Ezekieli 29 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ezekieli 29:1-21

Unabii Dhidi Ya Misri

1Katika mwaka wa kumi, mwezi wa kumi, siku ya kumi na mbili, neno la Bwana likanijia kusema: 229:2 Yer 25:19; Isa 19:1-17; Yer 46:2; Eze 25:2; 30:1-26; 31:1-18“Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Farao mfalme wa Misri na utabiri dhidi yake na dhidi ya Misri yote. 329:3 Yer 44:30; Za 68:30; Isa 27:1; Eze 32:2; Yer 46:8Nena, nawe useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Mimi ni kinyume nawe, Farao, mfalme wa Misri,

joka kubwa ulalaye katikati ya vijito vyako.

Unasema, “Mto Naili ni wangu mwenyewe;

niliufanya kwa ajili yangu mwenyewe.”

429:4 2Fal 19:28; Ay 41:2; Eze 38:4Lakini nitatia ndoana katika mataya yako

nami nitawafanya samaki wa vijito vyako

washikamane na magamba yako.

Nitakutoa katikati ya vijito vyako,

pamoja na samaki wote

walioshikamana na magamba yako.

529:5 Yer 7:33; 34:20; 8:2; Eze 31:13; 32:4-6; 39:4Nitakutupa jangwani,

wewe pamoja na samaki wote wa vijito vyako.

Utaanguka uwanjani,

nawe hutakusanywa au kuchukuliwa.

Nitakutoa uwe chakula

kwa wanyama wa nchi

na ndege wa angani.

629:6 2Fal 18:21; Isa 36:6Ndipo wale wote waishio Misri watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.

“ ‘Umekuwa fimbo ya tete kwa nyumba ya Israeli. 729:7 Yer 17:5; Eze 17:15-17; 2Fal 18:21; Isa 36:6Walipokushika kwa mikono yao, ulivunjika na kuchana mabega yao; walipokuegemea, ulivunjika na migongo yao ikateguka.

829:8 Eze 14:17; 25:13; 32:11-13“ ‘Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitaleta upanga juu yako na kuua watu wako na wanyama wao. 929:9 Eze 30:7-8, 13-19; Mit 16:18; Yer 46:8Misri itakuwa ukiwa na isiyolimwa wala kukaliwa na watu. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.

“ ‘Kwa sababu ulisema, “Mto Naili ni wangu; mimi niliufanya,” 1029:10 Eze 30:6-12; Yer 21:13; Kut 3:22; Yer 46:19; Kut 14:2; Isa 18:1kwa hiyo mimi ni kinyume nawe na kinyume na vijito vyako, nami nitaifanya nchi ya Misri kuwa magofu na ukiwa isiyolimwa wala kukaliwa na watu kuanzia Migdoli hadi Aswani, hata kufikia mpakani wa Ethiopia. 1129:11 Eze 32:13Hakuna unyayo wa mtu au mnyama utakaopita ndani yake, wala hakuna yeyote atakayeishi humo kwa muda wa miaka arobaini. 1229:12 Yer 46:19; Eze 30:7; 34:10Nitaifanya nchi ya Misri ukiwa, miongoni mwa nchi zilizo ukiwa, nayo miji yake itabaki ukiwa miaka arobaini miongoni mwa miji iliyo magofu. Nami nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huku na huko katika nchi nyingine.

1329:13 Isa 19:23; Yer 46:26“ ‘Lakini hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mwishoni mwa hiyo miaka arobaini, nitawakusanya Wamisri kutoka mataifa walikotawanywa. 1429:14 Isa 11:11; Eze 30:14; 17:14; Isa 19:22; Yer 46:26Nitawarudisha hao Wamisri kutoka kwenye kutekwa kwao na kuwaweka katika Pathrosi,29:14 Pathrosi ni Misri ya Juu. nchi ya baba zao. Huko watakuwa na ufalme usiokuwa na nguvu. 1529:15 Zek 10:11Utakuwa ufalme dhaifu kuliko zote na kamwe Misri haitajikweza tena juu ya mataifa mengine. Nitaufanya ufalme wake dhaifu sana kiasi kwamba kamwe hautatawala tena juu ya mataifa mengine. 1629:16 2Nya 32:10; Isa 20:5; Hos 8:13; Isa 30:2; Mao 4:17; Hes 5:15Misri haitakuwa tena tumaini la watu wa Israeli bali itakuwa kumbukumbu ya dhambi yao kwa kuigeukia kuomba msaada. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana Mwenyezi.’ ”

1729:17 Eze 30:20; 24:1; 40:1Katika mwaka wa ishirini na saba, mwezi wa kwanza, siku ya kwanza, neno la Bwana likanijia, kusema: 1829:18 Yer 27:6; Law 13:40; Ay 1:20; Yer 39:1“Mwanadamu, Nebukadneza mfalme wa Babeli aliongoza jeshi lake kufanya kazi ngumu dhidi ya Tiro; kila kichwa kilipata upaa na kila bega likachunika. Lakini yeye na jeshi lake hawakupata malipo yoyote kutokana na muda wote aliongoza hiyo vita dhidi ya Tiro. 1929:19 Yer 43:10-13; Eze 32:11; Yer 27:6; Isa 19:4; Eze 26:5; 30:4, 10Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitaitia Misri mikononi mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli, naye atachukua utajiri wa Misri. Atateka mateka na kuchukua nyara mali za Misri kama ujira kwa ajili ya jeshi lake. 2029:20 Isa 45:1; Yer 25; 9; Isa 43:3; 10:6-7Nimempa mfalme wa Babeli nchi ya Misri kuwa ujira kwa juhudi zake kwa sababu yeye na jeshi lake walifanya kwa ajili yangu, asema Bwana Mwenyezi.

2129:21 Lk 1:69; 1Sam 2:10; Za 132:17; Eze 33:22; 3:27; 24:27“Katika siku hiyo nitaifanya nyumba ya Israeli iwe na nguvu nami nitakifungua kinywa chako miongoni mwao. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana.”

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

以西結書 29:1-21

預言審判埃及

1第十年十月十二日,耶和華對我說: 2「人子啊,你要說預言斥責埃及王法老和埃及全國, 3你要告訴他,主耶和華這樣說,

埃及王法老啊,

你這躺臥在自己河中的大怪物,

我要與你為敵。

你說這尼羅河屬於你,

是你為自己造的。

4但我要鉤住你的腮,

使河中的魚貼在你的鱗甲上,

把你連同貼在你鱗甲上的魚一起從河中拉上來,

5丟棄在曠野。

你必曝屍野外,無人收殮。

我要讓你成為野獸和飛鳥的食物。

6「『這樣,所有的埃及人就知道我是耶和華,因為你不過是一根蘆葦,以色列人無法依靠你。 7當他們用手握住你的時候,你就斷裂,刺傷了他們的肩;當他們倚靠你的時候,你就折斷,閃了他們的腰。

8「『因此,主耶和華說,看啊,我要使刀劍臨到你,消滅你的人畜, 9使埃及一片荒涼。這樣,他們就知道我是耶和華。因為你說這尼羅河屬於你,是你造的。 10因此,我要攻擊你和你的河流,使埃及密奪色弗尼,一直到古實的邊界全都荒廢。 11四十年之內,這裡必無人居住,人獸蹤跡滅絕。 12我必使埃及成為荒地中的荒地,讓埃及的城邑淪為廢墟中的廢墟,長達四十年。我要將埃及人驅散到列國,分散到列邦。』

13「主耶和華說,『四十年之後,我要把分散的埃及人從各國聚集起來。 14我要把被擄的埃及人帶回來,使他們回到故土巴特羅,成為一個卑微的國家, 15在列國中最衰微,再也不能雄居列國之上。我要使埃及國勢衰弱,再也不能統治列國。 16埃及不再是以色列人的指望,反而會使以色列人想起自己投靠埃及的罪。這樣,他們便知道我是主耶和華。』」

17第二十七年一月一日,耶和華對我說: 18「人子啊,巴比倫尼布甲尼撒派兵苦攻泰爾,以致士兵的頭都禿了,肩也破了,卻是徒勞無功。 19所以主耶和華說,『我要把埃及賜給巴比倫尼布甲尼撒,他必擄掠埃及的財富為戰利品,犒賞自己的軍隊。 20他和他的軍隊為我效力,所以我把埃及賜給他作為酬勞。』這是主耶和華說的。

21「到那天,我必復興以色列29·21 我必復興以色列」希伯來文是「我必使一隻角從以色列興起」。,使你以西結在他們當中開口說話,這樣他們就知道我是耶和華。」