Ezekieli 41 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ezekieli 41:1-26

141:1 Zek 6:12; Mt 16:18; Ufu 3:12Kisha yule mtu akanileta katika sehemu ya nje ya patakatifu, naye akaipima miimo; upana wake ulikuwa dhiraa sita41:1 Dhiraa 6 ni sawa na mita 2.7. kila upande. 241:2 2Nya 3:3Ingilio lilikuwa la upana wa dhiraa kumi na kuta zilizojitokeza kila upande zilikuwa na upana wa dhiraa tano. Pia akapima sehemu ya nje ya patakatifu, nayo ilikuwa na urefu wa dhiraa arobaini41:2 Dhiraa 40 ni sawa na mita 18. na upana wa dhiraa ishirini.

3Kisha akaingia sehemu takatifu ndani ya Hekalu na kupima miimo ya ingilio, kila mmoja ulikuwa na upana wa dhiraa mbili. Ingilio lilikuwa na upana wa dhiraa sita, na kuta zilizotokeza kila upande zilikuwa na upana wa dhiraa saba.41:3 Dhiraa 7 ni sawa na mita 3.15. 441:4 1Fal 6:20; Kut 26:33; Ebr 9:3-8Naye akapima urefu wa sehemu takatifu ndani, nao ulikuwa dhiraa ishirini, na upana wake ulikuwa dhiraa ishirini hadi mwisho wa sehemu ya nje ya sehemu takatifu. Akaniambia, “Hapa ndipo Patakatifu pa Patakatifu.”

5Kisha akapima ukuta wa Hekalu, nao ulikuwa na unene wa dhiraa sita, na kila chumba cha pembeni kuzunguka Hekalu kilikuwa na upana wa dhiraa nne. 641:6 Eze 40:17; 1Fal 6:5-6Vyumba vya pembeni vilikuwa na ghorofa tatu, kimoja juu ya kingine, kila ghorofa ilikuwa na vyumba thelathini. Kulikuwa na boriti katika ukuta wote wa Hekalu ili kuimarisha vyumba vya pembeni, kwa hiyo boriti hizo hazikushikamanishwa kwenye ukuta wa Hekalu. 741:7 1Fal 6:8Vyumba vya pembeni vilivyozunguka Hekalu vilizidi kupanuka kulingana na sakafu zilivyokwenda juu. Ujenzi uliozunguka Hekalu ulijengwa kukwea juu, kwa hiyo vyumba vilipanuka kwa kadiri ya kila kimoja kilivyokwenda juu. Ngazi za kupandia zilianzia sakafu ya chini hadi sakafu ya juu kabisa kwa kupitia sakafu ya kati.

841:8 Isa 28:16; Eze 40:5Nikaona pia kuwa Hekalu lilikuwa na kitako kilichoinuliwa pande zote, huu ulikuwa ndio msingi wa vile vyumba vya pembeni ambao ulikuwa na urefu wa ule ufito mmoja wa kupimia, yaani, dhiraa ndefu sita. 9Ukuta wa nje wa vyumba vya pembeni ulikuwa na unene wa dhiraa tano. Eneo la wazi katikati ya vyumba vya pembeni vya Hekalu 10na vyumba vya makuhani lilikuwa na upana wa dhiraa ishirini kuzunguka Hekalu pande zote. 11Kulikuwa na maingilio kwenye vyumba vya pembeni kutokea eneo lililo wazi, moja upande wa kaskazini na lingine upande wa kusini, nao msingi uliounganisha lile eneo la wazi ulikuwa na upana wa dhiraa tano ukilizunguka lote.

12Jengo lililoelekeana na ua wa Hekalu upande wa magharibi lilikuwa na upana wa dhiraa sabini. Ukuta wa jengo hilo ulikuwa na unene wa dhiraa tano, kulizunguka lote, urefu ulikuwa wa dhiraa tisini.41:12 Dhiraa 90 ni sawa na mita 40.5.

13Kisha akapima Hekalu, lilikuwa na urefu wa dhiraa mia moja na ua wa Hekalu na jengo pamoja na kuta zake vilikuwa na urefu wa dhiraa mia moja pia. 1441:14 Eze 40:47Upana wa ua wa Hekalu upande wa mashariki, pamoja na upande wa mbele wa Hekalu ulikuwa dhiraa mia moja.

1541:15 Eze 42:3Kisha akapima urefu wa jengo linaloelekeana na ua upande wa nyuma wa Hekalu, pamoja na vyumba vyake kila upande, ilikuwa dhiraa mia moja.

Sehemu takatifu ya nje, sehemu takatifu ya ndani, pamoja na baraza inayoelekeana na ukumbi, 1641:16 1Fal 6:4, 15; Eze 42:3; Isa 54:12; 1Kor 13:12pamoja na vizingiti, madirisha membamba na vyumba vyote vitatu, kila kimoja pamoja na kizingiti vilifunikwa kwa mbao. Sakafu, ukuta mpaka kwenye madirisha na madirisha yenyewe vilifunikwa kwa mbao. 17Katika nafasi iliyokuwa juu ya upande wa nje wa ingilio la sehemu takatifu ya ndani, na katika kuta zilizozunguka sehemu takatifu ya ndani na sehemu takatifu ya nje, kwa nafasi zilizo sawa, 1841:18 1Fal 6:18; Kut 37:7; 1Fal 7:36; Eze 10:21; Mwa 3:24; Kut 25:22; 1Fal 2:26kulinakshiwa makerubi na miti ya mitende. Miti ya mitende ilikuwa kati ya kerubi na kerubi. Kila kerubi alikuwa na nyuso mbili: 1941:19 Eze 10:14; 1:10upande mmoja uso wa mwanadamu kuelekea mti wa mtende na upande mwingine uso wa simba ukielekea mti mwingine wa mtende. Ilinakshiwa kuzunguka Hekalu lote. 20Kuanzia sakafu mpaka eneo lililo juu ya ingilio, palinakshiwa makerubi na miti ya mitende pamoja na kwenye ukuta wa nje wa patakatifu.

2141:21 Eze 41:1Mahali patakatifu pa nje palikuwa na miimo ya mlango uliokuwa mraba na ule uliokuwa katika Patakatifu Pa Patakatifu ulikuwa unafanana na huo mwingine. 2241:22 Kut 30:1; 25:23; Mal 1:7-12; Wim 1:12; Eze 23:41Kulikuwa na madhabahu ya mbao kimo chake dhiraa tatu na ilikuwa dhiraa mbili mraba pande zote, tako lake na pande zake zilikuwa za mbao. Yule mtu akaniambia, “Hii ni meza ambayo iko mbele za Bwana.” 2341:23 1Fal 6:32Mahali patakatifu pa nje na Patakatifu Pa Patakatifu zilikuwa na milango miwili. 2441:24 1Fal 6:34Kila mlango ulikuwa na vipande viwili, vipande viwili vilivyoshikwa na bawaba vyenye kufunguka kwa kila mlango. 25Juu ya hiyo milango ya Patakatifu palinakshiwa makerubi na miti ya mitende kama yale yaliyonakshiwa kwenye kuta, na kulikuwa na ubao ulioningʼinia mbele ya baraza kwa nje. 2641:26 Eze 40:16Katika kuta za pembeni za ukumbi kulikuwa na madirisha membamba yaliyonakshiwa miti ya mitende kila upande. Vyumba vya pembeni vya Hekalu pia vilikuwa vimefunikwa kwa mbao.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

以西结书 41:1-26

1那人带我进入殿堂,量两边的墙柱,各三米宽。 2殿的入口宽五米,两边的墙各宽二点五米。殿堂面积长二十米,宽十米。 3他到内殿的入口,量两边的墙柱,各一米宽,门宽三米,两边的墙各宽三点五米。 4他量了内殿,长宽各十米。他对我说:“这是至圣所。”

5他又量殿墙,厚三米,殿的外围有厢房,每间宽二米。 6厢房是一层叠一层的,共有三层,每层有三十个房间。殿墙外围有支撑厢房梁木的墙坎,以免梁木插入殿墙中。 7这些厢房的设计是阶梯形的;因此,厢房越往上层越宽,有楼梯自下层经过中层到上层。 8殿的周围有突出的平台,高一竿,构成厢房的根基。 9-10厢房外墙厚二点五米,厢房与祭司房之间的空地宽十米。 11有两个门从空地通往厢房,一南一北。厢房周围与空地相连的平台宽二点五米。

12在殿前空地向西的地方有一栋建筑物,宽三十五米,长四十五米,墙厚二点五米。

13他量了殿,长五十米。殿的院子,那栋建筑物和墙共长五十米。 14殿东边的空地宽五十米。

15他量了殿后面、空地对面的那栋建筑物及其两边走廊的长度,共长五十米。

16圣所、至圣所、院子对面的门廊及它们周围的门槛、格子窗和走廊从地面到窗沿都镶有木板。 17殿的入口和里外四周的墙也按尺寸镶着木板。 18木板上刻着基路伯天使和棕树,两者彼此相间排列。基路伯天使有两个面孔: 19一个是人的脸,面向一边的棕树;一个是狮子的脸,面向另一边的棕树。 20从地板到门以上殿内墙壁上都刻着基路伯天使和棕树。

21圣所的门框是方形的,至圣所前的门框也一样。 22里面有一座木头做的祭坛,高一点五米,宽一米,坛的四角、底及四面都是木造的。他对我说:“这是耶和华面前的桌子。”

23圣所和至圣所各有一道双扇的门, 24每扇都是可以折叠的双页门, 25上面也刻有基路伯天使和棕树,与殿内墙上所刻的一样。门廊上有木造的廊檐。 26圣殿门廊的墙壁上有格子窗和棕树雕刻,厢房都有房檐。