Danieli 2 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Danieli 2:1-49

Ndoto Ya Nebukadneza

12:1 Mwa 20:3; 41:8; Ay 33:15-18; Es 6:1; Dan 6:18; 4:5Katika mwaka wa pili wa utawala wake, Nebukadneza aliota ndoto. Mawazo yake yakasumbuka na hakuweza kulala. 22:2 Mwa 41:8; Kut 7:11; Yer 27:9; Isa 9:13; 44:25; Dan 4:6Hivyo mfalme akawaita waganga, wasihiri, wachawi na wanajimu ili wamwambie ndoto yake aliyokuwa ameota. Walipoingia ndani na kusimama mbele ya mfalme, 32:3 Dan 4:5akawaambia, “Niliota ndoto inayonisumbua, nami nataka nijue maana yake.”

42:4 Ezr 4:7; Neh 2:3; Dan 5:10Ndipo wanajimu wakamjibu mfalme kwa lugha ya Kiaramu,2:4 Kutoka hapa hadi Dan 7:28, mwandishi aliandika na Kiaramu. “Ee mfalme, uishi milele! Waambie watumishi wako hiyo ndoto, nasi tutaifasiri.”

52:5 Ezr 6:11; Dan 3:29; Mwa 41:32Mfalme akawajibu wanajimu, “Nimeamua hivi kwa uthabiti: Ikiwa hamtaniambia ndoto yangu ilikuwa ipi na kuifasiri, mtakatwa vipande vipande na nyumba zenu zitafanywa kuwa vifusi. 62:6 Dan 5:7, 16Lakini mkiniambia ndoto yangu na kuielezea, mtapokea kwangu zawadi, tuzo na heshima kubwa. Basi niambieni ndoto yangu na mnifasirie.”

7Wakajibu kwa mara nyingine, “Mfalme na awaambie watumishi wake ndoto yake, nasi tutaifasiri.”

8Ndipo mfalme akajibu, “Nina hakika kuwa mnajaribu kupata muda zaidi, kwa sababu mnatambua kuwa nimeamua hivi kwa uthabiti: 92:9 Es 4:11; Isa 41:22-24; 2:10Ikiwa hamtaniambia ndoto yangu, ipo adhabu moja tu kwenu. Mmefanya shauri kuniambia habari za kunipotosha na mambo maovu, mkitumaini kwamba hali itabadilika. Hivyo basi, niambieni hiyo ndoto, nami nitajua kuwa mwaweza kunifasiria.”

102:10 Dan 3:8; 4:7; 5:8Wanajimu wakamjibu mfalme, “Hakuna mtu duniani ambaye anaweza kufanya analotaka mfalme! Vilevile hakuna mfalme hata awe mkuu na mwenye uweza namna gani, aliyeuliza kitu kama hicho kwa mganga au kwa msihiri, wala kwa mnajimu yeyote. 112:11 Kut 8:10; Mwa 41:38; Dan 5:11Anachouliza mfalme ni kigumu mno. Hakuna yeyote awezaye kumfunulia mfalme isipokuwa miungu, nao hawaishi miongoni mwa wanadamu.”

122:12 Dan 3:13-19; Mit 16:14; 28:15Jambo hili lilimkasirisha na kumghadhibisha mfalme mno hata kuagiza kuuawa kwa wenye hekima wote wa Babeli. 132:13 Dan 1:20; 5:19Hivyo amri ikatolewa ya kuwaua wenye hekima, nao watu wakatumwa kuwatafuta Danieli na rafiki zake ili wawaue.

14Wakati Arioko, mkuu wa askari wa walinzi wa mfalme, alikuwa amekwenda kuwaua watu wenye hekima wa Babeli, Danieli akazungumza naye kwa hekima na busara. 15Akamuuliza huyo afisa wa mfalme, “Kwa nini mfalme ametoa amri kali hivyo?” Ndipo Arioko akamweleza Danieli jambo hilo. 16Aliposikia jambo hili, Danieli akamwendea mfalme, akamwomba ampe muda ili aweze kumfasiria ile ndoto.

17Ndipo Danieli akarudi nyumbani kwake na kuwaeleza rafiki zake Hanania, Mishaeli na Azaria jambo hilo. 182:18 Isa 37:4; Yer 33:3; Ufu 11:13; Ezr 1:2; Neh 1:4Aliwasihi waombe rehema kutoka kwa Mungu wa mbinguni kuhusu siri hii, ili yeye na rafiki zake wasije wakauawa pamoja na wenye hekima wengine wa Babeli. 192:19 Ay 33:15; Dan 1:17; Hes 12:6; Yos 22:23Wakati wa usiku lile fumbo lilifunuliwa kwa Danieli katika maono. Ndipo Danieli akamhimidi Mungu wa mbinguni, 202:20 Za 113:2; 145:1-2; Ay 9:4; Yer 32:19; Ay 12:13na akasema:

“Lihimidiwe jina la Mungu milele na milele;

hekima na uweza ni vyake.

212:21 Dan 7:25; Ay 12:19; Rum 13:1; Yak 1:5; Yer 27:5; Za 75:6-7; 2Sam 14:17; Dan 4:17Yeye hubadili nyakati na majira;

huwaweka wafalme na kuwaondoa.

Huwapa hekima wenye hekima,

na maarifa wenye ufahamu.

222:22 Mwa 40:8; 1Kor 2:10; Ay 12:22; Ebr 4:13; Isa 45:7; Yak 1:17; Za 139:11-12; Dan 4:17Hufunua siri na mambo yaliyofichika;

anajua yale yaliyo gizani,

nayo nuru hukaa kwake.

232:23 Mwa 31:5; Kut 3:15; Dan 1:17; Eze 28:3Ninakushukuru na kukuhimidi,

Ee Mungu wa baba zangu:

Umenipa hekima na uwezo,

umenijulisha kile tulichokuomba,

umetujulisha ndoto ya mfalme.”

Danieli Aifasiri Ndoto

242:24 Eze 28:3Ndipo Danieli akamwendea Arioko, ambaye mfalme alikuwa amemteua kuwaua wenye hekima wa Babeli, akamwambia, “Usiwaue wenye hekima wa Babeli. Nipeleke kwa mfalme, nami nitamfasiria ndoto yake.”

252:25 Dan 5:13; 6:13; Kum 21:10; Dan 1:6Arioko akampeleka Danieli kwa mfalme mara moja na kumwambia, “Nimempata mtu miongoni mwa watu wa uhamisho kutoka Yuda ambaye anaweza kumwambia mfalme maana ya ndoto yake.”

262:26 Dan 1:7Mfalme akamuuliza Danieli (aliyeitwa pia Belteshaza), “Je, unaweza kuniambia nilichoona katika ndoto yangu na kuifasiri?”

272:27 Mwa 41:8Danieli akajibu, “Hakuna mwenye hekima, msihiri, mganga au mwaguzi anayeweza kumweleza mfalme siri aliyouliza, 282:28 Yer 10:7; Amo 4:13; Dan 4:5; Mwa 40:8; Dan 10:14; Mt 24:6; Eze 28:3; Dan 1:20lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri. Amemwonyesha Mfalme Nebukadneza kitakachotokea siku zijazo. Ndoto yako na maono yaliyopita mawazoni mwako ulipokuwa umelala kitandani mwako ni haya:

29“Ee mfalme, ulipokuwa umelala kitandani, yalikujia mawazo kuhusu mambo yatakayotokea baadaye, naye mfunuaji wa siri akakuonyesha ni kitu gani kitakachotokea. 302:30 Mwa 41:16; Mdo 3:12; Isa 45:3; Amo 4:13; Dan 1:7Kwangu mimi, nimefunuliwa siri hii, si kwa sababu nina hekima kubwa kuliko watu wengine wanaoishi, bali ni ili wewe, ee mfalme, upate kujua tafsiri, na ili uweze kuelewa kile kilichopita mawazoni mwako.

312:31 Isa 25:3-5; Hab 1:7“Ee mfalme, ulitazama, na mbele yako ilisimama sanamu kubwa, kubwa mno kupita kiasi, sanamu iliyongʼaa na kutisha kwa kuonekana kwake. 32Kichwa cha ile sanamu kilikuwa kimetengenezwa kwa dhahabu safi, kifua chake na mikono yake vilikuwa vya fedha, tumbo lake na mapaja yake vilikuwa vya shaba, 33miguu yake ilikuwa ya chuma, na nyayo zake zilikuwa chuma nazo sehemu nyingine zilikuwa udongo wa mfinyanzi uliochomwa. 342:34 Ay 12:19; Zek 4:6; Isa 60:12; Dan 8:25; Ay 34:24; Za 2:9Ulipokuwa unaangalia, jiwe lilikatwa, lakini si kwa mikono ya mwanadamu. Lile jiwe liliipiga ile sanamu kwenye nyayo zake za chuma na udongo wa mfinyanzi, na kuivunja. 352:35 Isa 41:15-16; 2:3; Ufu 11:15; Za 37:10; Isa 17:13; Zek 12:3; Za 1:4Ndipo ile chuma, ule udongo wa mfinyanzi, ile shaba, ile fedha na ile dhahabu vikavunjika vipande vipande kwa wakati mmoja, na vikawa kama makapi katika sakafu ya kupuria nafaka wakati wa kiangazi. Upepo ukavipeperusha bila kuacha hata alama. Lakini lile jiwe lililoipiga ile sanamu likawa mlima mkubwa mno na kuijaza dunia yote.

362:36 Mwa 40:12“Hii ndiyo iliyokuwa ndoto, nasi sasa tutamfasiria mfalme. 372:37 Ezr 7:12; Eze 26:7; Yer 27:7; Dan 4:26Ee mfalme, wewe ni mfalme wa wafalme. Mungu wa mbinguni amekupa wewe utawala, uweza, nguvu na utukufu. 382:38 Dan 4:21; Yer 27:6; Dan 5:18Mikononi mwako amewaweka wanadamu, wanyama wa kondeni, na ndege wa angani. Popote waishipo amekufanya wewe kuwa mtawala juu yao wote. Wewe ndiye kile kichwa cha dhahabu.

392:39 Dan 7:5“Baada yako, ufalme mwingine utainuka, ulio dhaifu kuliko wako. Baadaye utafuata ufalme wa tatu, ule wa shaba, nao utatawala juu ya dunia yote. 402:40 Dan 7:7; Yn 11:48; Dan 7:232:40 Ufu 12:3; Eze 40:2; Dan 8:7-10Hatimaye, kutakuwako na ufalme wa nne, wenye nguvu kama chuma, kwa maana chuma huvunja na kupondaponda kila kitu; kama vile chuma ivunjavyo vitu vipande vipande, ndivyo ufalme huo utakavyopondaponda na kuvunjavunja nyingine zote. 41Kama vile ulivyoona kuwa kwa sehemu nyayo na vidole vilikuwa vya udongo wa mfinyanzi uliochomwa na kwa sehemu nyingine chuma, hivyo huu utakuwa ufalme uliogawanyika; hata hivyo utakuwa na sehemu zenye nguvu za chuma ndani yake, kama vile ulivyoona chuma imechanganywa na udongo wa mfinyanzi. 42Kama vile vidole vyake vya miguu vilikuwa kwa sehemu chuma na sehemu udongo wa mfinyanzi, hivyo ufalme huo kwa sehemu utakuwa na nguvu na kwa sehemu udhaifu. 43Kama vile ulivyoona chuma kikiwa kimechanganyikana na udongo wa mfinyanzi uliochomwa, ndivyo watu watakavyokuwa mchanganyiko, wala hawatabaki wameungana tena, kama vile chuma kisivyoweza kuchanganyikana na udongo wa mfinyanzi.

442:44 Mwa 27:29; Mt 21:43-44; 1Sam 9:20; Isa 60:12; Ufu 11:15; 1Kor 15:24-25; Za 145:13; Isa 9:7; Dan 4:34; 6:26; 7:14, 27; Oba 1:12; Mik 4:7, 13; Lk 1:33“Katika siku za wafalme hao, Mungu wa mbinguni atauweka ufalme ambao kamwe hautaangamizwa, wala hautaachiwa taifa jingine. Utaziponda zile falme zote na kuzikomesha, bali wenyewe utadumu milele. 452:45 Isa 28:16; Dan 8:25; Mwa 41:25; Ufu 22:6Hii ndiyo maana ya maono ya jiwe lililochongwa kutoka mlimani, lakini si kwa mikono ya mwanadamu, lile jiwe ambalo lilivunja chuma, shaba, udongo wa mfinyanzi, fedha na dhahabu vipande vipande.

“Mungu Mkuu amemwonyesha mfalme kile kitakachotokea wakati ujao. Ndoto hii ni ya kweli na tafsiri yake ni ya kuaminika.”

462:46 Mdo 10:25; Dan 8:17; Mdo 14:13; Ezr 6:10Ndipo Mfalme Nebukadneza akaanguka kifudifudi mbele ya Danieli kumpa heshima, akaagiza wamtolee Danieli sadaka na uvumba. 472:47 Kum 10:17; Dan 11:36; 4:25; 1Tim 6:15; Dan 4:25; 4:9Mfalme akamwambia Danieli, “Hakika Mungu wako ni Mungu wa miungu, na Bwana wa wafalme, na mfunuaji wa siri zote, kwa maana umeweza kufunua siri hii.”

482:48 Es 8:2; Dan 8:27; Mwa 41:40; 2Fal 25:28; Dan 1:20; 4:9; 5:11Ndipo mfalme akamweka Danieli nafasi ya juu, na kumpa zawadi nyingi tele. Akamfanya kuwa mtawala wa jimbo lote la Babeli, na kumweka kuwa mkuu wa wenye hekima wote. 492:49 Dan 3:30; Mit 28:12; 1:7; Es 2:19; Amo 5:15; Dan 6:2; 3:30Zaidi ya hayo, kwa ombi la Danieli, mfalme akawateua Shadraki, Meshaki na Abednego kuwa wasimamizi wa jimbo la Babeli, huku Danieli akibaki katika ukumbi wa mfalme.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

但以理书 2:1-49

尼布甲尼撒的梦

1尼布甲尼撒在执政第二年做了梦,心里烦乱,无法入睡, 2便派人召来术士、巫师、行法术的和占星家2:2 占星家”亚兰文作“迦勒底人”,同下2:4510节;3:84:75:711,为他解梦。他们都来到王面前。 3王对他们说:“我做了一个梦,心里烦乱,想知道梦的意思。” 4占星家用亚兰话对王说:“愿王万岁!请将梦告诉仆人,仆人好解释梦的意思。” 5王对占星家说:“我的旨意已定,你们若不能将梦和梦的意思告诉我,必被碎尸万段,你们的家必沦为废墟。 6你们若能将梦和梦的意思告诉我,我必给你们礼物、赏赐和极大的尊荣。所以你们要将梦和梦的意思告诉我。” 7他们再次对王说:“请王将梦告诉仆人,仆人好解释梦的意思。” 8王说:“我敢肯定,你们是在拖延时间,因为你们知道我的旨意已定, 9你们若不将梦告诉我,我必惩治你们。你们串通起来在我面前胡言乱语,期待情况会改变。现在将梦告诉我,我就相信你们能解梦。” 10占星家说:“王所要求的,世上无人能做到,因为再伟大、再有权势的君王也没问过术士、巫师或占星家这样的事。 11王问的事太难,除了不在人间居住的神明外,无人能为王解答。” 12王大怒,下令处死巴比伦所有的智者。 13于是,处死智者的谕旨发出,但以理和他的同伴都在被杀之列。

14王的护卫长亚略奉命要处死巴比伦的智者,但以理机智、谨慎地应对。 15他问王的护卫长亚略:“王的命令为何这样紧急?”亚略就把情况告诉他。 16但以理便进宫求王宽限,以便为王解梦。 17然后,他回到居所将这事告诉同伴哈拿尼雅米沙利亚撒利雅18要同伴祈求天上的上帝施怜悯,显明这奥秘,以免他们和其他巴比伦的智者一起被杀。 19这奥秘在夜间的异象中向但以理显明,他便颂赞天上的上帝, 20说:

“上帝的名永永远远当受称颂,

因为智慧和能力都属于祂。

21祂改变时令和季节,废王立王,

赐智慧给智者,赐知识给哲士。

22祂显明深奥隐秘之事,

洞悉暗中的隐情,

有光与祂同住。

23我祖先的上帝啊,我感谢你,赞美你,

因你赐我智慧和能力,

应允我们的祈求,

使我们明白王的梦。”

但以理解梦

24于是,但以理去见王指派处死巴比伦智者的亚略,对他说:“不要处死巴比伦的智者,请带我去见王,我要为王解梦。” 25亚略急忙带但以理去见王,对王说:“我在被掳的犹大人中找到一个能为王解梦的。” 26王就问又名伯提沙撒但以理:“你能将我做的梦和梦的意思告诉我吗?” 27但以理回答说:“没有智者、术士、巫师或占星家可以解答王所问的奥秘, 28-30但天上的上帝能揭开奥秘,祂已把将来要发生的事告诉了王。王啊,你在床上梦见了将来的事,揭开奥秘的上帝已把将来的事指示给你。上帝将王做的梦启示给我,并非因为我的智慧胜过其他人,而是要让王知道梦的意思和王的心事。以下是王在床上做的梦和脑中出现的异象。

31“王啊,你梦见一个高大宏伟、极其明亮的塑像站在你面前,相貌可怕, 32有纯金的头、银的胸和臂、铜的肚腹和大腿、 33铁的小腿和半铁半泥的脚。 34在你观看的时候,有一块非人手凿出的石头打在塑像半铁半泥的脚上,砸碎了脚。 35铁、泥、铜、银、金随即粉碎,犹如夏天麦场上的糠秕,被风吹得无影无踪。但打碎这像的石头变成一座大山,充满整个大地。

36“这就是梦的内容。现在我们要为王解梦。 37王啊,你是万王之王,天上的上帝已将国度、权柄、能力和尊荣赐给你, 38也将居住在各地的世人、走兽和飞禽都交在你手中,让你管理。你就是那金头。 39在你之后,必有另一国兴起,不及你的国强大。之后是将要统治天下的第三个国,是铜的。 40接着是坚如铁的第四国,能击垮、打碎列国,正如铁能击垮、打碎一切。 41你看见半铁半陶泥的脚和脚趾,表示那将是一个分裂的国。正如你看见铁和泥混杂在一起,它必有铁一般的力量。 42半铁半泥的脚趾表示那国必半强半弱。 43你看见铁和泥混杂在一起,这表示那国的民族彼此混杂通婚,却不能团结,正如铁和泥无法混合。 44在以上列王统治的时候,天上的上帝必设立一国——永不灭亡、外族无法夺其政权。这国将击垮、消灭列国,并且永远长存。 45你看见那块非人手从山中凿出的石头打碎铁、铜、泥、银和金。伟大的上帝已把将来的事告诉了王。这梦是真实的,解释是可靠的。”

46尼布甲尼撒王俯伏在地,向但以理下拜,并下令给他献供物和香。 47王对但以理说:“你们的上帝真是万神之神、万王之主、奥秘的启示者,因为你能揭开这个奥秘。” 48王赐但以理高官及许多贵重的礼物,派他治理巴比伦全省,管理巴比伦所有的智者。 49王又应允但以理的请求,派沙得拉米煞亚伯尼歌负责巴比伦省的事务。但以理仍在朝中供职。