Ezekieli 40 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ezekieli 40:1-49

Eneo La Hekalu Jipya

140:1 2Fal 25:7; Yer 52:4-11; Eze 29:17; Yer 39:1-10Katika mwaka wa ishirini na tano wa uhamisho wetu, mwanzoni mwa huo mwaka, siku ya kumi ya mwezi, katika mwaka wa kumi na nne baada ya kuanguka kwa mji, siku hiyo hiyo mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu, naye akanipeleka huko. 240:2 Kut 24:10; Dan 7:7; Yer 31:12; Ufu 21:10Nikiwa katika maono ya Mungu alinichukua mpaka nchi ya Israeli, naye akaniweka kwenye mlima mrefu sana, ambako upande wa kusini kulikuwepo baadhi ya majengo ambayo yalionekana kama mji. 340:3 Dan 10:6; Ufu 1:15; Zek 2:1-2; Ufu 11:1; Eze 47:3Akanipeleka huko, nami nikamwona mtu ambaye kuonekana kwake kulikuwa kama kuonekana kwa shaba. Alikuwa amesimama kwenye lango akiwa na kamba ya kitani na ufito wa kupimia mkononi mwake. 440:4 Yer 26:1; Eze 44:5; Kum 6:6Mtu huyo akaniambia, “Mwanadamu, angalia kwa macho yako na usikie kwa masikio yako nawe uzingatie kitu nitakachokuonyesha, kwa kuwa ndiyo sababu umeletwa hapa. Iambie nyumba ya Israeli kila kitu utakachoona.”

Lango La Mashariki Kuelekea Ukumbi Wa Nje

540:5 Isa 26:1; Eze 42:20Nikaona ukuta uliozunguka eneo lote la Hekalu. Ule ufito wa kupimia uliokuwa mkononi mwa yule mtu ulikuwa na urefu wa dhiraa ndefu sita,40:5 Dhiraa ndefu 6 ni sawa na mita 3.18. yaani, dhiraa ndefu ni sawa na dhiraa na nyanda nne, akapima ule ukuta. Ukuta huo ulikuwa na unene wa dhiraa ndefu sita na kimo cha dhiraa ndefu sita.

640:6 Eze 8:16Kisha akaenda kwenye lango linaloelekea mashariki. Akapanda ngazi zake akapima kizingiti cha lango, nacho kilikuwa na kina cha huo ufito. 7Vyumba vya kupumzikia vya walinzi vilikuwa na urefu wa huo ufito mmoja na upana wa huo ufito, kuta zilizogawa vyumba hivyo vya mapumziko zilikuwa na unene wa dhiraa tano.40:7 Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25. Nacho kizingiti cha lango lililokuwa karibu na ukumbi unaoelekea hekaluni ulikuwa na kina cha huo ufito.

8Kisha akapima baraza ya njia ya lango, 9ambayo ilikuwa na kina cha dhiraa nane40:9 Dhiraa 8 ni sawa na mita 3.6. na miimo yake ilikuwa na unene wa dhiraa mbili.40:9 Dhiraa 2 ni sawa na sentimita 90. Baraza ya lango ilielekea Hekalu.

10Ndani ya lango la mashariki kulikuwepo vyumba vitatu vya kupumzikia kila upande, vyote vitatu vilikuwa na vipimo vilivyo sawa, nazo nyuso za kuta zilizotenganisha kila upande zilikuwa na vipimo vilivyo sawa. 11Kisha akapima upana wa ingilio la lango, ilikuwa dhiraa kumi na urefu wake ulikuwa dhiraa kumi na tatu. 12Mbele ya kila chumba cha kupumzikia kulikuwepo ukuta uliokuwa na kimo cha dhiraa moja40:12 Dhiraa 1 ni sawa na sentimita 45. kwenda juu, navyo hivyo vyumba vilikuwa dhiraa sita mraba. 13Kisha akapima njia ya lango kuanzia juu ya ukuta wa nyuma wa chumba kimoja cha kupumzikia hadi juu ya ukuta wa nyuma wa chumba upande wa pili; kukawa na nafasi ya dhiraa ishirini na tano kuanzia lango la ukuta mmoja hadi lango la ukuta uliokuwa upande mwingine. 1440:14 Kut 27:9; Isa 62:9Akapima pia ukumbi, urefu wa dhiraa ishirini40:14 Dhiraa 20 ni sawa na mita 9. na lango linalofuatia hiyo nguzo kila upande wa huo ukumbi. 15Umbali kuanzia ingilio la njia ya lango hadi mwisho kabisa wa baraza yake ulikuwa dhiraa hamsini.40:15 Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5. 1640:16 2Nya 3:5; Eze 41:6; 42:1; 1Fal 6:4; Eze 41:26Kulikuwa na vidirisha kwenye hivyo vyumba vya walinzi na nguzo za hivyo vyumba zilikuwa kwenye mzunguko wa hilo lango, vivyo hivyo kulikuwa na madirisha yaliyozunguka kuelekeana na ua na juu ya kila nguzo kulikuwa na mapambo ya miti ya mitende.

Ukumbi Wa Nje

17Kisha akanileta katika ukumbi wa nje. Huko nikaona vyumba vingine pamoja na njia iliyokuwa imejengwa kuzunguka ukumbi wote, kulikuwa na vyumba thelathini vimepangana kando ya hiyo njia. 18Njia hii iliyojengwa iliambaa na lango, ikiwa na urefu sawa na lango, hii ilikuwa ni njia ya chini. 1940:19 Eze 40:23, 27; 46:1Kisha akapima umbali kutoka ndani ya lango la chini mpaka nje ya ukumbi wa ndani, nao ulikuwa dhiraa mia moja40:19 Dhiraa 100 ni sawa na mita 45. upande wa mashariki na dhiraa mia moja upande wa kaskazini.

Lango La Kaskazini

20Kisha akapima urefu na upana wa lango linaloelekea kaskazini, kukabili ukumbi wa nje. 2140:21 Eze 40:7Vyumba vyake vilikuwa vitatu kila upande, kuta zilizogawanya vyumba na baraza ilikuwa na vipimo sawa na zile kuta za lango la kwanza. Zilikuwa na urefu wa dhiraa hamsini na upana wa dhiraa ishirini na tano.40:21 Dhiraa 25 ni sawa na mita 11.25. 2240:22 Eze 40:16, 26, 49Madirisha yake, baraza yake na nakshi yake ya miti ya mitende vilikuwa na vipimo sawasawa na vile vya lango linaloelekea mashariki. Kulikuwa na ngazi saba za kupandia huko, pamoja na baraza yake mkabala nazo. 2340:23 Eze 40:19Kulikuwa na lango kwenye ukumbi wa ndani lililoelekea lile lango la kaskazini, kama vile ilivyokuwa ule upande wa mashariki. Akapima kutoka lango moja hadi lile lililo mkabala nalo, lilikuwa dhiraa mia moja.

Lango La Kusini

2440:24 Eze 40:32, 35Ndipo akaniongoza mpaka upande wa kusini, nami nikaona lango linaloelekea kusini. Akaipima miimo yake na baraza yake, navyo vilikuwa na vipimo sawa kama hivyo vingine. 2540:25 Eze 40:33Lango na baraza yake vilikuwa na madirisha membamba pande zote, kama madirisha ya huko kwingine. Ilikuwa na urefu wa dhiraa hamsini na upana wake dhiraa ishirini na tano. 2640:26 Eze 40:22Kulikuwa na ngazi saba za kupandia huko, pamoja na baraza yake mkabala nazo. Ilikuwa na nakshi za miti ya mitende kwenye kuta zilizogawanya vyumba kila upande. 2740:27 Eze 40:19, 32Ukumbi wa ndani pia ulikuwa na lango lililoelekea kusini. Naye akapima kutoka lango hili mpaka kwenye lango la nje upande wa kusini; ilikuwa dhiraa mia moja.

Malango Ya Kuelekea Ukumbi Wa Ndani

2840:28 Eze 40:35Kisha akanileta mpaka ukumbi wa ndani kwa kupitia lango la kusini, naye akapima lango la kusini, ambalo lilikuwa na vipimo sawa na yale mengine. 2940:29 1Fal 6:5-10; 1Nya 28:11-12; Neh 10:38-39Vyumba vyake, kuta zilizogawanya vyumba na ukumbi wake zilikuwa na vipimo sawasawa na zile nyingine. Hilo lango na baraza yake vilikuwa na madirisha pande zote. Navyo vilikuwa na urefu wa dhiraa hamsini na upana wa dhiraa ishirini na tano. 3040:30 Eze 40:21(Baraza za malango zilizozunguka ukumbi wa ndani zilikuwa na upana wa dhiraa ishirini na tano na kina cha dhiraa tano.) 3140:31 Eze 40:22, 34, 37Baraza yake ilielekeana na ukumbi wa nje, miimo yake ilinakshiwa miti ya mitende, kulikuwa na ngazi nane za kupandia huko.

32Kisha akanileta mpaka kwenye ukumbi wa ndani ulioko upande wa mashariki, naye akalipima lango hilo, lilikuwa na vipimo vilivyo sawasawa na yale mengine. 3340:33 Eze 40:7Vyumba vyake, kuta zake na baraza yake vilikuwa na vipimo vilivyo sawa na vile vingine. Lile lango pamoja na baraza yake vilikuwa na madirisha pande zote. Urefu wake ulikuwa dhiraa hamsini na upana wake dhiraa ishirini na tano. 3440:34 Eze 40:22Baraza yake ilielekea ukumbi wa nje, miimo yake ilinakshiwa miti ya mitende pande zote. Kulikuwa na ngazi nane za kupandia huko.

3540:35 Eze 44:4; 47:2Kisha akanileta mpaka kwenye lango la kaskazini na kulipima. Lilikuwa na vipimo sawa na yale mengine, 3640:36 Eze 40:7kama vile ilivyokuwa kwa vyumba, kuta zake na baraza yake, tena kulikuwa na madirisha pande zote. Ilikuwa na urefu wa dhiraa hamsini na upana wake dhiraa ishirini na tano. 3740:37 Eze 40:22, 34Baraza yake ilielekeana na ukumbi wa nje, miimo yake ilinakshiwa miti ya mitende pande zote, kulikuwa na ngazi nane za kupandia huko.

Vyumba Vya Kutayarishia Dhabihu

3840:38 2Nya 4:6; Eze 42:13; Ebr 9:14Kulikuwa na chumba na mlango karibu na baraza katika kila njia ya ndani ya lango ambamo sadaka za kuteketezwa zilioshwa. 3940:39 Eze 46:2; Law 4:28; Hes 6:12; Ebr 10:12-14; 2Kor 5:21Kwenye baraza ya lile lango kulikuwepo meza mbili kila upande, ambako sadaka za kuteketezwa, sadaka za dhambi na sadaka za hatia zilichinjiwa. 40Karibu na ukuta wa nje wa baraza ya lile lango karibu na ngazi kwenye ingilio kuelekea kaskazini kulikuwa na meza mbili, nako upande mwingine wa ngazi kulikuwepo na meza mbili. 41Kwa hiyo kulikuwa na meza nne upande mmoja wa lango na nyingine nne upande mwingine, zote zilikuwa meza nane, ambapo dhabihu zilichinjiwa. 4240:42 Kut 20:25Pia kulikuwa na meza nne za mawe yaliyochongwa kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, kila meza ilikuwa na urefu wa dhiraa moja na nusu,40:42 Dhiraa 1.5 ni sawa na sentimita 67.5. upana wake dhiraa moja na nusu na kimo cha dhiraa moja. Juu ya meza hizo viliwekwa vyombo vya kuchinjia sadaka za kuteketezwa na dhabihu nyingine mbalimbali. 43Kulikuwa na kulabu, urefu wake nyanda nne,40:43 Nyanda 4 ni sawa na sentimita 8. zilikuwa zimeshikizwa ukutani pande zote. Meza zilikuwa kwa ajili ya nyama za sadaka.

Vyumba Kwa Ajili Ya Makuhani

4440:44 1Nya 6:31; Kol 3:16; Efe 5:19Nje ya lango la ndani, kwenye ukumbi wa ndani, kulikuwa na vyumba viwili, kimoja upande wa lango la kaskazini nacho kilielekea kusini, kingine upande wa lango la kusini nacho kilielekea kaskazini. 4540:45 1Nya 9:23; Law 8:35Akaniambia, “Chumba kinachoelekea upande wa kusini ni kwa ajili ya makuhani ambao wana usimamizi wa hekaluni, 4640:46 Hes 18:5; 16:5; 2Sam 8:17; Eze 48:11; 42:13; Kol 4:12; Eze 43:19; Ezr 7:2; Eze 44:15nacho chumba kinachoelekea upande wa kaskazini ni kwa ajili ya makuhani wenye usimamizi wa madhabahuni. Hawa ni wana wa Sadoki, ambao ndio Walawi pekee wanaoweza kumkaribia Bwana ili kuhudumu mbele zake.”

4740:47 Eze 41:13-14Ndipo alipopima ukumbi: nao ulikuwa mraba wa dhiraa mia moja urefu na upana. Madhabahu yalikuwa mbele ya Hekalu.

Hekalu

4840:48 1Fal 6:2Akanileta mpaka kwenye baraza ya Hekalu naye akaipima miimo ya hiyo baraza, nayo ilikuwa na upana wa dhiraa tatu40:48 Dhiraa 3 ni sawa na mita 1.35. kila upande. Upana wa ingilio ulikuwa dhiraa kumi na nne40:48 Dhiraa 14 ni sawa na mita 6.3. na kuta zake zilikuwa na upana wa dhiraa tatu kila upande. 4940:49 1Fal 6:3; 7:15Baraza ilikuwa na dhiraa ishirini kwenda juu na dhiraa kumi na mbili40:49 Dhiraa 12 ni sawa na mita 5.4. kuanzia mbele hadi nyuma. Kulikuwa na ngazi kumi za kupandia huko, pia kulikuwa na nguzo kwa kila upande wa miimo.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

以西結書 40:1-49

新聖殿的異象

1在我們被擄的第二十五年,就是耶路撒冷淪陷的第十四年一月十日,耶和華的靈降在我身上。 2在異象中上帝把我帶到以色列的一座高山上,山的南面彷彿有一座城。 3祂把我帶到那裡。城的入口站著一個面色如銅的人,手中拿著一條麻繩和一根量竿。 4那人對我說:「人子啊,你要留心用眼看,專心用耳聽,注意我指示你的一切,因為我帶你來這裡正是為了要指示你。你要把所見到的一切告訴以色列人。」

外院的門

5我看見殿的四周有牆,那人拿了一根三米長的量竿測量這牆,量出牆厚一竿,高一竿。

6然後,他帶我到殿的東門,走上石階,來到門口。他量了門洞,寬一竿。 7門內有守衛室,長度和寬度都是一竿。室與室之間相距二點二米,通往聖殿的內門洞寬一竿, 8通往聖殿的門廊寬度也是一竿, 9連牆柱在內共四點二米寬,牆柱寬一點零五米。 10東門內共有六間守衛室,每邊三間,大小面積都是一樣,兩邊的牆尺寸也相同。 11通道盡頭有一道門廊,寬五米,長六點五米。 12兩邊守衛室前面的矮牆高五十釐米,守衛室都是三米寬的正方形。 13他又量門廊的寬度,即這邊守衛室的屋頂到對面守衛室的屋頂,是十二點五米。 14他從門口的牆量到外院的牆柱,是三十米。 15由門口到通道盡頭的內廊共二十五米, 16守衛室、牆柱上和門廊周圍都有格子窗,牆柱上刻著棕樹。

外院

17他帶我到外院,外院靠牆的四周是鋪石地,上面共有三十間廂房。 18鋪石地在門口的兩邊,比內院低,寬度與入口的長度一樣。 19他從外院的內門口量到內院的門口,距離是五十米。

北門

20他又量了外院的北門, 21通道兩邊各有三間守衛室,牆和廊子長度和寬度跟東門一樣,分別是二十五米和十二點五米。 22它的窗戶、門廊、牆柱上雕刻的棕樹都和東門的尺寸相同。登上七級石階便到達門口,通道的盡頭是門廊。 23內院的北門與外院的北門相對,正如它的東門和外院的東門相對,門與門之間的距離是五十米。

南門

24他又帶我到南門,量了牆柱和門廊,都與其他門的尺寸相同, 25通道與門廊四周的窗戶也和其他的門一樣,通道長二十五米,寬十二點五米。 26登上七級石階便到門廊,兩邊的牆柱也同樣刻著棕樹。 27內院也有南門,與外院南門之間的距離是五十米。

內院的門

28他帶我從南門走進內院,量了南門,跟其他門的尺寸一樣。 29守衛室、牆柱和門廊都和其他的尺寸一樣,通道與門廊四周有窗戶,通道長二十五米,寬十二點五米。 30內院周圍的門廊都是長十二點五米,寬二點五米。 31這些門廊靠外院,兩邊的牆柱刻著棕樹,上去的石階共有八級。

32他又帶我從東門進入內院,量了東門,跟其他門的尺寸一樣, 33守衛室、牆柱、門廊和其他門的尺寸一樣,通道與門廊的四周也有窗戶,通道長二十五米,寬十二點五米。 34門廊靠外院,兩邊的牆柱刻著棕樹,那裡的石階共有八級。

35他又帶我到北門,量了北門,跟其他門的尺寸一樣。 36守衛室、牆柱、門廊和其他門的尺寸一樣,通道長二十五米,寬十二點五米,四周有窗戶。 37門廊靠外院,兩邊的牆柱刻著棕樹,那裡的石階共有八級。

廂房

38門口的牆柱旁邊有一個房間,供祭司洗燔祭牲。 39門廊兩邊各有兩張用來屠宰燔祭牲、贖罪祭牲和贖過祭牲的桌子。 40內院北門的兩邊各有兩張桌子, 41即裡外各有四張桌子,共八張,供祭司屠宰祭牲之用。 42另有四張用石頭鑿成的桌子用來預備燔祭牲,屠宰燔祭牲及其他祭牲的器具都放在桌上。桌子長寬各七十五釐米,高五十釐米。 43廊內四周掛著七點五釐米長的雙鉤。桌上放著祭肉。

44在內院有歌樂手用的廂房,一間向南,在北門旁,一間向北,在南門旁。 45他對我說:「向南的廂房是給殿內供職的祭司用的, 46向北的廂房是給壇前供職的祭司用的。他們都是撒督的子孫,利未的後裔,在耶和華面前專職事奉。」 47他量了殿前的院子,是五十米寬的正方形,祭壇在殿的前面。

聖殿

48他帶我來到殿前通往聖所的門廊,量了兩旁的牆柱,各二點五米寬,門兩邊的牆一點五米厚, 49門廊長十米,寬四點九米。上門廊靠近牆柱的石級兩旁各有一根柱子。