Ezekieli 16 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ezekieli 16:1-63

Yerusalemu, Mwanamke Asiye Mwaminifu

1Neno la Bwana likanijia kusema: 216:2 Eze 20:4; 8:17; 22:2; 23:36; Isa 57:12“Mwanadamu, ijulishe Yerusalemu kuhusu mwenendo wake wa machukizo 316:3 Mwa 11:25-29; Eze 21:30; Mwa 10:15; Yos 24:14-15; Mwa 12:18; 16:15na useme, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi, analomwambia Yerusalemu: Wewe asili yako na kuzaliwa kwako ni katika nchi ya Kanaani, baba yako alikuwa Mwamori, naye mama yako alikuwa Mhiti. 416:4 Hos 2:3Siku uliyozaliwa kitovu chako hakikukatwa, wala hukuogeshwa kwa maji ili kukufanya safi, wala hukusuguliwa kwa chumvi wala kufunikwa kwa nguo. 5Hakuna yeyote aliyekuonea huruma au kukusikitikia kiasi cha kukutendea mojawapo ya mambo haya. Badala yake, ulipozaliwa ulitupwa nje penye uwanja, kwa kuwa katika siku uliyozaliwa ulidharauliwa.

616:6 Kut 19:4; Eze 18:23, 32“ ‘Ndipo nilipopita karibu nawe nikakuona ukigaagaa kwenye damu yako, nawe ulipokuwa umelala hapo penye hiyo damu nikakuambia, “Ishi!” 716:7 Kum 1:10; Kut 1:7Nilikufanya uote kama mmea wa shambani. Ukakua na kuongezeka sana, ukawa kito cha thamani kuliko vyote. Matiti yako yakatokeza na nywele zako zikaota, wewe uliyekuwa uchi na bila kitu chochote.

816:8 Rut 3:9; Kut 19:5; Hos 2:7-20; Mal 2:4; Yer 2:2; 11:10“ ‘Baadaye nikapita karibu nawe, nilipokutazama na kukuona kuwa umefikia umri wa kupendwa, nililitandaza vazi langu juu yako na kuufunika uchi wako. Nikakuapia na kuingia kwenye Agano na wewe, asema Bwana Mwenyezi, nawe ukawa wangu.

916:9 Rut 3:3“ ‘Nilikuogesha kwa maji, nikakuosha ile damu na kukupaka mafuta. 1016:10 Kut 26:36; Isa 19:9; Eze 27:16; Isa 3:23Nikakuvika vazi lililotariziwa na kukuvalisha viatu vya kamba vya ngozi. Nikakuvika nguo za kitani safi na kukufunika kwa mavazi ya thamani kubwa. 1116:11 Yer 4:30; Eze 23:40; Isa 3:19; Eze 23:42; Mwa 41:42; Za 73:6Nikakupamba kwa vito: nikakuvika bangili mikononi mwako na mkufu shingoni mwako, 1216:12 Isa 3:21; 28:5; Yer 13:18; Mwa 35:4nikaweka hazama puani mwako, vipuli masikioni mwako na taji nzuri sana kichwani mwako. 1316:13 1Sam 10:1; 1Fal 4:21; Es 2:9, 17; Za 48:2; Es 5:1; Kum 32:13-14Kwa hiyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha, nguo zako zilikuwa za kitani safi, hariri na nguo iliyokuwa imetariziwa. Chakula chako kilikuwa unga laini, asali na mafuta ya zeituni. Ukawa mzuri sana ukainuka kuwa malkia. 1416:14 1Fal 10:24; Es 1:11; Za 48:2; Mao 2:15; Eze 5:5Umaarufu wako ulifahamika miongoni mwa mataifa kwa ajili ya uzuri wako, kwani ulikuwa mkamilifu kwa ajili ya utukufu wangu niliokuwa nimeuweka juu yako, asema Bwana Mwenyezi.

1516:15 Yer 2:20; Isa 57:8; Mik 3:11; Eze 23:3; 27:3“ ‘Lakini ulitumainia uzuri wako na kutumia umaarufu wako kuwa kahaba. Ulifanya uzinzi kwa kila mtu aliyepita, uzuri wako ukawa kwa ajili yake. 1616:16 2Fal 23:7; Hos 2:8; Isa 57:7Ulichukua baadhi ya mavazi yako ukayatumia kupamba mahali pako pa juu pa kuabudia miungu, mahali ambapo ulifanyia ukahaba wako. Mambo ya namna hiyo hayastahili kutendeka wala kamwe kutokea. 1716:17 Eze 7:20; Hos 2:13Pia ulichukua vito vizuri nilivyokupa, vito vilivyotengenezwa kwa dhahabu yangu na fedha yangu, ukajitengenezea navyo sanamu za kiume na ukafanya ukahaba nazo. 1816:18 Yer 44:5Ukayachukua mavazi yako niliyokupa yaliyotariziwa na ukazivalisha hizo sanamu, ukatoa mbele ya hizo sanamu mafuta yangu na uvumba wangu. 1916:19 Isa 57:7; Yer 44:21; Za 78:58; Hos 2:8Pia chakula changu nilichokupa ili ule: unga laini, mafuta ya zeituni na asali, ulivitoa mbele yao kuwa uvumba wa harufu nzuri. Hayo ndiyo yaliyotokea, asema Bwana Mwenyezi.

2016:20 Yer 7:31; Kut 13:2; Za 106:37-38; Isa 57:5; Eze 23:37“ ‘Nawe uliwachukua wanao na binti zako ulionizalia mimi na kuwatoa kafara kuwa chakula kwa sanamu. Je, ukahaba wako haukukutosha? 2116:21 2Fal 17:17; Yer 19:5Uliwachinja watoto wangu na kuwatoa kafara kwa sanamu. 2216:22 Za 25:7; Hos 11:1; Za 88:15; Hos 2:15; Yer 2:2Katika matendo yako yote ya machukizo, pamoja na ukahaba wako hukukumbuka siku za ujana wako, wakati ulipokuwa uchi kabisa bila kitu chochote, ulipokuwa ukigaagaa kwenye damu yako.

2316:23 Eze 24:6“ ‘Ole! Ole wako! Asema Bwana Mwenyezi. Pamoja na maovu yako yote mengine, 2416:24 Za 78:58; Yer 44:21; Isa 57:7; Eze 20:28; Yer 2:20; 3:2Ukajijengea jukwaa na kujifanyia mahali pa fahari pa ibada za miungu kwenye kila uwanja wa mikutano. 2516:25 Mit 9:14; Yer 6:15; 3:2Katika kila mwanzo wa barabara ulijenga mahali pa fahari pa ibada za miungu na kuaibisha uzuri wako, ukiutoa mwili wako kwa kuzidisha uzinzi kwa kila apitaye. 2616:26 1Fal 14:9; Eze 8:17; Yer 11:15; Isa 57:8; 23:17; Eze 23:17; 33:19-21; 20:8Ulifanya ukahaba wako na Wamisri, jirani zako waliojaa tamaa, ukaichochea hasira yangu kwa kuongezeka kwa uzinzi wako. 2716:27 Eze 20:33; 25:13; 2Nya 28:18; Yer 34:20Hivyo nilinyoosha mkono wangu dhidi yako na kuipunguza nchi yako, nikakutia kwenye ulafi wa adui zako, binti za Wafilisti, walioshtushwa na tabia yako ya uasherati. 2816:28 2Fal 16:7; Amu 10:6; Eze 23:14; Isa 57:8Ulifanya ukahaba na Waashuru pia, kwa kuwa hukuridhika, hata baada ya hayo, ukawa bado hukutosheleka. 2916:29 Yer 3:1; Eze 23:14-17; Nah 3:4Ndipo ukaongeza uzinzi wako kwa Wakaldayo nchi ya wafanyabiashara, hata katika hili hukutosheka.

3016:30 Yer 3:3“ ‘Tazama jinsi ulivyo na dhamiri dhaifu, asema Bwana Mwenyezi, unapofanya mambo haya yote, ukifanya kama kahaba asiyekuwa na aibu! 3116:31 Eze 16:24, 39Unapojenga jukwaa lako kila mwanzo wa barabara na kufanyiza mahali pa fahari pa ibada za miungu katika kila kiwanja cha wazi, lakini hukuwa kama kahaba, kwa sababu ulidharau malipo.

32“ ‘Wewe mke mzinzi! Unapenda wageni, kuliko mume wako mwenyewe. 3316:33 Isa 30:6; 57:6; Hos 8:9-10; Mwa 30:15Kila kahaba hupokea malipo, lakini wewe hutoa zawadi kwa wapenzi wako wote, ukiwahonga ili waje kwako kutoka kila mahali kwa ajili ya ukahaba wako. 34Kwa hiyo wewe ulikuwa tofauti na wanawake wengine kwenye ukahaba wako, hakuna aliyekutongoza ili kuzini naye, wewe ndiye uliyelipa wakati hakuna malipo uliyolipwa wewe. Wewe ulikuwa tofauti.

35“ ‘Kwa hiyo, wewe kahaba, sikia neno la Bwana! 3616:36 Yer 19:5; Eze 23:10; Yer 2:34Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa kuwa umemwaga tamaa zako na kuonyesha uchi wako katika uzinzi wako kwa wapenzi wako na kwa sababu ya sanamu zako zote za machukizo na kwa sababu uliwapa damu ya watoto wako, 3716:37 Isa 47:2-3; Hos 2:10; Ufu 17:16; Eze 23:9; Yer 13:22; Hos 8:10kwa hiyo nitawakusanya wapenzi wako wote, wale ambao ulijifurahisha nao, wale uliowapenda na wale uliowachukia pia. Nitawakusanya wote dhidi yako kutoka pande zote na nitakuvua nguo mbele yao, nao wataona uchi wako wote. 3816:38 Mwa 38:24; Eze 23:25; Law 20:10; Za 79:3-5; Kut 21:12; Sef 1:17Nitakuhukumia adhabu wanayopewa wanawake wafanyao uasherati na hao wamwagao damu, nitaleta juu yenu kisasi cha damu cha ghadhabu yangu na wivu wa hasira yangu. 3916:39 Eze 23:26; Hos 2:3; Eze 21:31; 2Fal 18:11Kisha nitakutia mikononi mwa wapenzi wako, nao watabomoa majukwaa yako na kuharibu mahali pako pa fahari pa ibada ya miungu. Watakuvua nguo zako na kuchukua vito vyako vya thamani na kukuacha uchi na bila kitu. 4016:40 Yn 8:5-7Wataleta kundi la watu dhidi yako, watakaokupiga kwa mawe na kukukatakata vipande vipande kwa panga zao. 4116:41 Kum 13:16; Yer 19:13; Eze 23:10; 22:15; Rum 2:8; Eze 23:48Watachoma nyumba zako na kutekeleza adhabu juu yako machoni pa wanawake wengi. Nitakomesha ukahaba wako, nawe hutawalipa tena wapenzi wako. 4216:42 2Sam 24:25; Eze 5:13; Isa 40:1-2; 54:9Ndipo ghadhabu yangu dhidi yako itakapopungua na wivu wa hasira yangu utaondoka kwako. Nitatulia wala sitakasirika tena.

4316:43 Kut 15:24; Za 78:42; Eze 11:21; 22:31“ ‘Kwa sababu hukuzikumbuka siku za ujana wako, lakini ulinikasirisha kwa mambo haya yote, hakika nitaleta juu ya kichwa chako yale uliyotenda, asema Bwana Mwenyezi. Je hukuongeza uasherati juu ya matendo yako yote ya kuchukiza?

4416:44 Za 49:4“ ‘Kila mtu atumiaye maneno ya mithali hii, atayatumia juu yako: “Alivyo mama, ndivyo alivyo bintiye.” 4516:45 Eze 14:5; 23:5; Yer 44:19Wewe ni binti halisi wa mama yako, ambaye alimchukia kabisa mume wake na watoto wake, tena wewe ni dada halisi wa dada zako, waliowachukia kabisa waume zao na watoto wao. Mama yako alikuwa Mhiti na baba yako alikuwa Mwamori. 4616:46 Mwa 13:10-13; Ufu 11:8; Mwa 18:20; Yer 3:8-11; Eze 23:4Dada yako mkubwa alikuwa Samaria, aliyeishi upande wako wa kaskazini na binti zake, pamoja na dada yake, naye dada yako mdogo, aliyeishi kusini yako pamoja na binti zake, alikuwa Sodoma. 4716:47 2Fal 21:9; Eze 5:6-7Hukuziendea njia zao tu na kuiga matendo yao ya kuchukiza, bali kwa muda mfupi katika njia zako zote uliharibika tabia zaidi kuliko wao. 4816:48 Mt 10:15; 11:23-24; Lk 10:12; Mwa 15:2; 19:25Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, dada yako Sodoma pamoja na binti zake, kamwe hawakufanya yale ambayo wewe na binti zako mmefanya.

4916:49 Isa 1:10; Mwa 13:13; Eze 28:2; Amo 6:4-8; Yak 5:5; Lk 12:16-20“ ‘Sasa hii ilikuwa ndiyo dhambi ya dada yako Sodoma: yeye na binti zake walikuwa na majivuno, walafi na wazembe, hawakuwasaidia maskini na wahitaji. 5016:50 Mwa 18:20-21; Ay 18:18; Mwa 19:5; Za 18:27Walijivuna na kufanya mambo ya machukizo sana mbele zangu. Kwa hiyo niliwakatilia mbali nami kama mlivyoona. 5116:51 Yer 3:9-11; Eze 23:11; Mt 12:40-41; Eze 5:6-7Samaria hakufanya hata nusu ya dhambi ulizofanya. Wewe umefanya mambo mengi sana ya kuchukiza kuwaliko wao, nawe umewafanya dada zako waonekane kama wenye haki kwa ajili ya mambo haya yote uliyoyafanya. 5216:52 Yer 3:11; Eze 23:35Chukua aibu yako, kwa kuwa umefanya uovu wa dada zako uwe si kitu, nao waonekane kama wenye haki. Kwa kuwa dhambi zako zilikuwa mbaya zaidi kuliko zao, wameonekana wenye haki zaidi kuliko wewe. Kwa hiyo basi, chukua aibu yako, kwa kuwa umewafanya dada zako waonekane wenye haki.

5316:53 Kum 30:3; Yer 48:47; Rum 9:23; Isa 19:24-25; Eze 39:25“ ‘Lakini nitarudisha baraka za Sodoma na binti zake na za Samaria na binti zake, nami nitarudisha baraka zako pamoja na zao, 5416:54 Yer 2:26; Eze 14:22-23ili upate kuchukua aibu yako na kufedheheka kwa ajili ya yote uliyotenda ambayo yamekuwa faraja kwao wakijilinganisha na wewe. 5516:55 Eze 36:11; Mal 3:4Nao dada zako, Sodoma na binti zake na Samaria na binti zake, watarudishwa kama vile walivyokuwa mwanzoni, nawe pamoja na binti zako mtarudishwa kama mlivyokuwa hapo awali. 56Hukuweza hata kumtaja dada yako Sodoma kwa sababu ya dharau yako katika siku za kiburi chako, 5716:57 2Fal 16:6; 2Nya 28:18; Za 137:3kabla uovu wako haujafunuliwa. Hata hivyo, sasa unadhihakiwa na binti za Edomu na jirani zake wote, na binti za Wafilisti, wale wote wanaokuzunguka wanakudharau. 5816:58 Eze 23:49Utachukua matokeo ya uasherati wako na matendo yako ya kuchukiza, asema Bwana.

5916:59 Eze 17:19; Kum 29:12-14“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitakushughulikia kama unavyostahili, kwa kuwa umedharau kiapo changu kwa kuvunja Agano. 6016:60 Mwa 9:16; Yer 32:40; Kut 2:24; Hos 2:15; Mwa 6:18; Za 25:7Lakini nitakumbuka Agano nililolifanya nawe wakati wa ujana wako, nami nitaweka nawe Agano imara la milele. 6116:61 Eze 43:10; 44:13; Wim 8:8; Gal 4:26; Eze 20:43; Isa 43:6Ndipo utakapozikumbuka njia zako na kuona aibu utakapowapokea dada zako, wale walio wakubwa wako na wadogo wako. Nitakupa hao wawe binti zako, lakini si katika msingi wa Agano langu na wewe. 6216:62 Hos 2:19-20; Yer 24:7; Ebr 8:6-13; Eze 20:37, 43-44; Kum 29:14; Eze 34:25Hivyo nitalifanya imara Agano langu na wewe, nawe utajua kuwa Mimi ndimi Bwana. 6316:63 Rum 3:9; Za 79:9; 78:38; 39:9; Dan 9:7-8; Za 65:3Basi, nitakapofanya upatanisho kwa ajili yako, kwa yale yote uliyoyatenda, utakumbuka na kuaibika, nawe kamwe hutafumbua tena kinywa chako kwa sababu ya aibu yako, asema Bwana Mwenyezi.’ ”

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

以西結書 16:1-63

耶路撒冷的不忠

1耶和華對我說: 2「人子啊,你要使耶路撒冷知道她的可憎行徑。 3你要告訴她,主耶和華這樣對她說,『你祖居迦南,生於迦南。你的父親是亞摩利人,母親是人。 4你出生時沒人剪斷你的臍帶,沒人用水洗你的身體,用鹽擦淨你,用布包裹你。 5沒有人可憐你,同情你,為你做以上的事。你生下來便遭人厭惡,被扔在野外。

6「『我從你旁邊經過,見你在血泊中掙扎,便對血泊中的你說,活下去! 7我使你像田間的植物一樣茁壯生長。你漸漸發育成熟,長得亭亭玉立,雙乳豐滿,秀髮垂肩,但仍然赤身露體。

8「『後來我又從你旁邊經過,見你正值少女懷春,我便用衣襟遮蓋你的身體,向你起誓,與你定下婚約,你便屬於我。這是主耶和華說的。 9我用水洗淨你身上的血污,給你塗上馨香的油, 10穿上錦繡的衣裳和海狗皮的鞋,披上細麻衣和絲綢外袍。 11我用首飾來裝扮你,給你戴上手鐲、項鏈、 12鼻環、耳環和華冠。 13這樣,你戴的是金銀首飾,穿的是綾羅綢緞,吃的是細麵粉、蜂蜜和油。你變得美豔絕倫,晉升為王后。 14你的美貌名揚四方,因為我給你的華貴使你美貌無比。這是主耶和華說的。

15「『你卻仗著自己的美貌和名聲縱情淫亂,與所有過路的人苟合。 16你用自己的衣服在拜偶像的地方結彩,在那裡行淫。這樣的事真是空前絕後! 17你用我給你的金銀首飾為自己製造男人的像,與他們苟合。 18你給他們穿上錦繡衣服,把我給你的膏油和香料供奉他們。 19你把我賜你吃的細麵粉、油和蜂蜜作為馨香的供物奉獻在他們面前。這是主耶和華說的。 20你還把你給我生的兒女燒作燔祭獻給偶像。難道你淫亂還不夠嗎? 21你竟屠殺我的兒女,把他們焚燒獻給偶像。 22你做這一切可憎、淫亂的事,忘記了你幼年赤身露體,在血泊中掙扎的日子。

23「『主耶和華說,你有禍了!你有禍了!你不但做了這些惡事, 24還為自己築祭壇,在各廣場建高高的神廟。 25你在街頭巷尾建高高的神廟,糟蹋自己的美貌。你向每一個過路的人投懷送抱,縱情淫亂, 26甚至與放縱情慾的鄰邦埃及人苟合,激起我的憤怒。 27看吧,我要伸手攻擊你,削減你的口糧,把你交給憎恨你的非利士人,任他們宰割。他們會為你的淫蕩行為感到羞恥。 28你慾海難填,又跟亞述人行淫,但仍不滿足, 29於是又跟那商賈之地的迦勒底人行淫,但仍不滿足。

30「『主耶和華說,你的心敗壞至極,簡直就像不知羞恥的娼妓, 31因為你在街頭巷尾築祭壇,在廣場建高高的神廟,甚至不收淫資,實在連妓女都不如。 32你這蕩婦,寧願跟外人淫亂,也不愛自己的丈夫。 33妓女接受淫資,你卻送禮物給所有的情人,引誘他們從四方前來跟你淫亂。 34你賣淫不同於別的妓女,沒有人給你淫資,你倒貼錢給人,你真是與眾不同。

主對耶路撒冷的審判和應許

35「『你這淫婦,要聽耶和華的話。 36主耶和華說,你放縱情慾,赤身露體地與眾情人苟合。你祭拜一切可憎的偶像,把自己兒女的血獻給它們。 37因此,我要把你所愛和所恨的情人都聚集起來,從四方攻擊你,讓你赤裸裸地顯露在他們面前,讓他們看到你赤身露體。 38我要懲罰你,像懲罰淫亂和殺人的婦女一樣。我要把烈怒和義憤倒在你身上,報應你殺人流血的罪。 39我要把你交在你的情人手裡。他們必拆毀你的祭壇,夷平你高高的神廟,剝去你的衣裳,奪走你的珠寶,留下你赤身露體。 40他們要聚眾攻擊你,用石頭打你,用刀劍砍碎你, 41燒毀你的房屋,在眾婦女面前審判你。我要阻止你的淫亂行為,使你不再倒貼錢給情人。 42這樣,我的烈怒才會平息,我的義憤才會消除,我才會平靜下來,不再發怒。 43因為你忘記了幼年的日子,做這些事來惹我發怒,我要照你的所作所為報應你。因為你不僅行一切可憎的事,還放蕩淫亂。這是主耶和華說的。

44「『好說俗語的人都會譏諷你說,有其母必有其女。 45你和你母親及姊妹如出一轍,都厭棄自己的丈夫和兒女。你母親是人,你父親是亞摩利人。 46你姐姐是撒瑪利亞,她和她的女兒們住在你的北面。你妹妹是所多瑪,她和她的女兒們住在你的南面。 47你不僅追隨她們可憎的行徑,還很快超過了她們。 48我憑我的永恆起誓,與你妹妹所多瑪和她女兒們相比,你和你女兒們的行徑有過之而無不及。這是主耶和華說的。 49看啊,你妹妹所多瑪和她的女兒們傲慢狂妄,安逸飽足,對窮困的人漠不關心。 50她們心驕氣傲,在我面前做可憎的事,我看見後便除掉了她們。 51撒瑪利亞的罪還不及你的一半,你做的事比她們做的更可憎,以致與你相比,你的姊妹倒顯得公義了。 52既然你幫了你的姊妹,使她們顯得公義,你就蒙受羞辱吧!因為你犯的罪比你姊妹犯的罪更可憎,以致她們顯得比你更公義。因此,你就自取其辱,抱愧蒙羞吧!

53「『然而,我要使所多瑪撒瑪利亞及她們的女兒們復興,並使你一同復興, 54讓你自取其辱,深感羞愧,因為你的一切惡行使她們反得安慰。 55你姊妹所多瑪撒瑪利亞和她們的眾女兒,以及你和你的眾女兒必恢復起初的光景。 56-57在你驕傲的日子,你的惡行還沒有被揭露的時候,你覺得妹妹所多瑪不屑一提。但現在,你卻成為以東的眾女兒和她四鄰非利士的眾女兒的笑柄。你周圍的人都鄙視你。 58你要承擔淫蕩和可憎行徑帶來的懲罰。這是耶和華說的。

59「『主耶和華說,你背誓毀約,我必照你的所作所為報應你。 60然而,我顧念在你幼年時與你所立的約,我要與你立一個永遠的約。 61你接納你姊妹的時候,會想起自己的所作所為並自覺羞愧。我要將你姊妹賜給你作女兒,我這樣做並不是出於我與你所立的約。 62我要和你立約,使你知道我是耶和華。 63我要赦免你所有的罪,那時你想起這事會羞愧難當,不敢再開口。這是主耶和華說的。』」