Malkia Vashti Aondolewa
11:1 Ezr 4:16; Es 9:30Hili ndilo lililotokea wakati wa utawala wa Mfalme Ahasuero, yule aliyetawala juu ya majimbo mia na ishirini na saba tangu Bara Hindi hadi Kushi.1:1 Kushi hapa ina maana ya Ethiopia. 2Wakati huo Mfalme Ahasuero alitawala katika kiti chake cha enzi katika ngome ya mji wa Shushani. 31:3 1Fal 3:15Katika mwaka wa tatu wa utawala wake, alifanya karamu kwa ajili ya wakuu wake wote pamoja na maafisa. Akawaalika viongozi wa jeshi wa Uajemi na Umedi, wana wa wafalme na wakuu wa majimbo.
4Kwa siku zote 180 mfalme alionyesha utajiri mwingi wa ufalme wake, fahari na utukufu wa enzi yake. 51:5 Amu 14:17; 2Fal 21:18Siku hizo zilipopita, mfalme alifanya karamu kwa muda wa siku saba, katika bustani ya ndani katika jumba la kifalme, kwa ajili ya watu wote kuanzia mdogo hadi mkubwa, waliokuwa katika ngome ya mji wa Shushani. 61:6 Eze 23:41; Amo 3:12; 6:4Bustani ilikuwa na mapazia ya kitani nyeupe na buluu, yaliyofungiwa kamba za kitani nyeupe na kitambaa cha zambarau, kwenye pete za fedha juu ya nguzo za marmar. Kulikuwepo viti vya dhahabu na vya fedha vilivyokuwa vimewekwa kwenye ile sakafu iliyotengenezwa kwa mawe ya rangi, marmar, lulumizi na mawe mengine ya thamani. 7Vyombo vya dhahabu vilitumika kwa watu kunywea mvinyo, kila kimoja tofauti na kingine, naye mfalme akatoa mvinyo kwa wingi kwa kadiri ya ukarimu wake. 8Kwa amri ya mfalme kila mgeni aliruhusiwa kunywa alichotaka, kwa kuwa mfalme alitoa maagizo kwa watumishi wote wa kuhudumu mvinyo kumhudumia kila mtu kwa jinsi alivyotaka.
9Malkia Vashti pia akawafanyia wanawake karamu katika jumba la kifalme la Mfalme Ahasuero.
101:10 Rut 3:7; Dan 5:1-4Siku ya saba, wakati Mfalme Ahasuero alikuwa amesisimka roho yake kwa mvinyo, aliamuru matowashi saba waliokuwa wakimhudumia, yaani, Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari na Karkasi, 11kumleta Malkia Vashti mbele ya mfalme akiwa amevaa taji lake la kifalme, ili aonyeshe uzuri wake kwa watu na wakuu, kwa kuwa alikuwa ni mzuri wa kupendeza. 121:12 Mwa 39:19; Mit 19:12Lakini wakati watumishi walipotoa amri ya mfalme, Malkia Vashti alikataa kuja. Ndipo mfalme alighadhibika, na hasira yake ikawaka.
131:13 1Nya 12:32Kwa kuwa ilikuwa desturi ya mfalme kupata ushauri kwa wataalamu katika mambo ya sheria na haki, alizungumza na watu wenye busara, ambao walijua nyakati, 14nao waliokuwa karibu na mfalme ni Karshena, Shethari, Admatha, Tarshishi, Meresi, Marsena na Memukani, wakuu saba wa Uajemi na Umedi waliokuwa na nafasi ya pekee kwa mfalme nao walikuwa na vyeo vya juu kabisa katika utawala wake.
15Mfalme akauliza, “Kulingana na sheria, Malkia Vashti anapaswa kutendewa nini? Malkia hakutii amri ya Mfalme Ahasuero ambayo matowashi walimpelekea.”
16Kisha Memukani akajibu mbele ya mfalme na wakuu, “Malkia Vashti si kwamba amemkosea mfalme tu bali pia amewakosea wakuu wote na watu wa himaya yote ya Mfalme Ahasuero. 17Kwa maana tendo hili la malkia litajulikana kwa wanawake wote, kwa hiyo watawadharau waume zao na kusema, ‘Mfalme Ahasuero aliagiza Malkia Vashti aletwe mbele yake, lakini alikataa.’ 18Leo hii wanawake wa wakuu wa Uajemi na Umedi ambao wamesikia juu ya tabia ya malkia watawatendea wakuu wote wa mfalme vivyo hivyo. Hapatakuwepo na mwisho wa dharau na magomvi.
191:19 Es 8:6; Dan 6:8, 12“Kwa hiyo, kama itampendeza mfalme, atoe amri ya kifalme na iandikwe katika sheria ya Uajemi na Umedi, ambayo haitabadilika, kwamba Vashti kamwe asije tena mbele ya Mfalme Ahasuero. Pia mfalme na atoe hiyo nafasi yake ya umalkia kwa mwanamke mwingine aliye bora kumliko yeye. 20Kisha mbiu hii ya mfalme itakapotangazwa katika himaya yake iliyo kubwa sana, wanawake wote watawaheshimu waume zao, kuanzia mdogo hadi mkubwa.”
21Mfalme na wakuu wake walipendezwa na shauri hili, hivyo basi mfalme akafanya kama Memukani alivyopendekeza. 221:22 Neh 13:24Alipeleka barua katika sehemu zote za ufalme wake, kwa kila jimbo kwa maandishi yake mwenyewe na kwa kila watu katika lugha yao wenyewe, akitangaza kwa msemo wa kila watu kwamba inampasa kila mwanaume kuwa mtawala wa nyumba yake mwenyewe.
亚哈随鲁王大宴群臣
1亚哈随鲁在位期间,统治从印度到古实的一百二十七个省。 2亚哈随鲁王在书珊城登基, 3他在执政第三年大宴群臣,波斯和玛代的将领、各省的贵族和大臣都在场。 4整整一百八十天,他展示自己帝国的财富和王权的威荣。 5之后,他又一连七天在御花园宴请书珊城里所有的居民,无论尊卑。 6御花园里有白色的棉帐和蓝色的彩帐,用细麻绳和紫色绳系在大理石柱的银环上。有金银制成的床榻摆在各色斑岩、大理石、珍珠贝壳及其他贵重石头铺成的地上。 7饮酒用的是各式各样的金器皿,御酒大量供应,足显王的慷慨。 8喝酒有个规矩,不许勉强人,因为王吩咐过宫里所有的侍从,招待各人要随其所愿。 9瓦实提王后也在亚哈随鲁王的宫里设宴招待女宾。
瓦实提王后被废
10第七天,亚哈随鲁王喝得心中畅快,就吩咐在王身边服侍的米户幔、比斯他、哈波拿、比革他、亚拔他、西达和甲迦七位太监, 11去请瓦实提王后戴着后冠到王面前,向百姓和官员展现她的美貌,因为她非常美丽。 12但瓦实提王后违抗太监所传的谕旨,拒绝前来,王非常生气,怒火中烧。
13王有事习惯征求通晓律例和法则之人的意见,于是他去问精通时务的哲士。 14那时,靠近王的有甲示拿、示达、押玛他、他施斯、米力、玛西拿和米姆干七位波斯和玛代的大臣,他们常见王的面,在国中身居高位。 15王问他们:“瓦实提王后违抗太监所传的谕旨,按律该如何处置她?”
16米姆干当着王和大臣们的面说:“瓦实提王后不但冒犯了王,而且有害于举国的臣民。 17因为王后的事必传到所有妇女的耳中,致使她们藐视自己的丈夫,因为她们会说,‘亚哈随鲁王请瓦实提王后到他面前,她却不去。’ 18今天,波斯和玛代的贵妇听到王后这事,也会如此对待王的大臣,藐视和恼怒之事必层出不穷。 19王若愿意,就请降旨不准瓦实提再到王面前,把她王后的位分赐给比她更好的女子,并将此谕旨写入波斯和玛代的律法,永不更改。 20王的谕旨传遍王辽阔的国境后,所有的妇女,无论丈夫贵贱,都必尊重他们。”
21王和大臣们都赞同米姆干的建议,王便依照他的建议, 22用各省的文字和各族的语言写谕旨,通告各省,丈夫要做一家之主,说话有权柄。