Ezekieli 42 – NEN & NIVUK

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ezekieli 42:1-20

Vyumba Vya Makuhani

142:1 Kut 27:9; Eze 40:17; 41:12-14Ndipo yule mtu akaniongoza kuelekea kaskazini mpaka kwenye ua wa nje na kunileta mpaka kwenye vyumba vinavyoelekeana na ua wa Hekalu na kuelekeana na ukuta wa nje upande wa kaskazini. 2Jengo ambalo mlango wake ulielekea kaskazini lilikuwa na urefu wa dhiraa mia moja na upana wa dhiraa hamsini. 342:3 Eze 41:15-16Mbele ya zile dhiraa ishirini za ule ua wa ndani unaoelekeana na ile njia ya ua wa nje, kuliinuka vyumba virefu kimoja baada ya kingine vya ghorofa tatu. 442:4 Eze 46:19Mbele ya hivi vyumba kulikuwa na njia ya ndani yenye upana wa dhiraa kumi na urefu wa dhiraa mia moja. Milango yake ilikuwa upande wa kaskazini. 5Basi vyumba vya juu vilikuwa vyembamba zaidi, kwa kuwa ujia42:5 Ujia ina maana ya njia ndani ya nyumba. ulichukua nafasi zaidi ndani yake kuliko katika vyumba vya sakafu ya chini na vya katikati ya jengo. 6Vyumba katika ghorofa ya tatu havikuwa na nguzo, kama kumbi zilivyokuwa nazo, kwa hiyo eneo la sakafu ya vyumba vya juu lilikuwa ni dogo kuliko la sakafu ya chini na ya kati. 7Kulikuwa na ukuta wa nje uliokuwa sambamba na vile vyumba na ukumbi wa nje, ulitokeza urefu wa dhiraa hamsini. 8Wakati safu ya vyumba katika ua wa nje vilikuwa na urefu wa dhiraa hamsini, vile vyumba vilivyokuwa karibu zaidi na Hekalu vilikuwa na urefu wa dhiraa mia moja. 942:9 Eze 44:5; 46:19Vyumba vya chini vilikuwa na ingilio upande wa mashariki unapoingia kutoka ukumbi wa nje.

1042:10 Eze 41:12-14; 42:1Upande wa kusini kufuata urefu wa ukuta wa ukumbi wa nje, unaopakana na ukumbi wa Hekalu na kuelekeana na ukuta wa nje, kulikuwa na vyumba 1142:11 Eze 42:4vyenye ujia unayopita mbele yake. Hivi vilifanana na vile vyumba vya upande wa kaskazini, vilikuwa na urefu na upana ulio sawa, mahali pa kutokea na vipimo vyake vilikuwa sawa. Kama ilivyokuwa milango ya upande wa kaskazini, 12ndivyo ilivyokuwa milango ya vyumba vya upande wa kusini. Kulikuwa na ingilio kuanzia mwanzo wa njia ambao ulikuwa sambamba na ukuta wa pili uliokuwa upande wa mashariki, ambako ndiko kwa kuingia vyumbani.

1342:13 Kut 30:20; Eze 40:46; Law 6:29; 14:13; Kut 29:31; Kum 21:5; Hes 18:9-10; Yer 41:5; Eze 41:12-14Kisha akaniambia, “Vyumba vya upande wa kaskazini na vya upande wa kusini ambavyo vinaelekeana na ukumbi wa Hekalu ni vyumba vya makuhani, mahali ambapo wale makuhani ambao humkaribia Bwana watakula zile sadaka takatifu sana. Huko ndiko watakakoweka zile sadaka takatifu sana, yaani, sadaka za nafaka, sadaka za dhambi na sadaka za hatia, kwa kuwa mahali ni patakatifu. 1442:14 Law 16:23; Kut 28:40-43; Eze 44:19; Kut 29:9; Law 8:7-9; Kut 29:4-9Mara makuhani waingiapo mahali patakatifu, hawaruhusiwi kwenda kwenye ukumbi wa nje mpaka wayaache mavazi ambayo walivaa wakiwa wanahudumu, kwa kuwa hayo mavazi ni matakatifu. Inawapasa kuvaa mavazi mengine kabla hawajakaribia eneo lililo wazi kwa ajili ya watu.”

15Alipomaliza kupima vile vilivyokuwa katika eneo la ndani la Hekalu, akanitoa nje kupitia lango la upande wa mashariki na kupima eneo lote linalozunguka: 16Akapima upande wa mashariki kwa ule ufito wa kupimia, nao ulikuwa dhiraa 50042:16 Dhiraa 500 ni sawa na mita 225. 17Akapima upande wa kaskazini, nao ulikuwa dhiraa 500 kwa ufito ule wa kupimia. 18Tena akapima upande wa kusini, nao ulikuwa dhiraa 500 kwa ufito ule wa kupimia. 19Kisha akageukia upande wa magharibi na kuupima, ulikuwa dhiraa 500 kwa ufito ule wa kupimia. 2042:20 Eze 40:5; Zek 2:5-6; Eze 45:2; Ufu 21:16; Eze 22:26; 43:12Hivyo akapima eneo katika pande zote nne. Lilikuwa na ukuta kulizunguka wenye urefu wa dhiraa 500 na upana wa dhiraa 500, uliotenganisha mahali Patakatifu na eneo la watu wote.

New International Version – UK

Ezekiel 42:1-20

The rooms for the priests

1Then the man led me northward into the outer court and brought me to the rooms opposite the temple courtyard and opposite the outer wall on the north side. 2The building whose door faced north was a hundred cubits long and fifty cubits wide.42:2 That is, about 53 metres long and 27 metres wide 3Both in the section twenty cubits42:3 That is, about 11 metres from the inner court and in the section opposite the pavement of the outer court, gallery faced gallery at the three levels. 4In front of the rooms was an inner passageway ten cubits wide and a hundred cubits42:4 Septuagint and Syriac; Hebrew and one cubit long.42:4 That is, about 5.3 metres wide and 53 metres long Their doors were on the north. 5Now the upper rooms were narrower, for the galleries took more space from them than from the rooms on the lower and middle floors of the building. 6The rooms on the top floor had no pillars, as the courts had; so they were smaller in floor space than those on the lower and middle floors. 7There was an outer wall parallel to the rooms and the outer court; it extended in front of the rooms for fifty cubits. 8While the row of rooms on the side next to the outer court was fifty cubits long, the row on the side nearest the sanctuary was a hundred cubits long. 9The lower rooms had an entrance on the east side as one enters them from the outer court.

10On the south side42:10 Septuagint; Hebrew Eastward along the length of the wall of the outer court, adjoining the temple courtyard and opposite the outer wall, were rooms 11with a passageway in front of them. These were like the rooms on the north; they had the same length and width, with similar exits and dimensions. Similar to the doorways on the north 12were the doorways of the rooms on the south. There was a doorway at the beginning of the passageway that was parallel to the corresponding wall extending eastward, by which one enters the rooms.

13Then he said to me, ‘The north and south rooms facing the temple courtyard are the priests’ rooms, where the priests who approach the Lord will eat the most holy offerings. There they will put the most holy offerings – the grain offerings, the sin offerings42:13 Or purification offerings and the guilt offerings – for the place is holy. 14Once the priests enter the holy precincts, they are not to go into the outer court until they leave behind the garments in which they minister, for these are holy. They are to put on other clothes before they go near the places that are for the people.’

15When he had finished measuring what was inside the temple area, he led me out by the east gate and measured the area all around: 16he measured the east side with the measuring rod; it was five hundred cubits.42:16 See Septuagint of verse 17; Hebrew rods; also in verses 18 and 19.42:16 Five hundred cubits equal about 265 metres; also in verses 17, 18 and 19. 17He measured the north side; it was five hundred cubits42:17 Septuagint; Hebrew rods by the measuring rod. 18He measured the south side; it was five hundred cubits by the measuring rod. 19Then he turned to the west side and measured; it was five hundred cubits by the measuring rod. 20So he measured the area on all four sides. It had a wall round it, five hundred cubits long and five hundred cubits wide, to separate the holy from the common.