Ezekieli 25 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ezekieli 25:1-17

Unabii Dhidi Ya Amoni

1Neno la Bwana likanijia kusema: 225:2 Sef 2:9; Eze 21:28; Yer 49:1-6; Eze 13:17; 29:2“Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Waamoni utabiri dhidi yao. 325:3 Za 35:21; Eze 36:2; Mit 17:5; Sef 2:9; Eze 36:2Waambie, ‘Sikieni neno la Bwana Mwenyezi. Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa sababu ulisema, “Aha!” juu ya mahali pangu patakatifu palipotiwa unajisi, na juu ya nchi ya Israeli ilipoangamizwa, na juu ya watu wa Yuda walipokwenda uhamishoni, 425:4 Mwa 25:6; Amu 6:3-33; Kum 28:33; Mwa 45:18; Hes 31:10kwa hiyo nitawatia mikononi mwa watu wa mashariki mkawe mali yao. Watapiga kambi zao katikati yenu na kufanya makazi miongoni mwenu, watakula matunda yenu na kunywa maziwa yenu. 525:5 Kum 3:11; Isa 17:2; Eze 21:20; Sef 2:14Nitaufanya mji wa Raba kuwa malisho ya ngamia na Amoni kuwa mahali pa kondoo pa kupumzikia. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana. 625:6 Mao 1:12; Sef 2:8; Eze 6:11; Hes 24:10Kwa kuwa hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa kuwa umepiga makofi yako na kufanya kishindo kwa miguu, mkifurahia kwa mioyo yenu miovu juu ya yale mabaya yaliyoipata nchi ya Israeli, 725:7 Eze 21:31; Amo 1:14-15; Hes 14:3; Eze 13:14-17hivyo nitaunyoosha mkono wangu dhidi yako na kukutoa kuwa nyara kwa mataifa. Nitakukatilia mbali kutoka kwenye mataifa na kukungʼoa katika nchi. Nitakuangamiza, nawe utajua ya kuwa Mimi ndimi Bwana.’ ”

Unabii Dhidi Ya Moabu

825:8 Mwa 19:37; Yer 48:1; Kum 23:6; Isa 16:6; Mwa 14:6“Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: ‘Kwa sababu Moabu na Seiri wamesema, “Tazama, nyumba ya Yuda imekuwa kama mataifa mengine yote,” 925:9 Yos 13:19; Hes 32:3, 37; Yos 13:17; Hes 33:49kwa hiyo nitaiondoa ile miji iliyo kando ya Moabu, kuanzia miji iliyoko mipakani, yaani: Beth-Yeshimothi, Baal-Meoni na Kiriathaimu, iliyo utukufu wa nchi hiyo. 1025:10 Eze 25:4; 21:32Nitaitia Moabu pamoja na Waamoni mikononi mwa watu wa Mashariki kuwa milki yao, ili kwamba Waamoni wasikumbukwe miongoni mwa mataifa, 1125:11 Isa 15:9; Yer 48:9; Isa 16:1-14nami nitatoa adhabu kwa Moabu. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.’ ”

Unabii Dhidi Ya Edomu

1225:12 2Sam 8:13-14; Mao 4:22; Oba 1:10; Isa 11:14; 2Nya 28:17“Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: ‘Kwa sababu Edomu ulilipiza kisasi juu ya nyumba ya Yuda na kukosa sana kwa kufanya hivyo, 1325:13 Eze 29:8; Yer 25:23; Kut 7:5; Eze 16:27; Yer 49:10; Eze 14:17; Mwa 36:11-15kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitaunyoosha mkono wangu dhidi ya Edomu na kuua watu wake na wanyama wao. Nitaufanya ukiwa, kuanzia Temani hadi Dedani wataanguka kwa upanga. 1425:14 Eze 32:29; 35:2-3, 11; 36:5Nitalipiza Edomu kisasi kwa mkono wa watu wangu Israeli, nao watawatendea Edomu sawasawa na hasira yangu na ghadhabu yangu, nao watakijua kisasi changu, asema Bwana Mwenyezi.’ ”

Unabii Dhidi Ya Ufilisti

1525:15 Yer 25:20; 47:1; Yoe 3:4; Amo 1:6; 2Nya 28:18“Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: ‘Kwa sababu Wafilisti wamewalipiza kisasi kwa uovu wa mioyo yao na kwa uadui wa siku nyingi wakataka kuangamiza Yuda, 1625:16 2Nya 26:6; Yer 47:1-7; 1Sam 30:14; Eze 20:33kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi ninakaribia kuunyoosha mkono wangu dhidi ya Wafilisti, nami nitawakatilia mbali Wakerethi na kuwaangamiza wale waliosalia katika pwani. 1725:17 Hes 31:3; Yer 44:13; Kut 6:2; 8:22; Isa 11:14; 14:30; Yer 47:7; Yoe 3:4Nitalipiza kisasi kikubwa juu yao na kuwaadhibu katika ghadhabu yangu. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana, nitakapolipiza kisasi juu yao.’ ”

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

以西結書 25:1-17

預言審判外族人

1耶和華對我說: 2「人子啊,你要面向亞捫人,說預言斥責他們, 3告訴他們要聽主耶和華的話。主耶和華說,『當我的聖所被褻瀆,以色列變得荒涼,猶大人被擄的時候,你們竟然哈哈而樂。 4所以我要使東方人侵佔你們的地方。他們必在你們的土地上安營紮寨,吃你們出產的果子,喝你們牛羊的奶。 5我要使拉巴成為駱駝的草場,使亞捫人的土地變成羊群歇息之處,這樣你們便知道我是耶和華。

6「主耶和華說,『你們看到以色列的災禍,便幸災樂禍,手舞足蹈。 7因此,我要伸手攻擊你們,使你們成為各國的俘虜。我必從萬民中剷除你們,從萬國中消滅你們,使你們滅絕。這樣,你們就知道我是耶和華。』

斥責摩押

8「耶和華說,『摩押西珥嘲笑猶大與其他各國沒有兩樣。 9所以我要攻陷摩押邊界的城邑,就是那地方引以為榮的伯·耶西末巴力·免基列亭10我要將它和亞捫人一起交給東方人統治,使亞捫人從此被列國遺忘。 11我必審判摩押人,這樣他們就知道我是耶和華。』

斥責以東

12「耶和華說,『因為以東報復猶大,犯了大罪。 13所以,我要伸手攻擊以東,剷除那裡的人和牲畜,使地荒廢,從提幔直到底但以東人要倒在刀下。 14我要藉我以色列子民的手向以東報仇。以色列人會照我的烈怒懲罰他們。那時,他們就會嚐到我報應他們的滋味,這是主耶和華說的。』

斥責非利士

15「主耶和華說,『非利士人心存仇恨,為了報世仇要毀滅猶大16所以我必伸手攻擊他們,剷除基利提人,毀滅沿海殘餘的人。 17我要報應他們,發烈怒懲罰他們。我報應他們的時候,他們就知道我是耶和華。』」