Ezekieli 31 – NEN & NIV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ezekieli 31:1-18

Mwerezi Katika Lebanoni

131:1 Yer 52:5; Eze 32:17; 30:20Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa tatu, siku ya kwanza, neno la Bwana likanijia, kusema: 231:2 Eze 31:18“Mwanadamu, mwambie Farao mfalme wa Misri na makundi yake ya wajeuri:

“ ‘Je, ni nani awezaye kulinganishwa

na wewe katika fahari.

331:3 Nah 3:18; Isa 10:34; Eze 19:11; Sef 2:13; Yer 50:18; 2Fal 19:23; Hab 2:17; Zek 11:1Angalia Ashuru, wakati fulani ilikuwa mwerezi huko Lebanoni,

ukiwa na matawi mazuri ukitia msitu kivuli;

ulikuwa mrefu sana,

kilele chake kilipita majani ya miti yote.

431:4 Eze 17:7; Dan 4:10Maji mengi yaliustawisha,

chemchemi zenye maji mengi ziliufanya urefuke;

vijito vyake vilitiririka pale

ulipoota pande zote

na kupeleka mifereji yake

kwenye miti yote ya shambani.

531:5 Hes 24:6; Eze 17:5; Dan 4:11Hivyo ukarefuka

kupita miti yote ya shambani;

vitawi vyake viliongezeka

na matawi yake yakawa marefu,

yakitanda kwa sababu ya wingi wa maji.

631:6 Eze 17:23; Mt 13:32; Dan 4:12; Mwa 31:7-9Ndege wote wa angani

wakaweka viota kwenye vitawi vyake,

wanyama wote wa shambani

wakazaana chini ya matawi yake,

mataifa makubwa yote

yaliishi chini ya kivuli chake.

731:7 Ay 14:9Ulikuwa na fahari katika uzuri,

ukiwa na matawi yaliyotanda,

kwa kuwa mizizi yake ilikwenda chini

mpaka kwenye maji mengi.

831:8 Za 80:10; Mwa 2:8-9; 30:37Mierezi katika bustani ya Mungu

haikuweza kushindana nao,

wala misunobari haikuweza

kulingana na vitawi vyake,

wala miaramoni

haikulinganishwa na matawi yake,

wala hakukuwa na mti katika bustani ya Mungu

wa kulinganisha na uzuri wake.

931:9 Kut 9:16; Dan 4:22-24; Mwa 13:10; Eze 28:13Niliufanya kuwa mzuri

ukiwa na matawi mengi,

ulionewa wivu na miti yote ya Edeni

katika bustani ya Mungu.

1031:10 Isa 2:11; 14:13-14; Ay 40:11-12; Mit 16:18; Dan 5:20; Eze 28:17“ ‘Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa sababu ulikuwa mrefu sana, kilele chake kikiwa juu ya majani manene ya miti na kwa sababu ulikuwa na kiburi cha urefu wake, 1131:11 Dan 5:20niliutia mikononi mwa mtawala wa mataifa, ili yeye aushughulikie sawasawa na uovu wake. Nikaukatilia mbali, 1231:12 Eze 32:5; 28:7; 32:11-12; 35:8; Dan 4:12-14nayo mataifa mageni yaliyo makatili sana yaliukata huo mti na kuuacha. Matawi yake yalianguka juu ya milima na kwenye mabonde yote, vitawi vyake vikavunjika na kusambaa katika makorongo yote ya nchi. Mataifa yote ya duniani yakaondoka kutoka kwenye kivuli chake na kuuacha. 1331:13 Isa 18:6; Eze 29:5; 32:431:13 Isa 18:6; Eze 29:5; 32:4Ndege wote wa angani wakakaa kwenye ule mti ulioanguka na wanyama pori wote wakakaa katikati ya vitawi vyake. 1431:14 Za 82:7; Hes 14:11; Za 63:9; Eze 32:18; Za 49:14Kamwe hakutakuwa na miti mingine kando ya hayo maji itakayorefuka zaidi ya huo, vilele vyake vikiwa juu ya majani yote ya miti. Hakuna miti mingine, hata kama imekunywa maji vizuri namna gani, itakayofikia urefu huo. Yote mwisho wake ni kifo, na kuingia ardhini, kama vile ilivyo kwa wanadamu, pamoja na wale waendao shimoni.

1531:15 2Sam 1:21“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Katika siku ile mwerezi uliposhushwa chini kaburini31:15 Yaani Kuzimu, Sheol kwa Kiebrania; pia mstari 16, 17. nilizifunika chemchemi zenye maji mengi kwa maombolezo: Nilivizuia vijito vyake na wingi wa maji yake nikauzuia. Kwa sababu yake niliivika Lebanoni huzuni, nayo miti yote ya shambani ikanyauka. 1631:16 Yer 49:21; Eze 26:15; Isa 14:8; Eze 32:18, 31; Isa 14:15; Eze 14:22Niliyafanya mataifa yatetemeke kwa kishindo cha kuanguka kwake wakati nilipoushusha chini kaburini pamoja na wale washukao shimoni. Ndipo miti yote ya Edeni, miti iliyo bora kuliko yote na iliyo mizuri sana ya Lebanoni, miti yote ile iliyokunywa maji vizuri, ilifarijika hapa duniani. 1731:17 Za 9:17Wale walioishi katika kivuli chake, wale walioungana naye miongoni mwa mataifa, nao pia walikuwa wamezikwa pamoja naye, wakiungana na wale waliouawa kwa upanga.

1831:18 Yer 9:26; Eze 32:19-21; 28:10“ ‘Ni miti ipi ya Edeni inayoweza kulinganishwa nawe kwa fahari na utukufu? Hata hivyo, wewe pia, utashushwa chini pamoja na miti ya Edeni mpaka kuzimu, utalala miongoni mwa wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga.

“ ‘Huyu ni Farao pamoja na makundi yake yote ya wajeuri, asema Bwana Mwenyezi.’ ”

New International Version

Ezekiel 31:1-18

Pharaoh as a Felled Cedar of Lebanon

1In the eleventh year, in the third month on the first day, the word of the Lord came to me: 2“Son of man, say to Pharaoh king of Egypt and to his hordes:

“ ‘Who can be compared with you in majesty?

3Consider Assyria, once a cedar in Lebanon,

with beautiful branches overshadowing the forest;

it towered on high,

its top above the thick foliage.

4The waters nourished it,

deep springs made it grow tall;

their streams flowed

all around its base

and sent their channels

to all the trees of the field.

5So it towered higher

than all the trees of the field;

its boughs increased

and its branches grew long,

spreading because of abundant waters.

6All the birds of the sky

nested in its boughs,

all the animals of the wild

gave birth under its branches;

all the great nations

lived in its shade.

7It was majestic in beauty,

with its spreading boughs,

for its roots went down

to abundant waters.

8The cedars in the garden of God

could not rival it,

nor could the junipers

equal its boughs,

nor could the plane trees

compare with its branches—

no tree in the garden of God

could match its beauty.

9I made it beautiful

with abundant branches,

the envy of all the trees of Eden

in the garden of God.

10“ ‘Therefore this is what the Sovereign Lord says: Because the great cedar towered over the thick foliage, and because it was proud of its height, 11I gave it into the hands of the ruler of the nations, for him to deal with according to its wickedness. I cast it aside, 12and the most ruthless of foreign nations cut it down and left it. Its boughs fell on the mountains and in all the valleys; its branches lay broken in all the ravines of the land. All the nations of the earth came out from under its shade and left it. 13All the birds settled on the fallen tree, and all the wild animals lived among its branches. 14Therefore no other trees by the waters are ever to tower proudly on high, lifting their tops above the thick foliage. No other trees so well-watered are ever to reach such a height; they are all destined for death, for the earth below, among mortals who go down to the realm of the dead.

15“ ‘This is what the Sovereign Lord says: On the day it was brought down to the realm of the dead I covered the deep springs with mourning for it; I held back its streams, and its abundant waters were restrained. Because of it I clothed Lebanon with gloom, and all the trees of the field withered away. 16I made the nations tremble at the sound of its fall when I brought it down to the realm of the dead to be with those who go down to the pit. Then all the trees of Eden, the choicest and best of Lebanon, the well-watered trees, were consoled in the earth below. 17They too, like the great cedar, had gone down to the realm of the dead, to those killed by the sword, along with the armed men who lived in its shade among the nations.

18“ ‘Which of the trees of Eden can be compared with you in splendor and majesty? Yet you, too, will be brought down with the trees of Eden to the earth below; you will lie among the uncircumcised, with those killed by the sword.

“ ‘This is Pharaoh and all his hordes, declares the Sovereign Lord.’ ”