Ezekieli 35 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ezekieli 35:1-15

Unabii Dhidi Ya Edomu

1Neno la Bwana likanijia kusema: 235:2 Mwa 14:6; Kum 2:5; Yer 49:7-8; Amo 1:11“Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya mlima Seiri, utabiri dhidi yake 335:3 Yer 6:12; Eze 34:10; 25:12-14; Oba 1:10na useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi ni kinyume nawe, ee mlima Seiri, nami nitanyoosha mkono wangu dhidi yako na kukufanya ukiwa na usiyekaliwa na watu wala kulimika. 435:4 Yer 49:10; 44:2Nitaifanya miji yako kuwa magofu nawe utakuwa ukiwa. Ndipo utakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.

535:5 Za 137:7; Eze 21:29; Za 63:10; Oba 1:13“ ‘Kwa sababu ulificha moyoni uadui wa siku nyingi nawe ukawatoa Waisraeli wauawe kwa upanga wakati wa maafa yao, wakati adhabu yake ilipofikia kilele chake, 635:6 Isa 63:2-6; 34:3kwa hiyo hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, nitakutia katika umwagaji damu nao utakufuatia. Kwa kuwa hakuchukia kumwaga damu, kumwaga damu kutakufuatia. 735:7 Yer 46:19; 49:17Nitaufanya Mlima Seiri ukiwa na usiokaliwa na watu wala kulimika na kuukatilia mbali na wote wanaokuja na wanaokwenda. 835:8 Eze 31:12Nitaijaza milima yenu kwa watu wake waliouawa, wale waliouawa kwa upanga wataanguka juu ya vilima vyako na katika mabonde yako na katika makorongo yako yote. 935:9 Isa 34:5-6; Yer 49:13-17; Oba 1:10Nitakufanya ukiwa milele, watu hawataishi katika miji yako. Ndipo utakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.

1035:10 Za 83:12; Eze 36:2-5“ ‘Kwa sababu umesema, “Mataifa haya mawili na nchi hizi zitakuwa zetu nasi tutazimiliki,” ingawa hata mimi Bwana nilikuwa huko, 1135:11 Eze 25:14; Oba 1:15; Mt 7:2; Isa 26:9; Za 9:16kwa hiyo hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, nitakutenda kwa kadiri ya hasira na wivu uliouonyesha katika chuki yako juu yao nami nitafanya nijulikane miongoni mwao wakati nitakapokuhukumu. 1235:12 Yer 50:7; Za 9:16Ndipo utakapojua kuwa Mimi Bwana nimesikia mambo yote ya dharau uliyosema dhidi ya milima ya Israeli. Ulisema, “Wamefanyika ukiwa na kutiwa mikononi mwetu tuwararue.” 1335:13 Dan 11:36; Yer 49:16Ulijigamba dhidi yangu na kusema maneno dhidi yangu bila kujizuia, nami nikayasikia. 1435:14 Yer 51:48Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Wakati dunia yote inashangilia nitakufanya ukiwa. 1535:15 Mit 17:5; Eze 36:5; Oba 1:12; Mao 4:4-21; Yer 50:11-13; Isa 34:5-6; Eze 32:29Kwa sababu ulishangilia wakati urithi wa nyumba ya Israeli ulipofanyika ukiwa, hivyo ndivyo nitakavyokutendea. Utakuwa ukiwa, ee mlima Seiri, wewe na Edomu yote. Kisha ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Bwana.’ ”

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

以西結書 35:1-15

預言以東受懲罰

1耶和華對我說: 2「人子啊,你要面向西珥山,發預言斥責它, 3告訴它,主耶和華這樣說,『西珥山啊,我要與你為敵,伸手攻擊你,使你荒涼不堪。 4我要使你的城邑淪為廢墟,一片荒涼,這樣你就知道我是耶和華。 5因為你永懷仇恨,在以色列人遭遇危難、因罪惡受盡刑罰的時候,把他們交在刀下。 6所以主耶和華說,我憑我的永恆起誓,你既然不憎恨殺人流血之事,殺人流血之事必臨到你。 7我要使西珥山荒涼不堪,消滅一切來往此地的人, 8我要使喪身刀下的人遍佈你的高山、丘陵、山谷和溪流。 9我要使你永遠荒廢,你的城邑杳無人跡,這樣你就知道我是耶和華。

10「『因為你曾說,猶大以色列必歸我,即使上帝在那裡,我們也要吞併他們。 11所以主耶和華說,我憑我的永恆起誓,你憎恨他們,滿腹怒氣和嫉妒,我也必這樣對待你。我審判你的時候,以色列人就會認識我。 12那時,你必知道我耶和華聽見了你譭謗以色列山嶺的一切話,你說,這些山嶺荒廢了,歸我們所有了。 13你妄自尊大,肆意譭謗我,我都聽見了。 14主耶和華這樣說,普天下歡樂的時候,我要使你荒涼。 15你既因以色列的荒涼而幸災樂禍,我要讓你遭受同樣的下場。西珥山啊,你和以東都要荒涼。這樣,你們就知道我是耶和華。』