Bwana akamwambia Mose, 4516:45 Kut 32:10; 1Nya 16:21; Mt 26:39“Jitenge mbali na kusanyiko hili ili niweze kuwaangamiza mara moja.” Wakaanguka chini kifudifudi.

4616:46 Law 10:1-6; 26:25; Kut 29:36; Hes 1:53; 8:19; Za 106:29; Yos 7:1; 22:18; 1Sam 6:19; 2Sam 24:1; 1Nya 17:24Kisha Mose akamwambia Aroni, “Chukua chetezo chako na uweke uvumba ndani yake, pamoja na moto kutoka madhabahuni, nawe uende haraka kwenye kusanyiko ili kufanya upatanisho kwa ajili yao. Ghadhabu imekuja kutoka kwa Bwana, na tauni imeanza.” 4716:47 Hes 25:6-8Hivyo Aroni akafanya kama Mose alivyosema, akakimbilia katikati ya kusanyiko. Tauni ilikuwa tayari imeanza miongoni mwa watu, lakini Aroni akafukiza uvumba na kufanya upatanisho kwa ajili yao. 4816:48 Hes 25:8; Za 106:30; 2Sam 24:16-17; Ay 33:24; Yak 5:16; 1The 1:10; Ebr 7:24Aroni akasimama kati ya waliokuwa hai na waliokufa, nayo tauni ikakoma. 49Lakini walikufa watu 14,700 kutokana na tauni hiyo, licha ya wale waliokuwa wamekufa kwa sababu ya Kora. 50Ndipo Aroni akamrudia Mose kwenye mlango wa Hema la Kukutania, kwa maana tauni ilikuwa imekoma.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

民數記 16:1-50

可拉之亂

1可拉利未的曾孫、哥轄的孫子、以斯哈的兒子。他跟呂便支派以利押的兩個兒子大坍亞比蘭以及比勒的兒子心中狂妄, 2聯合二百五十名在以色列會眾中有聲望的首領反叛摩西3一起攻擊摩西亞倫,說:「你們太過分了!全體會眾都是聖潔的,有耶和華住在他們當中,你們憑什麼將自己置於耶和華的會眾之上?」 4摩西聽了這話,就俯伏在地, 5可拉一夥人說:「到了明天早上,耶和華必顯明誰是屬於祂的,誰是聖潔的。祂必讓祂所揀選的人到祂面前。 6可拉啊,你們要這樣做,你和你的同夥明天帶香爐來, 7在耶和華面前點火添香。耶和華揀選誰,誰就是聖潔的。你們利未人太過分了!」 8摩西又對可拉說:「利未人啊,你們聽我說! 9以色列的上帝把你們從以色列會眾中分別出來,使你們可以到祂面前,在祂的聖幕裡司職,替會眾辦事,你們還不滿足嗎? 10可拉啊,耶和華使你和其他利未人事奉祂,你們還不滿足,還要貪求祭司的職分嗎? 11其實你和你的同夥合謀反叛的是耶和華,而不是亞倫。」 12摩西派人去召以利押的兒子大坍亞比蘭,他們卻說:「我們不去! 13你帶我們離開奶蜜之鄉,要讓我們死在曠野,這還不夠嗎?你還想自立為王管轄我們嗎? 14你並沒有領我們到奶蜜之鄉,也沒有給我們田地和葡萄園作產業,你還想繼續矇騙我們嗎?我們不去!」

15摩西非常憤怒,就對耶和華說:「求你不要接納他們的祭物。我沒有取過他們一頭驢,也沒有害過他們任何人。」 16摩西可拉說:「明天你和你的同夥要跟亞倫一起站在耶和華面前。 17每人要拿一個香爐,放上香,帶到耶和華面前,共二百五十個。你和亞倫也要各拿一個香爐。」 18於是,他們都拿著香爐,盛著火和香,跟摩西亞倫一起站在會幕門口。 19可拉把全體會眾招聚到會幕門口,要對付摩西亞倫。這時,耶和華的榮光向會眾顯現。

20耶和華對摩西亞倫說: 21「你們離開這些會眾,我好在頃刻之間消滅他們。」 22摩西亞倫就伏在地上說:「上帝啊,賜人生命的上帝啊!一人犯罪,你就要向全體會眾發怒嗎?」 23耶和華對摩西說: 24「你叫會眾離可拉大坍亞比蘭的帳篷遠一點。」

25於是,摩西起來去大坍亞比蘭那裡,以色列的長老也跟著他。 26他對會眾說:「你們離這些惡人的帳篷遠一點,不要碰他們的任何東西,免得你們因他們的罪而受牽連,同遭毀滅。」 27會眾便離開可拉大坍亞比蘭的帳篷。大坍亞比蘭帶著妻小出來,站在自己的帳篷門口。 28摩西對會眾說:「你們很快就知道,我所做的事都是奉耶和華之命而行,並非出於私意。 29如果這些人像常人一樣死去,遭遇跟世人無異,我就不是耶和華派來的。 30但如果耶和華做一件前所未有的事,使地裂開,吞下他們和屬於他們的一切,使他們活生生地墜入陰間,你們就知道這些人藐視耶和華了。」

31摩西的話剛說完,這些人腳下的地就裂開, 32吞下了他們和他們的家眷及所有可拉一夥的人和財物。 33他們和屬於他們的一切就這樣活活地墜入陰間,地在他們上面合攏起來,他們就從會眾中滅亡了。 34他們四圍的以色列人聽到他們的喊叫聲,紛紛逃跑,生怕自己也被吞下去。 35耶和華又降下烈火,燒死了那二百五十個獻香的人。

36耶和華對摩西說: 37「你叫亞倫祭司的兒子以利亞撒去從火中把香爐撿起來,把炭火撒在遠處,因為那些香爐是聖潔的。 38要把那些因犯罪而喪命之人的香爐打成薄片,用來包祭壇,因為那些香爐曾被獻在耶和華面前,是聖潔的,並且可讓以色列人引以為戒。」 39於是,以利亞撒祭司取來被燒死之人所獻的銅香爐,叫人打成薄片用來包祭壇, 40以色列人引以為戒,使亞倫子孫以外的人不致到耶和華面前燒香,以免像可拉及其同夥一樣滅亡。這是按照耶和華藉摩西的吩咐做的。

41第二天,以色列全體會眾都埋怨摩西亞倫說:「你們害死了耶和華的子民。」 42會眾聚集起來反對摩西亞倫,他們向會幕觀看,忽然有雲彩遮蓋了會幕,耶和華的榮光顯現了。 43摩西亞倫來到會幕前, 44耶和華對摩西說: 45「你們離開這些會眾,我好在頃刻之間消滅他們。」他們二人就俯伏在地。 46摩西亞倫說:「取香爐來,裡面放些壇上的火,添上香,趕快帶到會眾那裡為他們贖罪,因為耶和華發怒了,瘟疫已經開始。」 47亞倫就照著摩西的吩咐取來香爐,跑到會眾當中。那時瘟疫已經在人群中蔓延起來。他就在爐中放上香為民眾贖罪。 48他站在活人和死人中間,瘟疫就止住了。 49除了在可拉事件中死亡的人以外,當天有一萬四千七百人死於瘟疫。 50瘟疫止住後,亞倫便回到在會幕門口的摩西那裡。