Hesabu 14 – NEN & KJV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Hesabu 14:1-45

Watu Wanaasi

114:1 Mwa 27:38; Kut 33:4; Hes 25:6; Kum 1:45; Amu 20:23-26; 2Sam 3:32; Ay 31:29Usiku ule watu wote wa jumuiya walipaza sauti zao na kulia kwa sauti kuu. 214:2 Kut 16:3; 15:24; Ebr 3:16; Hes 11:1; 16:13; 20:4; 21:5Waisraeli wote wakanungʼunika dhidi ya Mose na Aroni, nalo kusanyiko lote wakawaambia, “Laiti tungekuwa tumefia humo nchi ya Misri! Au humu kwenye hili jangwa! 314:3 Kut 5:21; Kum 1:39; Mwa 34:29; Za 109:11; Isa 33:4; Eze 7:21; 25:7; 26:5; Mdo 7:39Kwa nini Bwana anatuleta katika nchi hii ili tufe kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watachukuliwa kama nyara. Je, isingekuwa bora kwetu kurudi Misri?” 414:4 Neh 9:17; Mdo 7:36; Ebr 11:15Wakasemezana wao kwa wao, “Inatupasa kumchagua kiongozi na kurudi Misri.”

514:5 Law 9:24; 19:2; Hes 16:4, 22, 45; 20:6; Yos 5:12; Eze 1:28; 2Sam 14:4; 1Nya 21:16Ndipo Mose na Aroni wakaanguka kifudifudi mbele ya kusanyiko lote la Kiisraeli lililokusanyika hapo. 614:6 Hes 11:28; Mwa 37:29-34; Amu 11:35; 2Sam 13:31; 1Fal 19:1; Ezr 9:3; Es 4:1; Mk 14:63Yoshua mwana wa Nuni na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwa watu wale waliokwenda kuipeleleza nchi, wakararua nguo zao, 714:7 Hes 13:27; Kum 1:25wakasema na kusanyiko lote la Kiisraeli, wakawaambia, “Nchi tuliyopita katikati yake na kuipeleleza ni nzuri sana sana. 814:8 Kum 1:21; 7:8; 10:15; Za 18:19; 22:8; 37:23; 41:11; 56:9; 147:11; Mit 11:20; Isa 62:4; Mal 2:17; Hes 13:27Ikiwa Bwana anapendezwa nasi, atatuongoza kuingia katika nchi ile, nchi itiririkayo maziwa na asali, naye atatupa nchi hiyo. 914:9 Kum 1:21, 26; 7:18; 9:7; 20:1; Mwa 21:22; 26:24; 2Nya 13:12; 32:7; Za 118:6; Hag 2:4; 1:13; Yer 15:20; 41:18; 42:11; 46:28Ila tu msimwasi Bwana. Wala msiwaogope watu wa nchi hiyo, kwa sababu tutawameza. Ulinzi wao umeondoka, lakini Bwana yupo pamoja nasi. Msiwaogope.”

1014:10 Kut 17:4; 24:16; Law 9:24Lakini kusanyiko lote likazungumza juu ya kuwapiga kwa mawe. Ndipo utukufu wa Bwana ukaonekana katika Hema la Kukutania kwa Waisraeli wote. 1114:11 Kut 3:20; 4:17; 10:1; 23:21; Hes 15:31; 16:30; 1Sam 2:17; Yn 3:25; Eze 31:14; Mal 1:13; Kum 1:32; Za 78:22; 106:24Bwana akamwambia Mose, “Watu hawa watanidharau mpaka lini? Wataendelea kukataa kuniamini mimi mpaka lini, ingawa nimetenda ishara za miujiza miongoni mwao? 1214:12 Kut 5:3; 33:10; Kum 9:14; 29:20; 32:26; Za 109:13Nitawapiga kwa tauni na kuwaangamiza, lakini nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa lenye nguvu kuliko wao.”

1314:13 Kut 32:11; Za 106:23Mose akamwambia Bwana, “Ndipo Wamisri watasikia juu ya jambo hili! Kwa uweza wako uliwapandisha watu hawa kutoka miongoni mwao. 1414:14 Kut 13:21; 15:14; 33:16; Hes 5:3; 16:3; Yos 2:9; Kum 5:4; 34:10Nao watawaambia wenyeji wa nchi hii jambo hili. Wao tayari wameshasikia kwamba wewe, Ee Bwana, upo pamoja na watu hawa, na kuwa wewe, Ee Bwana, umeonekana uso kwa uso, nalo wingu lako hukaa juu yao. Tena wewe unawatangulia kwa nguzo ya wingu mchana na kwa nguzo ya moto usiku. 15Ikiwa utawaua watu hawa wote mara moja, mataifa ambayo yamesikia taarifa hii kukuhusu wewe watasema, 1614:16 Hes 11:12; Kut 32:12; Yos 7:7Bwana alishindwa kuwaingiza watu hawa katika nchi aliyowaahidi kwa kiapo; hivyo akawaua jangwani.’

17“Basi sasa nguvu za Bwana na zionekane, sawasawa na vile ulivyosema: 1814:18 Kut 20:5-6; 34:6; Za 145:8; Yon 4:2; Yak 5:11Bwana si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo na mwenye kusamehe dhambi na uasi. Lakini haachi kumwadhibu mwenye hatia, huadhibu watoto kwa ajili ya dhambi ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne.’ 1914:19 Kut 34:9; 1Fal 8:34; Za 85:2; 103:3; 10:6; 65; 78:38Kwa kadiri ya upendo wako mkuu, usamehe dhambi ya watu hawa, kama vile ulivyowasamehe tangu wakati walitoka Misri mpaka sasa.”

2014:20 Kut 34:6; Za 99:8; 106:23; Mik 7:18-20Bwana akajibu, “Nimewasamehe kama ulivyoomba. 2114:21 Hes 14:28; Kum 32:40; Amu 8:19; Rut 3:13; 1Sam 14:39; 19:6; Isa 6:3; 40:5; 49:18; Yer 4:2; Eze 5:11; Law 9:6; Za 72:19; Hab 2:14Hata hivyo, kwa hakika kama niishivyo, na kwa hakika kama utukufu wa Bwana uijazavyo dunia yote, 2214:22 Kut 14:11; 17:7; 32:1; Za 81:7; 1Kor 10:5hakuna hata mmoja wa watu hawa ambao waliuona utukufu wangu na ishara za miujiza niliyotenda huko Misri na huko jangwani, lakini ambaye hakunitii na akanijaribu mara hizi kumi, 2314:23 Kut 33:1; Hes 32:11; Kum 1:34; Ebr 3:18; Za 95:11; 106:26hakuna hata mmoja wao atakayeona nchi niliyowaahidi baba zao kwa kiapo. Hakuna hata mmoja ambaye amenidharau atakayeiona. 2414:24 Hes 13:6; 26:65; 32:12; Kum 1:36; Yos 14:8, 14; Za 25:13; 37:9-11Lakini kwa sababu mtumishi wangu Kalebu ana roho ya tofauti na ananifuata kwa moyo wote, nitamwingiza katika nchi aliyoiendea, nao wazao wake watairithi. 2514:25 Mwa 14:7; 10:18; Kum 1:40; Kut 23:31; Hes 21:4; 1Fal 9:26Kwa kuwa Waamaleki na Wakanaani wanaishi katika mabonde, kesho geukeni mwelekee jangwani kwa kufuata njia iendayo Bahari ya Shamu.”14:25 Yaani Bahari Nyekundu au Bahari ya Mafunjo.

2614:26 Kut 16:12; Kum 1:34-35Bwana akamwambia Mose na Aroni: 2714:27 Kut 16:28; Mt 17:17; Mk 9:19; Kut 16:12; 1Kor 10:10“Jumuiya hii ovu itanungʼunika dhidi yangu hadi lini? Nimesikia malalamiko ya hawa Waisraeli wanaonungʼunika. 2814:28 Hes 33:56; Ebr 3:17Hivyo waambie, ‘Hakika kama niishivyo, asema Bwana, nitawafanyia vitu vilevile nilivyosikia mkisema: 2914:29 Hes 1:45; 26:65; 32:13; 1Kor 10:5; Ebr 3:17; Yud 5; Kut 30:12Kila mmoja wenu mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi ambaye alihesabiwa na amenungʼunika dhidi yangu, miili yenu itaanguka katika jangwa hili. 3014:30 Kut 6:8; Kum 32:40; Neh 9:15; Za 106:26; Eze 20:5; 36:7; Hes 13:6; 11:28Hakuna hata mmoja wenu atakayeingia katika nchi niliyoapa kwa mkono ulioinuliwa kuwa makao yenu, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni. 3114:31 Law 26:43Lakini watoto wenu ambao mlisema watachukuliwa kama mateka, nitawaingiza humo ili waifurahie nchi ambayo ninyi mmeikataa. 3214:32 1Kor 10:5Lakini ninyi, miili yenu itaanguka katika jangwa hili. 3314:33 Kut 16:35; Mdo 13:18; Ebr 3:9Watoto wenu watakuwa wachungaji wa mifugo hapa kwa miaka arobaini, wakiteseka kwa ajili ya kukosa uaminifu kwenu, hadi mwili wa mtu wenu wa mwisho ulale katika jangwa hili. 3414:34 Hes 13:25; 14:32, 33; Za 95:10; Eze 4:6; Za 77:8; Ebr 4:1Kwa miaka arobaini, mwaka mmoja kwa kila siku katika zile siku arobaini mlizoipeleleza nchi, mtateseka kwa ajili ya dhambi zenu, na kujua jinsi ilivyo vibaya kunifanya mimi kuwa adui yenu.’ 3514:35 Hes 23:19Mimi Bwana nimesema, na hakika nitafanya mambo haya kwa jumuiya hii yote ovu, ambayo imefungamana pamoja dhidi yangu. Watakutana na mwisho wao katika jangwa hili; hapa ndipo watafia.”

3614:36 Hes 13:4-16, 32Hivyo watu wale ambao Mose alikuwa amewatuma kuipeleleza nchi, waliorudi na kuifanya jumuiya nzima kunungʼunika dhidi ya Mose kwa kueneza taarifa mbaya kuhusu hiyo nchi: 3714:37 Hes 13:32; 16:49; 25:9; 26:1; 31:16; 1Kor 10:10; Ebr 3:17; Kum 4:3watu hawa waliohusika kueneza taarifa mbaya kuhusu hiyo nchi walipigwa na kuanguka kwa tauni mbele za Bwana. 3814:38 Hes 13:4-16; Yos 14:6Miongoni mwa watu waliokwenda kuipeleleza hiyo nchi, ni Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune peke yao waliosalia.

3914:39 Kut 33:4; Mit 19:3; Mt 8:12; Ebr 12:17Mose alipotoa taarifa hii kwa Waisraeli wote, waliomboleza kwa uchungu. 4014:40 Hes 13:17; Kut 9:27; Kum 1:41Mapema asubuhi siku iliyofuata walipanda juu kuelekea kwenye nchi ya vilima virefu, wakasema, “Tumetenda dhambi. Tutakwea mpaka mahali Bwana alipotuahidi.”

4114:41 2Nya 24:20; Ay 9:4; Isa 59:1, 2; Yer 2:37Lakini Mose akasema, “Kwa nini hamtii amri ya Bwana? Jambo hili halitafanikiwa! 4214:42 Kum 1:42Msipande juu, kwa kuwa Bwana hayupo pamoja nanyi. Mtashindwa na adui zenu, 4314:43 Amu 1:19; 6:16; 3:13; Hes 13:29; Mwa 39:23; Kum 21:8; Yos 6:27; 1Sam 3:19; 18:14; 2Nya 1:1kwa kuwa Waamaleki na Wakanaani watapambana nanyi huko. Kwa sababu mmemwacha Bwana, hatakuwa pamoja nanyi, ninyi mtaanguka kwa upanga.”

4414:44 Kum 1:43; Hes 31:6Hata hivyo, kwa kiburi chao walipanda juu kuelekea nchi ya vilima virefu, ijapokuwa Mose hakutoka kambini wala Sanduku la Agano la Bwana. 4514:45 Hes 21:3; Kum 1:44; Yos 12:14; 15:30; 19:4; Amu 1:17; 1Sam 30:30; 1Nya 4:30Ndipo Waamaleki na Wakanaani walioishi katika hiyo nchi ya vilima wakateremka na kuwashambulia, wakawapiga njia yote hadi Horma.

King James Version

Numbers 14:1-45

1And all the congregation lifted up their voice, and cried; and the people wept that night. 2And all the children of Israel murmured against Moses and against Aaron: and the whole congregation said unto them, Would God that we had died in the land of Egypt! or would God we had died in this wilderness! 3And wherefore hath the LORD brought us unto this land, to fall by the sword, that our wives and our children should be a prey? were it not better for us to return into Egypt? 4And they said one to another, Let us make a captain, and let us return into Egypt.

5Then Moses and Aaron fell on their faces before all the assembly of the congregation of the children of Israel.

6¶ And Joshua the son of Nun, and Caleb the son of Jephunneh, which were of them that searched the land, rent their clothes: 7And they spake unto all the company of the children of Israel, saying, The land, which we passed through to search it, is an exceeding good land. 8If the LORD delight in us, then he will bring us into this land, and give it us; a land which floweth with milk and honey. 9Only rebel not ye against the LORD, neither fear ye the people of the land; for they are bread for us: their defence is departed from them, and the LORD is with us: fear them not.14.9 defence: Heb. shadow 10But all the congregation bade stone them with stones. And the glory of the LORD appeared in the tabernacle of the congregation before all the children of Israel.

11¶ And the LORD said unto Moses, How long will this people provoke me? and how long will it be ere they believe me, for all the signs which I have shewed among them? 12I will smite them with the pestilence, and disinherit them, and will make of thee a greater nation and mightier than they.

13¶ And Moses said unto the LORD, Then the Egyptians shall hear it, (for thou broughtest up this people in thy might from among them;) 14And they will tell it to the inhabitants of this land: for they have heard that thou LORD art among this people, that thou LORD art seen face to face, and that thy cloud standeth over them, and that thou goest before them, by day time in a pillar of a cloud, and in a pillar of fire by night.

15¶ Now if thou shalt kill all this people as one man, then the nations which have heard the fame of thee will speak, saying, 16Because the LORD was not able to bring this people into the land which he sware unto them, therefore he hath slain them in the wilderness. 17And now, I beseech thee, let the power of my Lord be great, according as thou hast spoken, saying, 18The LORD is longsuffering, and of great mercy, forgiving iniquity and transgression, and by no means clearing the guilty, visiting the iniquity of the fathers upon the children unto the third and fourth generation. 19Pardon, I beseech thee, the iniquity of this people according unto the greatness of thy mercy, and as thou hast forgiven this people, from Egypt even until now.14.19 until…: or, hitherto

20And the LORD said, I have pardoned according to thy word: 21But as truly as I live, all the earth shall be filled with the glory of the LORD. 22Because all those men which have seen my glory, and my miracles, which I did in Egypt and in the wilderness, and have tempted me now these ten times, and have not hearkened to my voice; 23Surely they shall not see the land which I sware unto their fathers, neither shall any of them that provoked me see it:14.23 Surely…: Heb. If they see the land 24But my servant Caleb, because he had another spirit with him, and hath followed me fully, him will I bring into the land whereinto he went; and his seed shall possess it. 25(Now the Amalekites and the Canaanites dwelt in the valley.) To morrow turn you, and get you into the wilderness by the way of the Red sea.

26¶ And the LORD spake unto Moses and unto Aaron, saying, 27How long shall I bear with this evil congregation, which murmur against me? I have heard the murmurings of the children of Israel, which they murmur against me. 28Say unto them, As truly as I live, saith the LORD, as ye have spoken in mine ears, so will I do to you: 29Your carcases shall fall in this wilderness; and all that were numbered of you, according to your whole number, from twenty years old and upward, which have murmured against me, 30Doubtless ye shall not come into the land, concerning which I sware to make you dwell therein, save Caleb the son of Jephunneh, and Joshua the son of Nun.14.30 sware: Heb. lifted up my hand 31But your little ones, which ye said should be a prey, them will I bring in, and they shall know the land which ye have despised. 32But as for you, your carcases, they shall fall in this wilderness. 33And your children shall wander in the wilderness forty years, and bear your whoredoms, until your carcases be wasted in the wilderness.14.33 wander: or, feed 34After the number of the days in which ye searched the land, even forty days, each day for a year, shall ye bear your iniquities, even forty years, and ye shall know my breach of promise.14.34 breach…: or, altering of my purpose 35I the LORD have said, I will surely do it unto all this evil congregation, that are gathered together against me: in this wilderness they shall be consumed, and there they shall die.

36And the men, which Moses sent to search the land, who returned, and made all the congregation to murmur against him, by bringing up a slander upon the land, 37Even those men that did bring up the evil report upon the land, died by the plague before the LORD. 38But Joshua the son of Nun, and Caleb the son of Jephunneh, which were of the men that went to search the land, lived still. 39And Moses told these sayings unto all the children of Israel: and the people mourned greatly.

40¶ And they rose up early in the morning, and gat them up into the top of the mountain, saying, Lo, we be here, and will go up unto the place which the LORD hath promised: for we have sinned. 41And Moses said, Wherefore now do ye transgress the commandment of the LORD? but it shall not prosper. 42Go not up, for the LORD is not among you; that ye be not smitten before your enemies. 43For the Amalekites and the Canaanites are there before you, and ye shall fall by the sword: because ye are turned away from the LORD, therefore the LORD will not be with you. 44But they presumed to go up unto the hill top: nevertheless the ark of the covenant of the LORD, and Moses, departed not out of the camp. 45Then the Amalekites came down, and the Canaanites which dwelt in that hill, and smote them, and discomfited them, even unto Hormah.