Habakuki 1 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Habakuki 1:1-17

11:1 Nah 1:1Neno alilopokea nabii Habakuki.

Lalamiko La Habakuki

21:2 Za 13:1-2; 22:1-2; 6:3; 27:7; Yer 14:9Ee Bwana, hata lini nitakuomba msaada,

lakini wewe husikilizi?

Au kukulilia, “Udhalimu!”

Lakini hutaki kuokoa?

31:3 Ay 9:23; Yer 20:8; Za 55:9Kwa nini unanifanya nitazame dhuluma?

Kwa nini unavumilia makosa?

Uharibifu na udhalimu viko mbele yangu;

kuna mabishano na mapambano kwa wingi.

41:4 Ay 12:6; Za 12:8; 58:2Kwa hiyo sheria imepotoshwa,

nayo haki haipo kabisa.

Waovu wanawazunguka wenye haki,

kwa hiyo haki imepotoshwa.

Jibu La Bwana

5“Yatazame mataifa,

uangalie na ushangae kabisa.

Kwa sababu katika siku zako nitafanya kitu

ambacho hungeamini,

hata kama ungeambiwa.

6Nitawainua Wakaldayo,

watu hao wakatili na wenye haraka,

ambao hupita dunia yote

kuteka mahali pa kuishi pasipo pao wenyewe.

7Ni watu wanoogopwa na wanaotisha;

wenyewe ndio sheria yao,

na huinua heshima yao wenyewe.

8Farasi wao ni wepesi kuliko chui,

na wakali kuliko mbwa mwitu wakati wa machweo.

Askari wapanda farasi wao huenda mbio;

waendesha farasi wao wanatoka mbali.

Wanaruka kasi kama tai ili kurarua;

91:9 Hab 2:5wote wanakuja tayari kwa fujo.

Makundi yao ya wajeuri yanasonga mbele

kama upepo wa jangwani,

na kukusanya wafungwa

kama mchanga.

101:10 2Nya 36:6; Yer 33:4Wanawabeza wafalme,

na kuwadhihaki watawala.

Wanaicheka miji yote iliyozungushiwa maboma;

wanafanya malundo ya udongo na kuiteka hiyo miji.

111:11 Yer 4:11-12; Dan 4:30Kisha wanapita kasi kama upepo na kusonga mbele:

watu wenye hatia, ambao nguvu zao ndio mungu wao.”

Lalamiko La Pili La Habakuki

121:12 Mwa 21:33; Isa 31:1; 37:23; Kut 33:22; Isa 10:6; Mwa 49:24; Za 118:17Ee Bwana, je, wewe sio wa tangu milele?

Mungu wangu, Uliye Mtakatifu wangu, hatutakufa.

Ee Bwana, umewachagua wao ili watekeleze hukumu;

Ee Mwamba, umewaamuru watuadhibu.

131:13 Za 18:26; Mao 3:34-36; Za 25:3; Ay 21:7Macho yako ni safi mno hata yasiweze kuutazama uovu,

wala huwezi kuvumilia makosa.

Kwa nini basi unawavumilia wadanganyifu?

Kwa nini unakuwa kimya wakati waovu

wanawameza wale wenye haki

kuliko wao wenyewe?

14Umewafanya watu kama samaki baharini,

kama viumbe wa bahari wasio na mtawala.

151:15 Yer 5:26; Isa 19:8; Ay 18:8; Yer 16:16Adui mwovu anawavuta wote kwa ndoana,

anawakamata katika wavu wake,

anawakusanya katika juya lake;

kwa hiyo anashangilia na anafurahi.

161:16 Yer 44:8Kwa hiyo anatoa kafara kwa wavu wake,

na kuchoma uvumba kwa juya lake,

kwa kuwa kwa wavu wake anaishi kwa starehe,

na anafurahia chakula kizuri.

171:17 Isa 14:6; 19:8Je, aendelee kuwatoa walio katika wavu wake,

akiangamiza mataifa bila huruma?

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

哈巴谷书 1:1-17

1以下是哈巴谷先知得到的启示。

哈巴谷的抱怨

2耶和华啊,

我要向你呼救到何时,

你才垂听呢?

暴虐横行,我向你呼求,

你却不拯救。

3你为何让我目睹罪恶?

你为何容忍邪恶?

我眼前尽是毁灭和暴力,

到处是纷争和冲突。

4因此律法失效,

正义不彰,

恶人包围义人,

正义被扭曲。

耶和华的答复

5耶和华说:“你们环顾列国,

仔细察看,

必惊奇不已,

因为我要在你们的时代行一件事,

即使你们听说了也不会相信。

6我要使凶残、暴虐的迦勒底人兴起。

他们要席卷天下,

强占别人的家园。

7他们任意妄为,

令人胆战心惊。

8“他们的马比豹子还快,

比夜狼还猛。

他们的骑兵从远方飞驰而来,

如鹰扑食。

9他们残暴成性,

像狂风一样扑来,

抓获的俘虏多如尘沙。

10他们嘲笑君王,讥讽首领,

对一切坚城嗤之以鼻,

修筑高台将其攻取。

11他们如狂风横扫而过,

这些有罪的人把自己的力量奉为神明。”

哈巴谷再次抱怨

12耶和华,

我的上帝,我的圣者啊,

你从亘古就存在,

你永不消逝1:12 你永不消逝”另有希伯来文抄本作“我们不会死”。

耶和华啊,你派迦勒底人来审判;

磐石啊,你立他们作施罚者。

13你的眼目极为清洁,

见不得邪恶,

也不能容忍罪恶。

但你为何容忍奸恶之人呢?

恶人吞灭比他们公义的人,

你为何默然不语呢?

14你为何使人像海里的鱼,

像没有首领的爬虫呢?

15迦勒底人用钩子钩住他们,

用渔网网住他们,

用拖网把他们聚在一起,

并因此而欢喜快乐。

16迦勒底人向渔网献祭,

向渔网烧香,

因为他们靠渔网而富裕,

食物充足。

17难道他们要无休止地撒网,

无情地毁灭列国吗?