Ezra 6 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ezra 6:1-22

Amri Ya Dario

16:1 Ezr 4:15; 5:17Kisha Mfalme Dario alitoa amri, nao wakafanya uchunguzi katika kumbukumbu zilizohifadhiwa katika hazina huko Babeli. 2Karatasi moja ndefu ya maandishi ilipatikana huko Ekbatana katika jimbo la Umedi. Haya ndiyo yaliyokuwa yameandikwa humo:

Kumbukumbu:

36:3 Ezr 3:10; Hag 2:3Katika mwaka wa kwanza wa kutawala Mfalme Koreshi, mfalme alitoa amri kuhusu Hekalu la Mungu katika Yerusalemu:

Hekalu na lijengwe tena mahali palepale Wayahudi walipokuwa wakitoa dhabihu, kwenye msingi ule ule. Iwe na kimo cha mikono sitini,6:3 Mikono 60 ni sawa na mita 27. upana wa mikono sitini, 46:4 1Fal 6:36; Ezr 7:20; Isa 60:6; Za 68:29kuta zijengwe kwa safu tatu za mawe makubwa kisha ifuate safu moja ya mbao. Gharama zitalipwa kutoka hazina ya mfalme. 56:5 1Nya 29:2; Yer 27:18-22; Ezr 5:14Pia, vyombo vya dhahabu na vya fedha vya nyumba ya Mungu, ambavyo Nebukadneza alivichukua kutoka kwenye Hekalu huko Yerusalemu akavileta Babeli, yapasa virudishwe mahali pake ndani ya Hekalu huko Yerusalemu, yapasa viwekwe ndani ya nyumba ya Mungu.

66:6 Ezr 5:3Sasa basi, Tatenai, mtawala wa Ngʼambo ya Mto Frati na Shethar-Bozenai pamoja na ninyi, maafisa wenzao wa jimbo hilo kaeni mbali na mahali hapo. 7Msiingilie kazi ya Hekalu hili la Mungu. Mwacheni mtawala wa Wayahudi na viongozi Wayahudi wajenge upya nyumba hii ya Mungu mahali pake.

86:8 1Sam 9:10Zaidi ya hayo, hapa natoa amri kuhusu mtakalofanya kwa ajili ya wazee wa Wayahudi katika ujenzi wa nyumba hii ya Mungu:

Gharama za watu hawa zitalipwa kikamilifu kutoka hazina ya mfalme, kutoka kwenye mapato ya Ngʼambo ya Mto Frati, ili ujenzi usisimame. 9Chochote kinachohitajika kama mafahali wachanga, kondoo dume, wana-kondoo kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa Mungu wa mbinguni, ngano, chumvi, divai na mafuta kama vitakavyohitajika na makuhani huko Yerusalemu, lazima wapewe kila siku pasipo kukosa, 106:10 Ezr 7:23; Yer 29:7; Law 1:9; Mwa 8:21; 1Tim 2:1-2ili waweze kutoa dhabihu inayompendeza Mungu wa mbinguni na kumwombea mfalme na wanawe hali njema.

116:11 Kum 21:22-23; Es 2:23; Ezr 7:26; Dan 2:5Zaidi ya hayo, ninaamuru kwamba mtu yeyote atakayebadilisha amri hii, boriti itangʼolewa kutoka nyumba yake, ichongwe upande mmoja na atumbuliwe nayo. Kwa ajili ya kosa hili nyumba yake ifanywe lundo la taka. 126:12 Kut 20:24; Kum 12:11; 1Fal 9:3; 2Nya 7:16; Za 132:13Naye Mungu, aliyeliweka Jina lake huko, amwangushe mfalme yeyote au watu watakaoinua mikono kubadili amri hii au kuharibu Hekalu hili lililoko Yerusalemu.

Mimi Dario nimetoa amri hii. Nayo itekelezwe kwa bidii na kwa makini.

Jengo Linakamilika Na Kuwekwa Wakfu

136:13 Ay 5:12; Ezr 4:9; Za 9:16; 1Kor 3:19Kwa sababu ya amri aliyotoa Mfalme Dario, Tatenai mtawala wa Ngʼambo ya Mto Frati na Shethar-Bozenai na wenzao wakaitekeleza kwa bidii na kwa makini. 146:14 Ezr 5:1; 7:1; Neh 2:1; Ezr 4:24Hivyo wazee wa Wayahudi waliendelea kujenga na kustawi kutokana na mahubiri ya manabii Hagai na Zekaria, mwana wa Ido. Wakakamilisha ujenzi wa Hekalu kulingana na agizo la Mungu wa Israeli na amri ya Koreshi, Dario na Artashasta wafalme wa Uajemi. 156:15 Zek 4:9Hekalu lilikamilika siku ya kumi na mbili ya mwezi wa Adari, ndio mwezi wa tatu, katika mwaka wa sita wa utawala wa Mfalme Dario.

166:16 1Fal 8:63; 2Nya 7:15; Yn 10:22Kisha watu wa Israeli: makuhani, Walawi na wengine wote waliohamishwa, wakaadhimisha kule kuwekwa wakfu nyumba ya Mungu kwa shangwe. 176:17 2Sam 6:13; 1Nya 16:1-3; 2Nya 29:21; Hes 7:2-3; Ezr 8:25Kwa ajili ya kuwekwa wakfu nyumba hii ya Mungu walitoa mafahali mia moja, kondoo dume mia mbili, wana-kondoo mia nne, sadaka kwa ajili ya dhambi ya Israeli yote walitoa mbuzi dume kumi na wawili, mmoja kwa ajili ya kila kabila la Israeli. 186:18 1Nya 24:1; 23:6; Hes 3:6-9; 8:9-11Wakawaweka makuhani katika nafasi zao na Walawi wakawekwa katika makundi yao ya huduma kwa Mungu huko Yerusalemu, kulingana na ilivyoandikwa katika Kitabu cha Mose.

Pasaka

196:19 Kut 12:11; Hes 28:16Katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza, waliorudi kutoka uhamishoni wakaadhimisha Pasaka. 206:20 2Nya 30:15-17; 35:11; Kut 12:25; 2Nya 29:34Makuhani na Walawi walikuwa wamekwisha kujitakasa nao wamekuwa safi kwa kufuata kawaida za ibada. Walawi wakachinja kondoo wa Pasaka kwa ajili ya wana wa waliorudi kutoka utumwani uhamishoni, kwa ajili ya ndugu zao makuhani na wao wenyewe. 216:21 Kut 12:48; Za 93:5Hivyo Waisraeli waliokuwa wamerudi kutoka utumwani uhamishoni wakaila Pasaka, pamoja na wale waliokuwa wamejitenga na matendo ya unajisi wa Mataifa ya jirani ili kumtafuta Bwana, Mungu wa Israeli. 226:22 Kut 12:17; Mit 21:1; Ezr 1:1Kwa muda wa siku saba waliiadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu kwa furaha, kwa sababu Bwana alikuwa amewajaza furaha kwa kubadilisha nia ya mfalme wa Ashuru kwamba awasaidie ujenzi wa nyumba ya Mungu, Mungu wa Israeli.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

以斯拉记 6:1-22

发现塞鲁士王的谕旨

1于是,大流士王下令查阅保存在巴比伦库房里的典籍。 2玛代亚马他城的宫内找到一卷书,书中记载如下:

3塞鲁士王元年,塞鲁士王就耶路撒冷的上帝之殿降下谕旨,要重建这殿作献祭之处,要奠立殿的地基。殿要高二十七米、宽二十七米, 4每三层巨石加铺一层木料,经费由国库支付。 5尼布甲尼撒耶路撒冷上帝的殿里掳到巴比伦的金银器皿,都要归还到耶路撒冷上帝的殿里,放回原处。”

6于是,大流士王降旨:

“河西总督达乃示他·波斯乃,以及你们的同僚——河西的官员,要远离那殿! 7不要干涉上帝殿的建造,要让犹太人的省长和长老在原址上重建这座上帝的殿。 8另外,我降旨命你们帮助犹太人的长老建造上帝的殿,要立刻从河西的王室税收中拨出款项作建殿之用,以免耽误工程。 9他们向天上的上帝献燔祭时所需的公牛犊、公绵羊、绵羊羔、小麦、盐、酒和油,都要照耶路撒冷祭司的话天天供给他们,不得有误, 10好让他们向天上的上帝献上蒙悦纳的祭物,并为王和众王子求寿。 11我再降旨,若有人更改这谕旨,必从他的房屋抽掉一根大梁,把他钉在梁上挂起来,他的房屋也要沦为粪堆。 12无论君王还是百姓,若有人擅自更改这命令或毁坏耶路撒冷的这殿,愿拣选这殿作其居所的上帝毁灭他!我大流士降此谕旨,务要速速遵行。”

建殿工程竣工

13于是,河西总督达乃示他·波斯乃及其同僚都认真执行大流士王的谕旨。 14哈该先知和易多的子孙撒迦利亚的劝勉下,犹太人的长老建造这殿,进展顺利。他们遵照上帝的命令和波斯塞鲁士大流士亚达薛西的谕旨,完成了建殿工程。 15大流士王第六年亚达月6:15 亚达月”即希伯来历的十二月,阳历是二月中旬到三月中旬。三日,建殿工程竣工。

举行献殿礼

16以色列人、祭司、利未人,以及其余流亡归来的人都满心欢喜地为上帝的殿举行奉献礼。 17他们为此献上一百头公牛犊,二百只公绵羊和四百只绵羊羔,又照以色列十二支派的数目献上十二只公山羊,作全体以色列人的赎罪祭。 18他们依照摩西律法书的规定,派祭司和利未人按班次在耶路撒冷事奉上帝。

守逾越节

19一月十四日,流亡归来的人守逾越节。 20祭司和利未人一起自洁,成为洁净的人,并为所有流亡归来的人、其他祭司同胞以及他们自己宰杀逾越节的羔羊。 21从流亡之地归回的以色列人,连同所有弃绝当地民族的污秽行为、寻求以色列的上帝耶和华的人,一起吃这羔羊。 22他们欢欢喜喜地守除酵节七天,因为耶和华使亚述王对他们心存善意,帮助他们重建以色列上帝的殿。